Huyu mdada kanipenda au ananionea huruma tu?

Huyu mdada kanipenda au ananionea huruma tu?

Vile watoa comment waki mwangalia mleta uzi, anaye subiri kuambiwa kapendwa
FB_IMG_17508595064934429.jpg
 
kakuonea tu huruma, kwanini wakaka mkionyeshwa wema kidogo mnahisi ni mapenzi..? ama mnadhani wanawake hawana mioyo yenye huruma na upendo pia..?
😁
Ni utoto tu.
Na by the way hii ni chai, sema imepikwa kitaalam sana. Unaanzaje kula vitumbua mchana mtu mzima, tena safarini bila kishushio? Hayo mambonya watoto tulupokua primary hukoo
 
You are a very ungrateful human being. Hapo Mungu kaamua kumtumia huyo binti kukupa chakula halafu unaanza kuwaza upuuzi. Na kama unatokea Njombe uwezekano wa wewe kuwa hata handsome au mwonekano wa kuvutia binti ni mdogo sana kwa hiyo suala la kukutaka kimapenzi halipo.

Mwaka 2004 naenda form 5 pale Mkwawa nilikutana na hali kama hiyo yako ila mimi nilimshukuru Mungu na kuchukulia kama muujiza. Nikiwa kwenye basi la Hood from Arusha mfukoni nina Tsh 1,000/= tu kama pocket money. Nilikuwa nawaza kinoma itakuwaje hii buku ndo ya kula njiani hapohapo pocket money shule??

Binti aliyekuwa pembeni yangu hatukusemeshana kabisa. Pale Chalinze akanunua chungwa na kunigawia. Nikashukuru. Morogoro pia kuna kitu alinunua akanigawia. Ilula akaninunulia chips. Tulipofika Iringa tukaagana na ndo ikawa mara ya kwanza na ya mwisho kuonana. Wote hatukuwa na siku wakati huo.

Bahati nzuri nilipofika shuleni kwa mhasibu nikajulishwa kuwa kuna michango kwenye joining instructions shule iliamua kuifuta. Nikapata muujiza mwingine wa kurudishiwa Tsh 17,000/=.
Nimeamini tuliosoma iringa tuna akili timamu, nilipiga Tosamaganga hapo five na six
 
Back
Top Bottom