Huyu ndiye Muigizaji Brian Deacon, aliyeigiza kama Yesu na anachokifanya kwa sasa katika Maisha

Huyu ndiye Muigizaji Brian Deacon, aliyeigiza kama Yesu na anachokifanya kwa sasa katika Maisha

kwahiyo kuna uwezekano mkubwa kwamba dini hetu inatupotosha?
Mkuu kuchangia vitu kinafiki ni sawa na kujiuliza maswali ya kijinga au kupanga mipango ya kijinga,utavuna ujinga. Appearance ya mtu inaweza danganya sana watu. Kuna wazungu kibao ni weusi .Kuna weusi kibao wapo karibu na wazungu kuliko waafrica. DNA ndio zinasema . Kuweka mijadala ya kipuuzi na maigizo ili kujaribu fanya dini ingine kuwa ni upotoshaji ni kujidanganya.Haifanyi dini yako kuwa sahihi,ila ni kufanya wote msiwe sahihi kwa waliokusikiliza n akupotoka..
 
kanisani ss tumejawa na uzuzu...et tunamuabudu picha ya huyu jamaaa.......upuuz mtupu
Kanisa gani unasali wewe? Kwa taarifa yako makanisa sio yote yana picture, na yenye picture wana maelezo yao kwanini wanazo na kuziheshimu. Hembu tueleze kwanini kanisani kwako zipo? Mnajidanganya sana nyie ,ndio walezi wa ccm.Kutwa mpo ktk mitandao mkijifanya pia kuwa nyie ni chadema.Ili muiongelee chadema kiupotoshaji km mnavyojifanya nanyi ni wakristu ili mpotoshe.
 
Ama kweli tulikua enzi za zama za ujinga wakristo zindukeni.
ISLAM IS A REAL RELIGION IN THE WORLD WIDE.
Google HOW CATHOLIC CREATED ISLAM? Ukiwa na akili za mwizi kumtaja mwizi mwingine akidhani kwamba yeye kwa vile hajatajwa basi anakuwa sio mwizi.Utakuwa ktk njia mbaya km ngamia wa kafara.
 
Ama kweli tulikua enzi za zama za ujinga wakristo zindukeni.
ISLAM IS A REAL RELIGION IN THE WORLD WIDE.

Google HOW CATHOLIC CREATED ISLAM? Ukiwa na akili za mwizi kumtaja mwizi mwingine akidhani kwamba yeye kwa vile hajatajwa basi anakuwa sio mwizi.Utakuwa ktk njia mbaya km ngamia wa kafara.
 
We don't talk or discuss about the real religion but we talk and discuss the glory of God. religions are just institutions created by human being with special purposes including yours
If you believe in God you already have a religion my Friend.
 
Google HOW CATHOLIC CREATED ISLAM? Ukiwa na akili za mwizi kumtaja mwizi mwingine akidhani kwamba yeye kwa vile hajatajwa basi anakuwa sio mwizi.Utakuwa ktk njia mbaya km ngamia wa kafara.
Hata mimi naweza kuandika jambo la uongo na nikakwambia u-google.
 
Ila jaman nyie watu ni wagum kuelewa sasa hapa mambo ya YESU je ccm na chedema cjui yamekujaje mm na shangazwa[emoji17]
 
1Wakorinto 10
14 Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu. 15 Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo.
 
1Wakorinto 10
14 Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu. 15 Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo.
wewe si umesoma na kuelewa.Basi katimize uliloelewa.Kama umeelewa mengi na unayaamini kutoka kwenye Biblia basi enenda ukamfuate Yesu kadiri ya uwezo wako, ukimshuhudia kadiri ya uwezo wako.Ila ikiwa huamini hiyo Biblia unayotaka ikusaidie kufikia matamanio na uongo wako, ikiwa hata huyo Yesu huna imani nae wala humfuati.Ni bora ukashika uongo wako kuliko kuomba msaada wake katika huo uongo.
 
If you believe in God you already have a religion my Friend.
Hata usipoamini uwepo wa Mungu pia ni dini. believing in ABSENCE or PRESENCE is still a belief. Na religion has nothing to do with bileiving in God.Hapo ndipo nyie mjifanyao wajuaji msipojua.Mnakimbilia kukomaa sijui dini gani ni ya kweli na gani ni ya uongo.Dini na nabii ni kama Punda dini ndio inatakiwa kuokoa watu,kutetea watu.Ila watu kutetea dini,au kumtetea nabii ni kama watu ndio manabii wa nabii, na dini ya hiyo dini.
 
Hata mimi naweza kuandika jambo la uongo na nikakwambia u-google.
Unaweza na umeshaandika mwingi tuu.Unadhani mapenzi yako ktk unachooamini una uwezo tena wa kuona uhasilia wa huko ulipo n auhasilia kule usipo. Kule ulipo upo ktk nia ya kukulinda, n akule usipo upo ktk nia ya kukubomoa.


Mimi najua mapungufu yake ndio maana sikuwahi litumia km defence,ila napenda tuu kukufundisha kitu hapa. HEMBU JILINDE HAPA KTK HILO .KAMA KWELI UNAO USHAHIDI KWAMBA UISLAM SIO KAMRADI KA VATICAN DHIDI YA WAYAHUDI?USIPOWEZA JITETEA HAPA NI WAZI HATA HIYO DINI UNAYOJIFANYA UPO TAYARI KUFA NA KUUA WENGINE HUJUI ULICHOFUATA.

Kwa taarifa UKRISTU NI ZAIDI YA MAISHA YA WAKRISTU. Wenye nguvu za kitaaluma na miundo mbinu ktk nchi za magharibi walishindwa uangamiza. Ndio waarabu na akili zao za kushikiwa?Waarabu wenyewe wamechagua njia ya kupiga marufuku si tuu wakristu kuonekana kwao ila hata kitabu kuonekana km ccm kwa upinzani na vyombo vya habari.
 
Yupo "Yesu mwingine" anaitwa Meil Gibson alicheza picha ya The Passion of Jesus Christ!

Meil Gibson anafanana sana na Yesu wa Nazareti. Mwaka jana alikuja Bongo na kila alipokwenda alifuatwa na makundi ya makubwa ya watu wakimuita na kumfananisha na Yesu wa Nazareti.

Baada ya kumaliza kucheza The Passion of Jesus Christ, Meil Gibson aliokoka na sasa anasambaza neno la Mungu.

Wakati wanacheza picha ya the Passion of Jesus Christ huko Israel/Palestine, kuna wakati waigizaji waligoma. Basi Director wa movie akamwambia Meil Gibson, Wewe Yesu hebu kaongee na wafuasi wako wamegoma. "Yesu" baada ya kuongea na wafuasi wake wakaacha mgomo na kuendelea ku act hiyo picha.
HAHAAA ETI MELL GIBSON NAE ANAFANANA NA YESU KAANGALIE GET THE GRINGO NDO UTAMJUA MELL GIBSON
 
Na ukubwa wangu woteeeee hadi leo najuaga yy ndo Yesu nmefurahi kufaham historia yake fupi
 
Christians faith is the living faith because you can turn the Jesus spoken words into reality.
 
Christians faith is the living faith because you can turn the Jesus spoken words into reality.
Christianity is a success and Jesus is the TRUTH and RATIONALITY. Ukristu popote ulipo pamoja na vikwazo vyote huwa ni kama taa .Ukristu bado ni taa ktk vikwazo vya budism, atheism, stanism, islam, communism/socialism,Maxism,materialism,hinduism, liberism,capitalism. and all other form of ..M bado umeleta tofauti. Nenda korea kusini, hong kong, malaysia, China, Lebanon,syria, ktk hizo nchi sehemu walipo kuna maisha tofauti,kuna mbegu tofauti ktk uchache wao.Western civilization yote ukristu ndio ulikuwa hope ya kuandika vitabu na tafiti ambazo sio maigizo.Wamejenga vitu vya kudumu kwa vile wana matumaini ya kuishi na si ya KUFA. Wakristu wanokoa maisha na mazingira.Imani nyingine hazioni shida kuharibu kwa vile miungu yao inaona Fahari kubomoa alivyojenga Mungu wa Kweli.
 
Huyu jamaa aliigiza vizuri ila kapotosh uma

Umma upi mkuu? Wakristu si wote wanaoweka picture au msalaba kuwa na sanamu. Hiyo ya Sinema ni vasual presentation .Kama ilivyo katika vitabu vya historia na dini pia.Vitabu dini jinsi vinajieleza vina historia na vita maono ya mbele.Wether kaandika mweye historia(si tofauti na kujichora,kujirecord, ) au mwingine kumrekodi au kumwelezea alichokiona na kukisikia. Unapoelezea jambo uliloliona au kulisikia kuna audio and video picture ktk brain inayokuongoza kuelezea. Issue ya cinema ya Yesu kuna wapumbavu wataabudu, na kuna wapumbavu watajumlisha na kuharamisha tukio zima.
 
Wakati wewe unasugua goti huku ukisema Yesu akuone.... Wenzio wanapiga nae sefie tu uswazi....

Katika picha hapa chini huyu mzungu anaitwa Brian Deacon, mwigizaji wa filamu ya Yesu na picha yake ulimwenguni hutumika kama picha ya Yesu.

Deacon ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi.

Ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.

Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.

Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.

Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi

Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.

Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.

Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

Kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.

Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel.

Kumjua Mungu [truncated by WhatsApp]
 
BRIAN DEACON NDANI YA FILAMU YA ”JESUS”
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon, ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.
Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.
Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.
Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho
Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo.
Deacon anaeleza kuwa wakati wa kucheza filamu hii kuna mambo mengi sana yaliyofanyika ambayo yalileta kizaa zaa kwani baadhi wa washiriki walitaka kuleta vurugu baada ya kuchelewa kupeta pesa yao.
Yesu akizungumzana wanafunzi wake
Wakati wa kuchukua filamu hii Deacon alibandikwa nta puani ili kuboresha umbo la pua yake ili iendane na ile ya Wayahudi ambako ndio asili ya Yesu Kristo.
Deacon alipoangikwa msalabani alikuwa anajisikia maumivu kwa sababu kuna makosa yalikuwa yanafanyika na ikamlazimu kukaa pale msalabani kwa muda mrefu.
Hakupigiliwa misumari bali alishikizwa na kamba ambazo zilikuwa hazionekani.
Brian Deacon amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu.
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.
Maisha yake ya kiroho
Baada ya kucheza filamu hii Deacon anasema ilimbadili sana kiroho. Aliamua kumfata Kristo.
BRIAN ANAWAAMBIA WATU WOTE DUNIANI KUWA YEYE SI YESU BALI YEYE NI MUIGIZAJI TU, WALA HAFANANI NA YESU KWANI ENZI ZA YESU HAPAKUWEPO NA TEKNOLOGIA YA CAMERA HIVYO HATA SURA HALISI YA YESU HAIJULIKANI ZAIDI YA WATU KUOTEA NA KUBUNI JINSI YESU ALIVYOFANANA KAMA DIRECTOR WAKE ALIVYOBUNI KWA DEACON
BRIAN PIA AMESHANGAZWA NA BAADHI YA WAUMINI KUWEKA PICHA ZAKE KWENYE MAJUMBA YAO NA KUVAA ROSARI ZENYE PICHA YAKE WAKIAMINI YEYE NI YESU KITU AMBACHO NI MAKOSA
AMESEMA ILI KUTHIBITISHA KUWA YEYE NI MUIGIZAJI TU AMEZITAJA filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985, The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
Huyu ndie Brian Deacon mtu maarufu sana duniani kutokana na kucheza filamu ilitazamwa na mamilioni ya watu.
Makala hii imeandikwa kwa msaada mkubwa wa Sadik Tv, The real Life of Brian. Jesus Film Project na www.comeandsee.com.

2 Timotheo:4.2
lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
 
Back
Top Bottom