Huyu Mkuu wa Mkoa wa Tanga sidhani kama kuna kiongozi pale; labda cheo alipewa Kwa connection

Huyu Mkuu wa Mkoa wa Tanga sidhani kama kuna kiongozi pale; labda cheo alipewa Kwa connection

Kinachowaumiza madaktari ni kosa la dharau kwa mamlaka zao, insurbodination kwa kupuuza agizo na wito halali wa mkuu wa mkoa wao, na kukataa kutoa maelezo au kufika eneo walilotakiwa la ajali. Watumishi wa Serikali wanaongozwa na kanuni za utumishi serikalini na miongozo mbalimbali, utii na nidhamu ndiyo msingi, hiyo siyo private hospital. Watajiju!
Ukikaa nyuma ya keyboard uanaadika unachojisikia tu. Unaweza kudhibitisha haya?
 
Timu iliyoundwa inatumia pesa za nani
Nchi hii Ina viongozi wa hovyo wasiokua na aibu kwa Mambo wanayofanya mbele ya umma!

Ajali ya barabarani imetokea na imeghraimu maisha ya watu!
Kuna DTO pamoja na Traffic kwanini wao Kama wataalam wasioewe responsibility ya kuinvestigate na kuleta majibu na mapendekezo.

Unaunda team unawapa perdeim wanachunguza for a month wanaleta makabrasa mezani unafungia kabatini hakuna tija yoyote!

Badala ya kufanya improvement kwenye usimamizi wa Sheria za usalama barabarani na usimamizi wa vyombo vya usafiri kwa uendelevu unasubiri ajali ili na wewe upige! Nonsense
 
Msisitizo na sheria kali ziwekwe ili kuepukana na uzembe na uhuni barabarani unao gharimu maisha ya watanzania.

Mtu au watu tu wameamua kuvunja sheria za usalama barabarani halafu hekaheka waje kuwapa watu innocent?!

Hapana!

Mwendokasi unaua!
 
Kabla ya kumkashifu Mkuu wa mkoa ni vyema ukapata Taarifa ya upande wa pili.
Je,Daktari wa zamu alikua kazini muda huo, nesi wa zamu je?
Kama hawakuwepo basi palikua na uzembe Fulani.

Huenda Daktari aliyetakiwa kuandika Rufaa hakuwepo ili wagonjwa wawahishwe Hospitali ya mkoa.
Huenda wagonjwa walichelewa kupata hata huduma ya kwanza kutokana na kuchelewa Kwa Madaktari.
Hata kama walikuwepo ndo wawaache wagonjwa wakimbilie hiyo ajari ???

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Nimemsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga sakata la ajali ya Costa iliyoua watu 17. Kwa kumsikiliza Tu unagundua Hana maarifa. Kama si zao la awamu ya tano basi ana vimelea vya Wakuu wa Mikoa wa awamu ya tano. Walikuwa wakuu wa Mikoa wa kukamata, kufunga ,weka maabusu nk

Hospitali zetu zinajulikana hazina magari yakutosha ya wagonjwa; tunaelewa kwamba Madaktari wa wilaya na Mikoa awaendi kwenye ajali wanasubiri waletewe majerui hospitalini, tunaelewa wazi kwamba usiku Madaktari wanakuwa wachache hospitalini na polisi wanakuwa wengi barabarani wakiwa na magari ya Doria. Nini kosa ya mganga mkuu wa wilaya na Mkoa?

Lakini pia kutokana na uchache wa wataalamu yawezekana hawa waliosimamishwa kazi ndio wataalamu wabobezi wanaotakiwa kuwahudumia hao wagonjwa na wagonjwa wengine kwenye maeneo Yao. Leo kuna watu wanakosa huduma zao hospitali Kwa Sababu wapo nybani wanasubiri uchunguzi kwanini walichelewa kwenda eneo la ajali.

Hebu tujiulize mkuu wa Wilaya alikuwa wapi wakati ajali inatokea? Tujiulize polisi walikuwa wapi? Mkuu wa mkoa na mganga mkuu wote wapo Tanga mjini, yeye alikuwa wapi hakuwahi kwenda kutoa huduma ya Kwanza? Kwanini kama yeye alishindwa kufika Kwa wakati anaamini Mganga mkuu angeweza kufika kwa wakati? Nani mwenye usafiri wa kuwahi eneo la tukio Kati ya mkuu wa mkoa na mganga mkuu?

Kama tunataka kuokoa maisha ya watu uchunguzi uendelee wakati hao wahusika wakiwa wanaendelea kutoa huduma. Tunaweza kutumia akili ndogo kwenye taaluma tukawapokonya uhai wagonjwa wengi.

Ilipotokea ajali ya ndege mwanza mafmdaktari mabingwa walikwenda kuokoa au walikaa kwenye vyumba vyao wakiwa na vifaa kutoa huduma?

Mkuu wa mkoa unataka kutuambia Mganga mkuu ana mobile hospital? Kwamba anaweza kwenda eneo la ajali na vifaa vya hospitali?

Nimetafakari Sana nikajiuliza wanaofanya kazi chini yake wapo salama? Ndio maana mkoa haupati maendeleo.
1.taarifa inasema madaktari hawakuwepo hospital na sio eneo la ajali
2.mkuu wa wilaya aliwahi kufika eneo la tukio masaa mawili baada ya ajali tena akitokea lushoto(ni dc wa lushoto anakaimu)
3.inakuwaje DC akupigie simu udharau
4.umuhimu wa kuwepo yeye kuna majeruhi walihitaji referral kwa haraka yeye anakuja saa11 ilibidi DC atoe referral
5.kifupi wamedharau mamlaka iliopo juu yao
 
Tupate kusikia na upande wa pili! Acheni siasa za kutafuta kulinda ugalinkwa gharama yanmadkatari wetu! Poor politicians
Nani Ana uhakika kuwa DC alikua Luushoto wakati wa ajali? Au amejitetea tu Kama yeye.
Alikuaje sehemu mbili kwa wakati mmoja yaani accident scene and hospital kujua madaktari hawapo?
Question, usiku wa manane Kama Dr ameenda Tanga mjini anatumia usafiri gani kurudi kituoni? Au mnadhani korogwe Ni Kama dms usafiri Ni twenty four hours?
 
Watu wengi wanependa kuajiriwa na mshahara lakini kufanya kazi hawataki.

Tukipenda kufanya kazi mambo kama hayo hayatakuwepo.
 
Kabla ya kumkashifu Mkuu wa mkoa ni vyema ukapata Taarifa ya upande wa pili.
Je,Daktari wa zamu alikua kazini muda huo, nesi wa zamu je?
Kama hawakuwepo basi palikua na uzembe Fulani.

Huenda Daktari aliyetakiwa kuandika Rufaa hakuwepo ili wagonjwa wawahishwe Hospitali ya mkoa.
Huenda wagonjwa walichelewa kupata hata huduma ya kwanza kutokana na kuchelewa Kwa Madaktari.
unaambiwa alichelewa kufika kwa masaa 6, ungesubiriukasoma comments kadhaa ukapatapicha kwanza.
 
Tusaidie Kwa uelewa wako, mganga mkuu WA wilaya na Mkoa wanatakiwa wakafanye rescue au wanapaswa kukaa kwenye vituo vyao kujipanga kupokea na kuhudumia wagonjwa?

Lini umewahi kuona Madaktari wa muhimbili wakikimbizana kwenda kufanya rescue? Incase wakienda nani atasimamia matibabu hospitalini?

Mkuu WA mkoa anaposema mganga mkuu alichelewa, je yeye wakati hao wanachelewa alikuwa wapi? Hao waliowahi ambao hajawasiamamisha kazi NI wakina Nani?
Ni vyema ukawa na taarifa sahihi Kabla ya kuandika. RC hajasema walichelewa kufika eneo la tukio Bali anasema walichelewa kufika Hospitalini
 
Tupate kusikia na upande wa pili! Acheni siasa za kutafuta kulinda ugalinkwa gharama yanmadkatari wetu! Poor politicians
Nani Ana uhakika kuwa DC alikua Luushoto wakati wa ajali? Au amejitetea tu Kama yeye.
Alikuaje sehemu mbili kwa wakati mmoja yaani accident scene and hospital kujua madaktari hawapo?
Question, usiku wa manane Kama Dr ameenda Tanga mjini anatumia usafiri gani kurudi kituoni? Au mnadhani korogwe Ni Kama dms usafiri Ni twenty four hours?
Mimi nipo korogwe dc jatojea lushoto ni kama lusaa tu kutoka lushoto mpaka eneo la tukio
Daktari alipigiwa simu na walithibitisha wapo korogwe na wamepata taarifa kabla ya dc
Kumbuka yule ni mganga mkuu gari zote za afya zipo chini yake na alitakiwa kuwepo tu hospital
 
Anyway yote hayo nayajua bro I know the distance kutoka Luushoto DC mpaka mombo ni 1hr na mpaka korogwe Ni almost 30mins. On top of that 17 people died on the scene wabgeenda kuwafufua?
 
Anyway yote hayo nayajua bro I know the distance kutoka Luushoto DC mpaka mombo ni 1hr na mpaka korogwe Ni almost 30mins. On top of that 17 people died on the scene wabgeenda kuwafufua?
Hapo hakuna anaeshuhulika na Maiti tunazungumzia majeruhi hatuwezi kuwa na watu ambao hata mabosi wao hawawaheshimu sisi raia wa kawaida inakuwaje
 
Binafsi huwa sioni kazi za hawa viongozi wa mkoa, wilaya and the like. Sijawahi kuona umuhimu wao kabisa zaidi ya kuleta taharuki tu
Nchi inetulia tuliii halafu imeshika zako magimbi huko kwenu Tukuyu unasema hujaona umuhimu wa RC na DC? unataka wakuletee ugali .mezani ?
 
Kuna muda unatakiwa ufanye zaidi ya majukumu yako pindi inapo tokea dharura sasa ajali inatokea alafu we hata hospital haupo unafika alfajiri kwenye kituo chako cha kazi na ajali kubwa imetokea tangu saa 4 usiku kwanini watu wasiwe na hasira na wewe?

Wa Tz wengi wana moyo wa kujitolea sana mfano kwenye ajali hizi watu huwa wanahairisha had safari zao wapo tayari kukaa hata zaid ya masaa 4+ ili tu wawasaidie majeruhi mifano ipo mingi sana kwenye ajali hizi kubwa hata juzi kwenye ajali ya precision air watu walivuta had ndege kwa mikono yao Sasa inapo tokea wewe ambae unatakiwa ulibebe jukumu Kama kazi yako unapo jiweka pembeni haileti picha nzuri
 
Umewahi kusikia kitu kinaitwa Emergency Operation Plan/mpango wa kushughulika na dharura?
Ipo kwenye mkoa, wilaya au Hospitali? Ilifuatwa katika hili tukio?

Back
Top Bottom