Asante
JF-Expert Member
- Dec 18, 2009
- 2,086
- 1,081
Hydroponic Fodder Solution for Farmers
Hydroponic farming ni mbinu mbadala ya kupanda mazao bila ya kutumia udongo. Ilianza miaka mingi, kama inavyosimuliwa katika historia ilianzia kwenye bustani zinazoninginia za Babylon. Kwa matumizi ya kibiashara kwa ajili ya kulishia mifugo ilianza mwaka 1960 nchini Australia, na imesambaa sehemu mbalimbali za dunia kuanzia kipindi hicho.
Mkulima anaweza kujenga nyumba yenye ukubwa wa mita 3 kwa mita 4, ambayo inaweza kuzalisha majani ya kulisha ngombe wawili wa maziwa, au nguruwe 10, au kuku 400 kwa mwaka mzima.
Hydroponic fodder kwa wanyama ni chakula kamili cha kulishia na siyo ziada baada kulisha vyakula vingine. Inaondoa kabisa matumizi ya kulisha vyakula vingine kama pollard, dairy meal, na poultry fed.
Faida za majani ya hydoponically
1. Yanakuwa haraka na yanakomaa haraka, hii ni kwa sababu mbegu haitumii nguvu nyingi na muda mwingi kuvunja udongo na kupenyeza mizizi chini ya ardhini.
2. Mavuno yanakuwa mengi, kwa sababu mmea hautumii sana mizizi kujijenga, hivyo nguvu ya ziada hutumika kukuza majani.
3. Inaondoa kabisa magonjwa yanayopatikana kwenye udongo kama bacteria kutokuwepo kwenye majani ya kulishia mifugo.
4. Yanaongeza vipindi vya kuvuna majani.
5. Inapunguza matumizi ya mbolea, maji na nafasi.
MAHITAJI
1. NYUMBA; ujenzi uzingatie hali ya hewa uwe kati ya 17⁰c-25⁰c Hii ni kwa sababu hali ya hewa ikiwa chini ya 17⁰c inasababisha ukuwaji kuwa wa polepole na hali ya hewa ikiwa juu ya 25⁰c shahiri itaanza kuchachuka.
2. MBEGU; Shahiri na mtama mweupe ndiyo bora kwa sababu zina nutrients na energy za kutosha, mbegu nyingine ni ngano, mtama, mahindi, millet n.k.
3. MAJI; maji ni lazima yawe masafi na yasiwe na aina yoyote ya takataka.
4. SUPPORT SURFACE; tray za aluminium ndiyo bora lakini gharama zake ziko juu. Treated polythene zinaweza kutumika lakini ni lazima zisafishwe na chlorine (JIK) kila baada ya mavuno.
5. MBOLEA; kwa sababu uvunaji hufanyika baada ya kipindi kifupi, matumizi ya mbolea siyo muhimu, wakulima wengine hutumia mbolea ili kuongeza uzito wa majani , ingawa bado ni salama kwa mifungo lakini kitaalamu bado siyo muhimu.
PROGRAMM YA KULISHA NGOMBE KWA SIKU
Ngombe mmoja analishwa fodder kilo 45, kilo 3 za nyasi kavu na chumvi ya calcium gram 150
FAIDA UTAKAZOPATA
1. Maziwa yataongezeka kwa asilimia 10
2. Ubora utaongezeka na uhakika wa kupata ndama mmoja kwa mwaka.
3. Utapata maziwa yenye ladha halisi, rangi na harufu itaimarika
4. Afya ya ngombe itaimarika
5. Utaokoa kiasi cha shilingi 4,000 hadi 8,000 kwa siku kwa kila ngombe
Kuotesha fodder za kutosha kulisha ngombe 2 kama mlo kamili utahitaji kilo 360 za mbegu ya shahiri au mtama mweupe kwa mwaka. Gunia moja la mbegu lina kilo 80.
Kuotesha fodder za kutosha kulisha ngombe 2 unatakiwa uwe na aluminium tray 42.
Kudhibiti hali ya hewa unashauriwa kutumia shade net.
Kuotesha fodder za kutosha ngombe wawili kwa mwezi utahitaji lita 3.5 za hydroponic nutrient solution.
KULISHA NGURUWE
Nguruwe alishwe vizuri fodder
FAIDA ZA KULISHA NGURUWE
1. Mafuta hupungua kwa asilimia 50 (Kutoka 14mm hadi 7mm)
2. Anakomaa haraka kabla ya wiki mbili
3. Harufu mbaya inayoambatana na nguruwe inapotea kwa kiwango kikubwa
4. Afya ya nguruwe kwa ujumla huimarika sana.
5. Utaokoa kiasi cha shilingi 8,000 hadi 12,000 kwa kila nguruwe