Mkuu hizo sio akili zako.
Depression ndo inakuletea hayo mawazo,inakudanganya uone kila kitu ni kibaya ila sio kweli mana una vitoto vyako vizuri.Hao ni sbb tosha ya wewe kutamani kuendekea kuishi.
Sasa wewe baba yao jembe lao,mwalimu wao,kipenzi chao,mlinzi wao na tena shujaa wao ukifa nani atakava hizo nafasi?
Nikwambie kitu!Haijalishi leo unapitia nini wewe na wanao ambao ndio faraja yako,trust me hivyo vijamaa kuna siku vita graduate,,vitaoa,vitanunua gari zao za kwanza,vitagombana na kuapizana undugu ufe na vitapata changamoto kama unqzopitia wewe leo sasa je hutamani kuwepo hayo yote yatakapowatokea?Nani atasimama nao kama sio wewe?
Mkuu mimi ni mwanamke ila ije jua ije mvua hqjiui mtu hapa sasa iweje wewe wa kiume ujiue?
Kama shida wote tunazo ila tunapambana hivyo hivyo.
Wewe sio dhaifu kiasi hicho mkuu usijiue.🙏🙏🙏🙏😍😍😍