Huyu Mkuu wa Mkoa wa Tanga sidhani kama kuna kiongozi pale; labda cheo alipewa Kwa connection

Serikali iacha blabla nyingi ..unakuta hospitali ina upungufu wa wa watumishi kwa 60 hao watu utawakuta wapi kila saa
 
Umewahi kusikia kitu kinaitwa Emergency Operation Plan/mpango wa kushughulika na dharura?
Ipo kwenye mkoa, wilaya au Hospitali? Ilifuatwa katika hili tukio?
Daktari wa wilaya anaishi karibu na hospital nyumba haipo hata umbali wa mita 30, ajali inatokea saa nne usiku watu wanaenda kwenye eneo la ajali wanaokoa wajeruhi na kutoa maiti wanapeleka Hadi hospital lakin daktari hayupo hospital anapigiwa sim anasema yeye anazo taarifa tena wao ndo walipata taarifa wa kwanza matokeo yake anaamua kwenda hospital alfajiri huo siyo uzembe?

Watu hawawalaumu kutofika eneo la ajali Ila wanalaumiwa kutokufika kituo cha kaz kutoa msaada katika hali ya dharura hali ya kuwa wanaishi mita 10 tu kutoka hospital ilipo, hizo nyumba kujengwa karibu na vituo vya kaz hazikujengwa bahati mbaya zilijengwa ili huduma ipatikane haraka wakati wa dharura
 

Ndani ya jeshi la Zimamoto na Uokoaji baadhi yao wafundishwe kuwa Paramedics na Advanced Paramedics.

Hao ndo watakaokuwa wanafanya kazi kwenye ambulances.

Inapotokea ajali wanaenda kwenye eneo la ajali na kutoa huduma kwa waliopata ajali ikiwa ni pamoja na kuwasafirisha wagonjwa kwenda hospitalini.

Ajali ikitokea, timu zifuatazo zifike eneo la tukio:
1. Ambulances (Paramedics)
2. Zimamoto na Uokoaji ( General)
3. Polisi - kwa ajili ya kulinda usalama

Ni muhimu polisi wawepo eneo la ajali kwa sababu inapotokea ajali baadhi ya wenyeji wa eneo husika huwa ni wezi badala ya kutoa msaada kwa wahanga.

Ila kwa ujumla, tuna safari ndefu kuweza kufikia viwango vinavyohitajika.
 
Huyo mkuu wa Mkoa yuko sahihi sana nimefuatilia sana mkuu.
Hao waliosimamishwa walipigiwa simu na mkuu wa Wilaya.
Mmoja alidanganya kuwa hayupo but asubuhi atatokea kwake ambapo ni mita chache kufika hospitalini.
 
Serikali iacha blabla nyingi ..unakuta hospitali ina upungufu wa wa watumishi kwa 60 hao watu utawakuta wapi kila saa
Sio kila kitu kuilaumu TU serikali .
Serikali imemwamini Daktari na kumpa kazi ya kulitumikia jamii inabidi afanye majukumu yake muda wote atakapo hitahika.

Kwenye hili la ajali ya Korogwe Blablaa aliifanya huyo Daktari Mwenyewe na sio Serikali .

Mtu unapigiwa simu na mkuu wa Wilaya Bado hustuki tuu kuwa Kuna jambo kubwa.

Hakuna mtu wa muhimu kuliko jamii.
Hilo linapaswa kueleweka hivyo. Kuna watu mara nyingine wanafikiri kuwa Elimu waliyoipata ni muhimu kuliko jamii. Jamii ndio inayatakiwa Ione umuhimu wa Elimu ya Mtu Kwa matendo yake ya kuisaidia jamii sio jamii impigie magoti mtu Kwa sababu ya Elimu au ujuzi Fulani . Hayo ni mambo ya kizamani.

Mara nyingi Tunawalaumu Polisi wa TRAFIKI lakini huwa hawachelewi kwenye eneo la ajali. Hata Kwa kutumia magari yao binafsi au kudandia malori lakini wanawahi haipiti nusu saa wanakua wamefika.
Unakuta wapo kwenye ajli hata kama ni usiku wa manane. Hilo nawapongeza TRAFIKI.
 
Mkuu wa mkoa anacheza libeneke la kwake mwenyewe.
One Man Show itamgharimu.
Ile kesi ya magendo, kuungua kwa ghala haikuwa bahati mbaya, wenziwe wanamfix.
Ajihadari, uongozi ni wa pamoja, watu wadogo chini yake wanaweza muharibia kabisa.
 
Huyu bwege katumia akili za kibwengo kufanya huo ujinga, Hospital zetu sio Redcross na haijawahi kuwa hivyo, atapata anachokitaka soon.
 
Binafsi naona sio fair kumuadhibu Mkwezi wakati nazi imeliwa na mwezi.

Imagine madereva waamue kuendesha kihuni bila tahadhari huku wakijua hawana cha kupoteza halafu ikitokea ajali Eti mtu au watu ambao ni innocence waache kulala na wake zao wakurupuke usiku wa Manane kwenda ku-rescue the situation?

Kwani hakukuwepo na madaktari wa zamu ?

Kama hawatoshi mwenye jukumu la kuajiri watoshe ni nani?
 
Wahuni waendeshe vibaya huko barabarani halafu Jumba bovu mtake kuwaangushia wengine?
 
Rudia tena kumsikiliza.
Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu wa mkoa yuko sahihi...daktari halaumiwi kwa kukosekana kwake ajalini bali analaumiwa kwa kukosekana kwake kituo cha kazi ambapo huduma ya dharula ilitakiwa kutolewa kuanzia kwa majeruhi na kuandikiwa kwa rufaa kwa wale ambao ni majeruhi.Hivyo kukisekana kwake kwa wakati ukute imepelekea hata kuongezeka kwa vifo.
 
umeongea vzr sana naunga mkono hoja zako.
 



What if nae alikuwa na dharura Kama binadamu?

Je amesikilizwa?
 
Umeandika kama "great thinker" wa ukweli.
Kongole na ubarikiwe sana.
 
Pingapinga wapo kazini hao hawana jema wala hawaoni jema lolote linalofanywa na Serikali. Mungu anawaona nyote mnaopingana na RC
 
Ijapokuwa Tanga ni kama ilivyo mikoa mingine mingi isivyo na wakuu wa mikoa isipokuwa mkoa wa Njombe, kinachokera Tanzania ni hawa makada wa CCM kujifanya wako juu ya wataalamu.
 
Katika hili namuunga mkono Mgumba, hii nchi hakuna watu wazembe na wanaochukulia ajira kama kitu cha mchezo kama watumishi wa Umma.

Tungekuwa na utaratibu wa kupima utendaji wa watumishi wa Umma kila baada ya mwaka,ukikuta ni mzembe unafukuza watu wanaotaka kufanya kazi wapewe kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…