Huyu jamaa anaitwa Kuringe kaingia mjini

Huyu jamaa anaitwa Kuringe kaingia mjini

Wala huyo jamaa sio mtu wa kupindisha kwa taarifa yako. Hela yake imenyooka ndio maana Magu mwenyewe hakumfanya kitu. Alex massawe mwenyewe alimuuzia nyumba zake zote pale kkoo.
Sasa ikawaje Kuringe kupeleka mabaunsa usiku wa manane na kubomoa frame za wapangaji bila kuwa na nyaraka za mahakama, kama clip inavyojieleza.
Au alipata mhemko wa pesa zake kufanya apendalo?
 
Kuna jamaa anaitwa Kuringe, kaingia mjini Dar es Salaam na shoka.
Na ana kata kulia na kushoto akiwanunua watu na viwanja vyao kama hana akili nzuri.

Ukienda wilaya ya Kinondon i utamkuta yupo tele kila mahali.
Mitaa ya Goig Mbezi Beach kanunua mtaa mzima.

Kama utafika Mbezi NSSF road ile RED Hall ni yake.
Ile Kuringe Sports Bar kulekea Baraza la Mitihani haya tena, na hivyo ni baadhi tu ya vitega uchumi na viwanja alivyonunua Kinondoni.

Jina halisi la Kuringe nasikia ni somebody Edward Mushi, kijana mdogo ambaye zimemtembelea.

Nimeona hii clip mahali, nikaona nimpe ushauri wa bure.

Namshauri tu, bwana Kuringe , aste aste brother, taratibu jiji hili la Chalamila, wengi wametajirikia hapa, ila wengi pia wamefilisikia hapa DSM.
Kula na kipofu, gusa mkono wa mwanasiasa wa Kinondoni, ndo utalijua Jiji.

======
Mwekezaji Joanna Chifunda aeleza kuhusu uvamizi wa eneo lake la biashara liliopo Mikocheni kwa Nyerere Jijini Dar es salaam. Inadaiwa kwamba fremu saba katika plot namba 27 zilivunjwa na Watu waliojitambulisha kwamba wametumwa na Kuringe ambaye anadai kwamba amenunua eneo hilo baada ya kuingia makubaliano na kumlipa Mmiliki aitwaye Zacharia Maftah.

Joanna Chifunda anaeleza kwa kirefu zaidi alipofanya mahojiano na Waandishi wa habari siku ya Jumamosi, Oktoba 12, 2024 mbele ya fremu hizo zilizovunjwa.

Abdulmajid Zakaria Maftah ambaye amejitambulisha kama ni mmojawapo wa watoto saba wa mzee Zakaria Maftah akieleza kuhusu uvamizi na mgogoro wa ardhi katika eneo liliopo kwenye plot namba 27, Mikocheni kwa Nyerere Jijini Dar es salaam.
Inadaiwa kwamba fremu saba katika eneo hilo zilivunjwa usiku wa kuamkia Oktoba 12, 2024 na Watu waliojitambulisha kwamba wametumwa na Kuringe ambaye anadai kuwa amenunua eneo hilo baada ya kuingia makubaliano na kumlipa Mmiliki aitwaye Zacharia Maftah.
Kuringe = Jilinde (kwa Kichaga cha marangu, kilema, kirua vunjo).
 
Sasa ikawaje Kuringe kupeleka mabaunsa usiku wa manane na kubomoa frame za wapangaji bila kuwa na nyaraka za mahakama, kama clip inavyojieleza.
Au alipata mhemko wa pesa zake kufanya apendalo?
Hicho ni kitengo ndani ya kampuni wala unaweza kukuta yeye hajui na pia hizo mambo wala isikupe shida mzee ukiona hivyo kama kahusika hesabu zilishapigwa kutoka mwisho kuja mwanzo. Japo mi sio msemaji ila jamaa namjua yuko very smat
 
Hapo ndio unazidi kumu expose huyu Kuringe a.k,a Edward Mushi, kwamba anaajiri mabaunsa, hooligans. kwenda kubomoa kijinai, akiwa hana mamlaka ya kisheria?
 
Wala huyo jamaa sio mtu wa kupindisha kwa taarifa yako. Hela yake imenyooka ndio maana Magu mwenyewe hakumfanya kitu. Alex massawe mwenyewe alimuuzia nyumba zake zote pale kkoo.
Ukisha nunua nyumba za Alex Massawe,tayari wwe umesha nunua mgogoro ambao hujui utajitokeza lini,na inawez hata ikawa kesho au baada ya muda flani!!
 
Ukisha nunua nyumba za Alex Massawe,tayari wwe umesha nunua mgogoro ambao hujui utajitokeza lini,na inawez hata ikawa kesho au baada ya muda flani!!
Story. Waoga hufa kabla ya siku zao usisahau. Niliwah kununua shamba kubwa kwelikweli miaka ya mwanzo ya 2000 kwa mzee mmoja mchawi kweli kweli kule ununio kila mtu anakataa kununua kwasababu mzee ni mchawi kwamba hapatalalika. Nililamba dume. Nilikuja kugawa nikauza vipande nilipiga mpunga wa kutosha. Acha kuishi life ya watu ishi yako. Vinginevyo utabakiwa kuhesbau magorofa ya wanaume mjini na kubaki kuita watu freemason.
 
Back
Top Bottom