Huyu mwanamke ni kweli hapendi kutumiwa pesa au ni janjajanja zake?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Wakuu kuna manzi mmoja anafanya kazi kwenye duka karibu na langu nimemzimika ile laana. Uzuri wa huyu manzi ni ngumu kuuelezea kwa lugha za kibinadamu. Wanawake wote duniani wakichanga uzuri ndo watafikia robo ya uzuri wa huyu manzi.

Huwa naenda dukani kwao kupata huduma za kifedha na nikafanikiwa kujenga mazoea hadi kubadilishana namba za simu. Sasa last week aliniomba nimnunulie lunch nami bila kusita nikatekeza kama Tsh 15,000/= kwa ajili ya lunch. Jana kwa raha zangu nikamtumia mpunga mida ya lunch akapate msosi ila jibu lake lilinishangaza sana. Alisema anashukuru ila tafadhali nisiwe namtumia pesa. Kwa upande wangu nimejiuliza kama kweli hapendi kutumiwa hela au ni kujifanya mkristo kuliko kristo mwenyewe?
 
Atakuwa na jamaa na sio mwepesi wa kufuta meseji!
 
MamaSamia2025 sasa nimeyathibitisha maneno ya MangeKimambi kwamba wewe ni msagaji.
 
Mkuu maelezo mazuri sana, ila kusifia mwanamke kupitiliza namna hiyo ni janga jingine la kitaifa hilo.

Uzuri wa mwanamke upo machoni pa mdau bhana, kila mwanaume humuona hivyo mwanamke anayemdatisha roho yake.

Kusifia kulikopitiliza namna hiyo ni kujiweka rehani kwa kupigwa tukio kiurahisi, maana si unakuwa hauna maamuzi ya kutafakari tena?

Wee ona hadi unapigwa marufuku mazoea ya kutuma tuma pesa, mwanamke kishagundua kuwa ushadata, sasa hapo anakulia timing ya demand ya jambo kubwa.
Kama haujamjengea hawara wewe, sijui!

Zama kwenye mapenzi utakavyo lakini zamia kwa akili na tahadhari kubwa.
 
Mkuu nimekuelewa vema sana. Naahidi kuiacha hii tabia ya kusifia manzi hadi pale ulazima wa kufanya hivyo utakapojitokeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…