Huyu ndiye Giriki, Dereva aliyetoka na basi Dar saa 12 asubuhi, akaingia Mbeya saa saba mchana

Nilipanda matema beach injini nyuma Toka kyela saa 12 asubuhi kwenda morogoro nlifiika Moro saa saba mchana huo mwendo haukuwa wa kawaida
 
Ipo ile taqwa iliyokuwa inakwenda kongo
Achana nayo kabisa,tuliyowahi/waliyowahi kupanda mziki
Wake wanaujuaa

Ova
 
Nzega au Dodoma?
 
Sio hivyo Mkuu, huyo Mwamba (Giriki) alikuwa ni balaa ana overtake upande wa kushoto ukimbania kulia halafu alikuwa anendesha kwa spidi kubwa kiasi kwamba abiria wenye mioyo miepesi waliomba kushuka njiani wapande basi lingine. Mimi binafsi nimepanda sana gari (Tawaqal) alilokuwa anaendesha, kwa nyuma lilikuwa na maandishi yaliyosomeka "Horse Power is the Best Time Will Tell". Vilevile, kulikuwa na mwenzake mmoja anaitwa Lwambo naye alikuwa anamfuatia Giriki kwa vituko. Fundi wao aliitwa Bakari naye alipinda vilevile kama madereva wake.
 
Hilo basi siwezi kupanda kwakweli.
 
Ndio maana alipofika Mbeya akapigwa pingu na kufunguliwa kesi
Huyo Giriki alikuwa haogopi Traffic hata kidogo. Kwake pingu ilikuwa kawaida sana. Kuna siku alikamatwa Mbeya Stand baada ya kuliondoa bus kwa mbwembwe na kutaka kusababisha ajali. Tulienda na bus Police Central pale Mbeya halafu akawekwa ndani, baada ya nusu saa tukakuta mwamba ameachiwa akashika usukani. Tuliondoka Mbeya saa 3.00 asubuhi, saa 11.00 jioni tupo Dar.
 
Kuna dereva wa basi la abood alitoka mwanza saa 1 asubuhi akafika morogoro saa 4 asubuh yaani alitumia masaa 4 tu. Ila alikamatwa chalinze
Aaah mkuu hii haiwezekani yaani kaipangua shinyanga,tabora ,singida,Dodoma ndani ya masaa matatu hii chai mkuuπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
πŸ˜‘πŸ˜‘ Wanaume wana michezo ya hatari sana sijui mkoje!!
 
Yaani ilikuwa burudani tosha namna alivyokuwa anaondoka pale stand, kuikata kona ya kuelekea Mabatini. Gia zilikuwa zinapigwa na kuhesabika , hadi raha ya SCANIA unaiona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…