Huyu mdada kanipenda au ananionea huruma tu?

Hahahaaaa ametamani figo Yako angalia usiamini watu asije kukurubuni ukaenda na maji shtuka hujapitia hata JKT ukimuamini tu mtu ana ondoka na MJEKI au MAGAZINE utalia
 
Hili ndilo tatizo la vijana wengi kuwaza kamanyola tu badala ya upendo.
 
Hivi una miaka kumi na ngapi dogo, yaani kuonewa huruma tu wewe unawaza mapinduzi?
 
Sijui hii mifano mnatoa wapi ndugu zangu wanaume wa Kitanzania, ila nimekutana na wadada wengi wenye roho zao nzuri tu kwa watu wasiowajua, tena wengine wananifanya mpaka nizidi kujifunza kuendelea kuwa mwema kupitia wao..!!
Unakutana nao wewe ila sisi malaika tunakutana na shetani kwa sura,mwili na roho yani iwe jua,mvua ni kimetulamba!
 
hebu zingatia hili...... njombe to dar ukae kwa dereva kisa kukosa siti( nauli huna)........ sehemu ya kula uchukue vitumbua na maji ( hata kama huli njiani hata kasoda mzee)....... akili yako ulipoiwekeza inaonyesha dhahiri ni jinsi gani unaweza pata mchongo ukaona mchongoma na ukapigiliwa mchongoma ukifurahia umepata mchongo
 
Amepiga hesabu ya umbali kutoka njombe to dar na akaona unakula vitambua na hayo maji kinyonge akaona hasipojiongeza wanaweza kupata msiba katikati ya milima kitonga
 
kakuonea tu huruma, kwanini wakaka mkionyeshwa wema kidogo mnahisi ni mapenzi..? ama mnadhani wanawake hawana mioyo yenye huruma na upendo pia..?

Eti mtu unakula vitumbua au chips dume za mihogo na maji ya jero. Halafu mtu anakupa msosi, unaanza kujiona hendisam
 

Hapo aya ya 1. Ina maana njombe hakuna mahendisam
πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Useme pia ulivyopewa chipsi kuku ulipokea kwa magoti kwa kutokuamini macho yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…