FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #21
TORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA KUMI NA NNE
TULIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU..........
maneno matamu sana ya majonzi yalikuwa yakimtoka Catherine alikuwa anaumia sana kutengana na mwanaume aliyekiri kuwa wa maisha yake. Mwanaume alimkumbatia kwa mahaba na kumpiga busu zito sana la hisia wakati huo kuna gari ilikuwa inamsubiri aliondoka huku akikimbia mkono ulikuwa juu akimpungia Catherine mkono wa kwaheri.
ENDELEA...................
"Aise ndugu yangu wanadamu wasiri sana huyu mzee tumeishi naye Kwa muda wote hapa akituzuga kumbe mwenzetu yupo kwenye dunia yake kabisa hivi umeona msafara ambao umekuja kumchukua hapa saivi?"
"Mhhhh maisha yamepiga hatua sana siku hizi wanadamu hatuaminiki tena tunabadilika mno, yule mzee mimi nilikuwa nina wasi wasi nae sana haiwezekani mshona viatu asiye na sehemu ya kulala aweze kunawiri namna ile nilikuwa namshangaa sana lakini hakuwahi kuonyesha dalili yoyote ile kuwa mtu mwenye vyake hii inaniogopesha sana kuwaamini wanadamu usije ukashangaa hata wewe kesho hapo naambiwa ni usalama wa taifa sitashangaa tena wanadamu siku hizi tunatisha sana"
"Usipende kujitoa kwenye listi kama vile wewe sio mwanadamu mwenzetu, nina imani atakuwa mpelelezi yule mzee sio bure hapa mtaani kaacha gumzo kubwa sana sikuwahi kutegemea kabisa leo hii mbona nimekoma mimi ama kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa ngoja nikalale sina hata hamu ya kutembea wala kuzunguka tena hapa mtaani naogopa" walikuwa ni vijana wawili maeneo ya Mburahati waliokuwa wanapiga stori kumhusu mzee mmoja fundi wa viatu ambaye alikuwa ameacha gumzo hapo mtaani. Kazi yake na kilichokuwa kimetokea hapo vilikuwa ni vitu ambavyo kwa mwanadamu yeyote wa kawaida asingeweza kuamini, gari zaidi ya kumi za kifahari zilifika hiyo sehemu majira ya saa saba za mchana kweupe kabisa na kumchukua huyo mzee kwa heshima moja kubwa kama vile ni raisi alikuwa anapelekwa ikulu, watu wa hapo mtaani hakuna aliyeweza kukiamini hicho kitu baada ya miaka mingi ya kuishi hapo akijulikana kama mtu asiyekuwa na makazi leo anakuja kuchukuliwa na magari ya kifahari ambayo ndani ya nchi yalikuwa yanahesabika ni watu wachache sana waliokuwa na uwezo wa kuyamiliki. Ukiaachana na kuwashangaza huko wakati anaondoka alichukua begi lililo jaa pesa mpya kabisa alizirusha juu zote watu wakabaki wanagombaniana yeye akaondoka na msafara wake uliokuja kumfuata ndani ya Mburahati.
Ni miaka miwili sasa ilikuwa imepita tangu alipoweza kutembelewa na makamu wa raisi wa Tanzania mheshimiwa Hakram Hamad ambapo alipigwa risasi mbili za mguu na kupewa majukumu ya kuweza kumtafuta Timotheo Jordan ambaye ndiye alikuwa tageti kubwa sana ya huyo mzee kukipata kitu ambacho kilionekana kugombaniwa sana bila kujulikana kama ni nini na humo ndani kulikuwa na nini hasa mpaka watu hao watoe mpaka uhai wa watu ili kukipata hicho kitu, huyu ndiye yule mzee ambaye alitoa maagizo hayo kwa makamu wa raisi wa nchi ya Tanzania. Safari ya huyu mzee ilienda kuishia maeneo ya Chanika, huko ndiko alikokuwa anaishi yeye. Gari ziliingizwa kwenye geti lililo onekana kuwa la kawaida sana na mbele yake kulikuwa na nyumba ya kawaida tu, ilikuwa inashangaza sana kivipi mtu mwenye nyumba ya kawaida sana namna hii kuweza kumiliki magari ya kifahari sana namna hii, baada ya yeye kushuka tu magari yote yaliondoka hapo haraka hakukaa sana akachukua pikipiki iliyokuwa humo ndani akiwa na mtu mmoja tu ambaye alikuwa akimuendesha walitokea uwanja wa nyuma bila kuonekana na mtu yeyote. Waliishia kwenye sehemu yenye miti miti mingi kidogo hapo ndipo yalipokuwa makazi ya huyo mzee, ni jumba la kifahari sana kupita maelezo lililokuwa linaonekana hapo, aliingia ndani kujisafisha vizuri akiwa amekifunga chumba chake kila sehemu na hakuna mtu aliyekuwa anaruhusiwa kuingia huko, ilikuwa siri ya peke yake ndani ya chumba chake switch iliyokuwa ikitumika kuwashia umeme ukiibonyeza kwa kuishikilia kwa sekunde thelathini bila kupunguza wala kuzidisha ulikuwa ukifunguka mlango wa siri ambao ulikuwa unampeleka mpaka chumba cha chini sana ya ardhi ndani ya hiyo nyumba na ndicho alicho kifanya hapo ndani safari yake ikaanza ya kuelekea chini ya hicho chumba.
Macho yalitazama anga lote la nchi ya Tanzania baada ya kuutua mguu wake kwa mara ya kwanza ndani ya ardhi ya nchi yake ya kuzaliwa kwa miaka miwili sasa, Jamal hakufurahia sana kuwa hapa kwani alihisi yupo gizani bado kitu pekee ambacho alikuwa anakifikiria kwa huo muda ni kukutana na baba yake ili apaswe kujijua kiundani yeye ni nini hasa na ni majukumu gani ambayo anapaswa kuyafanya, alikuwa na maswali mengi sana Jamal wakati anatoka hapo Airport gari za kijeshi tatu zilikuwa zipo mbele yake zikimsubiri sasa alikuwa ni komando ambaye alikuwa chini ya mkuu wa majeshi ya nchi ya Tanzania. Spidi kali ya hizo gari safari yao ilienda kuishia maeneo ya LUGALO kwenye ofisi maalumu ambayo kwa wanajeshi wa kawaida walikuwa hawaruhusiwi kabisa kuingia ndani ya ofisi hiyo. Wale watu waliokuwa wamemfuata na gari walimuacha baada ya kumfikisha mlangoni alijua wazi kwamba alikuwa anatakiwa kuingia humo ndani.
Mbele yake mkuu wa majeshi alikuw amekaa kwenye kiti akiwa hana hata wasi wasi wowote ule akimwangalia mtu huyo kwani alikuwa akitarajio ujio wake kwa asilimia miamoja.
"Umekuwa mtu mzima sasa kijana wangu nina imani huko ulikotoka utakuwa umejifunza mambo mengi sana na huenda umefurahia sana maisha kwa kiasi chake" mkuu wa majeshi alitamka maneno kwa furaha akiwa ameipotezea salamu aliyopewa na kijana Jamal, mtu huyu ni kiongozi mkubwa sana kwenye nchi hata kuonekana kwake ilikuwa ni ngumu sana Jamal alikuwa anapata wasi wasi kivipi akutanishwe kirahisi sana na mtu mkubwa kaisi hicho bila kuwepo sababu za msingi?, hakuwa na jibu aliamua kuwa mpole.
"Ni kitu kimoja tu kimenifanya nifurahie kuwa kule japo hakuna mwanadamu atakuja kulijua hili, nimekuwa mwanadamu ambaye ninaishi kama mkiwa mzee wangu sielewi chochote, sina kumbu kumbu za maisha ya nyuma, baba yangu nikimuuliza mama yuko wapi hakuna jibu la maana analonipa. Kitu kinacho nifanya niogope sana ni kwanini mtu wa maisha ya kawaida kama mimi nitengenezwe sana kiasi hiki kana kwamba mimi ni mpigania uhuru wa nchi kitu ambacho sio kweli kabisa na hakiwezi kutokea nina imani sana juu ya hilo.
"Mimi sifurahii kwa sababu wewe umerudi hapana ila nina furahi kwa sababu nimetimiza ndoto ya mwanaume ambaye huenda saivi yupo anaipigania pumzi yake ya mwisho kwenye maisha yake, sina imani kama atakuwa na maisha marefu huyo mtu kwenye uso wa dunia hii, yeye ni kama mimi mwingine, yeye ndiye ndugu pekee ambaye mimi nimebakiwa naye kwenye huu ulimwengu kiufupi ni kwamba nampenda sana lakini naskitika sana kila nikiiona hali yake kitandani inanifanya natamani sana kulia. Sio rahisi mwanaume wa kazi kama yule kuwa kwenye kitanda kwa zaidi ya miezi mitatu akiwa hana hata uwezo wa kuamka, huyo ndiye aliyetamani sana wewe uwe hivyo ulivyokuwa sasa kazi yangu nusu nimemaliza nimebakisha nusu tu yakwako wewe hivyo mimi sina cha kukwambia kuhusu maisha yako zaidi huyo mtu ndiye atakaye kupa sababu ya msingi ya yeye kuhitaji wewe uwe hivyo, hatuna muda jiandae tunaondoka sasa hivi mimi nawewe". Maneno yaliyo onekana kumtoa machozi mkuu wa majeshi aliyatamka kwa simanzi na msisitizo mkubwa ambao hata Jamal ulimtisha haikuwa rahisi namna hiyo kuweza kumuona mwanaume wa shoka kama huyo anatoa machozi kirahisi sana namna hiyo alijua lazima kutakuwa na tatizo kubwa.
Ndiyo kwanza alikuwa ameingia nchini hata kupumzika alikuwa hajapumzika kabisa lakini alikuwa ameanza kukutana na mambo mazito siku yake ya kwanza tu kurudi, alitamani sana kuulizia alipo baba yake kabla ya kitu chochote alitamani sana kumuona mzee huyo ni miaka miwili sasa alikuwa amemkumbuka sana huyo mzee ila kwa hali aliyokuwa amemuona nayo mkuu wa majeshi hakuona sababu ya msingi ya kufanya hivyo ustaarabu uliichukua nafasi yake.
Walitoka humo ndani gari la kawaida tu lilitolewa hapo na muendeshaji alikuwa ni mkuu wa majeshi mwenyewe kofia kubwa aliyokuwa ameivaa kwenye kichwa chake ilimfanya kutojulikana bendera tu ya jeshi iliyokuwa kwenye upande wa dereva ndiyo iliyofanya gari hilo lisiweze kukaguliwa kwenye mageti yote mpaka wanafika nje kabisa ya kambi hiyo. Breki zilifungwa kwenye geti moja la bluu maeneo ya Bunju, nje hapakuwa na mtu hata mmoja, geti lilijifungua lenyewe gari ikaingizwa ndani na kwenda kupakiwa sehemu yake. Jamal alishuka ndani ya hilo gari alishangaa ndani ya huo uzio kuna wanajeshi wengi sana wenye mitutu mikubwa ya bunduki wakionekana kulilinda mno hilo eneo, wote waliokuwa eneo la mbele walitoa heshima ya saluti ambazo zilimfanya nayeye kuitikia ila alishtuka baada ya kugundua kwamba hazikuwa zakwake bali zilikuwa za mkuu wa majeshi yeye hakuna aliyekuwa anamjua mpaka muda huo.
Waliongoza mpaka humo ndani kwenye nyumba hiyo ya gorofa mbili, walipandisha ngazi mpaka chumba cha juu kabisa ,
"Khooooooo khoooooooooo" ni sauti ya kikohozi kikali sana ambacho kilisikika kuonyesha mtu aliyekuwa humo ndani hakuwa na hali nzuri sana ya kuridhisha kabisa, mlango ulifungunguliwa heshima kubwa ikafuata kwa mkuu wa majeshi ambaye hakuwa na muda nayo kabisa macho yake yalikuwa mbele tu. Jamal alikuwa bado ameganda mlangoni hakuelewa lengo la yeye kuletewa hiyo sehemu lakini akaamua kujikaza kuingia humo ndani ambapo alipotupa macho yake mbele aliona kitanda kikubwa cha wagonjwa kukiwa na mwili wa mtu umelazwa ukiwa umezungukwa na wanaume sita walio onekana kuwa madaktari, walikuwa wakiupigania sana uhai wa huyo binadamu ambaye alionekana ni lazima awe hai kwa gharama yoyote ile japokuwa walijua inapofikia hatua ya MUNGU kukihitaji kiumbe chake basi kunakuwa hakuna namna tena ya kuweza kuiokoa nafsi yake kwenye umauti. Pembeni ya hicho kitanda kulikuwa kuna kiti kimoja ambacho alikaa kijana mmoja aliyekuwa na uso wa simanzi sana macho akiwa ameyaelekeza alipokuwa amelala mwanaume mmoja wa makamo kidogo kwenye hicho kitanda, Jamal alijongea taratibu kusogea mahali ambapo palikuwa na hicho kitanda, tabasamu la kutosha lilionekana kupitia machoni pa mgonjwa ambaye alikuwa amelazwa hapo baada ya kumuona Jamal.
Ilikuwa ni tofauti kidogo kwa Jamal alishtuka sana kumuona mtu huyo, sura ya huyo mwanaume ilikuwa ni sura ya mkuu wa majeshi lakini cha ajabu mkuu wa majeshi alikuwa amekaa nyuma akiwa kajiinamia, sura zao hazikuwa na utofauti wowote ule na ilikuwa ni ngumu sana kuweza kuzitofautisha hizo sura mbili zilihitaji mtu mwenye kuwajua tabia za ndani sana za hao wanaume ili kuweza kuwaelewa.
"Imekuwa ni neema kwangu kukuona tena kabla sijaweza kwenda kutubu baadhi ya dhambi ambazo nimezifanya kwenye haya maisha nikiwa kama mwanadamu wa kawaida sana kwenye maisha yangu, mwanangu nina imani umekua sasa na unaweza kujisimamia mwenyewe bila hata uwepo wa mtu yeyote yule duniani" mzee huyo aliongea akiwa ananyanyuka hapo kitandani baada ya kuchomwa sindano ya kuongeza nguvu kidogo kwa muda flani, maelezo yake yalimuacha Jamal kwenye kitendawili kizito sana hakuelewa kivipi mzee huyo amwite yeye mwanae hakuwahi kukutana naye kabisa zaidi ya kuhisi kwamba atakuwa ni ndugu wa mkuu wa majeshi kwa namna walivyokuwa wamefanana. Mzee huyo hata hakuhangaika kabisa na Jamal aliwapa ishara watu wote waweze kuondoka na kuwaacha wao wawili tu humo ndani, baada ya watu wote waliokuwa humo ndani kutoka alijikongoja na kwenda kuubana mlango akiwa anatembea kwa kuchechemea akiwa anakohoa, uimara wa mwili wake ndio uliokuwa unamfanya mpaka huo muda aweze hata kusimama kwa mtu goi goi kwa hali aliyokuwa nayo asingeweza hata kunyanyuka pale kitandani.
14 naweka kalamu chini tukutane sehemu inayofuata
Bux the story teller.
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA KUMI NA TANO
TULIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE.........
Mzee huyo hata hakuhangaika kabisa na Jamal aliwapa ishara watu wote waweze kuondoka na kuwaacha wao wawili tu humo ndani, baada ya watu wote waliokuwa humo ndani kutoka alijikongoja na kwenda kuubana mlango akiwa anatembea kwa kuchechemea akiwa anakohoa, uimara wa mwili wake ndio uliokuwa unamfanya mpaka huo muda aweze hata kusimama kwa mtu goi goi kwa hali aliyokuwa nayo asingeweza hata kunyanyuka pale kitandani.
ENDELEA................
“Baba kipi kimekukuta mpaka upo kwenye hiyo hali” sauti iliyokuwa nzito sana kwa sasa iliyo onyesha amekuwa mwanaume sasa kutoka kwa Jamal ndiyo iliyoweza kumshtua mzee huyu aliyekuwa akionekana kwa kila kitu kama mkuu wa majeshi ya nchi ya Tanzania, alishangaa bwana mdogo kamjuaje kwenye hiyo hali ambayo hakuna mwanadamu yeyote yule ambaye angeweza kumtambua kabisa isipokuwa ndugu yake tu mkuu wa majeshi.
“Umeweza vipi kunitambua nikiwa kwenye sura yangu halisia namna hii?” baba yake afahamikaye kwa jina la David au Daud Hauston ila kwa upande wa pili alikuwa akijulikana kama Timotheo Jordan ni upande wake wa siri mno ambao ni wanadamu wachache sana walikuwa wanaujua.
“Hakuna mwanadamu anaye kujua kwa usahihi kama mimi kwenye maisha haya, naijua harufu ya jasho lako, ninaweza kujua mapigo yako ya moyo yasipokuwa sawa hata hatua za kunyata za miguu yako nazijua na kuzikumbuka kuliko hata jina langu, nimeishi na kulala nawewe kitanda kimoja kama baba yangu kwenye kitanda kimoja hivyo nakujua kwa usahihi sana japokuwa nilijidanganya kuhusu kitu kimoja nilidhani hata maisha yako nayajua vizuri ila naanza kuona kabisa hakuna ninacho kijua kwenye maisha yako kwani wewe ni nani baba?” Jamal alimuuliza mzee wake huyo ambaye kwa upande wake alimjua kama baba yake mzazi kabisa wa kumzaa alirudi kitandani akakaa kwa kuegemea ukuta, hakutaka kuonekana dhaifu mbele ya kijana wake alikuwa anajikaza kwa mtu ambaye angefika hapo kama angeambiwa huyo mtu yupo kwenye hali mbaya sana ingekuwa ni ngumu kwa jinsi alivyokuwa anaongea ila kiuhalisia alikuwa anazihesabu siku zake za kuendelea kuishi kwenye huu ulimwengu.
“Jamal unaniamini mimi baba yako?” swali kutoka kwa David Hauston lilimshtua Jamal hakuelewa linamaanisha nini.
“Wewe ndiye binadamu pekee ambaye mimi nakuamini sana kwenye maisha yangu ukizingatia sina mtu mwingine yeyote yule ambaye mimi nipo naye kwenye upande wangu zaidi ya wewe hapo” Jamal alikuwa akijibu akiwa kwenye simanzi kwa hali aliyo mkuta nayo mzee huyo ilikuwa inasikitisha sana alitamani amuulize haraka kwamba ni kitu gani kimemkuta ikiwa ni miaka miwili tu pekee imepita tangu yeye aondoke ila kila kitu kilionekana kubadilika ndani ya huo muda.
“Mimi siyo baba yako mzazi” David Hauxton aliitamka hii kauli akiwa na macho makavu kabisa ambayo hayakuwa hata na tone la wasi wasi mbele yake.
“Baba naomba upumzike nitakuja baadae tuongee naona huo ugonjwa unaanza kukupelekea pabaya sana inaniuma sana kukuona kwenye hiyo hali, tafadhali nitahangaika kumtafuta daktari bora sana duniani aje kukutibu ila sio kuanza kuongea mambo ambayo hayaeleweki mbele yangu” Jamal wazo lake la kwanza alijua mtu huyo ni ugonjwa umemzidia ndio maana yupo kwenye hiyo hali alicho kisikia kwenye masikio yake hakikuwa sahihi kabisa kwa upande wake, ilimuuma sana kumuona baba yake kwenye hali kama hiyo hakutaka tena kuendelea kukaa hapo alihitaji kwenda kuhangaika kumtafutia madaktari bingwa ili waje kuitetea nafsi ya binadamu ambaye ndiye pekee aliyekuwa amebakia kwenye upande wake mpaka sasa.
“Janson Malisaba ndilo jina la baba yako” Sauti ambayo haikuwa na kitetemeshi chochote ilisikika vyema kwenye maskio ya Jamal, aligeuka kwa kuhamaki.
“whaaaaaaaaaaaaaaaaaaaat?” ni mshangao mkubwa alioutoa, hivyo vitu aliwahi kuvisikia vikionekana kwenye tamthilia tu pekee hakuwahi kuwa na imani kama vinaweza kutokea kwenye maisha ya kweli, alijipiga kibao kuona kama alikuwa ndotoni na huenda angeweza kuamka lakini haikuwa kweli hata kidogo alichokuwa anakiona na kukisikia ndio ulikuwa uhalisia wenyewe.
“Mimi sio baba yako mzazi wala sina undugu wowote nawewe namimi sijawahi kabisa kuwa na familia” kauli ya mzee huyu ilimfanya Jamal apate hata kitete cha kutembea wakati huo alikuwa ameshafika kwenye mlango akihitaji kutoweka, mwili ulikufa ganzi hakuwahi kufikiria kama kuna wanadamu wana siri za kufanya mambo ya ndotoni kama haya kuonekana kuwa ya kweli.
“Kivipi baba mbona sikuelewi wewe sio ndugu yangu how(kivipi)? And who are you (na wewe ni nani)” Jamal aliuliza akiwa kama amechanganyikiwa maisha yake yote yalikuwa kama mtu aliye ishi kwenye mchezo fulani ambao hata yeye mwenyewe hakuuelewa unachezwaje.
“kuanzia sasa sina imani kama nitamaliza hata masaa ishirini na manne ya kuendelea kuwa hai, mwili wangu umezoofishwa sana na baadhi ya walimwengu ambao dunia wameiweka kwenye viganja vyao, hawaogopi chochote na kibaya ndo watu wenye pesa na nguvu kubwa za mamlaka ndani ya nchi hii, kuwajua hawa watu inachukua mamia ya maisha ya watu na bado imekuwa ni vigumu sana kwa sababu watu wao wengine tupo tunaishi nao ila kabla sijaweza kwenda kupumzika na kuyatumikia malipo ya yale niliyo yatenda hapa duniani nahitaji wewe kwanza ujijue ni nani kwa sababu hapo ulipo hakuna unacho kijua chochote kwenye huu ulimwengu kuhusu maisha yako, khohoooooooooooo khoooooooo” kikohozi kikali sana kilimtoka huyo mzee baada ya kuongea maneno hayo machache, Jamal alikuwa amepigwa na bumbuwazi alitamani sana ajue hicho kitu ambacho kilisemekana ni mhimu sana kwenye maisha yake, alishikwa na kigugumizi hakuelewa cha kufanya, mawazo makali yalikuwa yanakivuruga kichwa chake asielewe anayapanga vipi lakini kwa mzee wake alitabasamu sana baada ya kuangalia kifuani kwa Jamal na kukiona kile kidani ambacho alimpatia kipo kama kilivyo.
“Nenda kalale kwenye kile kitanda pale” Sauti ya baba yake ambaye kwa sasa alikuwa anamkataa ndiyo iliyo mshtua kwenye dimbwi zito la mawazo mpaka muda huo hata ungemuuliza jina lake asingeweza kulikumbuka, mzazi ndicho kitu pekee ambacho kila mtoto huwa anajidai nacho sana popote pale anapokuwa kukataliwa na mtu aliye mjua ndiye baba yake ilimuuma sana japo hakuweza kubadili kitu chochote. Alienda taratibu akiwa hajiamini tena kwenye maisha yake mtu aliyempenda sana na kumjali kwa kila kitu leo alikuwa anamkataa kwamba hakuwa baba yake wala hana undugu nae wowote. Jamal alielekezwa avue nguo zote abaki kama yeye mwenyewe alivyozaliwa, hakuwa mbishi kwa sababu mtu aliyekuwa anampa hayo maagizo ndiye binadamu aliyekuwa akimheshimu kuliko mtu yeyote yule hapa duniani, alipandisha kwenye hicho kitanda ambacho kilikuwa kimetengwa upande wake pembeni kikizungukwa na komputa kubwa sita, baada ya kupanda hapo kitanda kilijiinua chenyewe vikatokea vioo vikubwa sana na kukiziba hicho kitanda mtu wa nje pekee ndiye aliyekuwa ana uwezo wa kuona kilichopo ndani ya kitanda ila kwa ambaye alikuwa ndani ya hivyo vioo hakuwa na uwezo wa kuona kilichokuwa kinaendelea nje.
Hicho hakikuwa kitanda cha kawaida kama kilivyokuwa kinaonekana bali ilikuwa ni mashine ya kisasa ya kuweza kumrudishia mtu kumbu kumbu zake, Jamal alipoteza kumbu kumbu? Kivipi?
“Kwenye ghorofa moja kubwa sana maeneo ya mikocheni ambalo lilikuwa halijamalizika kujengwa likiwa lipo pembeni ya hoteli moja nzuri sana, juu ya hilo ghorofa lilikuwa linaonekana dirisha moja likiwa lipo wazi kabisa, ndani ya hilo dirisha kuna mwanaume alikuwa anaifunga bunduki yake ya masaafa marefu kwa usahihi akiwa anaiangalia saa yake kwa umakini mkubwa mno, alionekana kuwa anahitajika kuifanya kazi yake kwa muda mwafaka kabisa na kutoweka kwenye hilo eneo. Kwenye chumba kimoja cha hiyo hoteli kubwa ambayo ilikuwa inachangamka sana siku za wikiendi ndani ya hiyo hoteli alikuwa anaonekana Ashrafu Hamad kwenye chumba kimoja akiwa na mwanamke mmoja mrembo sana, hakukuwa na kingine kwenye chumba alichokuwa yupo na huyo mtoto wa kike zaidi ya mahaba ambayo yanadaiwa kuuendesha sana ulimwengu.
Ni wazi watu hao walikuwa wanatamaniana sana kwenye kitanda kikubwa sana kilicho wafanya waweze kuifurahia dunia hiyo kwa ukubwa wake bila kuwa na wasi wasi na kitu chochote kile. Saa mbili kamili za usiku ndio muda ambao walikuwa wanamaliza shughuli nzito juu ya kitanda, walichukua taulo zao wakiwa wamekumbatiana na kutoka kwenye hicho chumba, ilichukuliwa lift iliyo wasaidia kufika chini kwa uharaka mkubwa. walikuwa wanaelekea kuogelea kwenye moja ya mabwawa mazuri sana yaliyokuwa ndani ya hoteli hiyo, wakati huo mwanaume aliyekuwa amesimama kwenye lile ghorofa ambalo lilikuwa bado linajengwa kwa wakati huo aliitazama tena saa yake kisha akainyanyua bunduki yake ya masaafa marefu na kuiweka vyema kwenye dirisha lililokuwa mbele yake, lenzi ndicho kilichokuwa kitu mhimu zaidi kwake, aliizungusha kwa usahihi sana akiwa anaielekezea kwenye bwawa la ile hoteli ambayo ilikuwa ipo pembeni ya lile jengo, hakuhitaji kutumia risasi zake nyingi sana huwa anatumia risasi mbili tu pekee pindi anapo ishika bunduki yake, ni mtu hatari sana, ni moja ya wadunguaji wa kuogopwa mno ambaye nchi ilikuwa inamtafuta kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu kupotea kwake gerezani.
Alexander ndiye mwanaume aliyekuwa ameishika hiyo silaha, ni miaka miwili sasa imepita anaonekana uraiani na alikuwa amefungwa ndani ya gereza la segerea. Alibinya jicho lake moja kwa mahesabu makali sana kisha zikaachiwa risasi mbili kwa haraka kubwa ya kutisha, bunduki za wadunguaji huwa zinachukua muda wa sekunde tano mpaka kumi na tano ili kuiruhusu risasi nyingine kutoka tena lakini kwake ilikuwa ni tofauti kidogo alikuwa na silaha yenye uwezo mkubwa sana risasi zilikuwa zikipishana kwa sekunde moja tu pekee. Ashrafu Hakim akiwa na mwanamke wake kwenye maji risasi ya kwanza ilizama kwenye paji la uso wake hakuweza hata kupiga kelele ni kwa muda mfupi nyingine ilizama pale pale taratibu akawa anashuka kwenye maji damu zikianza kutapakaa kwenye maji, dakika moja baada ya kuisha ndipo yule mwanamke aliyekuwa naye alipogundua kwamba Ashrafu alikuwa amepigwa risasi, alipiga makelele makubwa sana yaliyo washtua watu wakaanza kukimbia hovyo huku vyombo vya usalama ndani ya hiyo hoteli vikianza kusogea haraka sana kuweza kujua tatizo kubwa hasa ni nini lakini Ashraf Hamad hakuwa miongoni mwa wanadamu ambao walibahatika kuwa hai tena.
Mwanaume baada ya kuimaliza kazi yake alifunga vitu vyake haraka akavaa kofia lake kubwa akiwa na koti refu sana la kijivu alikuwa akishuka taratibu mno bila wasi wasi wowote ule kama vile ametoka kufanya biashara kumbe alikuwa ametoka kumuua binadamu mwenzake. Alitembea taratibu kuwahi kwenye gari yake aliyokuwa ameipaki chini kabisa, wakati anakaribia mahali alipokuwa ameipaki gari yake alipigwa mtama na mwanaume aliye onekana kukomaa vyema kwenye mwili wake, ni uimara wake ndio ulio mfanya asiweze kudondoka chini alijirusha kwa sarakasi mguu mmoja akaugusisha kwenye gari akasimama vizuri bila wasi wasi na begi lake kubwa lenye silaha likiwa mkononi mwake.
“Kakutuma nani uje kufanya mauaji kwa huyu mtoto?” swali kutoka kwa moja ya wanaume watatu ambao walikuwa wapo pembeni yake lilisikika vyema kwenye masikio yake, aliiangalia saa yake vizuri muda wake haukumruhusu kuendelea kuwepo hiyo sehemu.
“Nitafute siku nyingine kama una shida ya kuongea namimi nimeshamaliza kazi yangu hivyo sitaki usumbufu kwa sasa sina muda wa kuendelea kukaa hapa kwa leo” alisisitiza kwa sauti yake nzito sana, buti kali lilimpuliza usoni baada ya kujibu jeuri mmoja wa wale wanaume alikuwa amemfikia Alexander ambaye hakuweza kuliachia begi lake lililokuwa na silaha ndani yake, alimrushia yule mwanaume lile begi wakati analidaka alikuwa amesahamfikia alilipiga begi lake teke kali lililo lifanya begi hilo kurushwa juu sana huku akimshindilia mwanaume huyo aliyekuwa amelidaka begi lake teke zito lililo mpeleka mbali sana, wenzake walikuwa wanakuja kwa kasi sana wakiwa wanawahi kumshambulia Alexander, mkono wake mmoja ulilidaka begi lake lenye silaha, mkono mwingile ulitoa kitu kizito sana ambacho baada ya kukibonyeza kilitoa sauti nzito mno na moshi mwingi uliokuwa unaumiza macho yao iliwalazimu kufumba macho pamoja na kuziba masikio, dakika moja moshi ulikuwa umeisha na sauti haikuwepo tena lakini walipo jaribu kuangaza huku na huko hawakuona mtu yeyote wala gari lililokuwa hapo halikuonekana mwanaume alikuwa amesha potea muda mrefu sana. watu walianza kusika wakija upande huo baada ya kuona moshi mwingi ghafla iliwabidi nao kuondoka hiyo sehemu haraka.
Jamal ni kweli alipoteza kumbu kumbu na kama ni kweli alipotezaje na huyu mzee kajuaje? kweli Ashrafu Hamad maarufu kama omba omba wa Buguruni ndo kafa kirahisi sana namna hii?.....15 naweka nukta endelea kunifuatilia kwa umakini uweze kuuelewa mchezo wa akili huu ambao huenda mpaka sasa bado haujauelewa vizuri usipanic utaloose confidence.
Bux the story teller