Halafu nyie vijana wa kileo ndomaana mnaitwa kwa majina mengi!
Umefungua uzi na takribani 90% ya waliokuchangia, mnafanana mawazo pamoja na upeo wenu wa kuchukua maamuzi!
Unamchukua mwanamke hawara kwa ajili ya kustareheshana, baadaye anaipindua meza kwa nia ovu anakuwa mke!
Halafu kwa mwaka mmoja ulioishi naye unamuona kabisa kuwa hamuendani na hakufai, lakini umeshindwa kupata sababu ya kumuacha!
Hili jambo linawezekana kweli?
Mkuu una haiba ya kilokole kichungaji chungaji nini?
Mwanamke asiye mke wako, namaanisha msiyefunga naye ndoa, hana haki zozote anazozistahili kutoka kwako na pia hauwezi kuumiza sana nafsi pamoja na akili zako kutafuta njia namna ya kumuondoa.
Sababu uliyoijenga mwanzo kumweleza kuwa una mzazi mwenzako, hiyo ticket ilitosha kabisa kumuondoa bila ya kutafuta vijisababu vingine vya kufikirika.
Lakini nadhani mkuu kuna kiunganishi flani unakiwaza kuwa ukimtema kitakuuma sana, hakuna kingine.
Mtu unapewa papa unaila huku ukitoa machozi ya furaha, wadhani ni vyepesi kuzindukana na kuipotezea?
Tuwe wakweli bhana, huyo mwanamke bado unampenda, vinginevyo ni rahisi sana kumuondoa kwenye himaya yako mwanamke ambaye si mke wako, bila ya kusaka mbinu za ziada.