Kwa wasomi wa mambo ya siasa kama Kikwete (Kikwete alikuwa Kamisaa wa Siasa kwenye jeshi, kama si msomi wa mambo ya siasa angalau ana mwanga wa elimu ya siasa) kuna hoja moja ambayo kibongobongo si rahisi kuielewa au kuiheshimu.
Inaitwa "civilian control of the military" kwa zaidi soma wiki hapa
Civilian control of the military - Wikipedia
Hii dhana inasema kwamba, katika nchi ya kidemokrasia, uongozi wa kiraia ndiyo unaoongoza jeshi. Jeshi ni la wananchi, wananchi wanachagua uongozi wa kiraia, uongozi wa kiraia ndiyo unapanga jeshi lifanye nini. Hii ni tofauti na udikteta wa kijeshi ambao baraza la kijeshi au mwanajeshi mmoja anaongoza mambo kidikteta.
Sisi tunasema tuna uongozi wa kidemokrasia, ndiyo maana hata Amiri Jeshi Mkuu ni mtu anayechaguliwa kiraia, si mwanajeshi, anapata kuongoza jeshi, lakini yeye si mwanajeshi. Hii ni tofauti kubwa na ya muhimu. Amiri Jeshi Mkuu wetu si mwanajeshi, yeye ni raia, anaongoza jeshi.Tuliondoa habari za wanajeshi kuwa kwenye siasa tulivyoanza vyama vingi.
Sasa basi, unaweza kusema, ana haki ya kuvaa magwanda kwa sababu yeye ni Amiri Jeshi Mkuu. Hili ni kweli.
Lakini pia, haliendani na spirit ya "civilian control of the military". Kwa sababu, perception creates its own reality. Kwenye sheria kuna msemo, "Justice must not only be done, it must appear to be done".
Na kwenye "civilian control of the military" ni hivyo hivyo. The military must not only be controlled by civilians, it must appear to be controlled by civilians. Rais akishaanza kuvaa migwanda ya Kijeshi watu wanapata picha kwamba nchi inapelekwa kijeshi, si kidemokrasia.
Marais waliopita, kwa busara za kujua hili, hawakuvaa magwanda ya jeshi. Kikwete ndiyo kabisa, aliacha jeshi ili awe mwanasiasa na hakuvaa magwanda tena tangu alipoacha jeshi. Alijua maana ya hii hoja, ilimuondoa jeshini. Kina mzee Makamba, Chiligati, Nnauye, marehemu Ditopile etc wote walitoka jeshini ili wawe wanasiasa, kwa sababu ya kanuni hii ya "civilian control of the military".
Mkapa ndiyo kabisaaa, hakuvaa. Mwinyi naye hivyo hivyo. Nyerere nimemuona kavaa magwanda ya mgambo kuhamasisha wanajeshi katika vita vya Kagera tu, nje ya vita sijawahi kumuona.
Wote walielewa kanuni za "civilian control of the military".
Huyu rais wetu wa sasa ama haelewi, ama hajali.
Anaona ujiko kuvaa migwanda. Watu wanakosa kuelewa tunaongozwa kiraia au kijeshi?
Sasa hao wakuu wa wialaya na mikoa nao ndio wanaiga hilo, kwa sababu na wao wanajiona wako mkondo ule ule wa uongozi wa ulinzi wa mkoa na wilaya.
Maumivu ya kichwa huanza polepole, mwisho diwani naye anavaa magwanda ya jeshi.
Jeshi linatumika kisiasa.
Ndiyo maana wanajeshi wenyewe wanaona ujinga huu tunadharaulika, wametoa tamko kwa hao wakuu wa wilaya na mikoa waache ujinga huu.