Umenikumbusha mbali sana miaka hiyo kuna mwanamke mmoja hivyohivyo kama ilivyokutokea wewe alikuwa classmate wangu baadae tukakutana chuo nikachukua namba yake tukaanza kuchat baadae nikatupia ndoano tena.
Kwa kawaida mimi kwenye mambo ya mapenzi huwa natanguliza akili kwanza hisia na moyo vinakaa nyuma.
Basi nimetupia ndoano mara ya kwanza,ya pili,ya tatu demu analeta maringo baadae nikauchuna.
Baadae ikapita miezi kadhaa anaona kimya,siku moja akanitumia meseji inayosomeka"Ina maana kumbe wewe ulikuwa unanijaribu,haukuwa serious si ndio"
Mimi nikamjibu,wewe si ulikataa sasa hapo nina makosa gani?
Cha msingi mkuu iko hivi,ukitumia nguvu sana huwapati hao viumbe nenda nao kwa step.