Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Hydroponic Fodder Solution for Farmers

Hydroponic farming ni mbinu mbadala ya kupanda mazao bila ya kutumia udongo. Ilianza miaka mingi, kama inavyosimuliwa katika historia ilianzia kwenye bustani zinazoning’inia za Babylon. Kwa matumizi ya kibiashara kwa ajili ya kulishia mifugo ilianza mwaka 1960 nchini Australia, na imesambaa sehemu mbalimbali za dunia kuanzia kipindi hicho.


Mkulima anaweza kujenga nyumba yenye ukubwa wa mita 3 kwa mita 4, ambayo inaweza kuzalisha majani ya kulisha ng’ombe wawili wa maziwa, au nguruwe 10, au kuku 400 kwa mwaka mzima.


Hydroponic fodder kwa wanyama ni chakula kamili cha kulishia na siyo ziada baada kulisha vyakula vingine. Inaondoa kabisa matumizi ya kulisha vyakula vingine kama pollard, dairy meal, na poultry fed.


Faida za majani ya hydoponically

1.
Yanakuwa haraka na yanakomaa haraka, hii ni kwa sababu mbegu haitumii nguvu nyingi na muda mwingi kuvunja udongo na kupenyeza mizizi chini ya ardhini.
2. Mavuno yanakuwa mengi, kwa sababu mmea hautumii sana mizizi kujijenga, hivyo nguvu ya ziada hutumika kukuza majani.
3.
Inaondoa kabisa magonjwa yanayopatikana kwenye udongo kama bacteria kutokuwepo kwenye majani ya kulishia mifugo.
4.
Yanaongeza vipindi vya kuvuna majani.
5.
Inapunguza matumizi ya mbolea, maji na nafasi.

MAHITAJI

1.
NYUMBA; ujenzi uzingatie hali ya hewa uwe kati ya 17⁰c-25⁰c Hii ni kwa sababu hali ya hewa ikiwa chini ya 17⁰c inasababisha ukuwaji kuwa wa polepole na hali ya hewa ikiwa juu ya 25⁰c shahiri itaanza kuchachuka.
2.
MBEGU; Shahiri na mtama mweupe ndiyo bora kwa sababu zina nutrients na energy za kutosha, mbegu nyingine ni ngano, mtama, mahindi, millet n.k.
3. MAJI; maji ni lazima yawe masafi na yasiwe na aina yoyote ya takataka.
4.
SUPPORT SURFACE; tray za aluminium ndiyo bora lakini gharama zake ziko juu. Treated polythene zinaweza kutumika lakini ni lazima zisafishwe na chlorine (JIK) kila baada ya mavuno.
5. MBOLEA; kwa sababu uvunaji hufanyika baada ya kipindi kifupi, matumizi ya mbolea siyo muhimu, wakulima wengine hutumia mbolea ili kuongeza uzito wa majani , ingawa bado ni salama kwa mifungo lakini kitaalamu bado siyo muhimu.

PROGRAMM YA KULISHA NG’OMBE KWA SIKU

Ng’ombe mmoja analishwa fodder kilo 45,
kilo 3 za nyasi kavu na chumvi ya calcium gram 150

FAIDA UTAKAZOPATA

1.
Maziwa yataongezeka kwa asilimia 10
2.
Ubora utaongezeka na uhakika wa kupata ndama mmoja kwa mwaka.
3.
Utapata maziwa yenye ladha halisi, rangi na harufu itaimarika
4.
Afya ya ng’ombe itaimarika
5.
Utaokoa kiasi cha shilingi 4,000 hadi 8,000 kwa siku kwa kila ng’ombe

Kuotesha fodder za kutosha kulisha ng’ombe 2 kama mlo kamili utahitaji kilo 360 za mbegu ya shahiri au mtama mweupe kwa mwaka. Gunia moja la mbegu lina kilo 80.


Kuotesha fodder za kutosha kulisha ng’ombe 2 unatakiwa uwe na aluminium tray 42.
Kudhibiti hali ya hewa unashauriwa kutumia shade net.


Kuotesha fodder za kutosha ng’ombe wawili kwa mwezi utahitaji lita 3.5 za hydroponic nutrient solution.

KULISHA NGURUWE

Nguruwe alishwe vizuri fodder


FAIDA ZA KULISHA NGURUWE

1.
Mafuta hupungua kwa asilimia 50 (Kutoka 14mm hadi 7mm)
2.
Anakomaa haraka kabla ya wiki mbili
3.
Harufu mbaya inayoambatana na nguruwe inapotea kwa kiwango kikubwa
4.
Afya ya nguruwe kwa ujumla huimarika sana.
5.
Utaokoa kiasi cha shilingi 8,000 hadi 12,000 kwa kila nguruwe
 
Wakuu, shayiri inalimwa mikoa gani nchini Tanzania?

Soko gani ninaweza kuipata?
 
nusu ya watanzania tungekua hivi/kutumia electronics zetu kutafta maarifa haya..hakika tungekua mbali?
 
Mimi nitatumia mahindi kwa kuanzia. Sioni ulazima wa shayiri wakati kuna options nyingine
 
Safi mno mkuu mamaNa. Ila tu swali langu la pekee ni je umeona barley tu ndo ina uwezo kuzalisha madini au nutrients husika kwa mifugo. Shukran.
 
Last edited by a moderator:
Somo zuri ila nahitaji kupitia maelekezo kwa umakini kuna vitu vya muhimu hapa
 
Asante,

Hii teknolojia inapatikana wapi? Walau utujuze gharama na vifaa vinavyotakiwa kama mbegu za majani hayo na virutubisho vyake. Ukiweka contacts itakuwa bora zaidi
 
hizo mbegu zinadumbukizwa tuu kwa maji au ...hamjaelezea hapo.
 
94eafa643ad4e3ed9f5b27f02cb5e218.jpg
 
2-1-6 hii ni kwajili ya carrot na 2nitrogen,1phosphoric na6Mgnisium hii matumizi yake kwa mimea midogo ni kifuniko kimoja kwa lrt moja ya maji hapo sasa inategemeana na ukubwa wa shamba
 
growing carrots by hydroponic takes how many days? Very curious
 
tufafanulie mkuu,wengine weupe humu,ina kazi gani hyo formula??
 
Back
Top Bottom