Huyu ndiyo Msanii aliyedharaulika zaidi kwenye muziki wa Tanzania? – Kisa cha Rashidi Ziada (KR)

Huyu ndiyo Msanii aliyedharaulika zaidi kwenye muziki wa Tanzania? – Kisa cha Rashidi Ziada (KR)

Ninachokiona Kibra Sir Nature kabeba wasanii wengi sana, sikuwa najua kama KR alikuwa GWM Majitu zaidi ya kumuona na Kibra. Kuanzia Wachuja Nafaka mpaka Wanaume Halisi Nature hakuwahi kumuacha KR
 
Nchi zenye utamaduni wa kulinda urithi wa sanaa kama Marekani au Nigeria, watu walioanza muziki miaka ya 90 na kuleta mapinduzi ya mitindo hupewa tuzo za heshima hata mikataba ya ubalozi.

Lakini huku kwetu msanii akimaliza muda wake wa kuwa juu, wadau na vyombo vya habari wanammwaga na kumwona hana thamani tena kwa sababu tu hana wimbo mpya wa kisasa. Hii kasumba inawaumiza sana ma-legend waliofungua milango tunayoiona leo.
Ingekuwa US mtu kama Saigoni asingekuwa vile. Yeye, Sugu, Salehe Jabir na Balozi wameitoa gemu ya Rap mbali sana
 
Subiri afe atasifiwa.

Ni kweli jamaa hana kazi za solo.. lakini katika hizo hizo za makundi alifanya poa sana..
Huwezi itaja GWM bila kumtaja KR
 
Ninachokiona Kibra Sir Nature kabeba wasanii wengi sana, sikuwa najua kama KR alikuwa GWM Majitu zaidi ya kumuona na Kibra. Kuanzia Wachuja Nafaka mpaka Wanaume Halisi Nature hakuwahi kumuacha KR
Kipindi nature anatoka tmk wanaume familiy na kuanzisha tmk wanaume halisi, alimuacha KR TMK wanaume family
 
Mzee wetu Said Fella anaumwa wajameni hadi juzi Mstaafu PM- Mh. Majaliwa Majaliwa amemtembelea kumjulia Hali, inasikitisha sana wale aliowanyanyua katika tasnia hii ya muziki hawamkumbuki tena.

Twendeni tumtembelee tukamjulie Hali bhandugu
Dah jamaa ana stroke, tumuombee arejee kwenye afya yake
 
Ukizungumzia wasanii ambao hawajawahi kupewa heshima inayolingana na mchango wao kwenye muziki wa Tanzania, kwangu jina la kwanza ni Rashidi Ziada (KR).

KR alianza muziki tangu miaka ya 90. Amepitia makundi mbalimbali kama GWM, Wachuja Nafaka, hadi kuwa sehemu ya TMK Wanaume Family. Licha ya historia hiyo ndefu, ni vigumu kuona akitajwa miongoni mwa majina yanayopewa heshima kwa mchango wao.

Kinachoshangaza zaidi ni kwamba wengi wanaamini KR ndiye aliyeanzisha style ya kucheza ya "Mapanga", style ambayo baadaye ilikuja kuwa moja ya alama kubwa zilizolitambulisha TMK Wanaume Family. Lakini pamoja na mchango huo, hajawahi kupata utambuzi unaolingana na alichokitoa.

Mpaka leo, ni nadra sana kumuona KR akiitwa kwenye show kama solo artist, na hata interview za kuzungumzia muziki wake yeye binafsi zimekuwa chache sana. Mara nyingi amebaki kuwa mtu wa pembeni, wakati wenzake wameendelea kupata nafasi kubwa zaidi.

Jambo jingine linalonigusa ni tabia yake. Wanaomfahamu wanasema KR ni mtu mwenye roho nzuri sana. Kila anapoitwa kwenye event za wenzake huwa anajitokeza kutoa support na kuonyesha upendo. Lakini mara nyingi huonekana upendo huo haurudi kwake kwa kiwango kilekile.

Tumeshuhudia mara kadhaa sherehe za birthday au matukio ya member wenzake wa TMK yakipewa uzito mkubwa. Lakini sijawahi kuona juhudi kama hizo zikielekezwa kwa KR, jambo linalofanya wengi wahisi mchango wake haupewi thamani anayostahili.

Kwa maoni yangu, kama angekuwa kwenye nchi yenye utamaduni mkubwa wa kuthamini waanzilishi wa mitindo ya sanaa, huenda leo angekuwa ametambuliwa zaidi, angekuwa ameshinda tuzo mbalimbali, na pengine angekuwa amefanikiwa zaidi kutokana na mchango wake.

Inaumiza kuona msanii mwenye historia ndefu na mchango mkubwa anaweza kuzeeka bila kupata utambuzi unaolingana na alichokifanya kwa muziki wa Tanzania.

Je, ninyi mnakubaliana kwamba Rashidi Ziada (KR) ni mmoja wa wasanii waliodharaulika zaidi kwenye historia ya muziki wa Tanzania? Kama kuna wasanii wengine watajwe
ukitaka kuwini basi tulia maishani
 
Kwa wanaojuwa muziki hili siyo geni, kuna Wasanii wenye vipaji lakini ubora upo ndani ya makundi hawajaumbwa kuwa soul Artist licha ya kuwa na uwezo mkubwa.

Mfano Marekani Naughty by Nature wanashine wakiwa kundi.

HBC aliyeweza kutoka Soul Artist ni Profesa Jay peke yake lakini Fanani na Willy wana uwezo mkubwa ila talent yao ipo ndani ya kundi.

Msondo ngoma miaka yote ni Baba ya Muziki lakini utang'ara ukiwa ndani ya band, ni Hussein Jumbe.R.I.P pekee ndio aliweza kutoka na Soul project na kuanzisha Talent band.

Majibu sahihi ya mchokoza mada anayo Sugu ndiye aliyeamuwa kuanzisha Bongo Fleva honors nadhani KR atafikiwa kupitia kundi lao eithe GWM au Wachuja Nafaka.
 
Mzee wetu Said Fella anaumwa wajameni hadi juzi Mstaafu PM- Mh. Majaliwa Majaliwa amemtembelea kumjulia Hali, inasikitisha sana wale aliowanyanyua katika tasnia hii ya muziki hawamkumbuki tena.

Twendeni tumtembelee tukamjulie Hali bhandugu
Zile nyumba alizowapa watoto wa Yamoto bado wanazo!? Au aliwakodisha tu!? Sometimes hawa wadau wanapotezewa na waliowasaidia kwa sababu ya mengi yaliyojificha.
 
Ninachokiona Kibra Sir Nature kabeba wasanii wengi sana, sikuwa najua kama KR alikuwa GWM Majitu zaidi ya kumuona na Kibra. Kuanzia Wachuja Nafaka mpaka Wanaume Halisi Nature hakuwahi kumuacha KR
KR alitengana na Nature wakati Nature alipoenda Halisi. Yeye KR alibaki na Mkubwa Fella ndani ya Wanaume TMK pamoja na Temba na Chege. Unakumbuka goma lao "Kazi Ipo" feat. Q Chillah !?
 
Ingekuwa US mtu kama Saigoni asingekuwa vile. Yeye, Sugu, Salehe Jabir na Balozi wameitoa gemu ya Rap mbali sana
Hata huko nje wakongwe walioanza kuipigania game hawakupata hela sana kama waliokuja baadae. Na sababu kubwa ni kuwa wao ndio walikuwa pioneers wa game kabla haijawa biashara na unyonyaji uliokithiri wa makampuni kabla ya sheria zenye nguvu za Haki_Miliki.
 
Back
Top Bottom