Huyu mume kijana aliyemwua mke wake, ukweli ukoje wajameni?

Huyu mume kijana aliyemwua mke wake, ukweli ukoje wajameni?

Inasemekana.
Huyu mwanaume alikua ana uchumi mzuri, na kazi nzuri, pia kwao wako vizuri, ndipo akamuoa huyu mwanamke, wameishi na kuzaa watoto, kumbe mwanamke alikua na uwanja alinunua kabla ya kukutana na huyu mwanaume, ndipo akamuambia mumuwe wajenge nyumba ktk kiwanja hicho. Ila pesa na gharama zote za ujenzi wa nyumba ni za mwanaume.

Sasa hivi karibuni mume anaumwa kansa ya utumbo, na ameambiwa hawezi kupona, asubiri kifo tu, sasa mwanamke baada ya kujua mume muda wowote anang'ata shuka, ndipo kaanza harakati za kutaka nyumba hiyo iwe kwa jina lake na watoto pekee, ilifikia hali mbaya ya kutoelewana, ilibidi mwanaume aende kwao moshi akapumzike, na wakati huo huo mwanamke hakuwepo hapo nyumbani, mke akiporudi, majirani wakatuma taarifa kwa mume kuwa mkewe karudi. Bwana akatoa huko moshi usiku kwa usiku na kuwasili home bunju alfajiri, na kumkuta mkewe akijiandaa kwenda kazini, kilichofuata ni Paaah! Paaah! Paah! Jane chinii, na Laurent kujisalimisha polisi.
hai-make sense, kwa mtu anaesubiria kifo, kuua mke kwasababu ya mali...
 
Yaan concept ya mtu anaumwa huyu awaze kubadilisha majina ya umiliki badala wafocus na ugonjwa haiingii akilini !
Kama wangekua na maelewano mazuri before mume anawajua familia yake vizuri wangekaa wakayajenga !
Kuna story bado inafichwa !
sometimes ni bora ikaendelea kufichwa ,maana ikifichuka, mnaweza mfukua marehemu na kumpa viboko vingi,...
 
Kijana amekosea sana. Kuna mambo sio rahisi sana kuyarudisha nyuma. Hata kama anachangamoto gani, kuua ina maana amevuruga familia yake mazima.

Sidhani kama amefanya uamuzi sahihi...maghorofa yataachwa nyuma yetu siku moja.
Sasa hapo watoto itategemea huruma ya roho mtakatifu maana amewaulia mama yao.
 
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha huyu dada [Jane Urassa] alinitafuta sana, alifika ofisini mara kadhaa kwa lengo la kuonana na mimi bila mafanikio...

... lakini nilimuahidi tungeweza kuonana Ijumaa. Kwa bahati mbaya, sikuwahi hata kuonana nae japo alinipigia simu akiamini ningeweza kumsaidia" Ni andiko la wakili Saduni Isaack akizungumzia kifo cha Mwanamke aliyefariki, ikidaiwa ni baada ya kupigwa risasi na mumewe, katika eneo la Bunju A jijini Dar es Salaam, alfajiri ya kuamkia Oktoba 01, 2026.

Ikumbukwe kuwa alipoulizwa kuhusu tukio hilo mwenyekiti wa shina la mtaa wa Mkoani, aitwae Lucia Shirima, amesema kuwa "nahisi kuna mgogoro wa kubadilisha hati, na kuna barua [za Kweka, kutoka kwa mkewe] zilikuwa zinaletwa nyumbani za kuitwa ustawi wa jamii"
Mimi nitaanza kuamini humu JF wanaomiliki nyumba zenye hati ni wachache sana.

Hakuna swala gumu Tanzania kama kubadili hati au hata hati yako mwenyewe uliyopoteza unataka hati mpya mziki wake si wa kitoto mpaka kwa Kamishna wa ardhi.

Mimi binafsi kuna nyumba mpaka leo nimeachana na habari ya hati bado inasoma mmiliki wa wa kwanza wa kiwanja twna alipata offer na ninayo mimi.

Mpaka akili yangu itulie ndio nifuatiliw hati mziki wake siyo wa kitoto.

Sasa nashangaa eti mwanamke abadirishe tu hati anaanzaje?

Tuletewe hadithi nyingine siyo hii haingii masikioni mwa watu wenye akili.
 
Back
Top Bottom