Huyu ndiye Giriki, Dereva aliyetoka na basi Dar saa 12 asubuhi, akaingia Mbeya saa saba mchana

Huyu ndiye Giriki, Dereva aliyetoka na basi Dar saa 12 asubuhi, akaingia Mbeya saa saba mchana

Nakumbuka mwaka 2002 hadi 2005 nilikuwa napanda Basi za Urafiki, Shabiby na Hood kutokea Dodoma kwenda Mbeya kupitia Morogoro kipindi hicho barabara ya Dodoma Iringa bado haijakamilika.
Nazikumbuka basi za Shabiby zilikuwa TZR 924 na TZR 925.
Ila katika kukimbia Urafiki ilikuwa kiboko. Dodoma Mbeya via Morogoro saa 10 kamili mmeingia.
Hood alikuwa anachelewa kwakuwa lazima apite kwao Morogoro afanye checkup mtafika saa 1 jioni.
Shabiby nae alikuwa anapita Gairo but atleast saa 11:30 jioni mmekuwa mmefika.
Kwenye urafiki babu yangu kabisa mzee chove alidanji sahv kampuni imekufa.
 
Kwaiyo ilikua inakimbia km ngapi Kwa saa?
Stori za kwenye kahawa hizi.
 
Siku hizi magari hayakimbii. Zamani Embakassy lilikuwa ni basi lisilokimbia kabisa, la kupanda wazee na wagonjwa. Likitoka Dar saa 12 asubuhi Mbeya linaingia saa 10.30 jioni sio saa nne usiku
Zainab ya Kyela Nkamu, iliyomimina watu wote uwanja wa ndege pale kwenye kona kabla ya kiwira ile mashine mbio zake balaa .ila giriki ilikua habari ingine.
Na kuna Tyson alikua pia na Tawaqal njia ya Shy-Dar alitubwaga saranda pale tukala vumbi la kutosha ila tukafika poa tu.
 
Sure, huyu ndugu yangu ananiambia 120km/hr ni average, kwamba kuna muda basi litatembea hadi 160km/hr, nimeshangaa. Sikuwahi imagine kama basi la abiria linaweza kukimbia hata 140, let alone 160km/hr.
140 inafika vizuuri kabisa
Michina mingi ni 140.

Kipindi nipo group la whatsapp la RSA kuna basi ya Tawakal ilipigwa tochi 142kph

160[emoji15][emoji15]
 
Zainab ya Kyela Nkamu, iliyomimina watu wote uwanja wa ndege pale kwenye kona kabla ya kiwira ile mashine mbio zake balaa .ila giriki ilikua habari ingine.
Na kuna Tyson alikua pia na Tawaqal njia ya Shy-Dar alitubwaga saranda pale tukala vumbi la kutosha ila tukafika poa tu.
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]mkala vumbi ka kutosha
 
Zamani kulikuwa na magari machache barabarani, mabasi hayakuwa na speed governor (Ving'amuzi), polisi walikuwa wachache barabarani, vibao vya 50 havikuwa vingi kama leo, matuta(speed humps/pumps) yalikuwa maeneo machache
Minimum speed ilikuwa 60 Kph
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]mkala vumbi ka kutosha
Yaah tulikua tumekwama kwamtoro km wiki 2.kurudi huku njia ya manyoni tukaambiwa daraja liko tayari.
Jamaa sijui kammis mkewe unaambiwa mashine ilikua inapigwa Scania ile enzi hizo vumbi tu hadi Dom.
Kuteremka Saranda pale chini mimbio ile katupeleka porini huko ngoma ikalala.
Abiria tukaanza tena kusukuma bus mpk tukaondoka tena.
Hakufa mtu wala kuumia mungu mkubwa.
El ninyo 2000
 
Huyo hakuwa giriki , ila lawama alipata yeye, , Giriki kwanza njia yake kubwa ilikuwa ni Dar Mbeya , Songea alikuwa anaenda mara chache chache
Ilitokeaje mkuu, yaani aliingiaje lawamani ikiwa si yeye aliyesababisha?
 
Ilitokeaje mkuu, yaani aliingiaje lawamani ikiwa si yeye aliyesababisha?
Giriki alikuwa dereva maarufu tu, na hiyo gari iliyosababisha ajali alikuwa anaendesha , ila siku ya ajali ,hakuwa yeye ,alikuwa kijana mmoja deiwaka kutoka Iringa .
Sehemu ilipotokea ajali hadi leo hii ni sehemu hatari, shabiby hakuchuchukua tahadhari hadi anafika eneo la tukio
 
Super Najmunisa pia nimedandia Sgd. Du ilikua imetoka Shy au Mwanza.
Ilikua Nissan Diesel.
Sa 8 tuko kibaha.
Trafik wakaanza na dereva.
Ikabidi sasa ulitakiwa ufike sa moja umewai utakaa ndani mpk sa moja😂😂😂.
Abiria tukakaa tu kwenye Bus mpk jamaa atoke tuendelee na safari
 
Giriki alikuwa dereva maarufu tu, na hiyo gari iliyosababisha ajali alikuwa anaendesha , ila siku ya ajali ,hakuwa yeye ,alikuwa kijana mmoja deiwaka kutoka Iringa .
Sehemu ilipotokea ajali hadi leo hii ni sehemu hatari, shabiby hakuchuchukua tahadhari hadi anafika eneo la tukio
Ok naifahamu sehemu hiyo ilipotokea ajali ni pabaya sana
 
Zamani mabasi yalikua yanakimbia sana. Tumewahi ingia ubungo na Tawaqal ya kyela saa Tisa jioni. Hiyo ilikua 1996
Tumeingia na hekima sa tisa pia ubungo honi inapigwa.
Sijalala siku hiyo ilikua mbio tu mpk tunafika.
 
Back
Top Bottom