Huyu ndiye Giriki, Dereva aliyetoka na basi Dar saa 12 asubuhi, akaingia Mbeya saa saba mchana

Huyu ndiye Giriki, Dereva aliyetoka na basi Dar saa 12 asubuhi, akaingia Mbeya saa saba mchana

Alafu watu wanasema sauli zinakimbia nachekaga tu
Hao ni watoto hawajui kitu ,wasamehe bure , ati siku hizi na pesa ya kubet wanaweka .
Huyu mwamba tulishawahi toka mnazi mmoja saa saba mchana tujaingia mbeya saa mbili na nusu usiku, na hapo tulisimama iringa kwa dk kadhaa alikwenda kutoa pole kwa almaarufu flani aliyefariki.
 
Mmesahau kuwa barabara pia siku hizi magari yamekuwa ni mengi kuliko hiyo zamani. Pia safety measures ni nyingi kama kuwepo na police wengi, speed bumps n.k

Sasa kama zama hizo anatoka Dar mpaka Mbeya na njiani hapishani na gari hazifiki hata 100 si anatembea atakavyo.
Ukiniambia matuta na safety measures naweza kukuelewa , lakini swala la u bize ,barabara ya mbeya toka miaka hiyo ni barabara bize
Kumbuka barabara hii inalisha boarders mbili busy , kasumulu na Tunduma , na soon itaanza kulisha. Ile ya Sumbawanga..
 
Kuna dereva wa basi la abood alitoka mwanza saa 1 asubuhi akafika morogoro saa 4 asubuh yaani alitumia masaa 4 tu. Ila alikamatwa chalinze
Chai kama chai
JamiiForums-350917146.gif
 
Una uhakika na unachokiongea? Ulishawahi kuona msafara wa viongozi V8 zimeachiana nafasi zinavyopita kama upepo? Ile mara nyingi sana huwa ni 150. Imagine.

Hivi basi inaweza kukimbia zaidi ya magari ya msafara?, ulishawahi kupanda basi safari ndefu? Ikifikaga 120 tu, abiria wanazikimbia siti za nyuma! Basi la abiria likifika 140, abiria wote ndani wanakuwa majeruhi, maana mtagonga sana vichwa hadi mtaumia.

Inawezekana basi mimi naanza kuzeeka, labda nitulie nielekezwe vizuri.. Wewe ni mtu wa pili sasa,

Hivi basi la abiria linaweza kukimbia 160km/hr?
Mabasi ya zamani yalikuwa mechanical injector pump, , ungoverned , zinaweza fungua kupitiliza , Safina bus iliwahi pigwa tochi ikakutwa na speed 168, yan mshale wa speed unapita 120 unarudi hadi kwenye mark ya 10km/h, its called round the clock 10 star.
 
Kiswele ilikuwa ni basi ya songea dar , haikuwahi kwenda mbeya

Mkuu utakuwa una information nusu...

Kiswele, Kwacha, Zainabu, Fresh ya Shamba, Scandinavia...zote hizo zilipiga route ya Dar-Mbeya
 
Mkuu utakuwa una information nusu...

Kiswele, Kwacha, Zainabu, Fresh ya Shamba, Scandinavia...zote hizo zilipiga route ya Dar-Mbeya
Haha inaezekana nimesahau ,ila nature ya matajiri wa mabasi ya Ruvuma , huwa hawatoki nje ya base yao, ukiona basi inakwenda Dar songea , na Dar mbeya , jua tajiri huyo sio wa songea na usually badi hizo hazitadumu songea .
Juma ngalema (kiswele) kama alijaribu kwenda mbeya itakuwa ni kwa kipindi kifupi sana .
Ottawa , super feo , likungu , Ruvuma tours ,wote hao hawakuwahi kuwa na basi za dar mbeya.
 
Nakumbuka mwaka 2002 hadi 2005 nilikuwa napanda Basi za Urafiki, Shabiby na Hood kutokea Dodoma kwenda Mbeya kupitia Morogoro kipindi hicho barabara ya Dodoma Iringa bado haijakamilika.
Nazikumbuka basi za Shabiby zilikuwa TZR 924 na TZR 925.
Ila katika kukimbia Urafiki ilikuwa kiboko. Dodoma Mbeya via Morogoro saa 10 kamili mmeingia.
Hood alikuwa anachelewa kwakuwa lazima apite kwao Morogoro afanye checkup mtafika saa 1 jioni.
Shabiby nae alikuwa anapita Gairo but atleast saa 11:30 jioni mmekuwa mmefika.
 
kwa kuwa tumeamua kupiga story za kuchangamsha kijiwe basi acha na mimi nipige story yangu.

zamani jiji la mbeya lilikuwa mafinga, likaanza kusogea kidogo kidogo na kufika kule liliko sasa.

ndio maana iliwezekana kwa dareva wa bus giriki kuingia mbeya mapema kwa sababu mbeya ya zamani ilikuwa maeneo ya mafinga.
 
Inawezekana basi mimi naanza kuzeeka, labda nitulie nielekezwe vizuri.. Wewe ni mtu wa pili sasa,

Hivi basi la abiria linaweza kukimbia 160km/hr?
Scania kuanzia 81,111....zote kisahani ni 120 au 125km/h lakini huo mshale ukifika mwisho utagundua mwendo unaongezeka sisi tumewahi kuongozana na lucky star mikumi mshale wetu ukiwa 160 bado tulienda sawa.Ila naamini mshale kabla haujafika mwisho speedometer huwa ni accurate.
 
Huyo hakuwa giriki , ila lawama alipata yeye, , Giriki kwanza njia yake kubwa ilikuwa ni Dar Mbeya , Songea alikuwa anaenda mara chache chache
Kuna chuma kiliitwa turbo express songea-mbeya ndio lilikuwa basi la kwanza(sina uhakika)ila lilikuwa na carrier juu haya ma tawaqal aliendesha baadaye.
 
Back
Top Bottom