Huyu mjamzito amenyanyaswa na wahudumu wa mwendokasi hapa Mbezi Mwisho mpaka akazimia

Huyu mjamzito amenyanyaswa na wahudumu wa mwendokasi hapa Mbezi Mwisho mpaka akazimia

Nianze na Swali: Watoto wa kuanzia miaka mingapi wanapaswa kulipa nauli za mwendokasi?

Mida ya hii jioni huyu dada mjamzito alikuwa na mwanaye wakiwa wanasubiri mwendokasi za Kivukoni. Mtoto alikuwa na miaka kama mitano hivi.

Alipoingia kwenye gari cha ajabu mhudumu anayescan ticket akawa analazimisha yule dada amlipie na huyo mtoto nauli, ilhali ni mtoto mdogo anayeweza kupakatwa.

Pamoja na dada kuwaambia atampakata lakini walimgomea, ndipo ikatokea kukusukumana hapa na pale mpaka ikabidi watu wote watoke kwenye mwendokasi.

Haijalishi ni nani alikuwa na kosa hapa, lakini sijapenda namna huyu dada mjamzito alivyokuwa treated, maana wamemuharrass sana mpaka dada wa watu akazimia, huku mwanaye akilia kwa uchungu.

Hili shirika japo ni la umma, lakini staffs wake wana zero customer care, hawana utu na hawajali wateja hata kama ana hali inayohitaji kusaidiwa.

Mtoto waliyekuwa wanafosi alipie👇
View attachment 2960024

Mama mjamzito akiwa ameanguka chini👇
View attachment 2960027

View attachment 2960028

Mwendokasi iliyokuwa inaenda Kivukoni👇

View attachment 2960033
Kwenye mwendokasi Watoto wa miaka 5 na kuendelea wanalipia hiyo 200/ tofauti na kwenye panton ambapo wanafunzi wanapanda bure.

Wangemuelewesha tu. Sema kwakuwa na Dada mjamzito hakuwa na mpango wa kulipa hiyo 200/ ndiyo maana yakatokea hapo.
 
Hii siyo suluhisho la kudumu.
Kulipia nauli muhimu.
Kumsukuma mjamzito ni kosa.
Inawezekana hakutaka kuelewa. Ameelekezwa amlipie mtoto 200/ hakutaka. Mfanyakazi anasimamia maelekezo mama anasema atampakata
 
Back
Top Bottom