Uchaguzi 2020 Huyu siyo Abood ninayemjua. Huwezi kuwa mwema utotoni ukawa shetani uzeeni

Uchaguzi 2020 Huyu siyo Abood ninayemjua. Huwezi kuwa mwema utotoni ukawa shetani uzeeni

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Kuna mtu anamiki kampuni ya mabus, tunapanda tunalipa nauli na kusafirisha mizigo, anamiliki radio, tunasikiliza tunashirikiana naye anafanikiwa.

Fedha zetu za nauli anazitumia kuhonga kwa tume na wagombea asipige kampeni Bali apite bila kupingwa. Mtu huyu anashindwa kujua riziki inatoka kwa Mungu, anashindwa kujua kuna siku mali tutaziacha hapa Duniani. Anashindwa kujua dua za wanannchi wanaolilia haki ipo siku zitapokelewa na ataadhibiwa.

Unamiliki mabilioni ya fedha unaongaje kupata milioni kumi kwa mwezi? Unaongaje kupata kiinua mgongo za milioni mia tatu kwa miaka mitano? Mbona haya ni mapato yako ya siku?

Kwanini ufike mahali ushindwe kupambana jukwaani na mwenzako hadi utumie fedha kununua madaraka? Kuwapa watendaji wa serikali mafuta na usafiri kunakufanya wewe uwe exceptional kwenye uchaguzi? Kama unaamini umefanya kwanini usiende kwa wananchi kuwaeleza ulichofanya?

Naumia sana kuona huyu mzee anajiingiza kwenye Mambo ya giza wakati anao uwezo mkubwa wakumtumikia Mungu, kuwatumikia wananchi kwa haki na kusimamia adhi yake.

Huyu mzee sidhani kama alipaswa kuwa hapa alipo Sasa, natamani nikae nae Kama dada yake nimkanye ila sina nafasi yakumwona. This is not Abood i use to know! Lipo tatizo, uwezi kuwa mwema utotoni ukawa shetani uzeeni, it marks bad ending.
 
Chama cha Mapinduzi kitapeleka wengi sana jehanamu kwenye moto wa milele.

Imeandikwa, ashirikianaye na mwovu au kuunyamazia uovu machoni pake hata kimbia hasira za Mungu.
Ukizungumzia uovu hakuna atae pona hii nchi.
 
Kwa Mema ambayo Abood huwa anawafanyia wana Mkoa wa Morogoro hasa pale wakiwa na Shida ( Misiba ) na mpaka wakati wa Furaha ( Ndoa ) ambayo hata Mimi GENTAMYCINE nimeshawahi Kufaidika nayo kwa namna moja au nyingine nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Abood hafai kuwa Mbunge au Kuzipokea hizi Shutuma za Kisiasa dhidi yake.

Mapungufu yake haya hayaondoi Ukweli kwamba Jamaa ( Abood ) ni Mtu wa Watu sana na pia ni Mwema mno tu na asiyebagua wana Morogoro.
 
kiukweli kwa morogoro kulikuwa hakuna haja ya kufanya yote hayo... kama kweli yamefanyika...
Abood Morogoro huwa ni yake siku zote... kwa vyovyote vile angeshinda tu..
Kilevi cha madaraka na ukubwa ni kibaya kuliko madawa ya kulewa

Jr[emoji769]
 
Kwa Mema ambayo Abood huwa anawafanyia wana Mkoa wa Morogoro hasa pale wakiwa na Shida ( Misiba ) na mpaka wakati wa Furaha ( Ndoa ) ambayo hata Mimi GENTAMYCINE nimeshawahi Kufaidika nayo kwa namna moja au nyingine nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Abood hafai kuwa Mbunge au Kuzipokea hizi Shutuma za Kisiasa dhidi yake. Mapungufu yake haya hayaondoi Ukweli kwamba Jamaa ( Abood ) ni Mtu wa Watu na Mwema mno tu na asiyebagua wana Morogoro.
Waluguru bado hawajapata Uhuru.
 
Katika wanasiasa wavumilivu, Abood ni mmoja wapo. Huko nyuma kila alipokuwa akigombea, jina lake lilikuwa linafyekwa likifika Dodoma. Ameshafyekwa si chini ya mara mbili ila hakukata tamaa. Nakumbuka alishawahi kuwapa CCM Landcruiser mkonga nje (pick up la kijani kama sikosei). Sasa naona ni zamu yake kuvuna.
 
Huyu mzee miaka yote yeye hatakagi kufanya kampeni. Hajawahi kupita kwa siasa za majukwaani yaani ndio alivyo. Ila mwaka huu atake asitake atapanda jukwaani kunadi sera. Yaani yeye na Shabiby ni majambazi ya madaraka! Yamezoea kupitia mlango wa uani kila kipindi cha uchaguzi mkuu!
 
Huyu mzee miaka yote yeye hatakagi kufanya kampeni. Hajawahi kupita kwa siasa za majukwaani yani ndo alivyo. Ila mwaka huu atake asitake atapanda jukwaani kunadi sera. Yani yeye na Shabiby ni majambazi ya madaraka! Yamezoea kupitia mlango wa uani kila kipindi cha uchaguzi mkuu!
Sio kweli. Kwenye ukweli pasemwa, jamaa hakuna anaeweza kusimama nae na akashinda hapo Morogoro. Wananchi wanamkubali sana. Huwa anashinda kihalali kabisa bila zengwe.
 
Back
Top Bottom