Leo tumewaza sawa mkuu. Niimeshangaa. Nikiwa barabarani nikawaza Kagame alivyo na akili kubwa. Kiukweli kama ulivyosema namchukia,lakini napenda anavyoikimbiza Rwanda. Napenda sana alivyo advanced kuhusu usalama wa Taifa. Rwanda (FBI) ya ndani ya nchi na (CIA) ya nje. Yaani ipo inayohusika na maswala ya usalama ya upelelezi wa ndani tu na ipo inayohusika nje ya mipaka ya Rwanda. Kama ilivyo mfumo wa Marekani na Israel. Na wanafanyakazi vizuri sana. Hapo Kagame saluti kwake. Namchukia tu kwa anachowafanyia wapinzani kama kuwapoteza na mengine.
Rwanda nchi ndogo,isiyo na chochote,ukilinganisha na Tanzania,lakini iko mbali kiuchumi,kiusalama pia kijeshi. Kagame akili kubwa. Kwa ujumla ni kama anai-control Afrika mashariki na kati bila wao kujua.
Kagame ameifanya Rwanda iwe tajiri kwa rasilimali za nchi zingine.
Kwa andishi la hivi karibuni la
The bold ni kwamba Jamhuri ya Africa ya kati inalindwa na wanajeshi wa Rwanda na Polisi wa Rwanda huku hao wanajeshi zaidi ya 3000 wakichukua mishahara mizuri toka vyanzo vingine visivyo vya Rwanda. Wapo pia Mozambique kupambana na waasi. Kwa hiyo Kagema anaajiri vijana wengi jeshini na polisi kwa mikataba na nchi zingine.
Najiuliza Tanzania tumekosea wapi? Nchi kubwa yenye kila rasilimali za kutuendeleza zaidi hata ya Israel. Tanzania nchi yenye kila aina ya madini yapatikanayo duniani. Tanzania ina madini yasiyopatikana kokote isipokuwa Tanzania. Tanzania yenye mbuga zote kubwa duniani. Tanzania yenye gesi,mafuta. Tanzania yenye bandari kubwa ya kuhudumia nchi zaidi ya 5 mpaka 6,7 kufuatana tu kujipanga kwetu. Nchi yenye watu wengi lakini imekosa maarifa kabisa. Wapo wansojiita wasomi akina miguru na makatani wanawaongezea tu tozo kila kona za kuwakamua watu ambao hawajawatengeneza. Tuna watu wanajiita maprofeser humu nchini lakini hakuna hata mmoja na uprofeser wao mwenye plan moja yenye nguvu ya kutuvusha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine,kiuchumi. Tanzania nchi inayojisogeza tu bila dira,wala mwelekeo ,tunaishi leo tu. Wengi viongozi wanaangalia matumbo yao tu. Kweli Kagame ni bonge la kichwa