Huyu ndiyo Msanii aliyedharaulika zaidi kwenye muziki wa Tanzania? – Kisa cha Rashidi Ziada (KR)

Huyu ndiyo Msanii aliyedharaulika zaidi kwenye muziki wa Tanzania? – Kisa cha Rashidi Ziada (KR)

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Ukizungumzia wasanii ambao hawajawahi kupewa heshima inayolingana na mchango wao kwenye muziki wa Tanzania, kwangu jina la kwanza ni Rashidi Ziada (KR).

KR alianza muziki tangu miaka ya 90. Amepitia makundi mbalimbali kama GWM, Wachuja Nafaka, hadi kuwa sehemu ya TMK Wanaume Family. Licha ya historia hiyo ndefu, ni vigumu kuona akitajwa miongoni mwa majina yanayopewa heshima kwa mchango wao.

Kinachoshangaza zaidi ni kwamba wengi wanaamini KR ndiye aliyeanzisha style ya kucheza ya "Mapanga", style ambayo baadaye ilikuja kuwa moja ya alama kubwa zilizolitambulisha TMK Wanaume Family. Lakini pamoja na mchango huo, hajawahi kupata utambuzi unaolingana na alichokitoa.

Mpaka leo, ni nadra sana kumuona KR akiitwa kwenye show kama solo artist, na hata interview za kuzungumzia muziki wake yeye binafsi zimekuwa chache sana. Mara nyingi amebaki kuwa mtu wa pembeni, wakati wenzake wameendelea kupata nafasi kubwa zaidi.

Jambo jingine linalonigusa ni tabia yake. Wanaomfahamu wanasema KR ni mtu mwenye roho nzuri sana. Kila anapoitwa kwenye event za wenzake huwa anajitokeza kutoa support na kuonyesha upendo. Lakini mara nyingi huonekana upendo huo haurudi kwake kwa kiwango kilekile.

Tumeshuhudia mara kadhaa sherehe za birthday au matukio ya member wenzake wa TMK yakipewa uzito mkubwa. Lakini sijawahi kuona juhudi kama hizo zikielekezwa kwa KR, jambo linalofanya wengi wahisi mchango wake haupewi thamani anayostahili.

Kwa maoni yangu, kama angekuwa kwenye nchi yenye utamaduni mkubwa wa kuthamini waanzilishi wa mitindo ya sanaa, huenda leo angekuwa ametambuliwa zaidi, angekuwa ameshinda tuzo mbalimbali, na pengine angekuwa amefanikiwa zaidi kutokana na mchango wake.

Inaumiza kuona msanii mwenye historia ndefu na mchango mkubwa anaweza kuzeeka bila kupata utambuzi unaolingana na alichokifanya kwa muziki wa Tanzania.

Je, ninyi mnakubaliana kwamba Rashidi Ziada (KR) ni mmoja wa wasanii waliodharaulika zaidi kwenye historia ya muziki wa Tanzania? Kama kuna wasanii wengine watajwe
 
Kaka Rashidi (KR MULLAH) ni baadhi ya wasanii wachache ambao mchango wake unaonekana akiwa ktk kundi kuliko akiwa peke yake (Solo) tofauti na akina Saidi Omari (Chege), Amani James Temba (Mh. Temba) au Juma Kassim Ali (Juma Nature). Mfano, kuweka nakshi ktk mistari hata mitindo ya kucheza. Anafanana na Enock Bella aliyekuwa YAMOTO BAND yule mwenye sauti ya besi ambaye pia amekosa kung'aa akiwa Solo Artist kama wenzie akina Mbosso, Aslay na Baker Flavor
 
Taja hata nyimbo 2 alizofanya peke yake. Msanii anaetegemea kuimba na wenzake ndio afanye vizuri ujue kipaji chake ni cha kawaida sana so sioni hiyo heshima unayotaka apewe
Inaweza kuwa hajawahi kufanya solo project lakini katika project za kundi amefanya vizuri sana, na Style.ya Mapanga ndo utambulisho wa kundi la TMK
 
Nchi zenye utamaduni wa kulinda urithi wa sanaa kama Marekani au Nigeria, watu walioanza muziki miaka ya 90 na kuleta mapinduzi ya mitindo hupewa tuzo za heshima hata mikataba ya ubalozi.

Lakini huku kwetu msanii akimaliza muda wake wa kuwa juu, wadau na vyombo vya habari wanammwaga na kumwona hana thamani tena kwa sababu tu hana wimbo mpya wa kisasa. Hii kasumba inawaumiza sana ma-legend waliofungua milango tunayoiona leo.
 
Back
Top Bottom