Huyu ndiye Giriki, Dereva aliyetoka na basi Dar saa 12 asubuhi, akaingia Mbeya saa saba mchana

Huyu ndiye Giriki, Dereva aliyetoka na basi Dar saa 12 asubuhi, akaingia Mbeya saa saba mchana

Nilipanda matema beach injini nyuma Toka kyela saa 12 asubuhi kwenda morogoro nlifiika Moro saa saba mchana huo mwendo haukuwa wa kawaida
 
Ipo ile taqwa iliyokuwa inakwenda kongo
Achana nayo kabisa,tuliyowahi/waliyowahi kupanda mziki
Wake wanaujuaa

Ova
 
Hii kamba, ila kuna dereva mmoja wa Basi la ALLYS alitoka Dar 12 akafika Mwanza 12:45 alivyofika fika tu OCs wa nyegezi stand wa wakati huo mama mmoja bonge kupindukia (afande Groly) na trafiki mmoja Yinga wakampokea na kumsweka sero.Unaambiwa watu walishuka hawaamini wapo Mwanza au Nzega
Nzega au Dodoma?
 
Mmesahau kuwa barabara pia siku hizi magari yamekuwa ni mengi kuliko hiyo zamani. Pia safety measures ni nyingi kama kuwepo na police wengi, speed bumps n.k

Sasa kama zama hizo anatoka Dar mpaka Mbeya na njiani hapishani na gari hazifiki hata 100 si anatembea atakavyo.
Sio hivyo Mkuu, huyo Mwamba (Giriki) alikuwa ni balaa ana overtake upande wa kushoto ukimbania kulia halafu alikuwa anendesha kwa spidi kubwa kiasi kwamba abiria wenye mioyo miepesi waliomba kushuka njiani wapande basi lingine. Mimi binafsi nimepanda sana gari (Tawaqal) alilokuwa anaendesha, kwa nyuma lilikuwa na maandishi yaliyosomeka "Horse Power is the Best Time Will Tell". Vilevile, kulikuwa na mwenzake mmoja anaitwa Lwambo naye alikuwa anamfuatia Giriki kwa vituko. Fundi wao aliitwa Bakari naye alipinda vilevile kama madereva wake.
 
Ndio maana alipofika Mbeya akapigwa pingu na kufunguliwa kesi
Huyo Giriki alikuwa haogopi Traffic hata kidogo. Kwake pingu ilikuwa kawaida sana. Kuna siku alikamatwa Mbeya Stand baada ya kuliondoa bus kwa mbwembwe na kutaka kusababisha ajali. Tulienda na bus Police Central pale Mbeya halafu akawekwa ndani, baada ya nusu saa tukakuta mwamba ameachiwa akashika usukani. Tuliondoka Mbeya saa 3.00 asubuhi, saa 11.00 jioni tupo Dar.
 
Yaani ilikuwa burudani tosha namna alivyokuwa anaondoka pale stand, kuikata kona ya kuelekea Mabatini. Gia zilikuwa zinapigwa na kuhesabika , hadi raha ya SCANIA unaiona
 
Back
Top Bottom