Huyu Mkuu wa Mkoa wa Tanga sidhani kama kuna kiongozi pale; labda cheo alipewa Kwa connection

Wakati wenzio wako kwenye msiba mkubwa huko Rombo we umekalia umbea tu...watu 20 sasa wamefariki maana majeruhi watatu wamefariki.
Na jins unavyochukia wachaga utakuwa umefurahi sana msiba huo kutokea. Kwani nani hakujui humu jamvin?
 
Mimi na wewe hatujui exactly kilichopelekea RC kufanya uamuzi huo lakini ninaamini kuna jambo nyuma yake.

Najaribu kuwaza mbali kwa kutumia haya maswali:
i) Je, kama walipigiwa simu kusaidia jukumu hilo na wakatoa majibu mabaya? Unafikiri mkuu wa mkoa akitaka kupata huduma ya dharula za hospitali atawasiliana moja kwa moja na madaktari au wauguzi bila kupitia kwa RMO au DMO?

ii) Ili huduma ya kupatikana vifaa, magari na hata madaktari kwenda kusaidia mahanga ni Nani kwenye kuiwezesha ? ni RMO au ni zimamoto au Raia au RC?
 
Chadema maoni yenu ni km wavuta bangi
Are you serious au unatania? Mstari mmoja unaweza kujibu hoja zote zilizoanishwa?

How comes hoja hizo zihusishwe na CHADEMA na sio mwanaharakati au mwananchi yeyote yule ambaye anayeweza kuona kwa jicho la tatu kuwa maamuzi ya kisiasa yanaathiri maisha ya watu kwa sababu ya political popularity?

Kunapotokea ajali Ni waganga wakuu pamoja na wafawawidhi wanaoenda kwenye eneo la tukio au Ni zimamoto na uokoaji? Are u mad au mud?

Wapi ulisikia kwamba the first response team kwenye ajali Ni madaktari?

Umeulizwa hapo juu, mkuu wa ulinzi na usalama wa mkoa alikua wapi wakati tukio linatokea? Mbona yeye hakuwahi kufika kwenye scene? Analaumu watu ambao hawana facilities za kufika eneo la tukio Tena mid night?

Mkiwa mnatetea upuuzi msiwaumizw watu wengine for the sake of ugali na political popularity! Hilo swala sio la CHADEMA na bavicha wa la RMO na DMO Ni swala la serikali kushindwa kuweka Mazingira wezeshi ya huduma ya kwanza na uokoaji pamoja na response!

Nchi za wenzetu Kuna namba za dharura za Kila Idara au kitengo kinachohusiana na maisha ya watu moja kwa moja iwe afya na ulinzi na Mambo mengineyo!

Chukua simu yako hapo Sasa piga fire au polisi uone Kama itapokelewa na Kama ikipokelewa uone Kama Ni on time! Kama una ndugu yako Yuko state muulize ukipiga 911 inakueje!
 
Hii Ni hypothesis au ndio uhalisia? Tuzungumze Mambo halisia kwamba Ni kutokana na A and B sio Conspiracy theories?
 

Naomba nichangie kutokana na kichwa cha uzi, hakuna cheo kwenye hii nchi ambacho mtu anaweza kukipata bila connection. Ndio maana huko wamejazana watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri.
 
Kwanini unazungumzia "huenda" andikeni vitu empirical! RMO na DMO ndio wanaopanga roaster na KUANDIKA referrals? Serious? Kama Ni hivyo Basi kazi ipo Sana!
 
Huyu mtu hata hafai kuwa mkuu wa mkoa, afadhali naye akalime nyanya tu, ushamba unamsumbua. Hata huko kwenye utaratibu mzuri wa huduma za uokozi wanaoenda kutoa huduma ya kwanza sio madaktari wazoefu ni wahudumu wa ngazi za chini wanaoitwa Paramedics. Daktari mkuu wa wilaya na Mkoa wanaojua wajibu wao kama walipata taarifa mapema, walipaswa kwenda Hospitalini kuongeza nguvu na kuongoza shughuli nzima ya kuokoa majeruhi, kuhakikisha vifaa vinapatikana au kupanga namna ya ku-refer waliozidiwa. Shughuli ya kunasua au kubeba majeruhi ikiwa ni pamoja na kuzuia uvujaji wa damu inaweza kufanywa na polisi wakisaidiana na wananchi wa kawaida. Sio mganga mkuu ambaye ndiye mwenye uzoefu kuliko wenzake. Huyu mkuu wa mkoa asifanye mchezo na madaktari atatuletea matatizo maana hawezi kukaa kimya wakati siasa za kujipendekeza zinaingizwa kwenye taaluma yao. Sasa Mganga mkuu hayupo, nani atawachukulia hatua watendaji wa chini ambao labda kitaaluma hawakutimiza wajibu wao. Hata kama mganga mkuu ana tuhuma zinazochunguzwa kuna ushahidi gani atakaouingilia akibaki ofisini au kuendelea kutibu wagonjwa?
 
Kinachowaumiza madaktari ni kosa la dharau kwa mamlaka zao, insurbodination kwa kupuuza agizo na wito halali wa mkuu wa mkoa wao, na kukataa kutoa maelezo au kufika eneo walilotakiwa la ajali. Watumishi wa Serikali wanaongozwa na kanuni za utumishi serikalini na miongozo mbalimbali, utii na nidhamu ndiyo msingi, hiyo siyo private hospital. Watajiju!
 
Unaandika kwa kwa kudhani au ndio uhalisia hebu fikiri Tena ndio uje uaandike ! Yaani madaktari watoke hospital wende kwenye accident scene huku Kuna kitu inaitwa zimamoto na uokoaji! Wewe Ni mjinga Kama Mgumba mnahitaji elimu Sana!
 
Ungeweka hiyo audio clip ya RC nasi tukamsikiliza,ungetusaidia kufanya uchambuzi mzuri juu yake
 
Hawa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ndiyo maana watu wanawalalamikia,maamuzi mengine yanakuwa na mihemko sana,na actually ukitrace anaweza kuwa na Element za awamu ya tano huyu.

Ajali imetokea usiku unataka mda huohuo RMO awepo eneo la ajali kufanya nini kama watu wake wa chini huduma zinaendelea,hata kama kafika saa 10 usiku bado kaonyesha kujitoa kuachana na usingizi kuja eneo la tukio tuache uonevu,otherwise labda kama huduma zilisimama.
 
Ngoja kwanza akili zitukae sawa.
 
Anataka RMO awe eneo la ajari utafikiri.ndiye.askari wa barabarani. Vha ajabu utasikia kapandishwa cheo. HII nchi ukitumia Akili sana kuchambua mambo unakufa kwa kiharusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…