Huyu ndiye Giriki, Dereva aliyetoka na basi Dar saa 12 asubuhi, akaingia Mbeya saa saba mchana

Huyu ndiye Giriki, Dereva aliyetoka na basi Dar saa 12 asubuhi, akaingia Mbeya saa saba mchana

Kuna chuma kiliitwa turbo express songea-mbeya ndio lilikuwa basi la kwanza(sina uhakika)ila lilikuwa na carrier juu haya ma tawaqal aliendesha baadaye.
Ila jamaa hazeeki, maana Turbo Express, Movement Star, Amina Express (Aluta Continua), Kwacha, Kamata, Nyota ni basi za miaka mingi sana, Giriki alikuwepo
 
Ukiniambia matuta na safety measures naweza kukuelewa , lakini swala la u bize ,barabara ya mbeya toka miaka hiyo ni barabara bize
Kumbuka barabara hii inalisha boarders mbili busy , kasumulu na Tunduma , na soon itaanza kulisha. Ile ya Sumbawanga..
Nazungumzia miaka hiyo mkuu sio siku hizi.
 
MKUU samahani mimi nimeendesha basi pamoja na giriki huo muda hapana alifika mbeya mapema sana lakini muda napingana nao, huyo bwana namjua vyema yeye na Alyy Kilaweni marehemu tulikuwa tunajiuliza miyo yao niya model gani maana walikuwa na maajabu sana njiani. Nakuna mwingine Marehemu Selepion nae alikuwa moto sana hao 3 nilikiuwa nawaogopa kwakweli.

wamva nisaidie nani alikua anaendesha mabasi ya Ilangamoto kabla hayajafungiwa miaka ya 97-98?
 
Nakumbuka 2015 nikiwa natoka likizo MUST tulikodi Happy nation ikatufata chuo.. Aisee tuliingia Moro saa 8... Tukapigwa mkono na kuruhusiwa saa 10... Ajabu bado ikawa ndo gari ya 1 kuingia ubungo kutokea MBEYA... Sijawahi panda gari ikiwa speed zaidi ya ile...
 
Hii kamba, ila kuna dereva mmoja wa Basi la ALLYS alitoka Dar 12 akafika Mwanza 12:45 alivyofika fika tu OCs wa nyegezi stand wa wakati huo mama mmoja bonge kupindukia (afande Groly) na trafiki mmoja Yinga wakampokea na kumsweka sero.Unaambiwa watu walishuka hawaamini wapo Mwanza au Nzega

Mwaka gani maana hii story ni kama ya kijiweni? Kama 12 jioni ni sawa ila sio ya sa sita
 
Alikuwa jamaa fulani mweupe hivi, kipindi kile 2010-2012 kufika Mwanza saa 1 kamili jioni ilikuwa kawaida sana au kufika Dar saa 1;30 jioni jamaa alikuwa anaendesha hadi anazipita baadhi ya mabasi yanayotoka Kahama, kuna siku nilipanda siti ya mbele nilijuta kwa ule Mwendo

Saa moja sawa , mdau alivyoweka 12:45 imekaa kama alifika saa 6 kujiuliza singida alipita saa ngapi. Ally’s sport saa 2 kuingia dar ilikua kawaida
 
Ila sasa hivi tunaonewa sana. Dodoma - iringa masaa matano kwa basi? Sio poa kabisa. Dodoma mbeya masaa 10 na zaidi?
 
Back
Top Bottom