Huyu mwanamke ana tatizo gani?

Huyu mwanamke ana tatizo gani?

Kwani tatizo ni nini? Mali umemwandika mtoto sasa shida ipo wapi?
 
Binafsi nimezaa na mwanamke mmoja mbaye ameajiliwa na Jeshi moja wapo miongoni mwa majeshi hapa nchini. Huyu mwanake amekuwa na nyodo sana kutokana na kazi yake anayoifanya!

Huyu mwanamke anaijua nyumba yangu hapa Dar es salaam pamoja na mali kadhaa zinazoonekana hapa nyumbani zikiwemo gari zangu 2!

Kwa akili yake alikuwa (ga) anadhani hizo zinazoonekana ndizo mali zangu pekee; Mimi na yeye tulikosana kwasababu za kijinga sana, kwakuwa wakati tumekosana alikuwa mjamzito! Nilisubiri akajifungua salama na baada ya kujifungua kabla hajarudi kazini kila mwezi nilikuwa namtumia Tsh 1.5 M ili imsaidie yeye pamoja na mwanangu!.

Kiukweli baada ya kuwa namtumia hii hela ni kama alichanganyikiwa na alidhani mimi nafanya kwa ajili yake kumbe nilikuwa nafanya kwa ajili ya mwanangu!

kufupisha stori!

Mali zangu zote nimemuandika mwanangu, sababu ya kufanya hivyo ni historia mbaya ya wanawake niliyonayo kichwani mwangu!

Baada ya kumwambia kila kitu kuhusu mali zangu nimemuandika mwanangu, hapo ndipo ugomvi umeanza rasmi!

Kumbuka huyu mwanamke tayari anaye mshikaji wake ila anataka kuniona mimi zuzu!
Unamtumia 1.5 million kila mwezi kwaajili ya mtoto?!
 
Kwahiyo umezaa na mke wa mtu Braza??? Afu ukawa unamuhonga 1.5million ili azuzuke.? Braza inamaana hujui kuwa pesa hainunui upendo.???
Mkuu huyu mwanamke ni askari (Trafic) pale Karatu,na yeye ndiye alishoboka baada ya kuona matanuzi yangu!

Kama ilivyo kawaida kwa wanawake wote,nilimuuliza kama ameolewa eidha na Askari mwenzie au Raia wa kawaida na akakataa kabisa kwamba hajaolewa na hana mtu!,Hivyo mtu mzima nikajiweka kwake takribani miaka 2,ndipo dogo akapatikana,lakini akiwa na mimba tulikosana na ndipo sasa nashangaa hivi sasa ana mtu!
 
Unamtumia 1.5 million kila mwezi kwaajili ya mtoto?!
Yes,kwa ajili ya mtoto!

Akili ya kawaida najua ni kwaajili ya mtoto lakini najua mtoto hawezi tumia hela yote hiyo,nilitaka aone mwanangu ni wathamani kiasi gani!

Hiyo ilikuwa kipindi mwanangu akiwa mdogo but now namtumia laki 5 kila mwezi kwa ajili ya mahitaji ya mtoto,ingawaje amepanga kunipeleka mahakamani ili nitoe zaidi kwasababu anaelewa kipato changu ni zaidi ya hicho ninachotuma
 
Sijui kwanini nashindwa kuamini hii stori kama ni ya kweli
Tafuta pesa mdogo wangu,mbona haya mambo ya kawaida tu!

Mwenzio nikiwa nina miaka 25 tayari nilikuwa nimenunua eneo la Ujenzi hapo Salasala kwa gharama si chini ya milioni 100

Nyumba yangu ina thamani isiyopungua Tsh 250 Milioni,achana na ya pale Buswelu mkoani Mwanza ambayo thamani yake pamoja na uwanja ni Tsh 170 Milioni!.

Pale Kisongo mkoani Arusha pia nina eneo kubwa lakini bado sijajenga,hili nataka nijenge hoteli,eneo hili nikiachiwa na mzee wangu!

Huwa nikiona Vijana hapa JF mmekalia mipasho nabaki nawashangaa kwasababu mnapoteza muda tu,kama wewe na familia yenu hamna uwezo wa kuhudumia Tsh 1.5 Milioni kwa mwezi usidhani ni watanzania wote tunakosa hiyo hela,hiyo hela kwangu ni ndogo sana!
 
Kwani mlifunga ndoa? Kama hapana huna haja ya kustress na umesema ana mtu mwingine mwambie apambane na hali
Nishamchana makavu mkuu lakini naona kama anataka kuniletea kiwingu!

Sasa hivi kasema mtoto atasomea kwake kwakuwa anao uwezo wa kumlea,hivyo mimi niwe natuma tu hela!

Hilo kwangu si tatizo,tatizo ni yeye kutaka kung'ang'ania mali za mtoto wangu ambazo nimeandika majina yake!
 
We mu ignore tu fanya kutimiza majukumu kwa mtoto. Usijichanganye kumpa attention atakupoteza, women are ambassadors of the devil
 
Tafuta pesa mdogo wangu,mbona haya mambo ya kawaida tu!

Mwenzio nikiwa nina miaka 25 tayari nilikuwa nimenunua eneo la Ujenzi hapo Salasala kwa gharama si chini ya milioni 100

Nyumba yangu ina thamani isiyopungua Tsh 250 Milioni,achana na ya pale Buswelu mkoani Mwanza ambayo thamani yake pamoja na uwanja ni Tsh 170 Milioni!.

Pale Kisongo mkoani Arusha pia nina eneo kubwa lakini bado sijajenga,hili nataka nijenge hoteli,eneo hili nikiachiwa na mzee wangu!

Huwa nikiona Vijana hapa JF mmekalia mipasho nabaki nawashangaa kwasababu mnapoteza muda tu,kama wewe na familia yenu hamna uwezo wa kuhudumia Tsh 1.5 Milioni kwa mwezi usidhani ni watanzania wote tunakosa hiyo hela,hiyo hela kwangu ni ndogo sana!
Ukiwa na assets zote hizi hakuna mwanamke wa kukuletea dharau wala jeuri yoyote mayb awe anazaidi ya hizo ila ushasema ni traffic hawa njaa kali. Mkuu hapa unatupanga haiwezekani.
 
Back
Top Bottom