Hivi ni nani alisema mwanamke ukimtaka lazma umpate?...
Fikiria mkuu, kama mwanamke kamkataa toka wapo O-level hadi chuoni ambapo hata love huwa ipo kiasi flani kwa random dates. Unadhani shida ni kipato au ni kuwa tu hamtaki au kuna vitu havimvutii kuhusu jamaa
Mbaya zaidi, kwa wengi wakikataliwa ndio wanazidisha upendo zaidi bila kujua wanazidisha usumbufu tu na kuonekana ving'ang'anizi kiasi cha kupoteza haiba na mamlaka ya kiume. Mwisho wa siku wanakataliwa zaidi
Ukiona mtu umempa care ya kutosha kwa miaka na ulipoamua kumkalia kimya na yeye akakaa kimya. Hii inamaanisha uwepo wako kwenye maisha yake ni sifuri yani hata care yako haijali. Kiufupi haupendwi
Yani labda kama ana mtu wake wa muda mrefu halafu jamaa ampige tukio. Hapo ndo anaweza pata nafasi kama spare tyre. Kinyume na hapo asahau