Inasemekana.
Huyu mwanaume alikua ana uchumi mzuri, na kazi nzuri, pia kwao wako vizuri, ndipo akamuoa huyu mwanamke, wameishi na kuzaa watoto, kumbe mwanamke alikua na uwanja alinunua kabla ya kukutana na huyu mwanaume, ndipo akamuambia mumuwe wajenge nyumba ktk kiwanja hicho. Ila pesa na gharama zote za ujenzi wa nyumba ni za mwanaume.
Sasa hivi karibuni mume anaumwa kansa ya utumbo, na ameambiwa hawezi kupona, asubiri kifo tu, sasa mwanamke baada ya kujua mume muda wowote anang'ata shuka, ndipo kaanza harakati za kutaka nyumba hiyo iwe kwa jina lake na watoto pekee, ilifikia hali mbaya ya kutoelewana, ilibidi mwanaume aende kwao moshi akapumzike, na wakati huo huo mwanamke hakuwepo hapo nyumbani, mke akiporudi, majirani wakatuma taarifa kwa mume kuwa mkewe karudi. Bwana akatoa huko moshi usiku kwa usiku na kuwasili home bunju alfajiri, na kumkuta mkewe akijiandaa kwenda kazini, kilichofuata ni Paaah! Paaah! Paah! Jane chinii, na Laurent kujisalimisha polisi.