Huyu ndiyo Kikwete ambaye 'comfortably' ameweza kuwakutanisha 'mahasimu' Odinga na Ruto, ila mwaka 2020 alishindwa kuwakutanisha Magufuli na Lissu

Huyu ndiyo Kikwete ambaye 'comfortably' ameweza kuwakutanisha 'mahasimu' Odinga na Ruto, ila mwaka 2020 alishindwa kuwakutanisha Magufuli na Lissu

Kwa hiyo unataka tufanyeje? Jk atabaki kua raisi wa watu wenye akili tu nyie wengine mtajijua
 
Haha hivi mjomba Jiwe ulikua unamjua au unamsikia tu?

Sa ulitaka JK afanyaje yani kwa mfano?
 
Utaona ugumu
Wa kuwakutanisha watoto wako muda ilifika
Na ukiona hilo limekutokea basi ujue hakuna utakachoweza kukiongoza au kupatanisha na ukafanikiwa... Kumbuka taasisi ya kwanza ya uongozi inaanzia kwenye familia yako.
 
Siasa za kenya ni tofauti sana na za kibongo wenzetu wanajielewa sana , ulitegemea JK angeenda kinyume na chama chake cha mboga mboga hahaaaaa , na huku alishaambiwaga anawashwa washwa sana.
Hivi as president haiwezekani kweli kwenye kipindi cha miaka 10 kushindwa kuwasoma mawaziri wako na kujua bila shaka yoyote ambaye ni presidential material??
 
Hivi as president haiwezekani kweli kwenye kipindi cha miaka 10 kushindwa kuwasoma mawaziri wako na kujua bila shaka yoyote ambaye ni presidential material??
kwenye siasa hakuna hizo inaegemea sana kwenye upepo, utashangaa yule ambaye alikua anaonekana zoba akaja kuwa chaguo sahihi , so inategemea na upepo wa kipindi hukisa umekaaje.
 
Halafu wenye Akili kuwazidi tukiwa tunasema hapa hamna Mtu bali kuna Profesa wa Unafiki Tanzania nzima mnasema tuna Chuki nae Binafsi au tunatumika au ni Wadini na Wakabila.

Wenyewe Wavivu wa Kufikiri na mnaompenda mnamuita Mwamba wa Siasa na Diplomasia. Hivi inaingia Akili Mwamba na Bingwa wa Diplomasia akaweza Kutatua ya nchi nyingine ( jirani ) ila ya ndani ya nchi yake akayashindwa?

Haya nawasubiri sasa mje Kumtetea.
wewe kwenye maisha yako umeshawapatanisha kina nani ambao walikuwa hawaelewani?
 
Halafu wenye akili kuwazidi tukiwa tunasema hapa hamna mtu bali kuna Profesa wa unafiki Tanzania nzima mnasema tuna chuki nae binafsi, tunatumika au ni wadini na wakabila.

Mliokuwa wavivu wa kufikiri na mnaompenda mnamuita mwamba wa siasa na diplomasia. Hivi inaingia akili mwamba na bingwa wa diplomasia akaweza kutatua ya nchi nyingine(jirani) ila ya ndani ya nchi yake akayashindwa?

Haya nawasubiri sasa mje kumtetea!​
Angewakutanishaje Magufuli na Lisu wakati alikuwa na maslahi na upande fulani!?
 
Mosi, Mheshimiwa JK huko uliko pole sana.......haters wachache bado wako nawe!

Pili, mtoa mada tafadhali muogope Mungu (kama unaamini) kwa, angalau mara moja moja, kumpumzisha huyu mtu kwa kutomuhusisha na yaliyo nje ya uwezo wake. Unataka kutuambia kuwa hujui kuwa utawala wa awamu ya tano ulitumia 50% ya nguvu yake kumchafua Kikwete?!!!!!! Hata nyie mnaoendelea sasa hv kumchukia na kumzushia kila aina ya balaa ni zao la nguvu zile......huko nyuma nina uhakika haukuwa hivyo mtoa mada.

Ni kikwete aliyeambiwa anawashwawashwa!
Ni kikwete aliyetengenezewa kina musiba waliokuwa wanakesha kumtukana na kumzulia, yeye na familia yake!
Ni kikwete aliyeambowa hakufanya lolote lile katika nchi hii! N.k

Katika hali kama hiyo, just imagine kiwango cha kebehi na tusi ambalo angelipata; kwanza kutoka kwa kina makonda, polepole na bashiru kabla ya mwenyewe mzee baba kugongelea msumari ikiwa angekuja na habari zake za kutaka kumkutanisha na tundu lissu. Tujitahidi kutenda haki hata kwa tusiowapenda kwa 100%
 
Back
Top Bottom