Huyu ndege analindwa sana hapa jijini Mwanza. Kama wewe ni mgeni hapa chukua tahadhari

Ukanda wote wa kuzunguka ziwa Victoria yapo yanakula sana samaki, wakati tukiwa wadogo tulikuwa tunayaita bwana afya,
 
Alindwe kwa sababu ipi, maana ni ndege anayekula takataka na hakuna anayehangaika naye.......
 
Hao ndege wanaitwa ndege joni, au bwana afya.

Ukiwakuta wanachofanya sehemu za machinjio, utawakubali kuwa kweli wanastahili kuitwa ma bwana afya!

Masalia ya ngozi, mifupa, singa za mikia ya ng'ombe, vinyesi nk nk vinamezwa vizima vizima bila kuchenjuliwa!

Nasikia kwa raia wa Kichina wao ni mboga!

Ndege hao wameenea kila kona ya nchi hii na E Africa kwa ujumla popote palipo ama penye dalili za upatikanaji wa mizoga na machinjio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…