Huyu ndiye daktari aliyejichoma sindano ya UKIMWI ili kuthibitisha kuwa UKIMWI ni uongo!

Status
Not open for further replies.
Nadhani upo kwa ajili kupotosha ukweli kuhusu HIV ili watanzania waache ARVs na kuongezeke vifo kwa watanzania.....Kwavile tupo JF na hizi fake ID tungeweza kuweka mjadala wa ana kwa ana.

Unachanganya sana watu hapa kuhusu HIV na vipimo pamoja na ARVs sielewi lengo lako ni nini....mara useme HIV hakuna hiyo ni fake mara useme mtu yoyote akipimwa anaweza kuwa positive kwa HIV wakati hana kisa ni vipimo vimewekwa hivyo.Mara mtoto anaweza kuzaliwa HIV positive na mama ambaye ni HIV negative mimi kiukweli hata sikuelewi kabisa unachosema kuhusu mambo mengi ya HIV zaidi ya kuwavuruga watanzania wasiokuwa na elimu ya sayansi hasa hasa biology na medicine.
 
Sasa mkuu huyo retro_virus akiingia mwilini anakua na madhara gani? Kma mwili utashindwa kuzalisha antibodies za kupambana nae?
 
Kama unatumia line ya voda nenda kwa mawakala unawapa 10,000 uunganishwe na uni offer bandle zao zinaeleweka na mtandao wao uko poua kwa baazi ya maeneo!!
Dah.... hii huduma bado ipo?
 


Mkuu Nimekufuatilia katika kujenga hoja zako lakini nimepatwa na ukakasi kidogo kwaa namna unavyozielezea.

Unaposema "HIV/AIDS is a mindset disease na haupo" sijui unazungumzia nini kwa kweli. Huu ugonjwa kwa nilivyosoma na kuelewa umeanza miaka ya 1983 kwa hapa Bongo. Kipindi hicho Watanzania walijikuta katika vita kubwa na adui ambaye tokea dakika za awali walionekana kumshindwa na kuwapiga kwa huzuni na majonzi kwani ndugu, jamaa na rafiki wengi tulishuhudia wakipukutika mithili ya majani kipindi cha kiangazi.

Sana zaidi Gonjwa hili lilionyesha umahiri wake kwa namna lilivyowatesa wahanga kwa kuugua vibaya mno. Tulishuhudia jinsi ndugu zetu walivyokonda na kubaki kama miti mikavu huku nywele zao zikiyeyuka vichwani mwao. Madonda makubwa yaliyoacha majeraha yasiosemeka yalitosha kutafsiri maumivu makali ya gonjwa hili.

Vifo mahala mahala vilisikika, vifusi vya udongo viliongezeka na kufanya kumbukumbu isiyosahaulika kwenye nyoyo za watu. Hii ilifanya gonjwa hili likibeba umaarufu na umashuhuri dhidi ya magonjwa mengine kama Malaria kwa kigezo cha mateso makali na suala la tiba.

Namna ugonjwa huu unavyosambazwa ni namna ya kujamiana baina ya mtu mwenye HIV na yule ambaye hana. Pia ilieleezwa kuwa njia nyingine ni kama kubadilisha damu, kuchangia vitu vyenye ncha kali na mwenye hilo ZIMWI. Bila shaka njia hizi ndizo zilionekana ni msingi wa huu ugonjwa jambo ambalo mpaka leo hazijabadilika na hakuna aliyetoa njia Kinzani.

Uvumbuzi wa ARVs ulileta ahueni na tumaini kwa watu wote waishio katika bara giza la watu wenye ngozi zilizoungua. Wengi walizikimbilia na hakika matunda yalionekana kwa baadhi yao hasa wale waliofuata kanuni za msingi za dawa hizo na lishe bora. Kinachpstaajabisha ni kuwa pamoja na wahanga kubwia dawa hizo lakini hazikushinda pomoni, kwani hazikufua dafu zaidi ya kupunguza makali na vitisho vya gonjwa hili hatari. Kifo ndiye aliyekuwa rafiki mzuri katika pambano hili baina ya wahanga na Jitu lisiloonekana naam ndilo HIV.

Chisaye, naomba uniambie ni nini kilichokuwa kinawatesa ndugu zetu kwa ukatili mkubwa ule kabla ya ARVs kuvumbuliwa?

Mbili, Unaposema TB huwa na dalili kama hizo(Ni kweli) lakini kuenezwa kwa HIV na TB mbona ni tofauti? na Mbona kuna uhusiano wa karibu baina ya njia za kupata HIV kupitia kujamiana baina ya mwenye na asiye na HIV?

Je ikiwa mtu ataonyesha dalili za gonjwa ambalo umesema halipo unamshauri nini hasa endapo hata magonjwa mengine ya namna hiyo kama TB, Cancer nayo hayaonekani?

Karibu sana kwa hoja
 
Ttcl 1000 4Gb masaa 24. Speed full 4G. *148*30# 4. Bandika bandua. Kifurushi cha siku yaani masaa 24. Kuanzia saa 6 mpaka 12 asubuhi 1000 unapata 10gb. Muda wa kudownload series na muvi na kuupdate mashine.
Sie huku mikoani hawajatugikia kabisa
 
Nakuelewa sana Chisaye, ila kinachoniuma nina ndugu wengi wanatumia ARV kwa sasa, nifanyeje sasa kuwasaidia au niachane nao tu
Wasije wakaacha, nadhani wakiacha watakufa haraka zaidi kwa magonjwa nyemelezi kwani ARV's zimshadhoofisha sana kinga zao, na ndio kinachowaweka hai, ila pia wanavyoendelea kunywa ni lazima ini, figo na moyo vitakuja kufeli tu, kutumia ARV kwa maoni yangu ni death sentence
 
Ukimwi=Upungufu wa kinga mwilini,ukimwi hauambukizwi kwa jinsi yoyote ile kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine,asilan abadani hauambukizwi.Ukimwi ulikuwapo karne nyingi zilizopita kabla ya hata mwaka 1984 baada ya kutangazwa kwa HIV feki.Ukimwi si jambo la kutisha/kutishia maisha kama utajua sayansi yake kwa maana ya chanzo na jinsi ya kukikabili.Ukimwi unatibika kirahisi sana tena kuliko magonjwa mengi sana na ukimwi hausababishwi na HIV kama tulivyoaminishwa huko nyuma.
Sababu zinazosababisha ukimwi ziko nyingi sana.Katika hizi sababu nyingi HIV hayumo.Na ndio maana kuna wakati nasema sababu kubwa inayosababisha ukimwi ni lifestyle;

1.Malnutrition/utapiamlo,
2.Oxdative stress,
3.Repeated infections
4.Ukosefu wa maji safi ya kunywa
5.Alcohol abuse
6.Frequent use of drugs(eg antibiotics,diclofenac,ARVs,contraceptive pills,chemotherapy,radiations etc),
7.Frequent use of drugs(heroin,cocaine etc )
8.Stress/msongo

Ukimwi humtokea mtu yeyote wakati wowote,na wakati mwingine ukimwi hutoweka wenyewe bila hata mhusika kujijua,endapo tu atabadilisha lifestyle.Kila mtu alishawahi kupata ukimwi wakati fulani wa maisha yake,na ndio maana kuna wakati tunaumwa magonjwa ya kuambukizwa mara kwa mara halafu kuna wakati tunakaa muda mrefu sana bila kuumwa.Mwili hujikinga kwa namna tofauti tofauti kulingana na ugonjwa.Lakini endapo kinga itashuka kidogo basi ni rahisi kushambuliwa na magonjwa ya kuambukizwa au yasiyoambukizwa kama cancer.
Leo hii tumekuwa brainwashed na tunauona ukimwi ni ugonjwa wa kutisha sana tofauti na kipindi cha nyuma,watu watakuona wewe umechanganyikiwa kama utasema kwamba ukimwi hautishi na wala hauambukizwi.Jamaa hawa wamefanikiwa sana kuturubuni akili zetu.Njia wanazozitumia kurubuni akili zetu ni very scientific,kwa akili za watu wengi na hasa sisi weusi si rahisi kung'amua uongo huu wa kisayansi,wametumia sayansi kubwa sana kutudanganya.

Sasa kama una swali kuhusu ukimwi zaidi ya hayo niliyoeleza,kuwa huru,nakukaribisha.
 
Sasa mkuu huyo retro_virus akiingia mwilini anakua na madhara gani? Kma mwili utashindwa kuzalisha antibodies za kupambana nae?
Madhara yake ukitaka kuyajua, tafuta mtu, mpime, ukimkuta ni HIV negative (yaani hana kinga ya huyo Retro-virus), halafu tafuta hicho kirusi cha 'HIV' (hata sijui utakipata wapi) halafu mchome nacho, kisha kabla mwili wake haujatengeneza kinga (antibodies) anza kumnywesha ARV's kwa wingi ili mwili udhoofike ushindwe kupambana nacho, then majibu utakayopata tuletee mrejesho kwa faida ya watz wote.
 
Daah, mbona ameshaeleza vizuri mno kwenye post za nyuma? Fuatilia majibu yake ya nyuma
 
Nimewahi kusoma mada zake saaaaaaaaaaana ila sijawahi kuchangia, the guy anaongea the naked truth ila sababu timeshawekwa kwenye zone mbaya that's why tunampinga ila in reality there's nothing as UKIMWI
Mkuu upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) upo lakini hausababishwi na kirusi HIV, huyo kirusi anasingiziwa. Vijana wa mjini wanasema kaangushiwa jumba bovu.
 
Wewe ndio unajichanganya unashindwa kumuelewa ila ukitulia na ukaruhusu akili yako kumuelewa hutochanganyikiwa kabisa....!
 

Tukienda upande wa pili kwamba 'HIV' hayupo na AIDS haisababishwi na HIV pia na mimi nitakuletea scientific papers nyingi sana,halafu mwisho wa siku tutakuwa tunashindana kutoa scientific papers.Wewe umetoa scientific papers za watu unaowaamini na mimi nitatoa zangu za wale ninaowaamini,mwisho wa siku hata wana JF hawatang'amua chochote.

Hao unaowaamini wewe wameshindwa na wale ninaowaamini mimi kwenye lab experiments(ambazo kwa hapa ni vigumu kuwathibitishia watu maana tutajaza scientific papers tu humu) na real life experince.Yaani kile kinachoonekana kiuhalisia.

Tukienda kwenye body chemistry, hilo mimi sina tatizo na ninyi kwa kuwa hata nikikwambia uniletee electronics photos za hizo cells najua utaniletea kwa kuwa zipo kiuhalisia.Tatizo linakuja kwenye electronics micrographs za purified HIV.Najua hata ufanye vipi huwezi kuniletea hizo na ukileta lazima zitakuwa feki kwa kuwa hata hao unaowaamini walishakubali kwamba wameshindwa ku purify HIV,wewe unajua umuhimu wa purification hivyo sina haja ya kueleza mengi hapa.

Kama wameshindwa ku purify HIV,sasa ile picha ya HIV kwenye vitabu vyenu wameipata wapi?Evidence nzuri hapa ni ile ya matukio tunayoyaona mtaani.Maana hata niki disqualify hizo paper zako bado watu hawataelewa nini kinaendelea.

Robert Gallo na Luc Montaigner hawajawahi ku purify HIV.Hawawezi pia kuthibitisha kwamba HIV anasababisha AIDS.Usifikiri Kary Mullis ameingia uchizi kukataa kwamba HIV hasababishi AIDS wakati kipimo alichogundua cha PCR ndio kinategemewa kwenye haya mambo yenu.

Usifikiri Prof.Peter Duesberg ameingia uchizi kusema kwamba HIV hasababishi AIDS.Robert Gallo na Luc Montaigner wameshindwa kujibu hoja za hawa wachache tu niliowataja hapa,wewe ukiweza kujibu nitakushangaa sana umepata wapi maelezo hayo.Cha msingi ni kujibu hoja za hawa jamaa.Fahamu kwamba na hawa ni madaktari pia tena wenye hadhi ya juu duniani.

Pia fahamu kwamba Peter Duesberg anaijua virology vizuri zaidi ya hao wanaojiita wagunduzi wa HIV kwa maana ndio field yake hasa na ndio maana wanamkimbia hata kwenye open debate,ninyi hamlijui hili na hamuwezi kuambiwa.

Robert Gallo na Luc Montaigner(wagunduzi wa 'HIV') wameshindwa kujibu (kwa usahihi) hoja zifuatazo za Peter Duesberg.Naomba wewe uzijibu kama hutajali.

Nimeongeza neno kwa usahihi kwa kuwa mtu yeyote anaweza kutunga kitu chochote ili watu wamwamini hata kama hakina ukweli wa kisayansi.Hawa kina R.Gallo na L.Montaigner ndio ma father wa kutunga,wanachokisema ukilinganisha na lab experiment viko tofauti kabisa.Sasa jibu hoja hizo hapo chini.

 
Hii itabaki yangu moyoni, ila wazungu ni watu wabaya sana, wanatugeuza mitaji
 
naomba kuuliza mama mjamzito afanyaje anapokutwa baby HIV?
Na amkinge vipi mtoto dhidi ya HIV feki
 
Wewe ndio unajichanganya unashindwa kumuelewa ila ukitulia na ukaruhusu akili yako kumuelewa hutochanganyikiwa kabisa....!
Kwa maelezo yake wala siwezi kumuelewa na wala sitaruhusu akili yangu kuelewa ujinga anaoandika hapa kuhusu UKIMWI na HIV......Nimesoma sayansi tena biology O na A level na pia nimesoma chuo sayansi hicho anachokieleza ni kitu ambacho nadhani anachanganya na imani zingine zinazopingana na masuala mazima ya maendelo ya sayansi na teknolojia ya nchi za magharibi
 
YANI SIKU HIZI HOSPITALINI UNASHAURIWA KWA NGUVU ZOTE KUPIMA UKIMWI ALAFU WANAHAMASISHA UKIGUNDULIKA UNAO UANZE KUTUMIA KINGA.
 
ili twende sawa nijibu maswali yafuatayo...moja) Unigold huwa inapima specific antibody ipi mwilini ? na kwann unigold haijawah kusoma positive kwa mtu mwenye TB,skini diseasws,syphilis,gonnorrhea n.k apart from HIV virus infection...?? what does real unigold detect...?? (mbili) kama HIV hayupo accoeding to you sasa kwann wanapimwa wanakuta HIV specific antibodies zimeraise...?? if you 're real a molecular biotechnologist could you clarify more on that...??
 

Bado mimi nitaendelea kukuheshimu kwa kuwa wewe ni daktari na una uelewa mkubwa kuhusu mambo ya madawa.Hivyo wakati unaongea na mimi inabidi ujue kwamba unaongea na mtu anayekukubali kwenye field yako.Lakini pale ambapo huna uelewa nako sina budi kukujulisha, kwa maana hakuna anayejua vyote.



Hebu tuchukue mfano wa ARVs mojawapo inayoitwa Tenofovir Disoproxil Fumarate(TDF) ambayo inatumika na wagonjwa wengi wa AIDS,najua hapa nimekufikisha nyumbani kwako.
Dawa hii kwenye warning zake inasema "It can cause serious,life-threatening side effects.These include lactic acidosis and severe liver problems."
Najua unajua kwamba kiwango salama cha acid/alkali kwenye damu(yaani pH) ni 7.365,maana yake damu inatakiwa iwe slightly alkaline ili kinga ya mwili iweze kufanya kazi yake vizuri.Chini ya kiwango hicho ni majanga matupu,utakuwa na magonjwa yasiyohesabika na yasiyoisha mpaka unakufa.Najua mpaka hapa huna cha kupinga,labda urekebishe kidogo sana.
Sasa kama acid itajijenga kwenye damu yako,maana yake pH ya damu yako ita drop na kuwa chini ya 7.365.ARVs na specifically hii TDF ndivyo inavyofanya kwenye damu za wale wanaoitumia.TDF inaongeza kiwango cha acid kwenye damu.Acid ni sumu kwenye damu,acid inapokuwa nyingi INI haliwezi kufanya kazi yake inavyotakiwa na ndio maana kwenye dawa hizo severe liver problems imetajwa kama mojawapo ya effects.
Pia najua unajua ya kwamba kama damu ina acid nyingi,hewa ya oxygen inapungua sana hivyo seli za damu zinakosa oxygen ya kutosha kufanya kazi yake,najua unajua nini kinatokea kama seli za damu zitakosa oxygen.Hata wewe mwenye ukikosa oxygen unajua kitakutokea nini.Hapa najua huna hoja ya kupinga pia.

Sasa kutokana na ukweli huo,Je,ARVs hazisababishi mapungufu kwenye kinga?Na kutokana na effects hizo ndio maana magonjwa mengi sana huzaliwa kwa wale ambao wametumia ARVs muda mrefu.Baadhi ya magonjwa hayo ni kama vile;
-Cancer:Ukimpima mgonjwa yeyote wa cancer lazima utakuta damu yake ni acidic(yaani pH yake ni chini ya 7.365)
-Ini
-Figo
-Anaemia
-Heart disease
nk.

Fanya uchunguzi kwa wagonjwa wote waliolazwa mahospitalini,lazima utawakuta na moja/mawili/matatu.... kati ya magonjwa niliyotaja hapo juu.
Kuhusu cancer,usifikiri kama zile NGO za mambo ya HIV/AIDS zilivyoanzisha kitengo maalumu kwa ajili ya cervical cancer kwa wanawake ilikuwa ni coincidence.Hiyo cancer inasababishwa na ARVs,fanya uchunguzi wewe mwenyewe kama una muda.
Hivyo basi,nataka nikwambie kwamba ARVs zinasababisha AIDS,hii sio speculation ndugu yangu,its real.Kama unataka evidence tena kuhusu hizo side effects niambie nitakupa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…