hai-make sense, kwa mtu anaesubiria kifo, kuua mke kwasababu ya mali...Inasemekana.
Huyu mwanaume alikua ana uchumi mzuri, na kazi nzuri, pia kwao wako vizuri, ndipo akamuoa huyu mwanamke, wameishi na kuzaa watoto, kumbe mwanamke alikua na uwanja alinunua kabla ya kukutana na huyu mwanaume, ndipo akamuambia mumuwe wajenge nyumba ktk kiwanja hicho. Ila pesa na gharama zote za ujenzi wa nyumba ni za mwanaume.
Sasa hivi karibuni mume anaumwa kansa ya utumbo, na ameambiwa hawezi kupona, asubiri kifo tu, sasa mwanamke baada ya kujua mume muda wowote anang'ata shuka, ndipo kaanza harakati za kutaka nyumba hiyo iwe kwa jina lake na watoto pekee, ilifikia hali mbaya ya kutoelewana, ilibidi mwanaume aende kwao moshi akapumzike, na wakati huo huo mwanamke hakuwepo hapo nyumbani, mke akiporudi, majirani wakatuma taarifa kwa mume kuwa mkewe karudi. Bwana akatoa huko moshi usiku kwa usiku na kuwasili home bunju alfajiri, na kumkuta mkewe akijiandaa kwenda kazini, kilichofuata ni Paaah! Paaah! Paah! Jane chinii, na Laurent kujisalimisha polisi.
sometimes ni bora ikaendelea kufichwa ,maana ikifichuka, mnaweza mfukua marehemu na kumpa viboko vingi,...Yaan concept ya mtu anaumwa huyu awaze kubadilisha majina ya umiliki badala wafocus na ugonjwa haiingii akilini !
Kama wangekua na maelewano mazuri before mume anawajua familia yake vizuri wangekaa wakayajenga !
Kuna story bado inafichwa !
Sasa hapo watoto itategemea huruma ya roho mtakatifu maana amewaulia mama yao.Kijana amekosea sana. Kuna mambo sio rahisi sana kuyarudisha nyuma. Hata kama anachangamoto gani, kuua ina maana amevuruga familia yake mazima.
Sidhani kama amefanya uamuzi sahihi...maghorofa yataachwa nyuma yetu siku moja.
Hii kesi ngumu sana.Sasa hapo watoto itategemea huruma ya roho mtakatifu maana amewaulia mama yao.
Mimi nitaanza kuamini humu JF wanaomiliki nyumba zenye hati ni wachache sana."Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha huyu dada [Jane Urassa] alinitafuta sana, alifika ofisini mara kadhaa kwa lengo la kuonana na mimi bila mafanikio...
... lakini nilimuahidi tungeweza kuonana Ijumaa. Kwa bahati mbaya, sikuwahi hata kuonana nae japo alinipigia simu akiamini ningeweza kumsaidia" Ni andiko la wakili Saduni Isaack akizungumzia kifo cha Mwanamke aliyefariki, ikidaiwa ni baada ya kupigwa risasi na mumewe, katika eneo la Bunju A jijini Dar es Salaam, alfajiri ya kuamkia Oktoba 01, 2026.
Ikumbukwe kuwa alipoulizwa kuhusu tukio hilo mwenyekiti wa shina la mtaa wa Mkoani, aitwae Lucia Shirima, amesema kuwa "nahisi kuna mgogoro wa kubadilisha hati, na kuna barua [za Kweka, kutoka kwa mkewe] zilikuwa zinaletwa nyumbani za kuitwa ustawi wa jamii"
Watu wanauana jamani duhh!!