Mitume na Manabii karibu wote wanaopatikana katika Biblia takatifu, wametengenezewa filamu ya kuigiza matendo na maneno yao.
Ziko filamu za Manabii na Mitume kama Nuhu, Ibrahimu, Lutu, Isaka, Yakobo, Musa, Haruni, Yoshua, Samweli, Daudi, Sulemani, Eliya, Elisha, Yesu Kristo, Paulo, nk.
Kila mtu anaelewa kuwa Wahusika wa Filamu hizo ni wabandia tu na sio Manabii au Mitume halisi.
Filamu hizo zinasaidia kwa watu ambao hawajui kusoma au wasioona kupata ujumbe kwa njia ya Sauti za maigizo au picha.
Mtu anayewaabudu wahusika wa filamu hizo ni mtu mjinga ambaye hana uelewa wowote ule wa maswala ya Ibada.