Huyu mzazi wangu Anakosa msaada Kwa sababu ya usanii wa kipuuzi

Hakuna kitu inakata kama kuombwa hela kila mara bila sababu ya msingi hata utume vipi atakuja na sababu tu.

Kuna shangazi yangu asee inafikia kipindi nawaza kumchapa block kabsa.
Yeye kila baada ya siku 2 anapiga simu kutaka hela. Nikaja kufanya uchunguzi ni anafanya hvyo kwa familia yetu nzima mme na mke kila mmoja anapigiwa simu.... wenzangu washaacha kupokea simu zake.....
Kinachokera ana watoto 13 na almost wote wanafanya kazi halafu anapigia simu watoto wa mdogo wake wampe hela mara anaumwa! Mara atumiwe hela ya palizi mara hiki mara kile.

Huwa najiuliza watoto wake ina maana hawamjali maza yao?????
 
Huyo ni mzazi wako, mambo ya ndani humalizwa ndani, sio mitandaoni. Yabebe madhaifu yake, ndio mzazi wako.

Shukuru tu mzazi wako sio mchawi.
umeongea bonge la neno... wazazi wengi wa kiafrika ni wachawi sana. wanawaharibu wenyewe watoto wao.. tena ashukuru sana.
 
Huyo ni mzazi wako, mambo ya ndani humalizwa ndani, sio mitandaoni. Yabebe madhaifu yake, ndio mzazi wako.

Shukuru tu mzazi wako sio mchawi.

Unaongea kwa sababu hutaki kuvaa kiatu chake, Mkuu hiyo hali sikia kwa wenzio kuna muda mtu unashindwa kuweka akiba au kufanya mambo yako kwa sababu ya tabia kama hiyo ya mzazi kujiendekeza na anatumia udhahifu huo wa kuwa yeye ni mzazi wako kuku-manipulate
 
Sio kwa ubaya ila mngemuuliza pesa anapeleka wapi

Kuna wazazi wengine wanawekeza kwaajili yenu unaweza shangaa hela anatunza kwaajili ya kununua mashamba au kujenga
Kwa haraka haraka tu huyo mzazi ni mwanaume ana videmu vya 2000 vinamchuna
 
Mkuu, Mimi nimeshuhudia zaidi ya hayo. Unaweza kulalamika kwa kukosa pesa ya kununua viatu, kumbe kuna wengine wana pesa, na hawana miguu.

Wazazi wa namna hiyo wanavumilika, na wanarekebishika, kama walivyofanya kwetu.
 
wakati unasoma uliwahi kumwambia mzazi wako huta fanya mtihani bila hela ya hydrojen apo mzazi hajui hata ni nn ulichomwambia akauza vi mbuzi vyake akakutumia na ukajiona mjanja haya tulia Kijana dawa ikuingie saiv ni wakati wake Bado ajakwambia akafanye chek up ya tez dume bili 150000 na ww uez kumwangalia mzee uko uvungun itabid uitoe tu 😳
 
Kumbe tuko wengi aisee hata mimi ndo hivo mzazi anaomba hela kama anakudai lakini ndo mzazi aisee no namna tutafanyaje ndugu yangu.
 
Sidhani Kama huyu alijitoa Kwa Lolote kwenye kusoma Kwangu..
 
huyu mukimfuatilia vizuri,si ajabu akawa mdokozi au mwizi mwizi,....inakera sana kuwa na mwanafamilia mwenye vibweka vibweka vya kishenzi,.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…