Huyu ndiyo Bruce Lee

Huyu ndiyo Bruce Lee

Bruce Lee aliweka rekodi ya dunia baada ya kupiga 'push up' 200 kwa kutumia vidole viwili vya mkono moja na kurusha punje ya mchele hewani na kuidaka kwa kutumia kijiti chembamba cha kulia chakula (chop stick).

Bruce Lee alizaliwa tarehe 27 november 1940 California, Marekani na alifariki tarehe 20 July 1973 Hong Kong akiwa na miaka 32.

Bruce Lee nguvu ya ngumi yake (punching force) ilikuwa na kilo 158 sawa na Mohammed Ali, lakini maajabu Bruce Lee alikuwa na kilo 58 na Mohammed ali kilo 117.

Bruce Lee alikuwa na uwezo wa kupiga ngumi tisa kwa sekunde moja, na ngumi yake ya inchi moja (one inch punch) ilikuwa na uwezo wa kumrudisha nyuma mita 5-6 mwanaume mwenye kilo 68.

Alikuwa na uwezo wa kupiga mateke tisa kwa sekunde moja, alipiga teke kiroba cha mchanga chenye kilo 135 na kuruka urefu wa futi tano kwenda juu. Alikuwa na uwezo wa kufungua kizibo cha soda kwa kutumia vidole viwili.

Aliweka rekodi ya dunia kwa kupiga 'push up' 1500 kwa mikono miwili bila kupumzika, 'push up' 400 kwa mkono moja, 'push up' 200 kwa kutumia vidole viwili vya mkono moja, na 'push up' 100 kwa kidole gumba cha mkono moja.

Bruce Lee alikuwa mchina wa kwanza kurekodi filamu Hollywood Marekani katika sanaa ya kupigana (martial arts). Bruce Lee pekee ndiye alievunja rekodi ya dunia mara kumi ndani ya miaka 2 tu.

Mwamba ( Mngwena ) huyu aenziwe popote pale kwani Sanaa yake ya Kimapigano imeweza kutumika vyema na Watu wote tu Wema na Wabaya ( hasa Vibaka ) maeneo mbalimbali. Namkubali na Kumpenda mno japo sijui Karate ya Kupigana ila ya Kichwani na ya Kudanganyia naijua pamoja na Mbio zangu pale nikizidiwa.
 
Hapana, movie zake ni local sana, ni mara mia niwaangalie Jet Lee, Do Yen na Jack Chan
Bruce Lee kafariki miaka ya 70...jack chan kacheza kwenye enter the dragon ya Bruce Lee Ila ndiyo wale wa kupigwa mwanzo,umri wako utakua mdogo,sisi ambao 1980s tunaenda cinema tulimuelewa Sana Bruce Lee..ndiyo cinema za kipindi hicho
 
Ndo Maana nasisitiza, unachokipenda wewe sio lazima mimi nikipenda. Avalon sinema nimekwenda sana katikati ya miaka 1980 na mwanzoni 90, lakini huyo mwamba muvi zake zilikuwa hazinivutii kabisa. hazina manjonjo nilikuwa naona bora kuangalia hata kina Mithun Chakraborty na disco dansa yake
 
Disco dancer udwanzi,wale mafala walitupata Sana,picha la ukweli la India andhaa kaanuni...Ila mbona Bruce Lee kaweka blue print Sana ya movie zilizofata,dinamo blue print ya movie za akina Damme (blood sport) na billy blanks na wengine wengi tu, Bruce Lee na chuck Norris blue print ya movie nyingi tu
 
FfhvLWLVEAA1Y3O.jpeg
 
Back
Top Bottom