Huyu mwanamke ni mzuri kama malaika, halafu mlokole

Huyu mwanamke ni mzuri kama malaika, halafu mlokole

Ndipo yatakapotimia yaliyotabiriwa [emoji16] umeyasema kilokole, umeokoka? Unampenda Yesu?
Yaliyotabiriwa na Mwana yule ajae 😅😅

Lakini Wasijekusahau kutumia zana za kilimo.

😀😀😄sijaokoka ndugu yangu.maisha ya walokole yamejaa unafiki sana.mpende jirani yako kama nafsi yako..hii amri ni ngumu sana kwao.

😄mimi ni mdhambi sanaaa…lakini ninaamini Mungu yupo.ninaweza nisiende kanisani hata mwaka mzima lakini karibu kila siku ninamgusa Mungu Kwa namna ya kipekee kabisa na Mungu anajidhihirisha maishani mwangu.yapo mengi ya kumtukuza nayo lakini mimi si mlokole.

Again…mimi ni mdhambi kishenzi 😄
 
Dooh! Hivyo Mtani mpaka leo bado ulikuwa unatafuta. Lol
 
Sijawahi wasikia Kwanza hata Leta picha zao na mm nikupe picha moja useme Nani mzuri
images.jpeg-1.jpg

Sijasema mimi ila ni world records
 
View attachment 2463213
Wakati wa kufunga shule nilienda kumchukua kijana wangu shule moja ipo Kahama. Katika kusubiri maelekezo nikaona dada mmoja akiwa amekaa peke yake huku akichezea simu. Moyo ulilipuka sana baada ya macho yetu kugongana.

Nikawa kama nimepigwa shoti ya umeme. Niliona ni kama nimekutana na malaika aliyeshuka toka mbinguni. Nikatamani kumsogelea yule mrembo lakini nikawa na shaka kama niko presentable kwake?

Nikajivuta na kusogea karibu yake. Nikakoki sauti yenye mvuto na kumsalimia kikakamavu. Tukapiga stori mbili tatu za kuisifia shule yetu na hatimaye akanitaka nivute kiti tukae pale kubadilishana mawazo. Akajitambulisha anaitwa M (ufupisho) na anaishi kanda ya ziwa.

M ni mwanamke mzuri wakuu, fikiria naamka muda huu kuandika kuhusu uzuri wake. Licha ya kuvaa mavazi yenye stara, hiyo haikuwa sababu ya kuficha uzuri wa asili mwanadada huyu. Kwa umri wangu mpaka sasa huyu ni mwanamke mzuri zaidi ukilinganisha na wanawake wote duniani. Licha ya usemi unaosema uzuri upo machoni kwa mtu, lakini ukweli utabaki palepale M ni mzuri kiasi cha kusisimua.

Wengi tumekuwa na fikra kuwa pengine Angelina Jolie na Aishwarya Rai, ndiyo wanawake wazuri duniani lakini hapa hawaingii hata nusu. Hiyo
imesababishwa na umaarufu tu walionao walimbwende hao.

Ni mwanamke mrefu kiasi, maji ya kunde wa kung'aa kama kamwagiwa chocolate, ana mguu, ana kifua, ana macho ya kurembua, nyuma kafungasha,kiuno kimekatika. Mbaya zaidi anajiremba, nilimnusa kajipulizia utuli wa kuvutia sana. Nilijiridhisha huyu mwanamke hana kasoro kwa asilimia 90. 10 naziacha kwa viungo vya ndani.

Mara nyingi nilimtazama kwa macho ya kushangaa hata yeye akagundua. Nikataka kumjua zaidi, ananiambia yeye ana mtoto mmoja aliyemfuata pale, ni mwajiriwa lakini pia ameokoka anampenda Yesu. Baadae stori zake zikawa ni shuhuda mbalimbali za mambo ambayo Yesu amemtendea. Hakika nilivutiwa sana na M kiasi cha kuona nimewahi sana kuoa.

M amekuwa rafiki yangu,hakuna siku anaacha kunijulia hali. Nikimpotezea hulazimika kunipigia simu akilalamika kuwa kimya.

Kwa hiyo najiona kama mtu mwenye cheo. Cheo cha rafiki wa mwanamke mzuri kuliko wote duniani. Mzuri wa sura na yupo karibu na Mungu.
Akisha kutenda ndo utajua ni malaika au laaah
Enyiwei usiache kuleta mrejesho ukishapigwa na kitu kizito
 
Ni mzuri zaidi ya CEO mstaafu wa timu yetu pendwa?
 
Tusipoteze muda em turushiane asali hiyo.

Pm iko wazi, acha namba zake pale
 
Back
Top Bottom