I want to die a judge

I want to die a judge

STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA KUMI NA NNE

TULIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU..........

maneno matamu sana ya majonzi yalikuwa yakimtoka Catherine alikuwa anaumia sana kutengana na mwanaume aliyekiri kuwa wa maisha yake. Mwanaume alimkumbatia kwa mahaba na kumpiga busu zito sana la hisia wakati huo kuna gari ilikuwa inamsubiri aliondoka huku akikimbia mkono ulikuwa juu akimpungia Catherine mkono wa kwaheri.

ENDELEA...................

"Aise ndugu yangu wanadamu wasiri sana huyu mzee tumeishi naye Kwa muda wote hapa akituzuga kumbe mwenzetu yupo kwenye dunia yake kabisa hivi umeona msafara ambao umekuja kumchukua hapa saivi?"
"Mhhhh maisha yamepiga hatua sana siku hizi wanadamu hatuaminiki tena tunabadilika mno, yule mzee mimi nilikuwa nina wasi wasi nae sana haiwezekani mshona viatu asiye na sehemu ya kulala aweze kunawiri namna ile nilikuwa namshangaa sana lakini hakuwahi kuonyesha dalili yoyote ile kuwa mtu mwenye vyake hii inaniogopesha sana kuwaamini wanadamu usije ukashangaa hata wewe kesho hapo naambiwa ni usalama wa taifa sitashangaa tena wanadamu siku hizi tunatisha sana"

"Usipende kujitoa kwenye listi kama vile wewe sio mwanadamu mwenzetu, nina imani atakuwa mpelelezi yule mzee sio bure hapa mtaani kaacha gumzo kubwa sana sikuwahi kutegemea kabisa leo hii mbona nimekoma mimi ama kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa ngoja nikalale sina hata hamu ya kutembea wala kuzunguka tena hapa mtaani naogopa" walikuwa ni vijana wawili maeneo ya Mburahati waliokuwa wanapiga stori kumhusu mzee mmoja fundi wa viatu ambaye alikuwa ameacha gumzo hapo mtaani. Kazi yake na kilichokuwa kimetokea hapo vilikuwa ni vitu ambavyo kwa mwanadamu yeyote wa kawaida asingeweza kuamini, gari zaidi ya kumi za kifahari zilifika hiyo sehemu majira ya saa saba za mchana kweupe kabisa na kumchukua huyo mzee kwa heshima moja kubwa kama vile ni raisi alikuwa anapelekwa ikulu, watu wa hapo mtaani hakuna aliyeweza kukiamini hicho kitu baada ya miaka mingi ya kuishi hapo akijulikana kama mtu asiyekuwa na makazi leo anakuja kuchukuliwa na magari ya kifahari ambayo ndani ya nchi yalikuwa yanahesabika ni watu wachache sana waliokuwa na uwezo wa kuyamiliki. Ukiaachana na kuwashangaza huko wakati anaondoka alichukua begi lililo jaa pesa mpya kabisa alizirusha juu zote watu wakabaki wanagombaniana yeye akaondoka na msafara wake uliokuja kumfuata ndani ya Mburahati.

Ni miaka miwili sasa ilikuwa imepita tangu alipoweza kutembelewa na makamu wa raisi wa Tanzania mheshimiwa Hakram Hamad ambapo alipigwa risasi mbili za mguu na kupewa majukumu ya kuweza kumtafuta Timotheo Jordan ambaye ndiye alikuwa tageti kubwa sana ya huyo mzee kukipata kitu ambacho kilionekana kugombaniwa sana bila kujulikana kama ni nini na humo ndani kulikuwa na nini hasa mpaka watu hao watoe mpaka uhai wa watu ili kukipata hicho kitu, huyu ndiye yule mzee ambaye alitoa maagizo hayo kwa makamu wa raisi wa nchi ya Tanzania. Safari ya huyu mzee ilienda kuishia maeneo ya Chanika, huko ndiko alikokuwa anaishi yeye. Gari ziliingizwa kwenye geti lililo onekana kuwa la kawaida sana na mbele yake kulikuwa na nyumba ya kawaida tu, ilikuwa inashangaza sana kivipi mtu mwenye nyumba ya kawaida sana namna hii kuweza kumiliki magari ya kifahari sana namna hii, baada ya yeye kushuka tu magari yote yaliondoka hapo haraka hakukaa sana akachukua pikipiki iliyokuwa humo ndani akiwa na mtu mmoja tu ambaye alikuwa akimuendesha walitokea uwanja wa nyuma bila kuonekana na mtu yeyote. Waliishia kwenye sehemu yenye miti miti mingi kidogo hapo ndipo yalipokuwa makazi ya huyo mzee, ni jumba la kifahari sana kupita maelezo lililokuwa linaonekana hapo, aliingia ndani kujisafisha vizuri akiwa amekifunga chumba chake kila sehemu na hakuna mtu aliyekuwa anaruhusiwa kuingia huko, ilikuwa siri ya peke yake ndani ya chumba chake switch iliyokuwa ikitumika kuwashia umeme ukiibonyeza kwa kuishikilia kwa sekunde thelathini bila kupunguza wala kuzidisha ulikuwa ukifunguka mlango wa siri ambao ulikuwa unampeleka mpaka chumba cha chini sana ya ardhi ndani ya hiyo nyumba na ndicho alicho kifanya hapo ndani safari yake ikaanza ya kuelekea chini ya hicho chumba.

Macho yalitazama anga lote la nchi ya Tanzania baada ya kuutua mguu wake kwa mara ya kwanza ndani ya ardhi ya nchi yake ya kuzaliwa kwa miaka miwili sasa, Jamal hakufurahia sana kuwa hapa kwani alihisi yupo gizani bado kitu pekee ambacho alikuwa anakifikiria kwa huo muda ni kukutana na baba yake ili apaswe kujijua kiundani yeye ni nini hasa na ni majukumu gani ambayo anapaswa kuyafanya, alikuwa na maswali mengi sana Jamal wakati anatoka hapo Airport gari za kijeshi tatu zilikuwa zipo mbele yake zikimsubiri sasa alikuwa ni komando ambaye alikuwa chini ya mkuu wa majeshi ya nchi ya Tanzania. Spidi kali ya hizo gari safari yao ilienda kuishia maeneo ya LUGALO kwenye ofisi maalumu ambayo kwa wanajeshi wa kawaida walikuwa hawaruhusiwi kabisa kuingia ndani ya ofisi hiyo. Wale watu waliokuwa wamemfuata na gari walimuacha baada ya kumfikisha mlangoni alijua wazi kwamba alikuwa anatakiwa kuingia humo ndani.

Mbele yake mkuu wa majeshi alikuw amekaa kwenye kiti akiwa hana hata wasi wasi wowote ule akimwangalia mtu huyo kwani alikuwa akitarajio ujio wake kwa asilimia miamoja.

"Umekuwa mtu mzima sasa kijana wangu nina imani huko ulikotoka utakuwa umejifunza mambo mengi sana na huenda umefurahia sana maisha kwa kiasi chake" mkuu wa majeshi alitamka maneno kwa furaha akiwa ameipotezea salamu aliyopewa na kijana Jamal, mtu huyu ni kiongozi mkubwa sana kwenye nchi hata kuonekana kwake ilikuwa ni ngumu sana Jamal alikuwa anapata wasi wasi kivipi akutanishwe kirahisi sana na mtu mkubwa kaisi hicho bila kuwepo sababu za msingi?, hakuwa na jibu aliamua kuwa mpole.

"Ni kitu kimoja tu kimenifanya nifurahie kuwa kule japo hakuna mwanadamu atakuja kulijua hili, nimekuwa mwanadamu ambaye ninaishi kama mkiwa mzee wangu sielewi chochote, sina kumbu kumbu za maisha ya nyuma, baba yangu nikimuuliza mama yuko wapi hakuna jibu la maana analonipa. Kitu kinacho nifanya niogope sana ni kwanini mtu wa maisha ya kawaida kama mimi nitengenezwe sana kiasi hiki kana kwamba mimi ni mpigania uhuru wa nchi kitu ambacho sio kweli kabisa na hakiwezi kutokea nina imani sana juu ya hilo.

"Mimi sifurahii kwa sababu wewe umerudi hapana ila nina furahi kwa sababu nimetimiza ndoto ya mwanaume ambaye huenda saivi yupo anaipigania pumzi yake ya mwisho kwenye maisha yake, sina imani kama atakuwa na maisha marefu huyo mtu kwenye uso wa dunia hii, yeye ni kama mimi mwingine, yeye ndiye ndugu pekee ambaye mimi nimebakiwa naye kwenye huu ulimwengu kiufupi ni kwamba nampenda sana lakini naskitika sana kila nikiiona hali yake kitandani inanifanya natamani sana kulia. Sio rahisi mwanaume wa kazi kama yule kuwa kwenye kitanda kwa zaidi ya miezi mitatu akiwa hana hata uwezo wa kuamka, huyo ndiye aliyetamani sana wewe uwe hivyo ulivyokuwa sasa kazi yangu nusu nimemaliza nimebakisha nusu tu yakwako wewe hivyo mimi sina cha kukwambia kuhusu maisha yako zaidi huyo mtu ndiye atakaye kupa sababu ya msingi ya yeye kuhitaji wewe uwe hivyo, hatuna muda jiandae tunaondoka sasa hivi mimi nawewe". Maneno yaliyo onekana kumtoa machozi mkuu wa majeshi aliyatamka kwa simanzi na msisitizo mkubwa ambao hata Jamal ulimtisha haikuwa rahisi namna hiyo kuweza kumuona mwanaume wa shoka kama huyo anatoa machozi kirahisi sana namna hiyo alijua lazima kutakuwa na tatizo kubwa.

Ndiyo kwanza alikuwa ameingia nchini hata kupumzika alikuwa hajapumzika kabisa lakini alikuwa ameanza kukutana na mambo mazito siku yake ya kwanza tu kurudi, alitamani sana kuulizia alipo baba yake kabla ya kitu chochote alitamani sana kumuona mzee huyo ni miaka miwili sasa alikuwa amemkumbuka sana huyo mzee ila kwa hali aliyokuwa amemuona nayo mkuu wa majeshi hakuona sababu ya msingi ya kufanya hivyo ustaarabu uliichukua nafasi yake.

Walitoka humo ndani gari la kawaida tu lilitolewa hapo na muendeshaji alikuwa ni mkuu wa majeshi mwenyewe kofia kubwa aliyokuwa ameivaa kwenye kichwa chake ilimfanya kutojulikana bendera tu ya jeshi iliyokuwa kwenye upande wa dereva ndiyo iliyofanya gari hilo lisiweze kukaguliwa kwenye mageti yote mpaka wanafika nje kabisa ya kambi hiyo. Breki zilifungwa kwenye geti moja la bluu maeneo ya Bunju, nje hapakuwa na mtu hata mmoja, geti lilijifungua lenyewe gari ikaingizwa ndani na kwenda kupakiwa sehemu yake. Jamal alishuka ndani ya hilo gari alishangaa ndani ya huo uzio kuna wanajeshi wengi sana wenye mitutu mikubwa ya bunduki wakionekana kulilinda mno hilo eneo, wote waliokuwa eneo la mbele walitoa heshima ya saluti ambazo zilimfanya nayeye kuitikia ila alishtuka baada ya kugundua kwamba hazikuwa zakwake bali zilikuwa za mkuu wa majeshi yeye hakuna aliyekuwa anamjua mpaka muda huo.

Waliongoza mpaka humo ndani kwenye nyumba hiyo ya gorofa mbili, walipandisha ngazi mpaka chumba cha juu kabisa ,

"Khooooooo khoooooooooo" ni sauti ya kikohozi kikali sana ambacho kilisikika kuonyesha mtu aliyekuwa humo ndani hakuwa na hali nzuri sana ya kuridhisha kabisa, mlango ulifungunguliwa heshima kubwa ikafuata kwa mkuu wa majeshi ambaye hakuwa na muda nayo kabisa macho yake yalikuwa mbele tu. Jamal alikuwa bado ameganda mlangoni hakuelewa lengo la yeye kuletewa hiyo sehemu lakini akaamua kujikaza kuingia humo ndani ambapo alipotupa macho yake mbele aliona kitanda kikubwa cha wagonjwa kukiwa na mwili wa mtu umelazwa ukiwa umezungukwa na wanaume sita walio onekana kuwa madaktari, walikuwa wakiupigania sana uhai wa huyo binadamu ambaye alionekana ni lazima awe hai kwa gharama yoyote ile japokuwa walijua inapofikia hatua ya MUNGU kukihitaji kiumbe chake basi kunakuwa hakuna namna tena ya kuweza kuiokoa nafsi yake kwenye umauti. Pembeni ya hicho kitanda kulikuwa kuna kiti kimoja ambacho alikaa kijana mmoja aliyekuwa na uso wa simanzi sana macho akiwa ameyaelekeza alipokuwa amelala mwanaume mmoja wa makamo kidogo kwenye hicho kitanda, Jamal alijongea taratibu kusogea mahali ambapo palikuwa na hicho kitanda, tabasamu la kutosha lilionekana kupitia machoni pa mgonjwa ambaye alikuwa amelazwa hapo baada ya kumuona Jamal.

Ilikuwa ni tofauti kidogo kwa Jamal alishtuka sana kumuona mtu huyo, sura ya huyo mwanaume ilikuwa ni sura ya mkuu wa majeshi lakini cha ajabu mkuu wa majeshi alikuwa amekaa nyuma akiwa kajiinamia, sura zao hazikuwa na utofauti wowote ule na ilikuwa ni ngumu sana kuweza kuzitofautisha hizo sura mbili zilihitaji mtu mwenye kuwajua tabia za ndani sana za hao wanaume ili kuweza kuwaelewa.

"Imekuwa ni neema kwangu kukuona tena kabla sijaweza kwenda kutubu baadhi ya dhambi ambazo nimezifanya kwenye haya maisha nikiwa kama mwanadamu wa kawaida sana kwenye maisha yangu, mwanangu nina imani umekua sasa na unaweza kujisimamia mwenyewe bila hata uwepo wa mtu yeyote yule duniani" mzee huyo aliongea akiwa ananyanyuka hapo kitandani baada ya kuchomwa sindano ya kuongeza nguvu kidogo kwa muda flani, maelezo yake yalimuacha Jamal kwenye kitendawili kizito sana hakuelewa kivipi mzee huyo amwite yeye mwanae hakuwahi kukutana naye kabisa zaidi ya kuhisi kwamba atakuwa ni ndugu wa mkuu wa majeshi kwa namna walivyokuwa wamefanana. Mzee huyo hata hakuhangaika kabisa na Jamal aliwapa ishara watu wote waweze kuondoka na kuwaacha wao wawili tu humo ndani, baada ya watu wote waliokuwa humo ndani kutoka alijikongoja na kwenda kuubana mlango akiwa anatembea kwa kuchechemea akiwa anakohoa, uimara wa mwili wake ndio uliokuwa unamfanya mpaka huo muda aweze hata kusimama kwa mtu goi goi kwa hali aliyokuwa nayo asingeweza hata kunyanyuka pale kitandani.

14 naweka kalamu chini tukutane sehemu inayofuata

Bux the story teller.

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
TORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA KUMI NA TANO

TULIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE.........

Mzee huyo hata hakuhangaika kabisa na Jamal aliwapa ishara watu wote waweze kuondoka na kuwaacha wao wawili tu humo ndani, baada ya watu wote waliokuwa humo ndani kutoka alijikongoja na kwenda kuubana mlango akiwa anatembea kwa kuchechemea akiwa anakohoa, uimara wa mwili wake ndio uliokuwa unamfanya mpaka huo muda aweze hata kusimama kwa mtu goi goi kwa hali aliyokuwa nayo asingeweza hata kunyanyuka pale kitandani.

ENDELEA................

“Baba kipi kimekukuta mpaka upo kwenye hiyo hali” sauti iliyokuwa nzito sana kwa sasa iliyo onyesha amekuwa mwanaume sasa kutoka kwa Jamal ndiyo iliyoweza kumshtua mzee huyu aliyekuwa akionekana kwa kila kitu kama mkuu wa majeshi ya nchi ya Tanzania, alishangaa bwana mdogo kamjuaje kwenye hiyo hali ambayo hakuna mwanadamu yeyote yule ambaye angeweza kumtambua kabisa isipokuwa ndugu yake tu mkuu wa majeshi.

“Umeweza vipi kunitambua nikiwa kwenye sura yangu halisia namna hii?” baba yake afahamikaye kwa jina la David au Daud Hauston ila kwa upande wa pili alikuwa akijulikana kama Timotheo Jordan ni upande wake wa siri mno ambao ni wanadamu wachache sana walikuwa wanaujua.

“Hakuna mwanadamu anaye kujua kwa usahihi kama mimi kwenye maisha haya, naijua harufu ya jasho lako, ninaweza kujua mapigo yako ya moyo yasipokuwa sawa hata hatua za kunyata za miguu yako nazijua na kuzikumbuka kuliko hata jina langu, nimeishi na kulala nawewe kitanda kimoja kama baba yangu kwenye kitanda kimoja hivyo nakujua kwa usahihi sana japokuwa nilijidanganya kuhusu kitu kimoja nilidhani hata maisha yako nayajua vizuri ila naanza kuona kabisa hakuna ninacho kijua kwenye maisha yako kwani wewe ni nani baba?” Jamal alimuuliza mzee wake huyo ambaye kwa upande wake alimjua kama baba yake mzazi kabisa wa kumzaa alirudi kitandani akakaa kwa kuegemea ukuta, hakutaka kuonekana dhaifu mbele ya kijana wake alikuwa anajikaza kwa mtu ambaye angefika hapo kama angeambiwa huyo mtu yupo kwenye hali mbaya sana ingekuwa ni ngumu kwa jinsi alivyokuwa anaongea ila kiuhalisia alikuwa anazihesabu siku zake za kuendelea kuishi kwenye huu ulimwengu.

“Jamal unaniamini mimi baba yako?” swali kutoka kwa David Hauston lilimshtua Jamal hakuelewa linamaanisha nini.

“Wewe ndiye binadamu pekee ambaye mimi nakuamini sana kwenye maisha yangu ukizingatia sina mtu mwingine yeyote yule ambaye mimi nipo naye kwenye upande wangu zaidi ya wewe hapo” Jamal alikuwa akijibu akiwa kwenye simanzi kwa hali aliyo mkuta nayo mzee huyo ilikuwa inasikitisha sana alitamani amuulize haraka kwamba ni kitu gani kimemkuta ikiwa ni miaka miwili tu pekee imepita tangu yeye aondoke ila kila kitu kilionekana kubadilika ndani ya huo muda.

“Mimi siyo baba yako mzazi” David Hauxton aliitamka hii kauli akiwa na macho makavu kabisa ambayo hayakuwa hata na tone la wasi wasi mbele yake.

“Baba naomba upumzike nitakuja baadae tuongee naona huo ugonjwa unaanza kukupelekea pabaya sana inaniuma sana kukuona kwenye hiyo hali, tafadhali nitahangaika kumtafuta daktari bora sana duniani aje kukutibu ila sio kuanza kuongea mambo ambayo hayaeleweki mbele yangu” Jamal wazo lake la kwanza alijua mtu huyo ni ugonjwa umemzidia ndio maana yupo kwenye hiyo hali alicho kisikia kwenye masikio yake hakikuwa sahihi kabisa kwa upande wake, ilimuuma sana kumuona baba yake kwenye hali kama hiyo hakutaka tena kuendelea kukaa hapo alihitaji kwenda kuhangaika kumtafutia madaktari bingwa ili waje kuitetea nafsi ya binadamu ambaye ndiye pekee aliyekuwa amebakia kwenye upande wake mpaka sasa.

“Janson Malisaba ndilo jina la baba yako” Sauti ambayo haikuwa na kitetemeshi chochote ilisikika vyema kwenye maskio ya Jamal, aligeuka kwa kuhamaki.

“whaaaaaaaaaaaaaaaaaaaat?” ni mshangao mkubwa alioutoa, hivyo vitu aliwahi kuvisikia vikionekana kwenye tamthilia tu pekee hakuwahi kuwa na imani kama vinaweza kutokea kwenye maisha ya kweli, alijipiga kibao kuona kama alikuwa ndotoni na huenda angeweza kuamka lakini haikuwa kweli hata kidogo alichokuwa anakiona na kukisikia ndio ulikuwa uhalisia wenyewe.

“Mimi sio baba yako mzazi wala sina undugu wowote nawewe namimi sijawahi kabisa kuwa na familia” kauli ya mzee huyu ilimfanya Jamal apate hata kitete cha kutembea wakati huo alikuwa ameshafika kwenye mlango akihitaji kutoweka, mwili ulikufa ganzi hakuwahi kufikiria kama kuna wanadamu wana siri za kufanya mambo ya ndotoni kama haya kuonekana kuwa ya kweli.

“Kivipi baba mbona sikuelewi wewe sio ndugu yangu how(kivipi)? And who are you (na wewe ni nani)” Jamal aliuliza akiwa kama amechanganyikiwa maisha yake yote yalikuwa kama mtu aliye ishi kwenye mchezo fulani ambao hata yeye mwenyewe hakuuelewa unachezwaje.

“kuanzia sasa sina imani kama nitamaliza hata masaa ishirini na manne ya kuendelea kuwa hai, mwili wangu umezoofishwa sana na baadhi ya walimwengu ambao dunia wameiweka kwenye viganja vyao, hawaogopi chochote na kibaya ndo watu wenye pesa na nguvu kubwa za mamlaka ndani ya nchi hii, kuwajua hawa watu inachukua mamia ya maisha ya watu na bado imekuwa ni vigumu sana kwa sababu watu wao wengine tupo tunaishi nao ila kabla sijaweza kwenda kupumzika na kuyatumikia malipo ya yale niliyo yatenda hapa duniani nahitaji wewe kwanza ujijue ni nani kwa sababu hapo ulipo hakuna unacho kijua chochote kwenye huu ulimwengu kuhusu maisha yako, khohoooooooooooo khoooooooo” kikohozi kikali sana kilimtoka huyo mzee baada ya kuongea maneno hayo machache, Jamal alikuwa amepigwa na bumbuwazi alitamani sana ajue hicho kitu ambacho kilisemekana ni mhimu sana kwenye maisha yake, alishikwa na kigugumizi hakuelewa cha kufanya, mawazo makali yalikuwa yanakivuruga kichwa chake asielewe anayapanga vipi lakini kwa mzee wake alitabasamu sana baada ya kuangalia kifuani kwa Jamal na kukiona kile kidani ambacho alimpatia kipo kama kilivyo.

“Nenda kalale kwenye kile kitanda pale” Sauti ya baba yake ambaye kwa sasa alikuwa anamkataa ndiyo iliyo mshtua kwenye dimbwi zito la mawazo mpaka muda huo hata ungemuuliza jina lake asingeweza kulikumbuka, mzazi ndicho kitu pekee ambacho kila mtoto huwa anajidai nacho sana popote pale anapokuwa kukataliwa na mtu aliye mjua ndiye baba yake ilimuuma sana japo hakuweza kubadili kitu chochote. Alienda taratibu akiwa hajiamini tena kwenye maisha yake mtu aliyempenda sana na kumjali kwa kila kitu leo alikuwa anamkataa kwamba hakuwa baba yake wala hana undugu nae wowote. Jamal alielekezwa avue nguo zote abaki kama yeye mwenyewe alivyozaliwa, hakuwa mbishi kwa sababu mtu aliyekuwa anampa hayo maagizo ndiye binadamu aliyekuwa akimheshimu kuliko mtu yeyote yule hapa duniani, alipandisha kwenye hicho kitanda ambacho kilikuwa kimetengwa upande wake pembeni kikizungukwa na komputa kubwa sita, baada ya kupanda hapo kitanda kilijiinua chenyewe vikatokea vioo vikubwa sana na kukiziba hicho kitanda mtu wa nje pekee ndiye aliyekuwa ana uwezo wa kuona kilichopo ndani ya kitanda ila kwa ambaye alikuwa ndani ya hivyo vioo hakuwa na uwezo wa kuona kilichokuwa kinaendelea nje.

Hicho hakikuwa kitanda cha kawaida kama kilivyokuwa kinaonekana bali ilikuwa ni mashine ya kisasa ya kuweza kumrudishia mtu kumbu kumbu zake, Jamal alipoteza kumbu kumbu? Kivipi?

“Kwenye ghorofa moja kubwa sana maeneo ya mikocheni ambalo lilikuwa halijamalizika kujengwa likiwa lipo pembeni ya hoteli moja nzuri sana, juu ya hilo ghorofa lilikuwa linaonekana dirisha moja likiwa lipo wazi kabisa, ndani ya hilo dirisha kuna mwanaume alikuwa anaifunga bunduki yake ya masaafa marefu kwa usahihi akiwa anaiangalia saa yake kwa umakini mkubwa mno, alionekana kuwa anahitajika kuifanya kazi yake kwa muda mwafaka kabisa na kutoweka kwenye hilo eneo. Kwenye chumba kimoja cha hiyo hoteli kubwa ambayo ilikuwa inachangamka sana siku za wikiendi ndani ya hiyo hoteli alikuwa anaonekana Ashrafu Hamad kwenye chumba kimoja akiwa na mwanamke mmoja mrembo sana, hakukuwa na kingine kwenye chumba alichokuwa yupo na huyo mtoto wa kike zaidi ya mahaba ambayo yanadaiwa kuuendesha sana ulimwengu.

Ni wazi watu hao walikuwa wanatamaniana sana kwenye kitanda kikubwa sana kilicho wafanya waweze kuifurahia dunia hiyo kwa ukubwa wake bila kuwa na wasi wasi na kitu chochote kile. Saa mbili kamili za usiku ndio muda ambao walikuwa wanamaliza shughuli nzito juu ya kitanda, walichukua taulo zao wakiwa wamekumbatiana na kutoka kwenye hicho chumba, ilichukuliwa lift iliyo wasaidia kufika chini kwa uharaka mkubwa. walikuwa wanaelekea kuogelea kwenye moja ya mabwawa mazuri sana yaliyokuwa ndani ya hoteli hiyo, wakati huo mwanaume aliyekuwa amesimama kwenye lile ghorofa ambalo lilikuwa bado linajengwa kwa wakati huo aliitazama tena saa yake kisha akainyanyua bunduki yake ya masaafa marefu na kuiweka vyema kwenye dirisha lililokuwa mbele yake, lenzi ndicho kilichokuwa kitu mhimu zaidi kwake, aliizungusha kwa usahihi sana akiwa anaielekezea kwenye bwawa la ile hoteli ambayo ilikuwa ipo pembeni ya lile jengo, hakuhitaji kutumia risasi zake nyingi sana huwa anatumia risasi mbili tu pekee pindi anapo ishika bunduki yake, ni mtu hatari sana, ni moja ya wadunguaji wa kuogopwa mno ambaye nchi ilikuwa inamtafuta kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu kupotea kwake gerezani.

Alexander ndiye mwanaume aliyekuwa ameishika hiyo silaha, ni miaka miwili sasa imepita anaonekana uraiani na alikuwa amefungwa ndani ya gereza la segerea. Alibinya jicho lake moja kwa mahesabu makali sana kisha zikaachiwa risasi mbili kwa haraka kubwa ya kutisha, bunduki za wadunguaji huwa zinachukua muda wa sekunde tano mpaka kumi na tano ili kuiruhusu risasi nyingine kutoka tena lakini kwake ilikuwa ni tofauti kidogo alikuwa na silaha yenye uwezo mkubwa sana risasi zilikuwa zikipishana kwa sekunde moja tu pekee. Ashrafu Hakim akiwa na mwanamke wake kwenye maji risasi ya kwanza ilizama kwenye paji la uso wake hakuweza hata kupiga kelele ni kwa muda mfupi nyingine ilizama pale pale taratibu akawa anashuka kwenye maji damu zikianza kutapakaa kwenye maji, dakika moja baada ya kuisha ndipo yule mwanamke aliyekuwa naye alipogundua kwamba Ashrafu alikuwa amepigwa risasi, alipiga makelele makubwa sana yaliyo washtua watu wakaanza kukimbia hovyo huku vyombo vya usalama ndani ya hiyo hoteli vikianza kusogea haraka sana kuweza kujua tatizo kubwa hasa ni nini lakini Ashraf Hamad hakuwa miongoni mwa wanadamu ambao walibahatika kuwa hai tena.

Mwanaume baada ya kuimaliza kazi yake alifunga vitu vyake haraka akavaa kofia lake kubwa akiwa na koti refu sana la kijivu alikuwa akishuka taratibu mno bila wasi wasi wowote ule kama vile ametoka kufanya biashara kumbe alikuwa ametoka kumuua binadamu mwenzake. Alitembea taratibu kuwahi kwenye gari yake aliyokuwa ameipaki chini kabisa, wakati anakaribia mahali alipokuwa ameipaki gari yake alipigwa mtama na mwanaume aliye onekana kukomaa vyema kwenye mwili wake, ni uimara wake ndio ulio mfanya asiweze kudondoka chini alijirusha kwa sarakasi mguu mmoja akaugusisha kwenye gari akasimama vizuri bila wasi wasi na begi lake kubwa lenye silaha likiwa mkononi mwake.

“Kakutuma nani uje kufanya mauaji kwa huyu mtoto?” swali kutoka kwa moja ya wanaume watatu ambao walikuwa wapo pembeni yake lilisikika vyema kwenye masikio yake, aliiangalia saa yake vizuri muda wake haukumruhusu kuendelea kuwepo hiyo sehemu.

“Nitafute siku nyingine kama una shida ya kuongea namimi nimeshamaliza kazi yangu hivyo sitaki usumbufu kwa sasa sina muda wa kuendelea kukaa hapa kwa leo” alisisitiza kwa sauti yake nzito sana, buti kali lilimpuliza usoni baada ya kujibu jeuri mmoja wa wale wanaume alikuwa amemfikia Alexander ambaye hakuweza kuliachia begi lake lililokuwa na silaha ndani yake, alimrushia yule mwanaume lile begi wakati analidaka alikuwa amesahamfikia alilipiga begi lake teke kali lililo lifanya begi hilo kurushwa juu sana huku akimshindilia mwanaume huyo aliyekuwa amelidaka begi lake teke zito lililo mpeleka mbali sana, wenzake walikuwa wanakuja kwa kasi sana wakiwa wanawahi kumshambulia Alexander, mkono wake mmoja ulilidaka begi lake lenye silaha, mkono mwingile ulitoa kitu kizito sana ambacho baada ya kukibonyeza kilitoa sauti nzito mno na moshi mwingi uliokuwa unaumiza macho yao iliwalazimu kufumba macho pamoja na kuziba masikio, dakika moja moshi ulikuwa umeisha na sauti haikuwepo tena lakini walipo jaribu kuangaza huku na huko hawakuona mtu yeyote wala gari lililokuwa hapo halikuonekana mwanaume alikuwa amesha potea muda mrefu sana. watu walianza kusika wakija upande huo baada ya kuona moshi mwingi ghafla iliwabidi nao kuondoka hiyo sehemu haraka.

Jamal ni kweli alipoteza kumbu kumbu na kama ni kweli alipotezaje na huyu mzee kajuaje? kweli Ashrafu Hamad maarufu kama omba omba wa Buguruni ndo kafa kirahisi sana namna hii?.....15 naweka nukta endelea kunifuatilia kwa umakini uweze kuuelewa mchezo wa akili huu ambao huenda mpaka sasa bado haujauelewa vizuri usipanic utaloose confidence.

Bux the story teller
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA

TULIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA TANO.........

mkono mwingile ulitoa kitu kizito sana ambacho baada ya kukibonyeza kilitoa sauti nzito mno na moshi mwingi uliokuwa unaumiza macho yao iliwalazimu kufumba macho pamoja na kuziba masikio, dakika moja moshi ulikuwa umeisha na sauti haikuwepo tena lakini walipo jaribu kuangaza huku na huko hawakuona mtu yeyote wala gari lililokuwa hapo halikuonekana mwanaume alikuwa amesha potea muda mrefu sana. watu walianza kusika wakija upande huo baada ya kuona moshi mwingi ghafla iliwabidi nao kuondoka hiyo sehemu haraka.

ENDELEA...................

“Kama wanipenda, ninunulie zeze nikilala kitandani lanibembelezaaaa,

Kama wanipenda, ninunulie zeze nikilala kitandani lanibembelezaaaa

Mateso moyoni, usiku silalii, hadithi sitakii, nataaaka zeze

Penzi lako la thamani, tanashati jamaani usiku silalii nakupenda zeeezeee……

Kama wanipendaaaa……….” Ni sauti ya wimbo mmoja bora sana kuwahi kuandikwa Tanzania, imepita miaka mingi tangu uandikwe lakini mpaka leo ukichezwa sehemu yoyote ile lazima utaguswa na hisia kali, pongezi kwa the former top in Dar TID, kama umebahatika kumjua mwanamziki wa kizazi kipya aitwaye Diamond Platnumz basi TID ndiye aliyekuwa Diamond wa zamani ndani ya jiji la Dar es salaam, ulikuwa huwezi kupita sehemu ya Dar usilisikie jina lake iwe ni kwa mashairi yake mazuri au kwenye kipaji chake cha ucheshi wa kuwafurahisha watu simply a gifted human creature wimbo wake unafahamika kwa jina la zeze. Sauti hiyo ilikuwa ikisikika vizuri ikionekana wazi mtu aliyekuwa akiitamka alikuwa ni mpenzi mkubwa wa huo wimbo kwa namna alivyokuwa akiuimba kwa hisia pamoja na furaha.

Kibamba Dar es salaam ndiyo mitaa iliyokuwa ikisikika sauti ya huo wimbo majira ya saa nne za usiku, mzee mmoja ambaye wengi walikuwa wanamjua kama maarufu kwa ufugaji wa kuku hapo mtaani ndiye aliyekuwa anauimba huu wimbo kwa fujo huku akipiga miluzi mingi kwa nguvu, nchi ya amani hakuwa na shaka na chochote kile. Sauti yake ilikatishwa baada ya kuhisi kama kuna mtu amepita mbele yake lakini hakufanikiwa kabisa kumuona alihisi huenda ni pombe kidogo alizoweza kuzinywa zilikuwa zikimfanya kuwa kwenye hiyo hali ila nafsi yake iligoma kabisa kuamini hicho kitu mwili ulikuwa ukimsisimka mno alitembea hatua tatu tu mbele ikabidi asimame vizuri hata kule kuyumba yumba kwa furaha kwa sababu ya chupa za pombe kadhaa alizokuwa ameziweka tumboni mwake zilimuisha kwanza, binadamu huwa ni mtu makini sana pale linapokuja suala la kuweza kuulinda uhai wake, vitu vinanunuliwa sokoni na kuuzwa kirahisi sana lakini maisha ni mara moja tu ukiipoteza au kuitumia vibaya nafasi uliyoweza kupewa na MUNGU maisha yako yataishia kwenye majuto makubwa sana kama sio kupotea kabisa kwenye uso huu wa dunia.

Mbele yake alikuwa amesimama mwanaume mmoja mwenye koti refu sana la kijivu, Alexander ndiye aliyekuwa mbele yake kulikuwa na giza lakini walionana kwa usahihi mkubwa pasipo kuweza kupepesa macho.

“Unapata tenzi tu mzee wangu baada ya kunifanya mimi mjinga kwa muda wote huu hivi unajua madhara ya hiki kitu ulicho kifanya kwako na kwa familia yako?” Alexander alikuwa anampa tahadhari mapema sana mzee ambaye hakueleweka kamfanya nini kiumbe huyu mpaka wafikie huku.

“Familia ipi labda ambayo unaisemea wewe hapo kijana wangu?” hakuonyesha dalili yoyote ile ya ulevi kwa sauti yake iliyokuwa inamtoka kwenye kinywa chake.

“Mtaa wa pili nyumba ya sita ndipo nyumbani kwako, unawezaje kunilaghai mtu kama mimi mwananchi wa kawaida sana kama wewe?” mdharau mwimba mguu humuota tende, kauli hii haikuwa na nafasi kabisa kwenye mdomo wa Alexander alimdharau pamoja na kumuonea huruma sana mzee aliyekuwa yupo mbele yake.

“Kuna sababu kubwa sana ya MUNGU kuumba usiku na mchana, mchana umeumbwa kwa sababu ya wale watu wa kawaida ambao hata uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana, kwao usiku ndio muda hatarishi zaidi duniani wakiamini ndio muda wa kulala lakini watu wakubwa na wenye akili zaidi ulimwenguni ndio muda ambao huwa wanautumia sana kufanya mambo makubwa duniani ndio maana unaona mtu anaye lala masaa machache sana mida ya usiku huwa anaheshimika sana na kuonekana ni mtu mhimu mno kwenye jamii wakati yeye analala hata mchana kumalizia usingizi wake ila heshima inabaki pale pale kwa sababu ya kuwa macho usiku. Nenda nitakuja kukutafuta mimi mwenyewe nitakapokuwa na kazi nawewe” huyo mzee hakuonekana kuwa na wasi wasi hata kidogo licha ya mtu aliyekuwa mbele yake kuonekana kuwa hatari sana kwenye maisha ya wanadamu alimrushia Alexander kadi ndogo(karata) ambayo ilikuwa na namba moja tu basi kisha akaanza kugeuka na kuondoka.

“Hey wewe mzee” Alexander aliita kwa sauti kubwa akiwa anamkimbilia mzee huyo ambaye alikuwa anapotelea gizani, alikuwa hajamalizana naye kabisa alikuwa anahitaji kujua kwanini alimdanganya kuhusu mtu aliyekuwa amemuulizia lakini pia alihitaji kujua hiyo kadi waweza kuiita karata moja ilikuwa inamaanisha nini. Huyu ndiye aliyeweza kumpa maelekezo kwamba usiku ule Ashrafu Hamad atakuwa kwenye ile hoteli ambapo yeye alienda kufanya mauaji, lengo la kumfuata hapa alihitaji kujua kipi kilimfanya huyu mzee ampe taarifa za uongo? Ilikuaje?

Baruan baada ya kutoka kufanya mauaji ndani ya hoteli kubwa sana Mikocheni na kufanikiwa kuwatoroka wanaume ambao walikuwa wapo karibu na gari yake wakijaribu kumzuia asiweze kuondoka na awape sababu ya kuweza kufanya mauaji ya huyo kijana, alifanikiwa kutoroka kabisa lile eneo. Baadae sana taarifa zilisambaa sehemu mbali mbali kuhusu tukio hilo hasa kwenye vyombo vya habari na kufanya kila mtu apate taarifa sahihi kabisa juu ya hilo tukio.

“Hello” sauti ya mamlaka ilitoka upande wa pili

“Hello” Alexander alijibu ikiwa ni saa moja tu tangu atoke kufanya mauaji ya Ashrafu Hamad.

“Ni wewe ndiye umefanya hilo tukio huko mikocheni” mtu wa upande wa pili aliongeza tena.

“Ndiyo”

“Kwanini umefanya kitu cha kijinga sana namna hiyo?”

“Sikuwa na namna ya kuweza kumuacha yule mtoto ilikuwa ni lazima afe kwa namna yoyote ile kukutana naye ningepoteza sana muda na kujulikana ndio maana nimeamua nimmalize moja kwa moja bila hata kuonana naye” alijigamba Alexander

“Nafikiri tangu upelekwe jela umekuwa mtu wa hovyo sana una akili ndogo kama , endapo ukirudia kufanya ujinga wa aina hii tena basi utanilazimisha niutumie vibaya mkono wangu kwako nadhani unanifahamu vizuri” upande wa pili ulisikika ukiongea kwa nguvu.

“Hakuna kitu kinaweza kutokea tena mtu ambaye angenifanya niende kinyume nilisha mmaliza tayari” jeuri ni kitu kibaya sana kwenye maisha na ndicho ambacho alibarikiwa sana Alexander japokuwa hakuwa mtu wa kuongea ongea sana kwa watu asio wajua

“Mhhhhhhhhh kwa huo ukurupukaji wako unadhani unaweza kumuua yule mtoto kipumbavu sana namna hiyo, hahahhaahahahahah acha kuota ndoto za mchana wewe, uwe na akili muda mwingine nilisha kuonya tangu muda kwamba huyo mtoto analindwa sana hata yeye mwenyewe ni mtu hatari sana unadhani hizo risasi zako mbili ndo zitampata au zitamuua kipumbavu sana namna hiyo, acha kuwaza vitu vya kijinga nenda kafanye mazoezi wiki ijayo nina kazi ya kukupa” simu ilikatwa kabla hata hajajibu chochote alibaki anaita tu

“Hello, hello” hakuna alicho ambulia simu hiyo ilikatwa na haikuwa ikipatikana tena, upande wa pili alikuwa anaongea mwanasheria mkuu wa nchi ya Tanzania alimcheka sana Alexander baada ya kusikia kwamba amemuua Ashrafu Hamad, Alexander alidhani labda amesikia kauli hiyo vibaya haikuwezekana mtu ambaye alishuhudia akimpiga risasi mbili za kichwa leo hii anaambiwa kwamba hawezi kabisa kumuua kijinga hivyo alichoka sana, ndiyo sababu alikuwa amemfuata huyo mzee ambaye alimpa hizo taarifa ili akathibitishe kwamba inawezekanaje mtu akaishi mara mbili lakini hakufanikiwa chochote hata mzee huyo alipotelea zake gizani na haikueleweka ameingia wapi. Alexander alikumbuka kwamba mzee huyo alikuwa akiishi maeneo jirani kabisa na hapo basi akaanza kukimbia kwa kasi ili aweze kuwahi lakini alicho kiona alichoka mpaka akakaa kabisa chini sehemu ambapo alikuwa na imani alikuwa anaiona hiyo nyumba siku zote alizo fanikiwa kufika hiyo sehemu hapakuwa na kitu chochote zaidi ya bustani ndogo ya mboga mboga za majani ambazo zilionekana sio muda sana zilitoka kumwagiliwa. Alikuwa ni binadamu mkatili na mwenye roho ngumu sana lakini alijikuta anaanza kuogopa na kuwaogopa wanadamu wenzie mambo aliyo yashuhudia na kuyaona kwa haya masaa machache yalimfanya alale hapo hapo kwenye bustani wala hakukumbuka hata kurudi nyumbani kwake alikuwa mtu mwenye mawazo kupitiliza.

“Babaaaaaaaaaa” ni sauti kali sana kutoka kwa Jamal, nusu saa ya kutoka kwenye usingizi mzito ilimfanya apige makelele huku jasho likimtoka mwili mzima, alikuwa amelazwa kwenye usingizi mzito sana ambao ulimfanya arudishe kumbu kumbu zake za maisha yake ya mwanzo kabla ya kuwa huyu Jamala ambaye yeye alikuwa anajijua sasa hivi. Miaka takribani 9 iliyokuwa imepita tangu siku ambayo mtoto Lenovatus Jonson aweze kuokolewa kutoka kwenye kifo kwa wanaume wawili ambao aliwashuhudia wazi mmoja wao akikikata kichwa cha baba yake mzazi na kuondoka nacho ndicho kitu ambacho leo kilikuwa kinatokea hapa ili kuweza kumfanya kijana aweze kulielewa hilo. Usiku wa siku ile baada ya kuweza kuokolewa na mtu asiyejulikana alizimishwa wakati yupo kwenye uzingizi huo wa kuzimishwa alichomwa sindano ambayo ilimfanya baada ya kuamka asikumbuke kitu chochote kile kwenye maisha yake alikuwa kama ni mtu ambaye ndo amezaliwa na anaenda kuyaanza maisha mapya kabisa duniani sababu kubwa ni kumlinda kuathirika kisaikolojia kwa umri aliokuwa nao muda ule hayo matukio yangemtesa sana.

Mwanaume ambaye hali ilikuwa ipo mbaya sana kwake na alikuwa mbele ya Jamal ndiye ambaye aliweza kumsaidia siku ile ya usiku kutoka kwa wale watu ambao walionekana wazi hawakudhamiria kabisa kumbakisha mtu hata mmoja baada ya mzee Jonson kushindwa kufanya chaguo sahihi kati ya machaguo matatu ambayo alipewa usiku ile ambapo hakufanikiwa kuingia hata ndani ya nyumba alifia nje ya nyumba yake bila hata kuiaga familia yake ambao nao waliuawa pale pale kabla yake.

Dakika tatu zilimfanya Jamal apunguze kuhema lile tukio la kukumbuka baba yake kuweza kuchinjwa kisu mbele yake kama kuku lilimtoa machozi na kumsisimua sana alitamani sana asingeweza kukumbuka hicho kitu kilitisha mno.

“nina maswali manne naomba unijibu kwa ufasaha sana la kwanza nahitaji kujua baada ya pale kilitokea nini? la pili wewe ni nani? la tatu aliyefanya haya yote ni nani? la nne ni kwanini afanye ukatili mkubwa sana kiasi hiki nini chanzo ya yote haya” Jamal alikuwa anatoa machozi sana kwa kitu kilichokuwa kimemjia kwenye kumbu kumbu zake, hapo alikuwa amekumbuka maisha yake akiwa na miaka 14 tu kurudi nyuma baada ya hapo hakuelewa nini kiliendelea kwenye maisha yake mpaka siku aliyokuja kujikuta yupo ndani ya jiji la Mbeya wilaya ya Kyela akiwa na mwanaume ambaye yeye alimjua kama ndiye baba yake mzazi kitu ambacho hakikuwahi kuwa cha kweli hata siku moja. Moyo ulikuwa unamuua mbele yake alikuwa na kazi nzito aliapa chakwanza anahitaji kujua hicho kichwa cha baba yake kilipelekwa wapi na ni mtu gani aliyekuwa na ujasiri wa kuweza kuufanya huo ukatili kwani hakuwa mtu wa kuachwa kabisa alikuwa amefanya kosa moja kubwa sana kwenye maisha yake kilichokuwa kinaenda kumtokea kama angepatikana kilikuwa ni kitu cha kutisha mno.

Nini kimetokea kwa Alexander, ni nani anaye mchezea huu mchezo? Ni kweli Ashrafu Hamad hajafa? Kama sio yeye kafa nani? inawezekana kweli mtu apigwe risasi mbili za kichwa asife? ………. na vipi kuhusu Jamal hatima yake ni nini? kipi kimetokea kwenye maisha yake ambacho yeye hakijui, ataweza kukipata kichwa cha mzee wake ikiwa ni miaka 9 sasa imepita? Mhusika wa haya yote ni nani? …. Usije ukawaza kuikosa sehemu hata moja ya hadithi hii tuliza akili sana unavyo isoma

Maiki naiweka pembeni kalamu yangu haina uwezo wa kuandika tena….16 tunafika mwisho tukutane wakati ujao.

Hiki ndicho kitabu changu bora zaidi cha kijasusi kuwahi kukiandika mpaka muda huu.......idea generation, mpangilio wa matukio, uwingi wa nchi na wahusika..Dope..... Tanzania X Japan [emoji119]......it's a movie not a tale ULIMWENGU WA WATU WABAYA [emoji2768]

ULIMWENGU WA WATU WABAYA PDF yake kwa mfumo wa nakala laini (soft copy) ndiyo hiyo hapo kwa mwenye shilingi 5000 tu unatumiwa na utaishi nayo milele.

0621567672
0745982347

FEBIANI BABUYA nicheki utumiwe muda huo huo.

Bux the story teller
Pic_1662892058329.jpg
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA

TULIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA SITA.........

Moyo ulikuwa unamuua mbele yake alikuwa na kazi nzito aliapa chakwanza anahitaji kujua hicho kichwa cha baba yake kilipelekwa wapi na ni mtu gani aliyekuwa na ujasiri wa kuweza kuufanya huo ukatili kwani hakuwa mtu wa kuachwa kabisa alikuwa amefanya kosa moja kubwa sana kwenye maisha yake kilichokuwa kinaenda kumtokea kama angepatikana kilikuwa ni kitu cha kutisha mno.

ENDELEA...........................

Kwa majina naitwa Nwonku Bateli Nyanike ni mzaliwa wa kusini magharibi mwa Tanzania karibu na wilaya ya Karatu katika jiji la Arusha huko ndiko nyumbani kwetu mimi, ni mhadizabe kwa kuzaliwa na ndilo kabila langu halisia kabisa, ni watu ambao robo tatu ya maisha yetu hatufungamani na watu wengine kabisa huwa tunaishi wenyewe tu na kuyaenzi maadili ambayo tumeyakuta kutoka kwa mababu zetu. Ukifika huko uwindaji ndio ushujaa wa kila kijana mwenye nguvu, nilikuwa mdogo sana kipindi hicho sina kumbu kumbu nzuri ila ni takribani miaka 50 iliyopita nilikuwa nina umri wa miaka nane pamoja na pacha wangu ambaye tulipishana muda kidogo wa kuzaliwa, tulizaliwa kwenye familia ambayo ilikuwa ni maarufu sana pale kijijini, umashuhuri wa baba yangu mzazi ndio uliofanya kila mtu aweze kutujua sana mpaka nje ya Kijiji chetu lakini kwenye kufanya mazuri chini ya jua hakukosi kukufanya kuwa na maadui wengi sana kila sehemu.

Ni siku moja majira ya usiku mida ya saa nne nadhani japokuwa hakukuwa na saa zaidi ya mbalamwezi kwa mbali ambayo kwetu ilikuwa ni zaidi ya hizi saa za kisasa kwenye maisha ya leo kuna mtoto mdogo alikuja kugonga kwenye nyumba yetu akilia na kuhitaji msaada kwamba mama yake alikuwa amevamiwa na wanaume wanahitaji kumfanyia kitu kibaya, baba yangu alikuwa mtu mwema sana hakujiuliza mara mbili ikambidi atoke huku akikimbia mama akawa anamfuata nyuma. Mimi nilikuwa mdogo lakini nilikuwa nimefundishwa ujasiri sana na baba yangu tangu nianze kupata uelewe kidogo hivyo niliamka bila kumwamsha mdogo wangu kwani kwa wakati huo yeye alikuwa kwenye usingizi mzito sana. Bila kujua kama ni hatari kwake baba yangu aliendelea kuelekea sehemu ambayo alielekezwa na mtoto mdogo japo kwangu alikuwa mkubwa kwa umri wake kwa wakati ule ulikuwa unakaribia hata miaka 10, baba yangu alisikia sauti moja tena kwa mbele yake kidogo sehemu ambayo ilikuwa na kichaka kidogo aliingia huko ndani ya kichaka akiwa ameshika silaha yake ya mkuki na upinde wake wa jadi ambao aliutumia kuwindia. Ni moja ya siku mbaya sana ambazo zimegoma kabisa kufutika kwenye maisha yangu, ndio kwa mara ya kwanza nilikuja kuanza kuwaogopa sana wanadamu badala ya kuishia tu kuwaheshimu baba yangu alikuwa amechezewa mchezo mmoja hatari sana na mwanaume mmoja ambaye alikuwa akichukia sana baba yangu akiwa maarufu mbele yake ndani ya kile kijiji.

Nwake ndilo lilikuwa jina lake yule mtu, kabla ya yule mtoto kuja nyumbani ilikuwa imechezwa karata moja ya hatari sana ya kuweza kumfanya baba yangu afe na kutoweka kabisa kwenye uso wa dunia. Ni kweli ile sehemu aliwekwa mwanamke ambaye alikuwa kama chambo, yule mtoto baada ya kuona baba yangu ameanza kuelekea ile sehemu alikimbilia kusikojulikana na sikufanikiwa kumjua kwani sikumuona vizuri kutokana na giza na kama ingetokea nikamjua basi ningemuua kifo kibaya sana hapa duniani na sina imani kama ningeweza kusamehewa kwa dhambi hiyo ambayo natamani hata kesho niifanye kabla sijakatika na kutoweka duniani. Yule mwanamke aliyekuwa amewekwa pale alikuwa ni mke wa mtu na aliwekwa kama mtego kwa kulipwa na bwana Nwake.

“Nabakwaaaaaaa nabakwaaa msaaada” ni sauti ambazo nilizisikia nikiwa nakaribia karibia kwenye lile eneo ambalo baba yangu alikuwa ameelekea, yule mwanamke alipiga kelele akiwa uchi wa mnyama kabisa amemkumbatia baba yangu na kumng’ang’ania kabisa, baba hakuelewa bado alibaki amesimama akishangaa akiwa haelewi nini kimemkuta mwanamke yule, mama yangu nilimuona amejishika kichwa wakati nafika pale kuna wanaume zaidi ya sita ambao kwa haraka harakat u niliweza kuelewa kwamba walikuwa wamepangwa kuwepo lile eneo kwa muda mrefu sana basi walimkamata baba yangu na kumvua nguo wakamfunga pamoja na yule mwanamke kwa kuwagusanisha sehemu zao za siri huku wakiwafunga kamba hivyo hivyo ili iwe kama ushahidi wa kuwaaminisha watu kwamba kweli alikuwa anabakwa, sikuwa na ujasiri wa kuweza kumuona baba yangu akiwa kwenye ile hali ilinibidi niangalie pembeni kwanza ila niliogopa baada ya kuona kundi kubwa sana la watu likiwa linakuja ile sehemu tena wakiwa na silaha kali za kuwindia wakiwa wameongozana na kiongozi mkuu wa ile sehemu ni haraka sana waliweza kumpatia taarifa.

Alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anaheshimiana sana na baba yangu hivyo alishangaa kumuona kwenye ile hali akiwa haamini.

“Nyanike hiki ni nini(kwa kihadizabe)?” kiongozi yule aliuliza akiwa haamini wakati huo nilimuangalia mama yangu alikuwa akitoa kilio kikali sana ni wazi wazi ulimwengu ulikuwa unamfanyia mumewe ukatili mkubwa sana, baba yangu hakuweza kutoa usemi wowote ule kwani kwa hali aliyokutwa nayo hapo hata angeeleza nini hakuna mtu ambaye angeweza kumuelewa.

“Alikuwa ananibaka tafadhali kiongozi naomba unisaidie mimi mume wangu ataniacha kwa ajili ya mwanaume katili kama huyu usimuache tafadhali(kihadizabe)” ndiyo siku ambayo niliapa kwamba sitakuja kumuamini binadamu yeyote yule kwenye maisha yangu yule mwanamke alikuwa akidanganya wazi wazi nikiwa nasikia kabisa kwa masikio yangu kitu ambacho hakikuwa cha kweli kwa asilimia miamoja. Niliona kuna mtu anakuja akiwa amefura kwa hasira, alikuwa ni mume wa yule mwanamke alifika na kumchoma kisu cha shingoni baba yangu wakati huo nilikuwa nimegeuka kuangalia kiliochokuwa kinaendelea, nilidhani naota ila ulikuwa ni uhalisia nilijikuta nguvu zinaniishia kabisa kwenye mwili wangu nilikaa chini nikiwa natokwa na machozi. Kwenye hali isiyo ya kutegemea mama alikimbilia sehemu aliyokuwa amedondokea mume wake hakujiuliza mara mbili alichomoa kile kisu na kujichoma nacho kwenye tumbo lake nadhani kwa wakati ule hakuweza kukumbuka kabisa kama ana watoto siwezi kumlaumu kwa hilo nilikuwa nikimheshimu sana yule mwanamke mpaka leo. Sikujua nimenyanyuka saa ngapi lakini nilinyanyuka pale na kuanza kukimbia sana kuondoka lile eneo nikiwa bado mtoto mdogo mno nilikuwa nimechanganyikiwa, kuwaona wazazi wangu wote wakifa kwa muda mmoja hicho ndicho kitu kigumu zaidi cha kutisha kuwahi kukishuhudia kwenye maisha yangu, wakati naendelea kukimbia kuelekea nyumbani kwenye mti mmoja pembeni nilisikia watu wakiwa wanacheka sana nikasogea ile sehemu bila kuonekana kutokana na giza lililokuwepo. Palimulikwa tochi mtu alikuwa anakabidhiwa zawadi ya Wanyama sita wa mwituni baada ya kufanikisha ziezi la kutengeneza mpango wa kummaliza baba yangu na aliyekuwa akikabidhiwa hapo alikuwa ni ndugu wa kiume wa yule mwanamke ambaye alipiga kelele kwamba anabakwa na baba yangu, yule mwanaume ambaye alikuwa anafurahia na kuwakabidhi watu hao wanayama hao ni mtu ambaye nilikuwa namjua Nwake ndilo jina lake na hakuwahi kuufurahia umashuhuri wa baba yangu, ni mtaa wa sita tu ndiyo sehemu ambayo alikuwa akiishi. Sikumbuki ujasiri ule niliutoa wapi ila niliokota jiwe moja kubwa ambalo lilichongoka mbele nilinyata mpaka pale walipokuwa wao nilimpiga yule mwanaume sehemu ya nyuma ya kichwa chake alipata mshtuko akaanza kutapa tapa yule mwenzake hakuelewa kilicho tokea kutokana na kiza maana tochi ilidondokea mbali na pale baada ya kumpiga Nwake na jiwe ambaye ndiye aliyekuwa ameishika, alishtuka na kuanza kukimbia akidhani ni watu wamewavania pale ila bahati mbaya kwake wakati anageuka nyuma yake kulikuwa na kisiki kikubwa anbacho kilionekana miezi kadhaa nyuma yake kuna mtu aliweza kuutoa mti ambao ulikuwa hapo, mwanaume huyo alidondokea shingo ambapo kile kisiki kilimtoboa alikufa nikiwa namuona hata yule ambaye ndiye aliyekuwa anatamani baba yangu afe hiyo nafasi aichukue yeye hakumaliza hata dakika mbili kwa jiwe nililokuwa nimempiga nalo alikuwa amekufa.

Niliua watu wawili nikiwa na miaka nane tu kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu, sikuwa nikijielewa nilikimbia mpaka nyumbani nikamuamsha pacha wangu ambaye bado alikuwa usingizini akiwa haelewi kwamba huenda ndiyo siku yetu mbaya zaidi duniani, nilitoka naye nje sikuhitaji tena kuendelea kukaa hiyo sehemu niliogopa sana, alikuwa mbishi sana ila uzuri wake alikuwa mtu wa kunisikiliza.

“Kaka baba na mama wako wapi nataka kula mimi(kihadizabe)” alikuwa ametoka tu usingizini lakini alikuwa akihitaji kula chakula, ilikuwa ni kawaida yake alikuwa akideka sana. Nilimuangalia na kutoa machozi maana alikuwa anataka kumuona mtu ambaye kwenye maisha yake yote asingeweza kabisa kumuona tena. Nilishtuka baada ya kusikia kwa mbali watu wakiongea kwa kilugha chetu kumaanisha wanahitaji sisi tuuawe inawezekana kuzaliwa mapacha ndiko laana ilikotokea, niliogopa sana nilimhitaji mdogo wangu ambaye tulikuwa tunafanana kwa kila kitu asipige kelele kabisa ilinibidi nijivishe ujasiri mkubwa sana, tulizunguka nyuma ya nyumba yetu hatua mia moja kutoka hapo kulikuwa na miti miti ndiyo sehemu ambayo nilienda na ndugu yangu majira hayo ya usiku, tulipanda juu ya mti ili watu hao wasiweze kutuona japo ndugu yangu hakuelewa chochote kwani nilimdanganya kwamba baba na mama wameniagiza nimchukue nimpeleke waliko hiyo kidogo ilisaidia kupunguza maswali mengi.

Nilishuhudia ile nyumba yetu ambayo kwa maisha ya sasa tungesema kibanda lakini pale ndipo palikuwa nyumbani kwetu ikichomwa moto, kutokana na kiza kilichokuwepo nilipata bahati ya kutulia na kutoa machozi mengi sana ya uchungu, sikuona sababu ya kuendelea kuwa pale tena nilishuka na kumshika ndugu yangu mkono nikaanza kuelekea eneo ambalo lilikuwa na bara bara japokuwa kulikuwa ni mbali sana. Siku mbili za kutembea tukiwa tunakula matunda njiani zilitusaidia kutokezea kwenye bara bara kubwa ya vumbi, mdogo wangu alikuwa akilalamika tu kwamba anataka kumuona mama ila sikuwa tayari kuruhusu ajue chochote kuhusu kilichoweza kutokea. Tukiwa tunatembea kuna gari moja ilikuwa inapita nadhani ni moja ya watu ambao walikuwa wametoka kuiba mbao, ni majira ya jioni jua lilianza kuzama ndio muda ambao gari hiyo ilikuwa inapita na kutokana na ubovu wa bara bara ilikuwa inatembea taratibu sana. Hatukujua kilikuwa ni nini kwa sababu hatukuwahi kuona kitu kama hicho kabla ila tulipenda namna lilivyokuwa linatembea lilikuwa ni kama bembea ambazo tulizizoea kule kwetu kwenye miti lakini tofauti ya gari ni kwamba ilikuwa inatoka sehemu moja kwenda nyingine basi tukikimbilia na kuipanda gari hiyo, niligeuka nyuma baada ya kupanda kwenye mbao bila kujulikana nikaangalia kule msituni, sikujua tunaelekea wapi ila niliapa kutokuja kukanyaga hiyo ardhi tena kwenye maisha yangu.

Hiyo ndiyo ilikuwa safari yangu ya kwanza na ndio mwanzo wa mambo mazito sana yaliyo andikwa kwenye maisha yangu huenda hiyo ndiyo safari iliyo nifanya nikawa mtu hatari zaidi duniani.

Usipagawe sana najua unatamani kumjua huyu kiumbe mpya kwenye hadithi ni nani, kazi yako ukiwa unasoma hadithi hii ni kutuliza sana akili yako mimi mwenyewe mpaka sasa sijaelewa nini kinaendelea nina imani mpaka sasa huyaelewi matukio vizuri unabaki njiapanda.

17 naweka nukta tukutane wakati ujao.

SEHEMU YA KUMI NA NANE

TULIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA SABA.........

Hatukujua kilikuwa ni nini kwa sababu hatukuwahi kuona kitu kama hicho kabla ila tulipenda namna lilivyokuwa linatembea lilikuwa ni kama bembea ambazo tulizizoea kule kwetu kwenye miti lakini tofauti ya gari ni kwamba ilikuwa inatoka sehemu moja kwenda nyingine basi tukikimbilia na kuipanda gari hiyo, niligeuka nyuma baada ya kupanda kwenye mbao bila kujulikana nikaangalia kule msituni, sikujua tunaelekea wapi ila niliapa kutokuja kukanyaga hiyo ardhi tena kwenye maisha yangu.

ENDELEA........................

Duniani kuna matabaka makubwa mawili tu basi ambayo huwa yanawatofautisha watu na namna ya kuishi kwao, tabaka la kwanza ni la watu maskini hawa mara nyingi huwa wanaamini sana kwamba pesa ndicho chanzo kikubwa cha maovu yote duniani lakini ni tofauti sana kimtazamo na tabala la pili hili ni la watu matajiri ambao kwao huwa wanaamini kwamba kutokuwa na pesa ndicho chanzo cha maovu yote yanayo endelea ulimwenguni. Kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa ina ghorofa saba kushuka chini, ni nyumba ya kisasa mno kuwahi kutengenezwa ndani ya nchi hii japokuwa maeneo ambayo ilitengenezwa usingeweza kuamini maeneo ya Chanika kwenye jumba la kifahari la mtu asiyeweza kufahamika. Kwenye chumba cha chini kabisa mwa hiyo nyumba kulikuwa na binti mmoja ambaye alikuwa amekaa mbele ya komputa za kisasa zilizo zunguka kwenye chumba hicho kwa zaidi ya masaa ishirini sasa mikono yake na macho yake ndizo silaha kubwa ambazo zilikuwa zinampa uwezo wa kufanya kitu chochote atakacho mwenyewe anapokuwa mbele ya komputa hizo.

Baada ya muda mrefu wa kukaa hapo alionekana wazi kutabasamu baada ya komputa yake kuonyesha alama nyekundu kwenye ramani ambayo ilikuwa ipo mbele ya macho yake. Tiptop maeneo ya Manzese ndipo hicho kidoti chekundu kilipokuwa kimeishia, tabasamu murua lililo shamiri kwenye uso wake lilikuwa linauonyesha urembo wake asilia ambao weusi wake ulimfanya kuwa mwanamke bora sana kwenye kila sura ya mwanaume ambaye amekamilika. Aliprint page moja ambayo ilikuwa na hiyo ramani kisha akaiweka kwenye bahasha na kuandika neno done juu ya hiyo bahasha. Hatua saba kutoka kwenye mkono wake wa kulia kutoka sehemu aliyokuwa yupo kwa huo muda ndicho chumba ambayo alienda kuirushia bahasha hiyo kwa chini kabisa ambapo palikuwa na nafasi ndogo sana, hakuwahi kupata nafasi ya kuingia kwenye hicho chumba hata siku moja na wala hakuwahi kujua kwamba ndani ya hicho chumba kulikuwa na na nini alionekana kuwa mtu anaye ishi kwa mashariti makubwa mno ndani ya hii nyumba, ni miaka minne sasa alikuwa hajawahi hata siku moja kuliona jua kazi zake zilikuwa ni kuzunguka kwenye hivyo vyumba vya komputa na chumba chake cha kulala alikuwa anasema chochote anacho kitaka halafu analetewa, hayo ndiyo maisha aliyokuwa akiyaishi huyu mwanamke mrembo sana, maisha ya hivi huwa hayaji kwa bahati mbaya yanakusa na sababu zake nyingi sana.

Kwenye chumba ambacho bahasha hiyo ilikuwa imerushwa alikuwepo mwanaume mmoja ambaye alikuwa amevaa vitambaa usoni kwake alikuwa haonekani sehemu yoyote ya mwili wake.

"Bosi nywila imepatikana saivi inasoma Tiptop Manzese nasubiri amri yako mkuu" mwanaume huyo ambaye ndiye aliyeweza kuiokota hiyo bahasha alikuwa akisubiri amri ya mkuu wake baada ya kupiga simu sehemu isiyo julikana.

"Wape maelekezo vijana wa kule Manzese wamfuate namhitaji ndani ya masaa matatu yajayo nije nifanye naye mazungumzo" Aliye onekana kuwa ndo bosi wake alijibu bila wasi wasi akionekana wazi alikuwa kwenye eneo ambalo lilikuwa limetulia sana.

"Wale wa mtaani ni vijana wadogo sana nilitaka niende mwenyewe ili kama kutakuwa na tatizo nilimalize huko huko"

"Kinacho fuatwa ni kitu kidogo sana vijana wataishia Tazara wewe utamaliza palipo bakia" Baada ya kumaliza kutamka hayo maneno simu yake ilikatwa. Walikuwa wanaongea akijua bosi wake kwa wakati huo yupo mbali sana lakini jambo la kushangaza ni kwamba alikuwa chumba cha pili tu kutoka hapo na alikuwa anaona kila kitu kilichokuwa kinaendelea humo ndani akiwa mbele ya skrini yake kubwa iliyo muwezesha kutazama kila pembe ya nyumba yake kwa usahihi. Huyu ndiye yule mshona viatu wa Mburahati na hapa alikuwa yupo kwenye makazi yake ya Siri ambako walikujua walinzi wake wachache sana, watu wake wengi hawakuwahi kujua huyo binadamu alikuwa anaishi wapi kwa sababu walikuwa wanamuogopa mno kulingana na aliyokuwa akiyafanya kwenye maisha yake

TIPTOP
Ndani ya club kubwa sana kwenye hayo maeneo, ni club maarufu sana hiyo sehemu ukiwa unakatiza kwenye kila mtaa wa hili jiji kwa wale wala bata hakuna mtu ambaye angeshindwa kukupeleka hiyo sehemu. Ni bar na club ambayo kila siku huwa inafunguliwa, watu walikuwa wako busy kula maisha kama kauli za mjini zinavyo jieleza vizuri huku wengine wakivitumikisha viungo vya miili yao kwa baadhi ya warembo ambao walikuwa wanapendeza sana majira ya usiku hayo maeneo ili kuweza kupata sababu ya kupeleka mkono kinywani, wakati watafutaji wakiwa busy kuwekeza hususani boda boda wanao jaa kwenye hayo maeneo wakimuomba MUNGU awaongezee wapenda starehe zaidi ili wapate kipato cha kutosha kwenye hiyo kazi yao ngumu ambayo ilikuwa ikiwafanya wasilale kabisa baadhi ya maskini wengi au waweza kuwaita maskini watarajiwa walikuwa wanatumia pesa zao wakijifariji kwamba wanawaka lawama watajipa asubuhi

Kwenye kaunta moja hayo maeneo alikuwa amekaa binti mmoja ambaye alikuwa na mlinzi wake mmoja tu pekee, ilikuwa ni ngumu sana kuweza kumtambua kama ni mlinzi wake, kinywaji kizuri taratibu kilikuwa kikilainisha koo lake bila kuwa na wasi wasi wowote ule maisha mazuri ndiyo ilikuwa asili yake hakuwa na mawazo ya kujutia kesho pindi anapotumia pesa zake huyo mwanamke. Deodata Romeo ndilo lilikuwa jina halisi ya huyu binti ambaye kiumri bado alikuwa mdogo sana na miaka yake ishirini na miwili tu. Ghafla sana umeme ulizima hilo eneo kitu ambacho hakikuwa cha kawaida kabisa kwa sababu hata kama umeme wa Tanesco ungezima basi jenerata zilikuwa zinajiwasha zenyewe ila haikutokea hivyo hata kidogo. Meneja wa hiyo Club alikuwa akihangaika na jenereta zote zilizokuwa zinatumika hapo hakuna hata moja iliyokuwa imekubali kuwaka. Dakika moja mbele mlinzi wa Deodata alikuwa anawasha simu yake ili kuendelea kudumisha ulinzi kwa mwanamke huyo ambaye ndiye aliyekuwa anamfanya ale vizuri mjini baada ya kuona umeme haurudi lakini alishangazwa sana baada ya kuona mwanamke huyo hayupo kabisa kwenye hilo eneo alihisi huenda atakuwa kaenda uani alisubiri kama dakika tatu ikambidi aende kwa lazima kwenye vyoo vya kike hakukuwa na mtu yeyote yule.

"Madam!, Madam!" Alikuwa akiita kwa nguvu huku akiwasukuma watu ili apite haraka huyo mwanamke alikuwa ni hatari sana akipotea kwenye mikono yake, alitoka haraka sana mpaka nje lakini hakumuona kabisa na alishangaa umeme haukukata tu humo ndani bali ni Manzese nzima hakukuwa na umeme mpaka maeneo ya Urafiki, alihisi kuchanyikiwa alikaa chini akiita jina hilo kwa sauti kali ila hata hivi haikusaidia chochote binti alikuwa amepotea kwenye mikono yake kizembe sana.

Dakika tano nyuma
yela mwanamke ambaye alikuwa anashinda na komputa mpaka zilimkaa kichwani mwake alikuwa akiangalia wanaume watano ambao walikuwa wanaingia kwenye hiyo Club ya Tiptop baada ya kuhakikisha wameingia ndani na wamekiona walichokuwa wanakitafuta alizima umeme kwa komputa zake Manzese nzima na sehemu za karibu na hapo. Deodata akiwa amekaa pale baada ya umeme kuzima tu kuna mwanaume alipita karibu yake, vidole viwili ndivyo vilivyo tumika kumaliza kazi nzima vilipitishwa kwa nguvu kwenye shingo yake kwenye hicho kiza totoro, hakuweza hata kupiga kelele hapo hapo alizima wakati anataka kudondoka kwenye kiti chake alidakwa na mwanaume huyo ambaye aliondoka naye kwa kasi sana, alipiga mluzi mara moja tu wenzake wote walikuwa wapo nje waliondoka hapo bila kutazama nyuma wakiwa wanaelekea Kagera ambapo ndipo walikuwa wameliacha gari lao la kuwawezesha kumfikisha mwanamke huyo kwenye sehemu ambayo walihitajika kumpeleka na kumuacha hapo kisha mtu mwingine angemchukua.

Safari yao ilienda kuishia hapo Kagera kwenye kituo cha mwendokasi ambapo walikuwa kati Kati ya barabara hiyo, mwanaume wa mbele ambaye ndiye aliyekuwa amembeba mtoto wa kike huyo wakati amezimia alisimama ghafla baada ya kusikia harufu kali ya sigara, kulitulia sana hapo siku hiyo ya jumatano usiku wa manane huo, watu walikuwa wachache sana akikatiza mmoja mmoja harufu hiyo ya sigara ilimpa tahadhali kuna ugeni hapo kwa sababu kusingekuwa na mtu mwenye ujasiri wa kuweza kuwepo hayo maeneo kwa hali iliyokuwa hapo.

Juu ya mabati ya kituo hicho cha mwendokasi kuna mwanaume alikuwa amekaa hapo akiwa hana hata tone la wasi wasi, Moshi mwingi uliokuwa unatoka kwenye mdomo wake na kwenye pua zake mbili ndio uliomfanya asiweze kujulikana kirahisi aliitupa sigara hiyo kwa nguvu kuelekea walipokuwa hao wanaume hapo chini mmoja wao alijirusha juu na kuizima kwa nguvu ya teke lake tu kisha akatulia kimya. Sarakasi moja ya kasi kubwa ilimfanya sekunde mbili tu mwanaume huyo atue chini kabisa kwenye barabara hiyo ya mwendokasi mkononi mwake alikuwa anachezea kisu kidogo dogo akikizungusha, mwilini mwake ni koti kubwa ndilo lililokuwa linaonekana kwenye hicho kiza.

"Nipeni huyo binti halafu ondokeni msije kufanya tena hiki ambacho mlitaka kukifanya na msije mkarudia tena kufanya hicho kitu kwenye maisha yenu yote wala kumgusa huyo binti mtaishi maisha magumu sana na familia zenu". Huyo mwanaume alitamka kwa sauti yake ya kukwaruza ambayo ni wazi alionekana kuisikilizia hatufu kali ya sigara ghali sana ambayo ilikuwa inapita kwenye pua zake bado.

"Chukua na uondoke hatujaja kuua" mmoja kati yao alimrushia huyo mwanaume noti mbili za shilingi elfu kumi akijua huyo lazima ni kibaka na hapo alikuwa anatafuta kula, kosa moja lingegharimu maisha ya huyo kijana kwa dharau kubwa ambayo alikuwa ameionyesha. Mwanaume aliyekuwa amesimama mbele yake ni Alexander muuaji, hadithi ya maisha yake ilikuwa ya kutisha sana hata yeye mwenyewe alikuwa anatisha mno, huyu ndiye aliye muua Mr Jonson Malisaba na familia yake yote ilitisha hata kulisikia jina lake ni muuaji mkubwa sana mjini na leo alikuwa ametembelea mitaa ya Manzese hapa.

"Kitakacho kukuta leo inabidi kama ukitoka ukiwa hai kesho kafungue sehemu ya ibada uanze kuungama dhambi zako mapema huyo binti mdogo ndiyo roho yangu, huyo ndiyo maisha yangu na ndiyo sababu ya kunifanya mimi niendelee kuwa hai huenda mpaka leo ningekuwa nimeshajiua" kumalizika kwa sentensi yake kulifutiwa na urushaji wa kisu ambacho kilienda kuishia kwenye shingo ya yule kijana aliyekuwa akiongea kwa dharau kubwa sana, vijana walikuwa na uwezo mdogo sana kusimama na mtu wa kutisha sana mbele yao kama huyu. Hakuna ambaye alipelekea mkono wake mfupa ukaendelea kufanya kazi. Yule kijana ambaye ndiye alikuwa amembeba Deodata alipigwa na mtama ambao ulikuwa unampeleka chini akiwa anataka kudondoka na binti hilo lilikuwa ni kosa moja kubwa sana kama mwanamke huyo angefanikiwa kugusa chini, kabla ya kufika chini yule kijana alipigwa goti na ngumi ya shingo ambayo ilivunja shingo nzima kisha Deodata akadakwa na kuegemeshwa kwenye kuta za hicho kituo cha mwendokasi vizuri kabisa. Mwanaume aliivunja kila shingo ya kijana ambaye alikuwa hapo.

Alikuwa anaondoka taratibu mpaka alipofika Tiptop barabarani kabisa karibu na palipokuwa na Club hiyo alimkuta mlinzi wa Deodata akiwa njiani amepiga magoti analia alikuwa anaogopa Sana kumpoteza binti huyo angepatwa na matatizo mengi sana.

"Ni aibu sana kama watoto wadogo kama hao wanamchukua nawewe upo hapo hapo, kama ikitokea akaja kuumizwa hata damu yake ikatoka kidogo basi jiue mwenyewe kabla sijakupata nitakuchinja kama kuku, nyoosha na hiyo bara bara" ni sauti nzito ya Alexander akimpa maagizo mlinzi huyo wa Deodata ambaye alikuwa ameogopa sana kumuona huyo binadamu mbele yake moyo wake ulikuwa unataka kupasuka hakujua angemweleza nini baada ya binti huyo kupotea bahati nzuri yeye mwenyewe alikuwa yupo mitaa hiyo, Alexander baada ya kumaliza maelezo yake alimrushia kijana huyo maburungutu mawili yaliyo jaa pesa nyingi sana za kitanzania kisha yeye akapotelea gizani umeme ukiwa bado haujarudi. Kijana huyo alikusanya hizo pesa kwa uoga na kukimbia kwa kasi sana kuelekea sehemu ambayo alielekezwa atampata binti huyo ambaye hakuwa na fahamu mpaka huo muda.

Deotada ni nani hasa, ana nini mpaka anawindwa na hawa watu wazito sana kiasi hiki, Alexander muuaji wa kutisha huyu anahusiana vipi na binti mdogo kama huyu na ni nani hasa kwake mpaka awe na uchungu naye sana kiasi hiki?......ndo kwanzaaaaa tunaianza simulizi yetu taamu sana.

18 sina la ziada tena tukutane wakati ujao.

SEHEMU YA KUMI NA TISA

TULIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA NANE.........

ENDELEA......................

M96 OWNE'Z TOWER
Maeneo hayo ilipokuwepo ofisi kubwa ya kampuni iliyo julikana kwa kujihusisha sana na usindikaji wa nyama leo kulikuwa na mkutano mkubwa wa kumtambulisha kiongozi mkubwa sana wa hiyo kampuni, ni siku ambayo wafanyakazi wote walitakiwa kuwahi kuliko siku zozote zile ambazo waliwahi kufanya kazi kwenye kampuni hiyo, hawakuelewa ni nani ambaye alikuwa anasubiriwa kiasi hicho. Kwenye ukumbi mkubwa wa mikutano ndani ya hiyo kampuni uliokuwa na uwezo wa kubeba zaidi ya watu miambili ulikuwa umejaa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao wote walikuwa wamevaa suti safi sana nyeusi na shati za blue, nusu saa baadae gari moja ya kifahari sana ilikuwa inafika kwenye sehemu ya kuhifadhia magari chini kabisa kwenye hiyo kampuni. Ndani ya hiyo gari mlango ulifunguliwa alishuka kijana mmoja smati sana, Ashrafu Hamad ndiye mwanaume aliyekuwa ndani ya hiyo gari. Aliponaje wakati tuliona alipigwa risasi na Alexander ndani ya Mikocheni!, Hii ndio dunia ya baadhi ya wanadamu huwa wanaishi watakavyo wao, kwa umri wake alikuwa amefanya vitu vingi sana vya hatari bila kuwa na wasi wasi wowote wala kuogopa chochote ndani ya nchi, nguvu kubwa aliyokuwa nayo nyuma yake ndiyo iliyompa jeuri ya kufanya chochote kile ambacho alijiskia yeye.

Ndiye mtoto pekee wa mheshimiwa makamu wa raisi wa nchi ya Tanzania japo ilikuwa ni kwa siri kubwa mno. Akiwa kwenye lifti kupandisha kwenye ukumbi maalumu uliokuwa kwa ajili ya mitihani alikuwa ndani ya miwani yake ya gharama ambayo kiuhalisia haikuwa miwani ya kawaida kabisa, ndani ya miwani hiyo kulikuwa na mionzi mikubwa ambayo ilikuwa inampa uwezo wa kutoweza kuchukuliwa picha yoyote ile unapo mpiga, akiwa ndani ya hiyo miwani hauna uwezo kabisa wa kuweza kuipata picha ya sura yake hata kama ungekuwa nani, alikumbuka namna anavyo yaishi maisha yake mpaka watu wengi huwa wanashindwa kabisa kumpata mtu huyu anaishi ndani ya nafsi tano tofauti tofauti. Nafsi ya kwanza ni huyu yeye mwenyewe ambaye ndiye aliyekuwa anaingia leo rasmi ndani ya kampuni baada ya kutokuwepo Kwa muda mrefu sana ndani ya hiyo kampuni uongozi akiuacha kwa meneja wake wakati huo yeye alikuwa ni omba omba mitaa ya Buguruni sokoni, nafsi ya pili ni ile aliyokuwa anaishi kwenye sura ya uzee kama omba omba na kichaa, lakini nafsi ta tatu mpaka ya tano walikuwa ni watu wengine ambao walikuwa wametengenezwa kama yeye, sayansi imeenda mbali sana siku hizi, mashine zilifanya kazi kwa asilimia miamoja,wanaume watatu walikuwa wametengenezwa kwa mfano wake kwa kila kitu, mmoja wao ndiye huyo ambaye aliuawa na Alexander siku ile mikocheni akijua ni Ashrafu mwenyewe huku yeye akiwa salama kwa asilimia miamoja hivyo walikuwa wamebaki watu wawili wengine ambao wapo kwa mfano wake, huyo ndiye Ashrafu Hamad alikuwa ametengenezwa kuwa mtu hatari mno likiwa kama ndilo jicho kuu la M96 OWNE'Z.

Alitabasamu sana baada ya kukumbuka kile ambacho kilikuwa kimetomea maeneo ya Mikocheni kwa sababu wengi walikuwa wameiona picha yake na kujua kwamba ameshakufa japokuwa hawakuwahi kujua kama huyo kijana ni mtoto wa damu kabisa wa makamu wa raisi wa nchi. Yeye pekee ndiye aliyekuwa anasubiriwa ndani ya chumba hicho, akiwa amezungukwa na wanaume walioshiba vizuri wawili mlango wa kifahari wa chumba hicho ulifunguliwa na mwanaume alikuwa akiingia Kwa mbwembwe kubwa na sura yake hiyo ambayo ilimshangaza kila mmoja, wafanyakazi wote walisimama kutoa heshima ila wote walikuwa kwenye mshangao mkubwa sana, huyo mtu mbele yao siku kadhaa nyuma kila chombo cha habari kilitangaza kwamba tayari ameshakufa leo alikuwa anaonekana mbele yao akiwa mzima wa afya.

"Hili linawezekana vipi kutuletea mizimu hapa ndani, hili jambo halikubaliki kabisa siwezi kukubali mimi" Mwanaume mmoja ambaye alikuwa mfanyakazi humo ndani aliongea kwa hasira na kutoka kwenye hicho chumba cha mkutano, kitendo alicho kifanya kilimfanya awe miongoni mwa wanadamu waliokuwa na muda mchache sana wa kuendelea kuishi kwenye uso wa dunia, kuna mwanaume alimpiga ngumi nzito ya mbavu ambayo haikumuwezesha hata kutoa sauti yoyote ile risasi sita za mbavu zilimhusu ndani mkutano ukiwa unaendelea hakuna aliyeweza kushtukia chochote, alitolewa na kwenda kutupwa kwenye shimo kubwa la siri nyuma ya hilo jengo kubwa.

"Huyu mtu anaye onekana hapo mbele sio mimi nadhani ndipo utofauti wa MUNGU na wanadamu unapoweza kutokea, kuna watu huwa tunazaliwa kwa mfanano na kuwa sawa kwa kila kitu, kwa majina naitwa Ashrafu Hamad, ni kijana mdogo tu wa kawaida ambaye niliamua kuzitafuta ndoto zangu nikiwa bado mdogo sana na ndiyo sababu nilifanikiwa kuwa na mafanikio makubwa sana kwenye umri mdogo mno. Mimi ndiye mmiliki wa hii kampuni, Leo nimekuja hapa ili wafanyakazi wote muweze kunijua vizuri maana ni wachache sana kati yenu ambao walifanikiwa kunifahamu kwamba mimi ndiye mmiliki. Nadhani hakuna anaye ruhusiwa kwenda kusambaza popote pale kuhusu mimi kuwa mzima itaharibu sana taswira ya kampuni yetu acheni tu wanao amini kwamba nimekufa waamini hivyo ila zingatieni hakuna yeyote anaye ruhusiwa kuongea hili jambo popote pale itakuwa ni hatari sana kwake" hotuba yake fupi iliweza kuwaacha njiapanda watu wote waliokuwepo humo ndani baada ya skrini kubwa iliyokuwa imewashwa ikiwa na picha ya kijana aliyepigwa risasi ambaye kila kitu alikuwa kama Ashrafu kuzimwa, jambo la kwanza taarifa kuhusu kuishi kwake na kufanana na mtu aliyepigwa risasi zilikuwa ni chache sana walihitaji maelezo ya kutosha kwani hakukuwa na utofauti wowote baina ya hao watu, jambo la pili lilikuwa ni aina ya mkutano ambao alikuwa ameufanya, ilikuwa ni hotuba ya dakika mbili tu kujitambulisha kama yeye ndiye bosi hakuna mtu hata mmoja ambaye aliruhusiwa kuuliza maswali yoyote yale, walibaki njiapanda hata hivi hawakuwa na namna yoyote ile.

"Kama akifanya kitu cha kijinga muueni anaweza kuja kuwa na akili mbovu baadae huyu mtoto simuelewi elewi sana mambo yake, mfuatilieni kwa mwezi mmoja mkiona haridhishi sana sitaki uzembe nitamuua mwenyewe na baba yake" sauti yenye uzito wa kutosha ilikuwa imepenya Kwa wanaume ambaye alikuwa yupo karibu na chumba chenye komputa nyingi sana ndani ya Chanika kupitia spika ndogo ambayo ilikuwa ipo sikioni mwake. Mwili wake mkono mmoja huyo mwanaume ulikuwa umetengenezwa kwa chuma ilionekana kwamba sehemu moja ta mkono huo ulinyofolewa na mtu ambaye hakuwa wa kawaida.

Yale yote yaliyokuwa yanafanyika Mzee huyo ndani ya Chanika alikuwa kwenye chumba chake ambacho hakuna mfanyakazi aliwahi kuingia humo ndani, alikuwa amesimama anatazama kila hatua ya kilichokuwa kinafanyika ndani ya M96 OWNE'Z. Baada ya kutoa maagizo aliingia kwenye kordo ndogo iliyokuwa kwenye hicho chumba chake, alibonyeza herufi kadhaa ukutani ukuta ukajifungua akaingia huko ndani kisha mlango ukajifunga tena. Huko ndani ndipo kilipokuwa chumba chake cha mazoezi, kulikuwa na kila aina ya silaha za kutisha hapa duniani. Bastola za kisasa, bunduki za masaafa marefu zilijaa hapo ukutani lakini safari yake ilienda kuishia kwenye visu viwili vidogo vidogo, alivua shati lake kwa namna ambavyo mwili wake ulikuwa umepasuka usingeweza kuamini kwamba umri wake ulikuwa umeenda sana. Yalifuata mazoezi makali mno akiwa na visu vyake viwili mkononi yalitokea maroboti ambayo yalikuwa yametengenezwa na panga zao kwenye vufundo vya mikono ya chuma ya viumbe hivyo na hayo ndiyo yalikuwa mazoezi yake huyu Mzee, ilikuwa ni michezo ya hatari sana Kwa sababu kama angecheza vibaya alikuwa anakufa kweli. Kazi yake kubwa ilikuwa ni kucheza na hayo maroboti kwa dakika tano kama angefanikiwa kumaliza dakika hizo tano akiwa bado mzima basi yalikuwa yanapotea mshindi ni yeye ila kama angeshindwa kufikisha hizo dakika basi yalikuwa yanamuua yeye.

Dakika tano ni chache sana unapokuwa unazitamka mdomoni ila ukija kwenye kuzitekeleza kwenye mapigano unaweza ukahisi umetumia siku nzima, mzee huyu alikuwa amekomaa mikono yake kiasi kwamba hayo maroboti yalikuwa yakipinda kila akipitisha mikono yake kwenye hivyo vyuma, hakuwa na presha sana mpaka muda huo alikuwa ametumia dakika zake nne tu ikibakia moja alichanwa kidogo na kisu cha moja ya roboti, roboti jingine lilikuwa limelengesha upanga kwenye shingo yake alirusha visu vyake viwili Kwa nguvu vilienda kunasa ukutani alikimbia kwa nguvu kuelekea sehemu ya ukuta huo roboti likiwa linakuja nyuma alidunda kwenye hivyo visu vyake wakati anageuka alirusha ngumi nzito ambayo ilienda kulipata hilo toboti kichwani yote yakapotea kwa kasi dakika tano zilikuwa tayari zimeisha, haya ndiyo mambo ambayo huwa anayafanya kwa siri kubwa hakuna ambaye alikuwa anajua mzee huyu ni mtu wa kutisha namna hii wengi walijua anategemea tu nguvu ya vijana wake kuweza kufanya matukio ya hatari ila kama akiamua siku moja kujitokeza hadharani yatatokea maafa makubwa ya kutisha kwenye hili jiji la wapenda starehe.

Baada ya kumaliza alijiweka dawa kwenye hilo jeraha dakika tatu alikunja ndita maumivu aliyokuwa akiyapata hapo kwa mtu mwepesi ni lazima angepoteza fahamu aliingia kwenye mashine moja iliyokuwa inatoa mionzi mikali, aliielekezea mionzi hiyo kwenye hicho kidonda dakika moja mbele sehemu aliyokuwa amekatwa ilikuwa imejiunga lakini alikuwa akitoa machozi machoni pake mionzi ilikuwa imemuunguza vibaya sana kwenye kidonda hakukuwa na alama yoyote ile hata kama ungeambiwa hapo palikuwa na jeraha kubwa ungegoma kwa kula kiapo kabisa na hayo ndiyo maisha ya watu wa kutisha hata vitu vyao huwa ni vya kutisha sana. Alivaa suti yake nzuri leo kwa mara ya kwanza alikuwa ameingia kwenye chumba ambacho bibie mtaalamu wa komputa alikuwa akishinda ndipo kilipokuwa kituo chake cha kukaa kwa muda wote ambao alikuwa humu ndani.

"Uzembe wa baadhi ya watoto unakufanya uendelee kukaa hapa kwa mara nyingine, kuachiwa kwako ni mpaka huyo binti aletwe kwenye mikono yangu" sauti nzito ndiyo iliyo mshtua mwanamke huyo aliyekuwa ameanza kusinzia baada ya muda mrefu macho yake kuwa mbele ya komputa hizo.

"Naombeni tafadhali familia yangu isiguswe nitafanya chochote kile" huo ndio udhaifu ambao ukiwa nao kwenye maisha watu watakutumia watakavyo wao, mwanamke huyo alionekana kushikiliwa familia yake ndio maana alikuwa anafanya kazi na huyu mtu ambaye kwake ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kabisa kumuona kwenye maisha yake, mwanaume hakujibu chochote akaangalia saa yake kisha akageuka.

"Huwa siishi nje ya maneno yangu" ni maneno aliyo yatamka baada ya kuanza kuutoa mguu wake humo ndani, alisimama baada ya kusikia hatua za miguu ya mtu ikinyata, alitulia tu ghafla mbele yake akatokoea mfanyakazi mmoja ambaye alionekana wazi alikuwa akimvizia mwanamke aliyekuwa ndani ya hicho chumba cha komputa, alishtuka baada ya kumuona bosi wake hapo ni zaidi ya mwezi alikuwa hajawahi kumuona huyo mwanaume na lilikuwa ni kosa kumuona sura yake, ni kosa kubwa sana alilifanya la kumuangalia usoni tajiri wake huyo, Mzee huyo aliichomoa bastola yake na kumtandika huyo kijana risasi sita kichwani kisha akatoka humo ndani, bibie alibaki anatetemeka sana hakuwahi kabisa kushuhudia mtu akiuawa mbele ya macho yake leo alishuhudia hilo. Alikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha Deodata anapatikana ndipo aweze kuachiwa japokuwa alikuwa amesema yupo tayari kufanya lolote lile ili tu awe salama hakujua madhara ya hiyo kauli yake huenda angejua kinacho enda kumtokea asingethubutu kuongea kauli hiyo mbele ya huyo mzee ambaye kiundani hakumjua hata kidogo na ndo leo alibahatika kukutana naye kwa mara ya kwanza.

19 sina la ziada tena tukutane wakati ujao

SEHEMU YA ISHIRINI

TULIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA TISA.........

Alikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha Deodata anapatikana ndipo aweze kuachiwa japokuwa alikuwa amesema yupo tayari kufanya lolote lile ili tu awe salama hakujua madhara ya hiyo kauli yake huenda angejua kinacho enda kumtokea asingethubutu kuongea kauli hiyo mbele ya huyo mzee ambaye kiundani hakumjua hata kidogo na ndo leo alibahatika kukutana naye kwa mara ya kwanza.

ENDELEA...................

Mwananyamala ndilo eneo langu la kwanza kabisa kufika ndani ya jiji la Dar es salaam, kwa mara ya kwanza kabisa ndipo tulipoweza kuingia ndani ya jiji hili ambalo tulikuwa hatujawahi hata kulisikia wala kuelewa nini kinaendelea ndani yake, baada ya gari ile ambayo ilikuwa imebeba mbao kusimama mimi na pacha wangu tuliweza kushuka pale tukiwa tunashangaa sana, kila kitu kilikuwa kigeni kabisa kwetu, mataa, majengo makubwa sana ambayo mengine tulijua yanaweza kushuka na kudondoka chini tulikuwa tunayakimbia baada ya kushuka hapo chini. Maisha tuliyokulia hatukuwahi kujua kwamba kuna maisha mengine huku nje ambayo kuna watu wanaishi namna hiyo na kuweza kuvaa nguo hizi ambazo mpaka leo mimi mwenyewe nimekuwa mvaaji mkubwa tu kwenye dunia yenu, tumezaliwa kwenye maisha ambayo magome ya miti ndiyo nguo zetu kubwa tukiziba sehemu zetu za siri tu pekee. Huatukujua mwenyeji wetu angekuwa nani kwenye sehemu ambayo hatukuwahi kufika kabla na hatukuwa na mtu yeyote yule ambaye angeweza kutusaidia kwa kila kitu ambacho tulihitaji kukifanya ndani ya huu mji.

Kibaya sana lugha yetu haikuwa rafiki kabisa kuweza kuwasiliana na mtu yeyote yule, kwetu tulizoea mtu ukiwa una shida basi unaenda kwa jirani anakupatia kila kitu lakini ilikuwa tofauti sana na huku ambako kila kitu kilikuwa kikihitaji kitu ambacho kinaitwa pesa, hatukuwahi kuzijua kabla hivyo tulikuwa hatuelewi tunaanzia wapi, mvua nyingi zisizoisha na chakula cha majalalani ndiyo ilikuwa sehemu pekee ya kuweza kutufanya sisi tuendelee kuishi ndani ya sehemu ambayo mtu mwenye pesa pekeyake ndiye anayesikilizwa au mwenye uhuru wa kuweza kufanya chochote kile ambacho angehisi kwake ni sahihi. Iliisha zaidi ya miezi sita tukiwa tunahangaika mtaani kula kwetu ilikuwa ni neema za mwenyezi MUNGU bahati mbaya sana ndugu yangu alikuwa akinisumbua sana kuhusu kujua mama na baba walikuwa wapi kwa sababu hakujua chochote usiku ule ambao rasmi tuliingia kwenye ulimwengu wa watoto yatima, kila nikimuangalia mdogo wangu nilikuwa napata hasira kali sana kwenye maisha yangu hivyo nilianza rasmi kutafuta vibarua vya kufanya kazi hapa na hapa ili kidogo tuweze kupeleka mkono kinywani japo nilikuwa bado ni mdogo sana na watu wengi hawakuwa tayari kunipa kazi kwa sababu ya kuogopa sheria za serikali. Usiku mmoja nikiwa nimetoka kubeba mchanga nilikuwa narudi kwenye kibanda chetu ambacho ndicho kilitufanya tupate sehemu ya kuweza kulaza mbavu zetu, nilikuwa na mawazo mengi mno sikuangalia hata usalama wangu ndani ya bara bara niligongwa na gari vibaya sana sikuweza kuelewa nini kilikuwa kinaendelea, nilikuja kuzinduka nikiwa ndani ya hospitali siku ya kesho yake, nilishangaa sana hiyo sehemu natafuta nini ndipo nilipoweza kurejesha kumbu kumbu zangu kwamba mara ya mwisho nilikuwa nakatiza barabarani, nilikurupuka kitandani hapo na kuchomoa drip za maji ambazo nilikuwa nimefungwa kwenye mikono yangu, akili ilikuja kufunguka baada ya kumkumbuka pacha wangu, niliamka na kuanza kukimbia sana kwa sababu mpaka wakati huo sikujua atakuwa kwenye hali gani tangu jana yake sikuweza kufika kwenye kibanda chetu. Wakati nafika nje nilidakwa na mlinzi wakati nakaribia kufika getini pembeni alishuka kwenye gari mwanamke mmoja ambaye kwa mwonekano tu alionekana ana vyake mjini na ndiye aliye muamuru yule mlinzi aweze kunikamata.

“Unaitwa nani?” lilikuwa swali lake la kwanza kwangu

“Nwoku Bateli Nyanike” nilimjibu kiufupi kwa sababu nilikuwa kidogo nimeanza kuelewa elewa maneno kadhaa kwa miezi yangu kadhaa ambayo nilikuwa nimekaa hapa mjini, sikuwa nikijua kuongea vyema ila nilikuwa nina uwezo wa kujibu maswali madogo madogo.

“Wazazi wako wako wapi?” swali lake la pili lilinifanya nitoe chozi kwa sababu alinikumbusha kitu ambacho sikuwa nikihitaji kinirudie kichwani mwangu kabisa, nilimjibu kwa kutikisa kichwa tu kumaanisha kukataa kabisa hicho kitu alinisikitikia sana.

“Naomba unisamehe sana mwanangu mimi ndiye niliyeweza kukusababishia ajali siku ya jana hivyo niliamua kukuleta hapa hospitali ili kuweza kuokoa maisha yako kwa sababu umesema huna wazazi basi twende nikakuuguze nyumbani kwangu mpaka pale utakapo pata nafuu ndipo uweze kuendelea na maisha mengine siwezi kukuacha kwa sasa pekeako kwenye hiyo hali wewe bado ni mdogo sana” maneno yake yalinipa faraja lakini sikuweza kukubali kwa sababu nisingeweza kuishi bila ndugu yangu.

“Siwezi kumuacha ndugu yangu kamwe, nashukuru sana kwa wema wako” japo maneno yangu hayakueleweka vizuri ila alinielewa, ni miongoni mwa wanawake ambao walikuwa bora sana hapa duniani sijajua kama yupo hai au mwenyezi MUNGU alisha mchukua ila namuombea aweze kupumzika salama huko aliko amuweke sehemu salama sana ila kama yupo hai namuombea aishi kwa miaka mingi. Licha ya kumwambia hayo yote aliniomba niweze kumpeleka huko alikokuwa ndugu yangu, sikuwa na hiyana nilikubali nikapanda kwenye gari yake japokuwa bado hali yangu haikuwa nzuri sana, saa moja lilitufanya tufike huko tulikokuwa tunaenda, iliniuma sana baada ya kumuona ndugu yangu akiwa amejikumbata analia sana tangu jana hakuwa ameniona wala kula chochote, nilimkimbilia na kumkumbatia, nilimpenda kuliko kitu chochote kile. Yule mama alituambia tuache kila kitu tuweze kuingia kwenye gari yake, sikuwa na hiyana nikamchukua ndugu yangu tukaingia kwenye gari.

Safari yetu iliishia kwenye jumba moja la kifahari sana, sikuelewa tulienda pale kufanya nini lakini yule mwanamke alinitoa hofu kwamba tutaishi naye pale mpaka nitakapoweza kupona ndipo niondoke na ndugu yangu, kiukweli nilifurahi sana kwa sababu nilikuwa na uhakika kwamba ndugu yangu lazima angeishi maisha mazuri pale. Tulianza kufundishwa namna ya kuongea, watu wanavyo vaa, kusoma yaani kiufupi yule alikuwa kama mama kwetu, miaka saba ya kuishi kwa furaha mle ndani ilitufanya tusikumbuke kwamba tulikuwa yatima alifanya kila kitu kama mzazi kwenye maisha yetu. Sikuwahi kufikiria kama tutaishi kwenye maisha magumu tena ila hii hali ilianza baada ya mwanaume ambaye alikuwa ni mchumba wa yule mwanamke kurudi kutoka nje za nchi ambako alikuwa ameenda kwenye masomo kwa maelezo tuliyokuja kupewa pamoja na kufanya biashara, alikuwa tofauti sana na mwanamke wake, tulianza kupigwa sana na yule mwanaume bila sababu zozote zile. Ni wikiendi moja ambayo tulifukuzwa kwenye ile nyumba baada ya yule mwanamke ambaye alikuwa akitujali sana kama watoto wake kusafiri tukabaki na mumewake pamoja na wafanyakazi wa ndani tu, tulipigwa sana ile siku pamoja na kufukuzwa jumla kwa kutishiwa bastola kama tungekuwa wabishi basi ilikuwa inaenda kutumika kuweza kutuua. Iliniuma sana kwa sababu sikupata hata nafasi ya kumuaga mwanamke ambaye tuliishi naye kwa upendo kwa zaidi ya miaka saba ila hakukuwa na namna.

Tulikuwa wakubwa kiasi miaka kumi na mitano ilitosheleza kabisa kuweza kujisimamia mtaani, tulitafuta kazi za kuosha magari tulifanikiwa kupata sehemu moja ndani ya Magomeni. Tulikuwa wacheshi kwa kila mtu hivyo ilitufanya tupendwe sana tulikuwa watu wa kazi sana kwa sababu hatukuwa na msaada mwinginge wowote zaidi ya sisi wenyewe japo hatukuwahi kumsahau yule mwanamke aliye tusaidia tulizidi kumuombea kila siku iendayo kwa MUNGU. Ulivyofika mwezi wa tatu tukiwa pale kuna mzee mmoja ambaye alionekana ndio alikuwa anauaga aga ujana na kuianza safari ya uzeeni alikuwa kila akija pale lazima sisi pekee ndio tumuoshee gari lake, hakuwahi hata siku moja kumruhusu mtu mwingine yeyote yule aiguse hiyo gari, kuna muda nilikuwa nikipata maswali mengi sana kwamba kuna nini mpaka iwe hivyo lakini sikuwahi kupata jibu sahihi kuhusu uhalisia wa jambo hilo. Alizoea sana kufika hapo, siku moja mida ya jioni baada ya kuoshewa gari yake aliniita pembeni na kunipa kadi yake ya biashara ambayo ilikuwa na namba sifuri tano pamoja na namba moja ikiwa imejirudia mara tano, kwa uzoefu wangu tangu nifike hapa mjini sikuwahi kuona namba ya simu ya namna hiyo, alinisisitiza sana kwamba nihakikishe namtafuta kwa gharama yoyote ile nilikuwa muwazi na kumwambia kwamba sikuwa na simu ambayo ingenifanya nipate naye mwasiliano, aliingiza mkono wake kwenye droo ya mbele ya hiyo gari akatoka na simu ndogo mpya.

“Kuna laini humo ndani hakikisha hakuna mtu anaipata wala kumuonyesha namba yangu zingatia sana hilo” nilishangaa sana kuhusu yale maelezo yake lakini niliamua kukaa kimya kama alivyokuwa ameniomba hata ndugu yangu sikuwahi kumwambia kitu chochote kile. Zilipita siku tatu nikiwa najiuliza kama nimtafute au nisimtafute, zaidi ya asilimia sabini moyo wangu ulikuwa unasita kabisa kumtafuta yule mtu, nikiwa najishauri niliiona gari yake kwa mbali sana halikuweza kufika kwenye ile sehemu ambayo huwa tunaoshea kama ilivyokuwa siku zote. Nilijua alikuwa pale kwa ajili yangu ilinibidi niende japokuwa moyo wangu ulikuwa unanienda mbio sana.

“Mbona hukunitafuta kijana?” sikuwa na cha kujibu niliinama chini tu sababu ya msingi ya swali lake sikuwa nayo kabisa.

“Ingia kwenye gari” alitamka hivyo baada ya kuona simjibu chochote, ni miongoni mwa siku ambazo nilikuwa natetemeka sana ila sikuwa na namna niliingia japokuwa nilikuwa naogopa huenda atakuwa mtu mbaya sana. Ndani ya gari nilikuta bastola na vitambulisho vingi sana ambavyo sikuvitambua haraka vilikuwa vya nini, hali ya kuiona bastola ilinitisha sana nilikumbuka tukio la yule mwanaume ambaye alitufukuza kwake niliogopa mno.

“Unamuona yule mwanaume ambaye anaingia kwenye lile duka pale?” kauli yake ilinifanya nigeuze macho kuangalia hiyo sehemu ambayo alikuwa akinionyesha kwa nafasi ndogo sana ya kioo ambacho kilifunguliwa juu tu, ni mwanaume mmoja alikuwa amevaa suti ya gharama sana alikuwa anaingia kwenye duka moja kubwa sana la kusindika nyama hakuwa na muda maalumu wa kufika hapo kwa sababu leo haikuwa mara ya kwanza kumuona ni mara nyingi sana huwa anapita hapo tulipokuwa tukioshea magari, alikuwa ni kijana tu lakini alionekana wazi alitoka kwenye maisha mazuri mno, niliitikia kwa kichwa kuonyesha kukubali hicho alichokuwa ameniuliza.

“Nahitaji umfuatilie na uwe unaniambia kila ambacho huwa anakifanya kila akija kwenye hii sehemu kila siku muda anaokuja uwe unanipigia simu na kuniambia, hili jambo hatakiwi mtu mwingine yeyote yule zaidi yako aweze kulijua, zingatia hilo hakikisha hakuna mtu mwingine anayejua juu ya hili kama ukikaidi utamkosa ndugu yako” aliongea kwa msisitizo sana kiasi kwamba mpaka nilikuwa natetemeka kwa umri wangu wa miaka kumi na mitano sikuelewa kama mtu huyo amekosa watu wa kuwatuma mpaka aweze kunituma mimi. Nilitazama nje ambako nilimuona ndugu yangu akiwa anafanya kazi akiwa na furaha sana na hicho ndicho kitu pekee ambacho mimi nilikuwa nakihitaji kwenye maisha yangu.

“Jina lake anaitwa nani yule mtu?” ujasiri wangu na aina ya swali nililo uliza vilimfanya yule mwanaume atabasamu sana.

“Jonson Malisaba”

20 sina la ziada tena tukutane wakati ujao MUNGU akipenda.

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI........

Aliongea kwa msisitizo sana kiasi kwamba mpaka nilikuwa natetemeka kwa umri wangu wa miaka kumi na mitano sikuelewa kama mtu huyo amekosa watu wa kuwatuma mpaka aweze kunituma mimi. Nilitazama nje ambako nilimuona ndugu yangu akiwa anafanya kazi akiwa na furaha sana na hicho ndicho kitu pekee ambacho mimi nilikuwa nakihitaji kwenye maisha yangu.

“Jina lake anaitwa nani yule mtu?” ujasiri wangu na aina ya swali nililo uliza vilimfanya yule mwanaume atabasamu sana.

“Jonson Malisaba”

ENDELEA........................

Mvua kali zenye miungurumo mikubwa sana ya radi za kutisha kupita kiasi pamoja na baridi kali ambalo kama ungefanya uzembe lilikuwa linaondoka na maisha yako ndiyo yalikuwa maisha yangu miaka mitano tangu niweze kukutana na yule mzee aliyenipa kazi ya kumchunguza mwanaume mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Jonson Malisaba, juu ya milima ambako kulikuwa na baridi kali kwenye msitu mmoja ambao mpaka leo hata ukiniambia nikuelezee ni wapi ulipo sina huo uwezo kwa sababu tulikuwa tukifungwa macho mida ya usiku wa manane tukiwa tunapelekwa huko, kule sio duniani ni zaidi ya jehanamu, huna muda wa kulala zaidi ya nusu saa kwa siku hakuna kitu cha kukupatia joto hata kwa asilimia tano inakulazimu muda wote uwe kwenye mazoezi ili mwili uweze kuwa wa moto kulihimili baridi la ile sehemu.
Timotheo Jordan ndilo jina rasmi ambalo nilikuwa nimepewa na yule mzee baada ya kuifanya kazi yake kwa usahihi kwa kiasi chake japo sikufanikiwa kama ilivyokuwa inatakiwa. Yule mzee ambaye alikuwa kila siku akinifuatilia sehemu ambayo nilikuwa nafanya kazi ya kuosha magari sikuwahi kujua kama ni mkurugenzi wa usalama wa taifa wa nchi ya Tanzania mpaka pale alipokuja kuniambia mwenyewe kuhusu hili jambo. Nilikaa miaka mitano ndani ya ile milima na wenzangu watatu baada ya kuchaguliwa kwenda kupata mafunzo maalumu, wenzangu wote walikuwa ni wanajeshi lakini mimi nilipewa nafasi na aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa bila kujulikaka na mtu yeyote kwamba mimi ni kijana wa kawaida tu wa mtaani hata hivyo hakuna aliyekuwa na haki ya kuulizia kitu chochote kile zaidi ya kufanya tu kile alichokuwa ametumwa. Rasmi niliingia kwenye hesabu za serikali kama moja ya majasusi wa nchi hii rasmi hadi mimi mwenyewe nilibaki najishangaa sana hizo nafasi huwa wanapewa watu maalumu sana sikujua ni kwanini mzee yule aliamua kunipa hiyo nafasi ya upendeleo kwa wakati ule lakini sikujua kama ni nafasi ambayo itanifanya niishi maisha ya majuto kwenye maisha yangu yote.

"Sijakuelewa umemtaja baba yangu hapo kaingiaje na kwanini wewe ulipewa kazi ya kumfuatilia mpaka upate nafasi kubwa sana namna hiyo ndani ya usalama wa taifa wa nchi kubwa kama Tanzania" Jamal kwa mara ya kwanza aliingilia maongezi na maelezo ya baba yake mlezi tangu aanze kumsimulia hivyo visa japo yeye miaka yake yote alijua huyo ndiye baba yake mzazi, alitabasamu Mr Timotheo Jordan huku akikohoa kidogo ili bwaba mdogo apate kujua nini kikubwa ambacho kipo nyuma ya pazia mpaka yanatokea mambo ya hatari sana namna hii, alitazama shingoni kwa Jamal kwa umakini akiwa anakikadiria sana kile kidani mpaka Jamal mwenyewe alijishtukia akakiangalia kile kidani akakumbuka vyema mzee huyo alivyoweza kumuasia siku ya kwanza kumpatia kule Kyela kwenye safu za mlima Livingstone kwamba kwa gharama yoyote ile ahakikishe hicho kidani kinakuwa mahali salama sana kwenye maisha yake yote ni bora hata afe yeye.

"Hicho kidani chako ulicho nacho wewe shingoni ndicho chanzo cha haya yote unayo yaona yanaendelea hapa nchini Tanzania" mzee huyo aliongea bila hata kupepesa macho yake, Jamal alishtuka sana na kusogea nyuma kidogo, kidani alichokuwa amekivaa kilikuwa cha zamani sana ambacho hakikuwa na uzuri wa aina yoyote ile kiasi kwamba kitamvutia hata kibaka kukiiba yeye mwenyewe kilikuwa kinamkera sana kuwa shingoni kwake ila hakuweza kukitupa kwa sababu ya heshima tu ya baba yake.

"Hiki kidani ndiyo chanzo cha mambo yote yanayo endelea kivipi?" Ilikuwa ni lazima mwanadamu wa kawaida kuchanganyikiwa kwa maelezo ambayo alikuwa anapewa yalimchanganya mno kichwa chake mwanaume huyu.

"Baada ya kutoka ndani ya ile milima niliporudi uraiani huku kazi yangu kubwa ilikuwa ni kuendelea kumfuatilia Mr Jonson Malisaba pamoja na umoja wake ambao ulifahamika kwa jina la M96 OWNER'Z' mpaka leo kuna baadhi ya wanadamu wanalijua hili jina kama kampuni lakini huu ulikuwa ni umoja wa watu ambao walikuwa wanayafanya mambo yao ya siri kubwa sana wakiongozwa na baba yako huyo kijana Jonson Malisaba. Miezi ambayo niliweza kumfuatilia kwa usahihi pale mtaani sikuweza kugungua vitu vingi sana kwa sababu ya umri wangu pamoja na uwezo wangu kwenye hizi kazi, nilifanikiwa tu kujua kwamba hawa watu walikuwa na vitu vikubwa sana vya siri ambavyo viliendelea kwenye hizo ofisi zao ambazo kwa wanadamu wa kawaida huwa wanahisi kwamba mpaka leo zinahusika na usindikaji nyama. Siku moja nikiwa nimemaliza kazi nimekaa pale nilipokuwa nafanyia kazi pacha wangu alikuwa ameshaenda kulala, ilikuwa usiku wa manane sana yalipita magari matatu yakiwa kwenye kasi kubwa mno na yote yaliishia kwenye lile duka kubwa la usindikaji nyama ambalo mimi nilimjua mmiliki kwa sababu alikuwa akipita pale mara moja moja anavyokuja na ndiye niliyepewa kazi kumfuatilia, mtu huyo alikuwa ni Jonson Malisaba. Walishuka wanaume sita wenye miili iliyoshiba kisha akashuka huyo Mr Jonson ambaye bila shaka ndiye aliyekuwa bosi wa hao vijana, walishuka na mwili wa mwanamke mmoja ambaye alionekana wazi alikuwa akiomba msaada kwa kurusha mikono lakini hakuweza kupiga kelele ambazo zingesababisha yeye kusikika na kusaidiwa kwa sababu alikuwa amefungwa sehemu ya mdomo wake, niliogopa sana ikabidi nijibanze sehemu ili nisije nikaonekana mbele yao.
Walifanikiwa kuingia ndani ya lile duka kubwa, nilinyata kwa hofu nikiwa nahitaji kujua ni kipi hasa ambacho kilikuwa kinaenda kumtokea yule mwanamke, dunia ina siri kubwa sana Mr Jonson alimpiga risasi tano za kichwa yule mwanamke nilishika mdomo na kujishika kichwa nikipiga makelele kwa nguvu, nilijisahau kama nilikuwa sehemu ya hatari sana ila sikuweza kuvumilia kile kilichokuwa kinatokea mbele yangu, kilinitisha sana, zile kelele zangu ziliweza kuwafikia wale watu mle ndani kupitia kwenye sehemu ndogo ya dirisha nilipokuwa nachungulia

"Hapaaaaana ..no ..no..no huyo sio baba yangu labda kama majina yanafanana, baba yangu hakuwahi kumiliki bastola kwa miaka yangu yote kumi na minne ambayo nilipata kuishi naye japo kwa muda ule nilikuwa mdogo sana ila kumbukumbu zangu zimerudi vizuri sana baba yangu hakuwahi hata kujua namna ya kuua kuku tu mdogo, baba yangu alikuwa mtu wa MUNGU na alikuwa akiogopa sana kumuumiza mwanadamu mwenzake, hapanaaa ..noo huyo sio baba yangu, yule mzee asingeweza kumuua mwanadamu mwenzake hahahaha haha .......ishia hapo huyo siye baba yangu mimi" Jamal alikana kwa nguvu zote, hakutaka kuamini eti hicho alichokuwa anakisikia kilikuwa cha kweli, alikuwa akikataa lakini machozi yalikuwa yanamtoka alielewa mtu mzima kama huyu anapokuwa anaongea Jambo zito namna hiyo tena akiwa kwenye hali mbaya na hatua za mwisho wa maisha yake asingeweza kudanganya, alikumbuka maisha ambayo aliyaishi na baba yake mzazi kwa miaka yake ambayo alikuwa bado yupo hai, hakuwa sahihi kwa asilimia miamoja lakini alikuwa mtu safi sana mpenda kusaidia watu na hata dini alikuwa akiijua sana mzee yule leo kuambiwa huyo mzee alikuwa muuaji kwake ilikuwa ni miongoni mwa ndoto za kutisha zaidi alizowahi kuziota kwenye maisha yake.

"Unajua wewe bado ni mdogo sana sana mwanangu mambo mengi unayaona sasa ukiwa ndio umeanza kukua tu ila tukikwambia utupe hata uhalisia wa miaka ishirini na miwili iliyopita huwezo kuelezea chochote kile zaidi tu ya vichache ulivyo simuliwa. Binadamu ndiye kiumbe anaye tisha zaidi duniani kuliko kiumbe chochote kile na mwanadamu ndiye kiumbe hatari zaidi duniani ndiyo sababu MUNGU alimpa mamlaka ya kuvitawala vitu vyote vilivyo hai na visivyo hai, wanadamu wengi huwa wana sehemu kuu tatu sehemu ya kwanza ni upande ambao wanadamu wenzake huwa wanaujua kwake kwa mfano kama wewe ulivyokuwa unanijua mwanzo lakini hakikuwa na uhalisia wowote ule ndio maana mpaka leo unacho ambiwa unakishangaa sana, upande wa pili huu ndio hatari zaidi ambao huwa ni wa siri sana kwa mwanadamu yeyote yule duniani kwa sababu huo huwa anaujua mhusika mwenyewe na watu wachache mno ambao nao wakitaka kufanya watu waujue uhalisia wa mtu huyo lazima awaue kwa namna yoyote ile ili siri ibaki kuwa yake tu, ila upande wa tatu ni upande ambao yeye mhusika anaamua kuwaaminisha watu kwamba yupo hivyo hususani kwa wale watu ambao wapo karibu na wanadamu wanao jifanya ni wajuaji sana hivyo huwa wanaamua kuishi kama hao wanadamu watakavyo ila mambo yanapokuja kubadilika hawa watu kila mtu huwa anakaa chini kuwashangaa utasikia flani ndio kafanya hivi hapana haiwezekani kwa sababu unakuwa umejiaminisha kwamba huyo mtu unamjua kiundani kumbe hujui chochote kuhusu maisha yake.

Usiyaishi maisha kwa mazoea hata siku moja utapotea mapema sana kwenye uso wa hii dunia ambayo wanadamu ndiyo wapangaji sikuizi wakikufuru sana kwa kujipangia maisha ya wenzao mikononi mwao na hatuwezi kulizuia hilo kikubwa nafasi unayo ipata hakikisha inatumika sana kusaidia baadhi ya wanyonge wa nchi hii na kwa sasa hii kazi ipo kwenye mikono yako wananchi wote wanatembea mgongoni mwako wakitegemea kupelekwa nchi ya ahadi ingawa hawajui ni nani atakaye wapeleleka, tunafanya kazi ngumu sana kuhakikisha watu wanaishi vizuri, tunapoteza marafiki, ndugu, na maisha yetu yote yapo mikononi muda wowote unakufa lakini ndio watu tunao ongoza kutukanwa na wananchi na mara nyingine ndio wanaotuombea tufe mapema hiyo isjie ikakukatisha tamaa kwenye safari yako ndefu ambayo unaenda kuianza rasmi siku ya Kesho kwenye maisha yako kuwapigania watu wasiokuwa na shukrani kabisa kwenye maisha yao.

Kwa usiku ule baba yako alikuwa ni mtu mkatili na hatari sana kwenye macho yangu, lilikuwa ni tukio la pili la mauaji nalishuhudia kwenye maisha yangu ukiacha lile la baba yangu kuuawa kule kijijini, zile kelele ziliwafikia wale watu mle ndani nilianza kukimbia baada ya kuona wamenisikia tayari, nilikuwa nina hofu kubwa mno kiasi kwamba nilikuwa nakimbia nikiwa sijui wapi naelekea kwenye vichochoro usiku ule nilijuta kwanini sikwenda kulala mapema. Kwenye Kona moja nilidakwa ghafla na mtu ambaye hakuwa akionekana macho yake kwa kofia kubwa ambayo alikuwa ameivaa, alinionyesha ishara ya kutopiga kelele zozote pale. Sekunde kumi tu za kuhesabu walipita kwa kasi wanaume wawili mmoja alisimama ghafla ile sehemu, sijui alikuwa mwanadamu wa aina gani ila nadhani alikuwa anaweza kuyasikia mapigo ya moyo wangu ambayo yalikuwa yakienda kwa kasi sana, nilimuona akigeuka pale tulipokuwa kilirushwa kisu kikali lakini katika hali ambayo haikuwa ya kawaida kilidakwa kwa vidole viwili tu na mwanaume ambaye alikuwa amenisaidia pale, sikuweza kumjua kabisa kutokana na kofia kubwa aliyokuwa ameivaa, ni kitendo cha haraka sana alinizungushia kitambaa kwenye uso wangu nikiwa naonekana macho tu ni wazi hakuhitaji wale wanaume wanifahami kabisa sura yangu.

"Tupe huyo mtoto tuondoke naye" nilisogea nyuma kwa uoga baada ya kusikia yule mwanaume akinihitaji mimi ili tuondoke wote nilijua tu huko nikienda ni kuuawa kwa sababu nimekuwa shahidi wa mauaji na hilo jambo halikutakiwa kutokea kabisa kwenye maisha yangu. Yule mwanaume aliye nisaidia hakuonekana kuwa mtu mwenye maneno mengi sana alinisogeza nyuma kidogo akapanga mkono wake wakati huo yule mwanaume mwingine aliyekuwa amepitiliza pale alikuwa amefika. Sikuwahi kushuhudia namna wanadamu walivyo jaaliwa matumizi sahihi ya mikono lakini siku ile niliweza kushuhudia taaluma nzuri sana ya mapigano wanaume walikuwa wakiirusha mikono yao kwa ustadi mkubwa mno, yule mwanaume aliyeweza kunisaidia pale alijikunja hewani akatua kwenye vifua vya wale watu kwa double kick moja nzuri sana walirudi nyuma kwa hatua kadhaa hakuwapa nafasi ya kupumua zilifuata ngumi nzito ambazo mmoja zilimpata kwenye taya alivunjwa shingo kama muwa, aliyekuwa amebaki alikutana na ngumi nzito ya kwenye kichwa, sina imani sana ila nadhani alipata tatizo la ubongo kwa maana alianza kurusha ngumi hovyo hovyo akiwa anaongea maneno ambayo hayaeleweki kabisa hakuchukua muda mrefu alikatwa shingo na kisu alichokuja nacho yeye mwenyewe.

Nilianza kumuogopa yule mtu aliyeweza kunipa msaada kwa aina ya ukatili aliokuwa ameufanya ulikuwa unatisha mno lakini alinisihi hakuwa mtu mbaya kwangu, alinitanguliza mbele akinisihi nikimbie sana bila kutazama nyuma hatua miamoja kutoka hapo nitalikuta gari niingie haraka sana humo ndani nitamkuta mtu atakaye nisaidia huo muda. Nilishangaa sana kwa sababu hao watu walikuwa wamekufa sijui ni kwanini alitaka nikimbie sana, kwa ule muda sikumkumbuka hata ndugu yangu bado moyo wangu ulikuwa haujatulia kabisa hatua ya ishirini tangu nianze kukimbia nilisikia milio ya risasi, niligeuka nyuma nikaona yule mtu aliyekuwa amenisaidia akienda chini, niliogopa sana kuna watu niliwaona wakija kwangu, niligeuka na kukimbia kwa nguvu kweli mbele yangu kulikuwa na gari niliingia humo ndani kama mshale, gari haikumaliza hata sekunde tatu ilitolewa kwa nguvu sana, wale watu kule nyuma niliwaona wakipiga risasi ambazo hazikutufikia kabisa, niligeuza macho yangu kuona ni akina nani ambao walijua huo muda nipo kwenye matatizo wakati nilikuwa mwenyewe, mtu niliye muona nilishtuka sana almanusura niruke kwenye hiyo gari.

21 naweka nukta tukutane kwenye sehemu inayo fuata

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA........

Niligeuka nyuma nikaona yule mtu aliyekuwa amenisaidia akienda chini, niliogopa sana kuna watu niliwaona wakija kwangu, niligeuka na kukimbia kwa nguvu kweli mbele yangu kulikuwa na gari niliingia humo ndani kama mshale, gari haikumaliza hata sekunde tatu ilitolewa kwa nguvu sana, wale watu kule nyuma niliwaona wakipiga risasi ambazo hazikutufikia kabisa, niligeuza macho yangu kuona ni akina nani ambao walijua huo muda nipo kwenye matatizo wakati nilikuwa mwenyewe, mtu niliye muona nilishtuka sana almanusura niruke kwenye hiyo gari.

ENDELEA............................

MIAKA MIWILI ILIYOPITA (2 YEARS AGO)
Ndani ya mitaa ya Buguruni hali ya Julius Makasi ilikuwa ni mbaya sana huenda alikuwa kwenye hatua za mwisho kabisa za uhai wake, hakuwa na tumaini la kuendelea kuwepo kwenye huu ulimwengu mkono wake ulikuwa haufanyi kazi na baadhi ya viungo vya mwili wake kutokana na mivunjiko aliyo ipata baada ya kukumbana na mkono wa Timotheo Jordan, ukiongeza na risasi mbili alizopigwa na wanaume wawili miongoni mwa wale wanaume watano ambao walikuwa wanaonekana kuwa hatari sana akiwa ndani ya tenki la maji vilitosha kabisa kuufanya mwili wake kuwa dhaifu kuweza kuendelea kuihimili hali ya huu ulimwengu wa watu wabaya. Baada ya kutoka kwenye maji alikuwa amezimia chini ya hilo tenki kubwa la maji lakini kwa mbali kidogo na hapo kuna mwanaume mmoja alikuwa amesimama kwa muda mrefu sana na alikuwa akishuhudia kila kitu kilichokuwa kinaendelea hapo alionekana kutoingilia Jambo hilo kutokana na aina ya watu waliokuwa hilo eneo alionekana kuwa na taarifa za uhatari wao hao binadamu hata hivyo hiyo vita ilionekana kutomhusu sana ndio maana alikuwa amekaa tu sehemu akishuhudia kila kilicho kuwa kinafanyika hapo.

Alisubiri mpaka watu wote walipoweza kutoweka kabisa kwenye hilo eneo, ukimya pekee ndiyo kitu kilichokuwa kometawala hapo licha ya mlipuko mkali wa ile gari kutokea ambalo akina Julius Makasi na wenzake walikuja nalo bado hakuna raia ambaye alikuwa na moyo wa kujitokeza kwenye hayo maeno kushuhudia hicho kitu, alitembea kwa umakini mkubwa sana kiasi kwamba hatua zake kama wewe ni mtu wa kawaida usingeweza kabisa kuzisikia aliangalia miili iliyokuwa hapo wote walikuwa wamekufa kwa risasi nyingi ambazo walipigwa, hakuchukua muda mrefu alizunguka nyuma ya mgahawa wa huyo mama ntilie mdogo kwenye hilo eneo, huko ndiko ambako mwili wa Julius Makasi ulikuwa umelala chini akiwa ndani ya usingizi wa kifo. Aliinama na kuweka vidole vyake viwili karibu kabisa na pua ya Julius alihisi kupita kwa hewa japo ni kwa mbali sana alielewa mwanaume huyo bado alikuwa yupo hai akiwa kwenye hali mbaya alikuwa anahitaji msaada wa haraka sana kuona kama inawezekana kuokoa maisha yake, hakuchukua muda aliubeba mwili huo mgongoni kwake aliangalia huku na huko hakuona mtu yeyote yule aliondoka akikimbia huku mwili wa Julius Makasi ukiwa mgongoni kwake.

Julius alikurupuka kutoka kwenye usingizi mzito, alitaka kunyanyuka lakini viungo vya mwili wake viligoma kabisa kifua kilikuwa kikimuua sana ilimbidi kulala chini tena aweze kuona kinacho enda kutokea kweye hicho chumba. Mbele yake kulikuwa na komputa kubwa iliyokuwa inaonyesha mistari ya kupanda na kushuka ikionyesha namna mapigo ya moyo yalivyokuwa yakienda kwa usahihi, aligundua hayo mapigo ya moyo yalikuwa ni yakwake mwenyewe alitabasamu kuona hivyo ila mkono wake ulikuwa umefungwa plasta nyingi pamoja na mguu kuonyesha wazi kwamba hizo ndizo sehemu alizokuwa ameumia zaidi. Kumbu kumbu zake zilimrudisha namna alivyokumbana na mikono ya mtu waliyekuwa wamemfuata Buguruni, risasi mbili zilizokuwa zimezama kwenye mwili wake zilimfanya asisimke sana baada ya kutoka kwenye hiyo kumbu kumbu.

"Una bahati sana kijana wangu inaonekana wazi mifupa yako imekomaa vyema ndio maana umetumia muda mchache mpaka kuweza kuamka hapo nilijua utatumia hata miezi miwili" ni sauti ya daktari mmoja mzee ambaye alikuwa ameingia humo ndani bila yeye mwenyewe kujua ndiyo iliyokuwa imemshtua aligeuka kumuangalia mzee huyo kwa umakini.

"Ni muda gani tangu nikiwa nipo hapa kitandani" Julius aliuliza akiwa anamtazama vizuri huyo mzee hakuwa hata na uwezo wa kujongea.

"Hii ni wiki ya tatu tangu ukiwa kwenye huo usingizi wa kifo" maelezo ya daktari kidogo yalimshtua lakini akapotezea.

"Ni nani aliyeweza kunisaidia siku ile mpaka kunifikisha hapa nilipo?" Hakujibiwa chochote mpaka pale mlango ulipoweza kufunguliwa mbele yake walikuwa wamesimana wanaume wawili wote wakiwa wamevaa suti, aliyekuwa na suti ya blue alikuwa mbele huku mwenye suti nyeusi akiwa nyuma. Aliyekuwa na suti ya blue alikuwa ni mrefu halafu mwembamba, Julius alivuta kumbu kumbu zake kuona kama kuna sehemu aliwahi kuonana na huyo mtu lakini hesabu za kichwa chake zilimgomea kabisa kwamba hakuwahi kumuona huyo binadamu mahali popote pale kwenye maisha yake.

"Wewe ni nani na kwanini umenisaidia?"

"Subiri upone kwanza ndipo nitakapokuwa na mazungumzo nawewe"
"Vipi kama sitataka kuwa na hayo mazungumzo nawewe?"
"Sitakuwa na namna nyingine zaidi ya kukulazimisha kufanya hivyo" Mwanaume huyo baada ya hayo maelezo mafupi alitoka humo ndani huku akiwa ameahidi kurudi pale tu Julius atakapokuwa kwenye hali yake nzuri ili waweze kuongea pamoja na kujuana kiundani na sababu gani iliyo mfanya mpaka mtu huyo aweze kumsaidia alijua wazi hakuna msaada wa bure duniani lazima kuna kitu alitakiwa kukilipa hapo baadae.

ZAIDI YA MIAKA 15 ILIYOPITA
Inatuchukua zaidi ya kilomita 1543 za mraba ikiwa ni masaa ishirini na moja na dakika zake tano kwa saa za nchi ya Tanzania kutoka ndani ya jiji la Dar es salaam, tunasafiri mpaka kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania kwenye ardhi ya watu Wajivuni namaanisha Wahaya, ni ndani ya mkoa wa Kagera wenye idadi ya watu zaidi ya milioni mbili, laki nne, hamsini na nane elfu na ishirini na tatu karibu kabisa na mpakani kati ya Tanzania na Rwanda katika kijiji kijulikanacho kama Nyakakoni ndani ya wilaya ya Kyerwa ikiwa imepunguzwa kutoka kwenye wilaya ya Karagwe. Nyakakoni ni kijiji ambacho ni maarufu sana kwa ufugaji pamoja na uwindaji mkubwa hasa hasa wanyarwanda ndio watu walio shamiri sana ndani ya kijiji hicho, kipo karibu kabisa na hifadhi ya taifa ya Ibanda ambayo ni moja ya hifadhi zinazo ifanya nchi ya Tanzania kuzidi kuwa ya kupendeza mno.

Ndani ya kijiji hicho cha Kyerwa ilikuwa ikisikika sauti ya kijana mmoja ambaye kwa mtazamo alikuwa na umri usiopungua miaka 15 na kuendelea alikuwa akiita huku anakimbia

"Mama, mama, mamaaaa amka mama yangu nimekuletea daktari utapona mapema sana mama yangu" aliongea huku akitabasamu japo chozi lilikuwa linamtoka kwa maskitiko, ni kijana mmoja ambaye alikuwa ameenda kumtafuta daktari kwa ajili ya kuja kuitibu hali ya mama yake ambaye alikuwa mgonjwa wa muda mrefu lakini leo hali yake ilikuwa imebadilika sana hivyo ilimlazimu kijana huyo kwenda kuhangaika ili kumpata daktari kwa ajili ya kuja kumsaidia mama yake. Ilikuwa ni miongoni mwa familia za kimaskini ndani ya kijiji hicho ambacho kilitegemea sana ufugaji pamoja na uwindaji ili kuweza kujikimu kwenye mahitaji yao ya kila siku. Alikuwa ametoka hapo majira ya asubuhi kwenda kuomba msaada kwa baadhi ya wasamalia ambao walikuwa na roho za huruma kuweza kumsaidia mama yake mpendwa kuamka hapo alipokuwa amelala lakini hakuna mtu ambaye alionekana kuguswa na hicho kitu, hakupata msaada wowote ule hata alipokwenda kwa daktari aliweza kuambiwa kwamba mtu huyo anaishi kwa ratiba sana hivyo hawezi kutoka na kwenda sehemu ambayo kwake haikuwa na maslahi yoyote yale kimaisha ilimlazimu kwenda kwenye vibarua vya kazi ngumu sana kwa zaidi ya masaa matano akiwa hajajipa hata nafasi ya kupumzika aliweza kupata chochote ambacho aliona kinaweza kuinusuru nafsi ya mwanamke ambaye ndiye aliyekuwa amesalia naye kama mlezi wake pekee kwenye maisha yake.

Baada ya kukusanya kidogo alichokipata kwa masaa hayo matano alikimbilia nyumbani kwa huyo daktari ambaye kijiji kizima alikuwa mmoja tu pekee kutokana na kijiji hicho kutokuwa na huduma za kijamii kwa muda ambao zilikuwa zinahitajika sana, kwa sababu pesa ndicho kitu kilichokuwa kikiongea haikuwa tatizo daktari alizikunja shilingi hizo na hapo nafsi yake iliridhika kabisa kwenda kuifanya kazi akisahau kwamba taaluma yake inamlazimu kwanza kusaidia watu na kutanguliza utu kabla ya kuweka kipaumbele cha maslahi mbele Kwanza lakini kijana hakuwa na namna ndiyo dunia ambayo alikuwa amezaliwa tena akiwa mtoto wa kiume hakuwa na namna ya kuyakwepa majukumu zaidi ya kuyakabili kwa asilimia zote miamoja.

Mwendo wa nusu saa kutoka ilipokuwa nyumba ya huyo daktari ndio muda uliotumika kufika ilipokuwa nyumba ndogo ya chumba kimoja pekee ikiwa imeezekwa kwa nyasi ambayo ni kwao na huyo kijana, alikuwa anaona kama daktari huyo anatembea taratibu sana wakati alikuwa anaenda ni kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake ambaye aliambiwa alikuwa kwenye hali mbaya nadhani alikuwa amesahau kwamba ipo siku itafika nayeye atakuwa miongoni mwa wanadamu watakao uhitaji msaada wa wanadamu wenzao pale watakapokuwa wanaipigania pumzi yao ya mwisho hapa duniani.

Kijana huyo alishtuka na kuongesa kasi ya kukimbia baada ya kusikia sauti ya mtoto mdogo akiwa analia, ni sauti ambayo aliijua vizuri sana hata kama angekuwa usingizini basi asingeweza kuisahau, ilikuwa ni sauti ya dada yake wa pekee ambaye alikuwa na mwaka mmoja na kwao walikuwa wamezaliwa wawili tu pekee hivyo ilimpelekea kumpenda sana huyo mtoto wa kike aliyekuwa ni robo tatu ya furaha yake kila anapo muona na kumbeba mkononi mwake, mtoto huyo alikuwa ana mwaka mmoja tu na miezi miwili tangu kuzaliwa kwake lakini alikuwa akimuita dada kila wakati japokuwa mtoto huyo hakuwa na uwezo wa kusikia na kuelewa hayo majina ila alimheshimu sana. Kilio hicho kilimfanya ausukume mlango uliokuwa ukifungwa kwa kamba tu pekee kwa nguvu ili kuwahi ndani. Alicho kiona alitaka kudondoka chini mama yake alikuwa amelala kwa kusambaza mikono yake huku mdogo wake akiwa karibu na alipolala mama yake akiwa analia kwa sauti Kali sana ni wazi alikuwa anahitaji kunyonya kutoka kwa mwanamke huyo aliyekuwa amelala pembeni yake ambaye kiuhalisia alikuwa ni mama yake.

"Mamaaaaaaaaaaaaaaaaa" aliita kwa sauti kubwa akikimbilia pale ulipokuwa umelala mwili wa mama yake wakati huo daktari alikuwa akiingia humo ndani alionekana kutikisa kichwa kusikitika baada ya kuona huo mwili ukiwa umelala chini.

"Daktari msaidie mama yangu tafadhali" alikuwa akimuomba daktari huyo huku akiwa amepiga magoti, daktari alikuwa anajua ni nini kilikuwa kimetokea hapo japo alifanya tu vipimo kama kumridhisha kijana huyo, dakika tano mbele aliyafumba macho ya huyo mama akiwa anaandika andika kwenye karatasi yake pamoja na kuangalia saa yake ndogo ya mkononi.

"Saa saba kamili ndio muda ukiulizwa popote pale, mama hatupo naye tena duniani" huu ndio ukweli ambao ni mgumu sana kukubalika mbele ya mtoto yeyote yule duniani anapo ambiwa hiyo kauli, ni kauli nzito sana kuisikia kwenye maskio yako japokuwa unapo isikia kwa wengine inaweza kuonekana kuwa rahisi sana ila huwa inauma sana, hiki ndicho kilichokuwa kinamkuta huyu bwana mdogo ambaye hakuelewa afanye nini mpaka huo wakati.

"Hapana mama yangu hawezi kuondoka namna hii mdogo wangu bado anahitaji kunyonya na hapa saivi ana njaa sana hapanaaa mamaaaa" Ilikuwa ni ndoto ya kutisha sana ambayo ilikuwa ni ya kweli kabisa kwenye maisha yake, mwili wake ulikuwa umelowa jasho baada ya kutoka kwenye usingizi mzito ulio mkumbusha maisha yake ya zamani sana. Mwili wake ulikuwa umelowa kwa jasho akiwa anatetemeka, alinyanyuka na kulifuata friji lilipokuwa akachukua maji baridi akanywa zaidi ya lita moja kwa mkupuo kidogo aliona nafsi yake ikianza kupoa na kutulia, Alexander ndiye mwanaume aliyekuwa kwenye ndoto hiyo ya kutisha sana ambayo kiuhalisia ni ndoto ya kweli ya maisha yake.

Una mengi sana ya kujifunza humu ndani

22 naweka nukta leo ungana namimi wakati mwingine tena

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI........

ENDELEA.................
Mwanaume baada ya kupata maji alienda dirishani na kulifungua dirisha hilo, nje kulikuwa na kiza kikubwa cha kutisha sana, ni nyota tu pekee ndizo zilizokuwa zimetawala kwenye hilo giza . Aligeuka nyuma na kuangalia ukutani macho yake yote mawili aliyaelekeza ukutani sehemu ambapo ilikuwa imewekwa moja ya saa za dhahabu, saa tisa kasoro dakika kumi na tano (8:45) za usiku ndivyo saa hiyo ilivyokuwa ikisoma kwenye mshale wake, macho yake aliyageuza tena na kuendelea kuangalia nje ambako kulikuwa kimya sana na hakukuonekana kuwa na mpitaji yeyote yule kwenye majira hayo ya usiku wa manane kwenye mitaa hiyo ambayo aliishi mwanadamu aliyekuwa hatari sana kwenye maisha ya watu na machozi ndiyo ilikuwa sehemu ya kuumaliza usiku huo ambao kwake aliuona ukiwa mrefu kupita kiasi.

Hakuna nafsi ngumu duniani linapokuja suala la maumivu ya moyo licha ya kuwa mwanadamu mkatili na hatari sana machoni mwa watu lakini hata yeye alikuwa akipitia maumuvu mazito ambayo kila mwanadamu ameandikiwa kuyapitia hata aishi kwa furaha vipi ipo siku atalia tu, ndicho kilichokuwa kinampata Alexander, usiku huu kimiminika kitokacho kwenye macho kilikuwa kinamtoka na hapakuwa na mtu yeyote yule wa kuweza kumfuta, alitoa machozi, achana na nguvu alizokuwa nazo, achana na utajiri aliokuwa nao, majumba ya kifahari aliyokuwa akiyamiliki lakini hiyo haikuwa sababu ya yeye kuwa na maisha ya furaha kama ilivyo kwa baadhi ya wanadamu ambao hawajawahi kubahatika kuishi maisha mazuri sana lakini Wana utajiri mkubwa wa amani na furaha kwenye maisha yao. Tukio la saa saba mchana ndilo lililokuwa linamuumiza sana akili kwenye maisha yake yote, hiyo ni siku aliyo mpoteza mama yake ambaye ni mzazi pekee aliyekuwa amebahatika kubaki naye hapa duniani, amekuwa mtu wa kulikumbuka sana hilo tukio hasa mara nyingi likimtokea kwenye ndoto zake na kumfanya kukosa usingizi kabisa.

Saa saba ya siku ile,ni siku ambayo alitamkiwa na daktari kwamba mama yake hakuwa miongoni mwa viumbe vilivyo hai, siku ile aliweza kuyapata maumivu mara mbili kwenye maisha yake mchana ule licha ya kuumia kwa kumpoteza aliyekuwa malkia kwake mwanamke mhimu sana kwenye maisha yake lakini mtoto mdogo aliyekuwa pembeni yake ndiye aliyekuwa akimuumiza sana akili hakujua atamlea vipi mtoto aliyetegemea maziwa ya mama yake kuweza kuishi akiwa na mwaka mmoja tu pekee na miezi miwili, alitamani ajiue aondokane na dhahama ya huu ulimwengu ila kila akimuangalia mdogo wake huyo alikuwa akijutia hicho kitu hakuwa tayari kumuacha malaika kama huyo ambaye hakuwa na hatia yoyote bila msaada. Hakuwa na pesa, hakuwa na ndugu wala mtu yeyote aliye onyesha kuitambua thamani ya uwepo wake hapa duniani, alijikuta akipiga magoti bwana mdogo na kutoa machozi ya uchungu sana akiwa anautazama mwili wa mama yake kipenzi huku akiwa anajifariji kwamba huenda MUNGU akatenda muujiza mama huyo akanyanyuka tena.

Sauti kali ya kilio cha dada yake mdogo huyo ndicho kilicho mshtua kwenye mawazo akajifuta machozi na kumbeba mdogo wake akatoka naye nje na kuanza kumbembeleza huku akiwa anatembea.

Safari yake ilikuwa kwenda kwa mwenyekiti wa mtaa wake kwenda kumpatia taarifa za msiba wa mama yake, alibahatika kupata maziwa ambayo yalimfanya mdogo wake atulie wakati huo mama yake alikuwa anazikwa na wananchi wachache ambao walijitokeza baada ya kupatiwa taarifa na mwenyekiti wa mtaa wao. Usiku wa siku hiyo alikesha kwenye kaburi la mama yake akiwa amembeba mdogo wake ambaye alikuwa kwenye usingizi mzito akiwa amefunikwa na shuka zito ambalo ndilo pekee walikuwa nalo hapo kwao lakini kwa bwana mdogo hakuwa hata na muda na baridi lililokuwa linamsurubu usiku huo.

Wakati kunakaribia kukucha alinyanyuka na kuianza safari ya sehemu ambayo hata yeye mwenyewe hakuwa akiijua kwa usahihi, aliapa mbele ya kaburi la mama yake kabla hajatoka hapo kuyasaka maisha mazuri kwa namna yoyote ile ili kuhakikisha mdogo wake anaenda kuyaishi maisha bora tofauti na aliyo yaishi yeye kwenye dimbwi zito hilo la umaskini, safari yake ya masaa takribani matano akiwa anatembea ilimfikisha kwenye barabara ambayo ilikuwa inaruhusu magari kupita japokuwa lilikuwa likipita gari moja moja, alihema kwa nguvu kwa uchovu aliokuwa nao ila kila akikumbuka maisha yake yalivyo na anacho takiwa kukifanya uchovu wote ulimuisha akaanza kuifuata hiyo bara bara ambayo alikuwa na imani kwamba ingempeleka mpaka mjini kabisa ambako ndiko kulikuwa lengo lake kufika.

Hakuhitaji kuendelea kuyakumbuka hayo mambo mazito yaliyokuwa yakimuumiza akili muda mwingi, alichukua t-shirt laini akaivaa mwilini mwake, alitoka kwenye hicho chumba akaanza kushuka na ngazi kuelekea chumba cha kati kati ya ghorofa hilo, hicho ndicho kilichokuwa chumba cha mdogo wake wa damu aliye julikana kwa jina la Deodata, huyu ndiye binti ambaye alikuwa anatafutwa sana na watu wazito ambao waliamini kumpata huyu mwanamke kazi zao zilikuwa zinaenda kuwa rahisi sana, taaluma yake ilikuwa ni teknolojia ya taarifa wazungu wanaiita information technology (IT), hakuna kitu ambacho kilitengenezwa na binadamu wa kawaida kwenye teknolojia kikamshinda, mikono yake ilikuwa ni zaidi ya uchawi kila anapo kaa mbele ya komputa, akili yake ilikuwa inafanya kazi kuliko komputa yoyote ile, kupatikana kwake ilikuwa ni muhimu sana kwa sababu hakuna kitu ambacho kingeshindika kufanyika mtandaoni. Alitengenesa pesa nyingi mno kwenye mitandao kwa sababu watu wengi walikuwa wakinunua habari kubwa na za siri kwake, alikuwa na uwezo wa kutengeneza matukio ambayo hata ungeyapeleka sehemu gani yalikuwa yanaonekana yakweli kwa asilimia zote miamoja.

Umri wake ilikuwa ni miaka ishirini na miwili tu pekee ila watundu wa mitandaoni wote walikuwa wakimuogopa na kumhusudu mno, The Black Widow ndilo jina ambalo alikuwa maarufu sana kwenye mitandao, sio kaka yake wale mlinzi wake ambaye alikuwa anajua kwamba huyo mwanamke alikuwa mtu hatari sana linapokuja suala la mitandao japokuwa walijua kwamba amesomea hicho kitu kwani kaka yake ndiye akiyehakikisha mdogo wake anapata elimu hiyo ndani ya nchi ya India kwa miaka mitano, alivyorudi alikuwa mtu wa kuogopwa sana ila kwa umri wake hakuna binadamu ambaye angekubali kwamba huyo ndiye Black Widow na ni karata ya mhimu sana kwa watu wengi ambao walikuwa wanamtafuta kwenye maisha yake. Jopo la vibaka ambao walimvamia siku ile ndani ya Tiptop Club Alexander alifikiria kwamba huenda ni vijana tu walikuwa na shida na pesa ndiyo maana walimteka mdogo wake huyo bila kujua kwamba kuna watu waliokuwa hawafai hata kutajwa machoni pa watu ndio waliokuwa wanamtafuta huyo binti kwa udi na uvumba.

Baada ya kufika hapo mlangoni, hakuhitaji kumsumbua mdogo wake aliugusa mlango ulikuwa wazi aliusukuma ukafunguka, jicho lake lilikoswa na bisi bisi iliyokuwa imenolewa vyema baada ya kuikwepa kwa sarakasi maridadi, mbele yake alikuwa amesimama kijana ambaye alikuwa anahakikisha usalama wa Deodata kwa asilimia miamoja, Alexander alitabasamu baada ya kuona kijana huyo yupo makini na anaifanya kazi yake kwa usahihi.

"Kuwa na amani saivi unaweza kwenda kulala hakuna mtu mwenye hiyo jeuri ya kuingia nikiwa nipo hapa ndani" Alexander aliongea huku akimrushia kijana huyo kinywaji ambacho kilikuwa kipo kwenye friji nayeye akabeba kimoja na kuendela kushushia taratibu.

"Sawa bosi nashukuru sana" lilikuwa jibu kutoka kwa kijana huyo ambaye alionekana kumheshimu sana bosi wake huyo.
"Vipi hali yake kwa sasa, nikiwa mbali huwa ananitaja hata mara moja?" Alexander alimuuliza huyo kijana hilo swali akiwa amemkazia macho vizuri.
"Ndiyo yuko salama kabisa madam ila kuna muda huwa analia sana na kusema anakuchukia kila akiona picha ambazo mpo wote analalamika kwa sababu hupati hata muda wa kukaa naye sana hilo tu bosi" baada ya kusikia maneno hayo Alexander alitabasamu na kutoka humo ndani bila hata kuaga alipandisha kwenye chumba chake na kulibeba koti lake hakuchukua muda sana akatoka humo ndani akiwa anatembea taratibu kuufuata mlango mkubwa wa geti ulipokuwa.

***********************
Baada ya kuingia kwenye ile gari aliyekuwa mle ndani ni yule mzee ambaye alinipa kazi ya kumfuatilia Mr Johnson Malisaba, kwanza nilimshangaa saba sababu kubwa ni kwamba sikuelewa ameweza vipi kujua kwamba ule muda nimepatwa na matatizo mpaka aje kunisaidia kwa wakati ikimaanisha kwamba kama wangechelewa hata dakika moja tu nilikuwa nayapoteza maisha yangu pale pale.

"Mzee imekuaje upo hapa, umejuaje kama nipo kwenye hatari na yule mtu mbona tumemuacha kule inaonekana wazi watamuua wale watu" maswali yalinitoka mfululizo ila hata hivyo hilo sikulijali nilihitaji kujua hayo yote niliyokuwa nimeyauliza pale kwa yule mzee.

"Angalia kwenye hiyo mifuko yako kuna nini!" Ndicho kitu pekee ambacho aliniambia, niliingiza mikono yangu kwenye mifuko yangu ya suruali fupi ambayo nilikuwa nimeivaa, nilikutana na simu moja pamoja na ile kadi yenye namba ambazo sikuzielewa kabisa na nakumbuka hivyo vitu ni kweli niliviweka mimi ila bado sikuwa na jibu kwamba vilikuwa vikihusiana nini na swali ambalo nilikuwa nimeliuliza Mimi.

"Hivyo vitu ulivyo navyo ndivyo vinavyofanya uweze kuonekana kwangu popote pale utakapokuwa na muda wowote ule, tangu siku ya kwanza nilivyokupatia kazi ya kumfuatilia yule mtu ndiyo siku rasmi ambayo ulianza kulindwa, kila siku ya MUNGU umekuwa ukilindwa sana. Yule mwanaume aliyekuja kukusaidia pale amekufa kwa ajili yako, sio kwamba nimefurahi kufa kwake hapana ni hasara kubwa sana kwa taifa pamoja na kwa familia yake kwa sababu yametumika mabilioni ya pesa kuweza kumpata yule mtu, hivyo amefanya yale yote kwa sababu ya usalama wako kwa maana hiyo wewe ndiye unaye enda kuichukua nafasi yake kwa sababu yeye hatakuwepo tena.

Mimi hapa ni mkurugenzi wa usalama wa taifa wa nchi hii. Leo hii unaondoka rasmi nchini, kuhusu ndugu yako atachukuliwa siku ya kesho kupelekwa sehemu salama, ndani ya miaka mitano ukirudi naenda kukukabidhi rasmi kazi ya kupambana na hao watu nahitaji wajulikane kiundani wao ni akina nani hasa kwa sababu huwezi kuwafanya chochote bila kuwa na ushahidi wa kutosha nina imani kwa huo muda utakuwa na huo uwezo wa kuifanya hiyo kazi kwa usahihi sana, kwa Sasa lala upate muda wa kupumzika kwanza baadae unakuja kuchukuliwa na watu ambao watakupeleka unapotakiwa kuwa kwa hiyo miaka mitano, Mimi hatutaonana tena mpaka itakapoisha hiyo miaka unaweza kuniona tena" nilikuwa kwenye mshangao mkubwa niliambiwa habari ambazo ziliuwa ni mpya kwangu, kwanza niliogopa sana kusikia huyo mwanaume aliyekuwa mbele yangu alikuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, huwa nasikia sana uhatari wa hao watu kwenye maisha yao na wakiamua kukufuatilia basi jua wewe ni mwanadamu mwenye bahati mbaya mno kwenye maisha yako, ila kabla sijauliza wala kujibu chochote kuhusu hilo jambo tuliluwa tumefika mbali sana na nilipokuwa nafukuzwa.

Gari ilisimamishwa mzee huyo alishuka bila kuniaga wala kuniambia chochote kile nilikuja kuelewa baadae kwamba mtu huyo alikuwa amemaliza maelezo yake na hapo hakuja kuniomba ni kwamba kila alichokuwa amekiongea kilikuwa ni lazima kutekelezwa, nikiwa bado namshangaa mzee huyo aliingia mwanaume mwingine kwenye hiyo gari akionekana yeye kuwa kijana wa kawaida tu akiwa na nguo zake nyeusi pamoja na kofia kubwa kichwani, aliitoa gari kwa spidi bila kuongea chochote. Kesho yake ndipo nilipojikuta nashushwa kwenye ile milima yenye misitu iliyo jaa baridi kali nikiwa na wenzangu wanne kutoka kwenye helokopita ambayo kwa mahesabu tu japo tulifungwa macho tulidumu masaa saba tukiwa angani. Miaka mitano ndiyo muda tulio tumia kupata mateso ndani ya ile misitu, ilivyo isha ile miaka rasmi nilirudi mtaani wakati huo nilikuwa na miaka ishirini, nilikuwa natamani sana kumuona ndugu yangu ndicho kitu kilicho kuwa akilini kwa hiyo miaka mitano niliyokuwa mbali lakini ndio muda pekee ambao nikikabidhiwa kazi ngumu sana ya kuufuatilia umoja wa M96 OWNER'Z kuweza kujua huo umoja unahusiana na nini hasa mpaka wawe watu wa kuogopwa mpaka na usalama wa taifa wa nchi namna hiyo kwa mauaji waliyokuwa wanayafanya ya kutisha.
Binafsi kwenye sehemu ya 23 sina la ziada tena

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU........
Nikiwa bado namshangaa mzee huyo aliingia mwanaume mwingine kwenye hiyo gari akionekana yeye kuwa kijana wa kawaida tu akiwa na nguo zake nyeusi pamoja na kofia kubwa kichwani, aliitoa gari kwa spidi bila kuongea chochote. Kesho yake ndipo nilipojikuta nashushwa kwenye ile milima yenye misitu iliyo jaa baridi kali nikiwa na wenzangu wanne kutoka kwenye helokopita ambayo kwa mahesabu tu japo tulifungwa macho tulidumu masaa saba tukiwa angani. Miaka mitano ndiyo muda tulio tumia kupata mateso ndani ya ile misitu, ilivyo isha ile miaka rasmi nilirudi mtaani wakati huo nilikuwa na miaka ishirini, nilikuwa natamani sana kumuona ndugu yangu ndicho kitu kilicho kuwa akilini kwa hiyo miaka mitano niliyokuwa mbali lakini ndio muda pekee ambao nikikabidhiwa kazi ngumu sana ya kuufuatilia umoja wa M96 OWNER'Z kuweza kujua huo umoja unahusiana na nini hasa mpaka wawe watu wa kuogopwa mpaka na usalama wa taifa wa nchi namna hiyo kwa mauaji waliyokuwa wanayafanya ya kutisha.

ENDELEA..........................
Kichwani Alexander alikuwa na maswali makubwa mawili, lakwanza lilikuwa ni juu ya yule mzee aliyekuwa amemfuata maeneo ya Kibamba hakujua alipoteaje kirahisi namna ile mbele ya mtu kama yeye, alijiambia mwenyewe kwamba hesabu zake zilikuwa tofauti sana kuhisi anamjua vizuri yule mzee, alikiri wazi kwamba hakuna kitu alichokuwa anakijua kabisa kwa yule mtu. "Binadamu ni watu wa kuogopwa sana hivi yule mzee ni nani kwani haiwezekani azungumze namimi kirahisi sana namna ile lazima kuna kitu kikubwa sana natakiwa kumjua haraka sana vinginevyo mambo yangu yatakuwa kwenye wakati mgumu mno, hizi kazi nisipo angalia zitakuja kuondoka na nafsi yangu siku moja nikamuacha mdogo wangu anateseka kwanza inabidi nimtoe hapa nchini haraka sana inaonekana kuna hatari kubwa inaweza kutokea muda wowote ule" ni maneno ambayo alikuwa anajiambia mwenyewe akiwa ameshikilia mlango wa geti la jumba hilo la kifahari ambalo alilinunua kwa ajili ya mdogo wake yeye hapo alikuwa akija mara moja moja sana aliogopa usalama wa mdogo wake kutokana na kazi za kutisha alizokuwa anajihusisha nazo kwenye maisha yake, ilikuwa ni hatari kubwa sana kama wangejua ana ndugu yake hicho ni kitu ambacho kingetumika kumsambaratisha haraka mno, siku hizi watu wakisha ujua udhaifu wako basi habari yako inakuwa imeisha watu wanaenda na mahesabu makali mno.
Swali lake la pili alishangaa sana siku ile amemuua bwana mdogo Ashrafu Hamad lakini baadae anakuja kuambiwa huyo kijana ni mzima wa afya kabisa na hawezi kumuua kirahisi sana namna hiyo ni mtu ambae hata akikatiza maeneo yake vibaka wakimuona tu hawawezi kusimama wala kukaa sasa inawezekana vipi afe namna hiyo, kingine aliambiwa huyo ni mtoto wa kigogo serikalini ndio maana analindwa vibaya mno, alitamani sana kuhakikisha kama kweli huyo kijana alikuwa hai baada ya hapo wakutane nae, alikuwa na mazungumzo ya kikubwa na huyo kijana, siku moja ya kukutana kule Buguruni ambapo alipigwa risasi na kijana huyo miaka kadhaa iliyoweza kupita ilimfanya awe na hamu sana ya kukutana na huyo kijana alikuwa na maswali mengi sana ya kuweza kumuuliza. Mwanaume baada ya kujiuliza maswali yake hayo aliuvuta mlango mkubwa wa geti na kutokomea kusikojulikana majira hayo ya usiku mlango ukajifunga wenyewe mambo ya sayansi yanatisha sana siku hizi.

THE LAB
Ndiko yafari yake ilikokuwa usiku huo wa manane ilikuwa inaelekea majira ya saa tisa usiku karibu kabisa na RAMADA kuna night club moja ifahamikayo kama THE LAB ni club kubwa ambayo watu wasio penda kujichanganya sana huwa wanapenda kuzamia huko kwenda kupata starehe zao za kila siku, Alexander akiwa kwenye koti lake alikuwa amepaki piki piki lake kubwa akijifanya yuko bize na simu yake ili madereva wa ubber wasiweze kumshtukia pengine kuwa na wasi wasi naye alionekana wazi kuna kitu alikuwa anakisubiri hiyo sehemu, visu vyake viwili ndizo silaha kubwa zaidi alizokuwa anaziamini muda wote vilikuwa vipo kiunoni kwake. Ndani ya The Lab karibu na ilipo swimming pool alikuwa anaonekana kabisa Ashrafu Hamad akiwa ana meza yake mwenyewe na wanawake pamoja na walinzi wake sita, hakuna mteja yeyote mwingine ambaye alikuwa anaruhusiwa kusogelea kwenye hiyo meza. Tumia pesa ikuzoee au weka heshima bar ndiyo kauli iliyokuwa imetawala hapo akiwa kwenye kofia lake kubwa hakuna mtu angeweza kumtambua sura, mbele ya steji kulikuwa na live band watu wakiwa wamepandwa na midadi ya kucheza hakuna mtu aliyekuwa na muda wa kumuwazia mwenzie wakati huo, huyo ndiye mtu ambaye Alexander alikuwa amemjia usiku huo wa manane. Alikumbuka vyema sana kwamba kijana huyo hakuwa mtu wa starehe na kujichanganya sana na watu kiasi hicho hivyo alielewa huyo aliyepo hapo hakuwa mwenyewe ila alijua huyu atampeleka aliko huyo mwenyewe ambaye ndiye mlengwa wake.

Saa kumi kasoro ndio muda ambao mtu huyo na walinzi wake walikuwa wanatoka hapo ndani baada ya kutumia nusu saa nzima akiwa ameingia chumbani kufanya mapenzi na wanawake wote waliokuwa wamemzunguka, hakuwa akijali lolote lile kwa sababu pesa ilikuwepo alikuwa ana uwezo wa kumpata mwanamke yeyote yule na kwa muda wowote ule ambao angeutaka yeye hapa mjini hivyo hakukuwa na jipya sana kwake, starehe ndiyo kitu ambacho kilikuwa kipo kwenye moyo wake hakuwa na wikiendi hakuwa na siku ya kupumzika kila siku iendayo kwa MUNGU zilikuwa zinapangwa ratiba za club gani yenye wanawake wazuri sana hapa mjini basi hiyo ndiyo ilikuwa suluhisho la matatizo yake. Jina lake kamili alikuwa anaitwa Emiliano Mtambi kijana mmoja kutoka mkoani Morogoro, maisha yake kwenye hili jiji yalikuwa magumu mno wakati anaingia baada ya kukimbia ukata wa maisha kwenye familia yake huko Mlimba Morogoro ambako familia nzima walikuwa hawamtaki kabisa baada ya wazazi wake kufa, kilimo cha mpunga na kupalilia miwa ya watu kwa bei rahisi sana vilimfanya ashindwe kuvumilia manyanyaso na masimango ya ndugu zake upande wa wazazi wake ambao walimtesa na kumnyanyapaa kama vile haikuwa damu yao kabisa.

Vifo huwa vinatukumbusha umuhimu wa watu pale wanapokuwa hai, vifo vya wazazi huwa vinatupa taarifa ya kuwaheshimu sana pale wanapokuwa wapo Salama juu ya uso wa dunia, kama umebahatika kuishi na mama wa kambo basi lazima ulikumbuka sana umuhimu wa mama yako duniani, huwa wanasema nani kama mama sio kwamba ni ujinga hapana huyu kiumbe aliumbwa na moyo wa upekee sana, baba ni mhimu lakini amepewa hili jukumu mama kwa sababu yeye ndiye anaye kaa muda mrefu sana na watoto achana na wewe baba kuwa mpambanaji sana lakini huna muda na watoto wako hapo lazima kimbilio la watoto awe mama kwa namna yoyote ile, lakini pia mama ni kiumbe mwenye huruma sana, baba anaweza kukufukuza nyumbani kwa kosa dogo sana lakini mama atakutafuta huko mafichoni uliko akupatie chakula, pesa ya matumizi na kujua kama wewe ni mzima wa afya hiyo ni furaha sana kwake, MUNGU awape maisha marefu sana akina mama wote hapa ulimwenguni,machozi yalikuwa yanamtoka kijana Emiliano siku moja akiwa amejikunyata kwenye pembe ya nyumba baada ya kutukanwa sana na maisha ndivyo yalivyo ndugu wengi sana wataonekana kukujali kwa kiasi kikubwa pindi wazazi wako wanapokuwa hai ila pindi wazazi wanapo potea ndugu zako watakuonyesha rangi zao halisi, waheshimu sana wazazi wako angali bado wako hai hao viumbe ni mhimu sana hapa ulimwenguni kuliko hata unavyo fikiria wewe.

Maisha magumu ya kusimangwa na kunyanyaswa ndiyo yaliyo mfanya kijana huyu kukimbilia ndani ya jiji la Dar es salaam, alijichanganya na kuanza kuokota makopo kama ilivyo kwa vijana wengi hapa mjini ambao hawajui wanaweza vipi kuupeleka mkono kinywani, kwao kila siku maisha ni fumbo huku wengine wakichagua vyakula vya kula na bado wanalalamika MUNGU hawakumbuki hao ndio wanadamu, maisha ya miaka miwili yalimpa somo kubwa sana kwamba hakuna watu bora duniani zaidi ya wazazi kama ndugu alikuwa nao wengi sana lakini aliishi kama vile hakuwa na ndugu hata mmoja. Siku moja akiwa kwenye harakati zake za kutafuta mkate aliibukia Masaki karibu kabisa na M96 OWNER'Z hapo alikuwa amepita kuokota makopo, kwa uwingi wa makopo aliyo yapata pale palimvutia kila siku akawa anarudi mpaka ilifika muda alizoeleka sana yale maeneo, MUNGU sio athumani kumaanisha MUNGU sio binadamu alipata kazi ya kufanya usafi kwenye ile kampuni akawa mmoja wa wafanyakazi pale, aliachana na kuokota makopo akawa anapokea mshahara wake mwisho wa mwezi. Maisha yalienda kasi sana kwa umahiri wa kazi yake alikuja kujulikana mpaka kwa bosi na ndipo alipopata nafasi ya kuwa moja ya vijana waliokubali kutengenezewa sura ya bosi mwenyewe Ashrafu Hamad kwa kudanganywa kwamba atakuwa anakaa ofsini siku bosi hayupo maana huwa hakai ili kusiwe na lawama yeye atakuwa anaichukua hiyo nafasi, kwa pesa aliyo ahidiwa milioni mia saba na maisha yake yalivyokuwa asingeweza kuikataa kabisa alikubali haraka sana huo ndio ulikuwa mwanzo wake wa kuondokana na umaskini kwenye maisha yake lakini hakujua uhatari wa hiyo kazi ambayo alikuwa amepewa, alikuwa na hasira za manyanyaso hivyo aliamua kuzitumia pesa zake kula starehe kama kutuliza hasira kwa maisha ya dhihaka aliyo yaishi kwenye maisha yake.

Walitoka nje ya hiyo club gari aina ya BMW x6 ilikuwa kwa ajili yake aliipanda huku gari aina ya Hurrier ikiwa imewabeba watu waliokuwa wanahakikisha ulinzi wake kwa masaa 24, hayo yote Alexander alikuwa akiyashuhudia kwa usahihi sana aliacha wakapita naye hakuchukua muda sana alipanda kwenye piki piki yake akaanza kuwafuatilia hao watu. 6378 TZNI Kinondoni B ndiyo namba ya nyumba ambayo msafara wa kijana Emiliano waweza kumwita Ashrafu Hamad feki huyo ulipoishia, mlango ulifunguliwa na bosi huyo wa mchongo aliweza kuingia hapo ndani kwa madaha akihisi dunia nzima yote ni yake. Alexander alikuwa yupo nao hatua kwa hatua akiwa makini mno asiweze kugundulika aliona wote wakiingia ndani na geti likafungwa. Alitabsamu baada ya kuangalia saa yake ya mkononi 10:15, dakika kumi na tano tangu itimu saa kumi alfajiri ndivyo saa yake ilivyokuwa ikimuelekeza vyema sana hakuwa na muda mrefu sana wa kukaa hapo.

Visu viwili kiunoni vilichomolewa vyema piki piki ikiwa bado haijazimwa alihesabu mpaka tatu mwanaume akikimbia kuelekea ulipo ukuta huo alidunda hapo mara moja kisha visu vilitumika kupanda kwenye huo ukuta mrefu, nguvu za mikono zilitakiwa sana visu hivyo kuweza kuzama kwenye zege zito lililokuwa kimefunikwa na rangi nzuri kwenye ukuta huo, sekunde kadhaa alikuwa amefika juu kabisa ya ukuta almanusura mikono ishike kwenye nyaya zilizokuwa zikipitisha umeme mkubwa sana, alijigeuza haraka koti ndilo lililokuwa limegusa huo waya mmoja lilikuwa limeshika moto wakati huo Alexander alikuwa amedondokea ndani, alilivua haraka na kulizima, alishukuru MUNGU kwani huo waya ungemgusa ngozi yake tu habari yake ilikua inaishia hapo hapo. Moshi wa hapo uliweza kuwashtua wanaume wanne ambao walionekana kuwa walinzi wa nje walikimbilia haraka sana hilo eneo ni kweli walikuta kuna koti kubwa ambalo bado lilikuwa linafuka moshi lakini hakukuwa na mtu yeyote.

Mwanaume mmoja kati yao aliinama na kunusa koti hilo kisha alionekana kufurahia hicho kitu alivyo nyanyuka hapo aligeukia sehemu palipokuwa na bustani akatamka
"Tusipoteze muda ebu jitokeze utuambie unataka nini mpaka uje kwa wizi kwenye nyumba za watu" hivyo ndivyo viumbe hatari wanavyo ishi, huwa wana uwezo mkubwa wa kuitambua hatari ya aina yoyote ile kwa sababu ndiyo masha yao, licha ya ule moshi harufu ya pafyumu ya bei ghali bado ililuwa ikinukia kwenye hilo koti hicho ndicho kilichofanya huyo mtu atambue mahali alipokuwa amejificha Alexander, mwanaume baada ya kuona amegundulika tayari hakuwa na namna zaidi ya kujitokeza hadharani.

"Haya useme haraka unataka tukusaidie nini" sauti iliyokomaa ikionekana wazi aliye itamka alikuwa mtu mwenye kujiamini ilipenya sana kwenye maskio ya Alexander, hata hivyo haikumtisha chochote kile.
"Kuna kijana ametoka kutumia pesa zake vibaya saivi kwa wanawake huko ameingia hapa nina mazungumzo naye kidogo hivyo mwambieni aje hapa niongee naye"
"Unaweza ukasema shida yako ikamfikia kwa wepesi tu, ebu tusipoteze muda usipende tukuulize kwa nguvu" mwanaume yule aliongeza Alexander aligeuza macho yake kuwatazama wale vijana wengine watatu ambao ndio hao aliambiwa watamhoji kwa nguvu baada ya hapo alicheka kwa nguvu sana.
"Ndo hawa watoto unaniambia kwamba watanihoji mimi kwa nguvu?" Alikuwa anaongea huku mikono yake ikiwa inaelekea kiunoni alijua hapo sio salama sana hivyo umakini ndicho kitu pekee ambacho kingemhakikishia usalama wake.
"Ebu ongeeni naye kwanza apunguze jeuri" yule mtu aliwapa ishara vijana wawili wakazungumze na Alexander ili apunguze jeuri, mikono yake ilikuwa inafanya kazi mithili ya umeme visu viwili vilitolewa alilala chini kwa kujiburuza kijana aliyekuwa mbele alichanwa na kisu sehemu za siri, mkono ulishikwa chini mwanaume aliinuka wa nguvu kwa kuigeuza miguu yake ilienda kuishia kwenye shingo ya huyo kijana aliivunja shingo akiwa hajatua chini bado, wapili alikuwa amefika ngumi yake aliyoirusha kwa nguvu ilidakwa mkono ulivunjwa kabla hajashuka chini vidole viwili vilizamishwa kwenye koromeo lake kisu kikapitishwa sikioni na kuzamishwa ndani, wale wenzake waliogopa kidogo nusu dakika mwanaume alikuwa amepita na vijana wawili.
"Nifuate" yule kijana aliyekuwa amewaamuru vijana wake waongee vyema na Alexander alimpa ishara hiyo Alexander amfuate, yeye mwenyewe alisita kwanza kivipi kirahisi namna hiyo aweze kukaribishwa, alianza kusogea taratibu akiwafuata vijana hao wawili nyuma huku akiwa makini sana. Mlango mkubwa wa kuingilia ndani ulifunguka mbele yake walikuwa wamekaa vijana wawili walio fanana sana, wote walikuwa wanaonekana wakiwa kwenye sura ya Ashrafu Hamad na hawakuwa na wasi wasi kabisa juu ya ujio wake na hakuna hata aliyeshtuka wote walikuwa wapo bize tu na kuangalia televisheni ambayo ilikuwa imewekwa picha moja ya kutisha sana, hakuelewa ni yupi aliyekuwa amemfuatilia kuanzia kule The Lab wote walivaa nguo sawa na hakuna aliye onyesha dalili yoyote ya kulewa kama yeye alivyokuwa amemuona mmoja kule club alikuwa anayumba yumba sana lakini hapa ilikuwa tofauti, basi alijijua kabisa ameshaingia kweye mtego kipumbavu sana alijicheka yeye mwenyewe alikuwa anawinda kwa wawindaji.
"Nilijua utawahi kufika umechelewa sana mpaka sijalala kabisa nakusubiri wewe tu ila karibu sana nasikia unanitafuta mno mpaka umeamua kuniulia ndugu yangu mmoja hivyo nilitaka tuongee kidogo mimi nawewe leo" ni sauti ambayo ilitokea pembeni yake kutoka pale aliposimama, kilikuwa chumba kikubwa ambacho sehemu kubwa ilikuwa ipo tupu kabisa bila kitu chochote, mtu aliyekuwa anaongea ndiye aliyekuwa Ashrafu Hamad mwenyewe nayeye alivaa nguo kama zile za wale wenzake wawili, mwili wake tu na macho yake vilimpa ishara mbaya Alexander kwamba huto kijana sio mtu wa kawaida, hakuwa na wasi wasi kabisa kijana huyo mkononi alikuwa na glass ya maziwa akiwa anakunywa taratibu, Alexander aligeuza macho yake pembeni zaidi ya wanaume kumi na wawili wenye suti nyeusi na miwani myeusi wakiwa na silaha za moto walikuwa wamejipanga kwa usahihi sana hayo maeneo, aliogopa sana kitu kilichokuwa kinaenda kumkuta hakujua hatima yake itaamuliwa na nini.

Wasakana waonana, Alexander amejiingiza kwenye mtego kilaini sana, alikuwa ametaka show sasa anaenda kupewa, kijana ambaye alikutana naye miaka kadhaa iliyopita na akafanikiwa kumpiga risasi moja Alexander, leo alikuwa yupo mbele yake.....unadhani atatoboa hapa kwa huyu bwana mdogo??

Naachia kalamu sehemu ya 24, sehemu inayo fuata inaenda kuamua zaidi.....bado una mengi sana ya kuyajua humu ndani.

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE........
kilikuwa chumba kikubwa ambacho sehemu kubwa ilikuwa ipo tupu kabisa bila kitu chochote, mtu aliyekuwa anaongea ndiye aliyekuwa Ashrafu Hamad mwenyewe nayeye alivaa nguo kama zile za wale wenzake wawili, mwili wake tu na macho yake vilimpa ishara mbaya Alexander kwamba huto kijana sio mtu wa kawaida, hakuwa na wasi wasi kabisa kijana huyo mkononi alikuwa na glass ya maziwa akiwa anakunywa taratibu, Alexander aligeuza macho yake pembeni zaidi ya wanaume kumi na wawili wenye suti nyeusi na miwani myeusi wakiwa na silaha za moto walikuwa wamejipanga kwa usahihi sana hayo maeneo, aliogopa sana kitu kilichokuwa kinaenda kumkuta hakujua hatima yake itaamuliwa na nini.

ENDELEA..................
Moja ya makosa makubwa sana ambayo niliwahi kuyafanya kwenye maisha yangu ni ukurupukaji, baada ya kumaliza Ile miaka mitano ndani ya Ile milima ya kutisha nilijua nimemaliza kila kitu kwenye maisha yangu kitu ambacho hakikuwa cha kweli kabisa. Siku moja nikiwa kwenye kinyago changu majira ya usiku baba yako mzee Jonson Malisaba alikuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena sikuhitaji kumfuatilia sana nyuma nyuma nilitaka nimbane yeye mwenyewe ili anipe jibu sahihi ya kile nilichokuwa nakihitaji ila ndiyo siku ambayo huwa naijutia sana kwenye maisha yangu, ningejua sababu ya kwanini maafisa wengi wa usalama walikuwa wakiwaogopa wale watu basi huenda ningechukua tahadhari kubwa mapema sana.

Sikuwa mbali sana na yale maeneo kabisa, nilishindwa kujiongeza kwamba mikutano mingi ya waandishi wa habari nchini huwa inafanyika mchana kwanini wao waufanye usiku namna ile, alikuwa na watu wawili tu ambao ndio walionekana kuwa walinzi wake sikuwa na wasi wasi nilijua wale hawawezi kunisumbua sana nilikuwa mtu imara sana kwa wakati huo miaka yangu ilikuwa inasoma ishirini tu lakini mkononi tayari nilikuwa na kazi ngumu ya kufanya. Saa sita kamili alikuwa amemaliza mkutano wake yule mzee alitoka na kuingia kwenye gari yake akiwa anasindikizwa na walinzi wake wawili. Nilikuwa makini sana na gari yangu kuhakikisha wale watu hawanipotei kwenye macho yangu, nilishangaa safari yao inaenda kuishia kariakoo kwenye jengo moja refu ambalo lilionekana lililuwa la kupangisha ila muda huo palikuwa pako kimya sana, nilizima taa za gari nikashuka na kuanza kutembea kwa mguu kuelekea ile sehemu.

"Una shida namimi?" Ni sauti iliyo nishtua kutoka sehemu ambayo palikuwa na kiza kidogo, niliona hao watu wanapita hapo nikajua wamepandisha juu ya ghorofa hivyo nilikuwa naenda kwa kujiamini kumbe uwepo wangu pale ulikuwa umefahamika muda mrefu sana hata hivyo sikuogopa kabisa.

"Yes, nina mazungumzo nawewe kidogo" Nilimjibu kwa kujiamini japo moyoni nilikuwa nina wasi wasi sana
“kipi unahitaji kusaidiwa kijana” kwa mara ya kwanza nilipata bahati ya kuongea macho kwa macho na mr Jonson Malisaba mwenyewe, niliihitaji sana hiyo nafasi kwenye Maisha yangu ila huenda niliipata kwa wakati ambao haukuwa sahihi kabisa kwangu
“wewe ni nani hasa kwenye huu mji?” sikuwa na wasi wasi sana ndio maana nilimuuliza kwa kujiamini sana bila kupepesa macho kabisa kwa wakati ule nilikuwa nikijiamini hakuna kitu ungeniambia nikakuelewa
“Huu ni usiku mrefu sana nenda kaitunze vizuri familia yako achana na habari za kufuatilia maisha ya watu kwenye nyumba zao na usiku saivi ni hatari sana kwa sababu hiyo ni kesi kubwa sana kuvamia nyumba ya mtu bila ridhaa yake, ukihitaji kunijua kwa undani nenda kituo chochote cha polisi watakuelekeza mimi ni nani ila kama ni masuala ya kibiashara huwa siyafanyi usiku uje ofisini au utapiga simu wasaidizi wangu watakupatia msaada wa kile unacho kihitaji” alimaliza maneno yake kisha akaitazama saa yake kwa usahihi akageuka na kuanza kupandisha kwenye ngazi zilizokuwa zinapandisha juu kabisa ya nyumba hiyo walinzi wake wakiwa wamebaki pale chini kuhakikisha usalama wake

“Kama wewe kweli ni mfanya biashara kwanini unaua watu? Ndicho hicho unacho kiita biashara mbele za watu?” mguu wake haukumalizia kukanyaga kwenye ngazi ambayo alikuwa ametegemea kuifikia muda huo matokeo yake aliganda kama nusu dakika, nadhani alishtuka sana kusikia hayo maneno na alikuwa akijipanga namna ya kunijibu, aligeuka sura yake akiwa ameikunja kuliko ilivyokuwa kawaida

“Umetumwa na nani mpaka unafika hapa?” aliniuliza kiukali sana sikuwahi kumuona mtu huyo akiwa kwenye hiyo hali siku nyingi hata magazetini sura yenye tabasamu ndicho kitu kilichokuwa kinatawala sana kwake

“Utanijibu kwa kwa hiari tu au mpaka tutoane damu kwanza mzee wangu?” swali langu nadhani ilikuwa ni sababu mojawapo ya kuniponza siku ile nilishituka nashindiliwa na teke moja lililokuwa na uzito wa haja, mwili wangu ulikuwa umekomaa mno, ulikuwa kama umekufa ganzi lile teke la moja wa wale vijana wake halikunifanya niweze kutetereka nilicheka kwa nguvu nilikuwa na hasira na mtu ambaye sikuwa nikimjua kwa lolote ila nadhani ni kwa sababu ya sumu kali ambayo nilikuwa nimelishwa kuhusu mtu huyo na bosi wangu. Sikusubiri wanifuate tena mikono yangu niliitupa chini nilidunda kwa usahihi mahesabu yangu ilikuwa ni kupita na moja ya wale vinaja wawili ambao ndio walikuwa walinzi wa yule mzee ambaye kwa wakati ule alikuwa kijana tu wa makamo ya kawaida, nilitua kwenye mbavu za mmoja alilia alipiga kelele sarakasi yangu ilienda kumalizikia kwa mwingine aliyekuwa amesimama kando na pale goti langu lilikuwa halali ya sehemu ya kifua chake alipiga magoti akitapika damu, teke lililokuwa takribani kilo sabini nililishusha kwenye kifua cha yule kijana alivunjika vibaya mno mpaka mimi mwenyewe nilimuonea huruma. Mwenzake kwa alicho kiona alitamani asikutane namimi tena niliufungua mkanda wangu kiunoni wakati anajikongoja kunijia nilipokuwepo niliuzungusha shingoni mwake na kuugeuza shingo haikuweza kumfanya kuwa mwanadamu aliyekuwa hai tena ilivunjika halafu nikaurudisha mkanda wangu kiunoni.

Niligeuka kumuangalia Jonson Malisaba nikidhani pangine angekuwa ameondoka pale ila haikuwa kama nilivyofikiria alikuwa ameweka mikono yake mfukoni akionekana kuwa mtu mwenye amani zaidi duniani kuliko mwanadamu yeyote yule, neno wasi wasi nadhani halikuwahi kupata kibali kwenye Maisha yake, niliwaza sana kipi kinampa kiburi licha ya kile nilichokuwa nakifanya sikujua najiingiza kwenye matatizo zaidi ningejua ningekimbia mimi mwenyewe usiku ule pale ila kujiamini kwangu sana Pamoja na kazi yangu vilikuwa vikinilazimu mimi niendelee kuwa pale kwa ule wakati.

“Baba kipi mtu huyo alikufanyia siku ile mpaka unaongea kwa msisitizo namna hiyo?” Jamal alionekana kumkatisha mzee Timotheo Jordan kwenye stori nzuri lakini ya kutisha ya Maisha yake yeye mwenyewe kwani mpaka wakati huo alikuwa bado hajijui kwamba yeye ni nani hasa, licha ya mambo yote yaliyo tokea kwenye maisha yake ambayo mengine alikuwa amepata simulizi kidogo kwamba huyu mtu hakuwa baba yake wa kumzaa ila bado alimheshimu sana, huyu alikuwa kiumbe bora zaidi kwenye maisha aliyo yaishi hapa duniani, mzee huyu alitoa kikohozi kikali hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya sana lakini alijikaza mno kiasi kwamba hata Jamal alikuwa haelewi kama huyo mzee anavyozidi kuongea ndivyo anavyozidi kuyapunguza masaa yake ya kuivuta pumzi ya duniani tabasamu lilishamiri kwenye uso wake ili kumfariji mtoto wake wa kumlea huyo.

“Kama tutakuja kukutana tena wakati mwingine kwenye Maisha yako yote usije ukathubutu kufanya kitu kama hiki tena sitakuja kukusamehe kamwe, umekuja kwa dharau umeua vijana wa watu ambao hawana hatia yoyote kwa sababu unajihisi wewe ni binadamu mwenye nguvu sana ila nataka nikuambie kitu kimoja ulitakiwa kujiuliza sana kwamba kwanini huyo aliyekutuma hakuja mwenyewe hapa mpaka akaamua kukutoa sadaka wewe, zingatia hilo kijana” Kauli yake nadhani sikuielewa vyema kwa sababu nilikuwa nahisi kwamba tayari nimesha mbananisha kwenye njia zangu ndio maana alikuwa akijihami kitu ambacho nilijidanganya mwenyewe nilijiamini mno.

Mahesabu ya miguu sita nilijua nitakuwa nimemfikia pale alipo, nilijifyatua pale nilipo simama hatua sita zikiwa kichwani mwangu kuelekea sehemu aliyokuwepo Jonson Malisaba, hatua yatano kama kichwa changu kilivyokuwa kinanipa takwimu sahihi za hesabu zangu nilikutana na nyundo mbili moja ilitua kwenye mbavu zangu na nyingine ilitua kwenye kifua changu mpaka nilitapika damu, ukiachana na pambano ambalo nilipigana kwa muda mrefu zaidi nilipotumwa kwenye kazi ya kuwakomboa mateka kule Nigeria siku ile ilikuwa ni siku ya kwanza kupigana kwa muda mrefu zaidi kwenye Maisha yangu, yule jamaa ni muuaji hahitaji kukupiga ngumi kumi, akikupata ngumi zake nne maeneo sahihi hauwezi kupona hata mganga wako awe nani vinginevyo nawewe uwe ni mtu mwenye uwezo kama wake ili kuihimili mishindo ya ngumi zake, zile hazikuwa nyundo bali yalikuwa ni mateke mawili ambayo yalirushwa na yule mwanaume kutoka kwenye sehemu isiyo julikana, ilikuwa siku ya kwanza mimi kutapika damu kwa sababu ya kupigwa mara mbili tu tena na binadamu kama mimi na ndiyo siku ya kwanza kabisa kukutana na yule mtu.

Alex ndilo lilikuwa jina lake ila ni maarufu sana kama Alexander, huyu ni binadamu wa kutisha sana, amefanya mauaji ya watu wengi mno hapa duniani, sio mtu wa kuombea kukutana naye mara mbili kwenye Maisha yako inaweza kuwa hatari kwa maisha yako yote mpaka unakufa, ni watu wachache sana kwenye uso wa dunia hii huwa wanakuwa na uwezo kama alio nao yule mtu. Nilikuwa nimetoka kupata mafunzo ya kutisha mno kama ningekutana na mtu asiyekuwa imara sana hata ngumi yake tu nisingeweza kuisikia kwenye mwili wangu ila yule mtu nilimuogopa sana, sikuweza kujihami kumkimbia kwa sababu mara ya kwanza nilijua ameniotea tu pengine. Baada ya Alex kujitokeza Mr Jonson hata hakusimama tena pale nilimuona anapandisha taratibu kabisa kwenye ngazi kuelekea ghorofa ya juu. Koti refu lilikuwa kwenye mwili wa mwanaume aliyekuwa mbele yangu, nilijikusanya pale chini kwa nguvu zangu zote nilimshambulia ngumi kumi mfululizo ni tatu tu ndizo zilimfika mwilini mwake na zilionekana kumuingia vyema sana japokuwa hakutikisika sana, wote tulikuwa watu hatari kupita kiasi, dakika ishirini na tano tukiwa hapo tunapigana nilihisi kama naanza kuchoka ila kwa mwenzangu ilikuwa ni tofauti alikuwa kama ndo kwanza anaanza kubadilisha kwake mapigo ndiko kulikoanza kunilegeza taratibu nikianza kuishiwa nguvu,kuna ngumi nilipigwa sikutamani kama ningekuwa miongoni mwa binadamu waliokuwa hai. Kumaliza dakika ishirini na tano na yule mtu nilistahili pongezi mno nadhani alikuwa ameniacha tu mikono yake ilikuwa inazidi kukakamaa na kuwa migumu kila dakika ilivyokuwa inasogea kilicho nishangaza naye alikuwa ni kijana mdogo tu sikujua uwezo ule aliupatia wapi.
Sikuwa na uwezo wa kusimama naye tena, teke kali la paja lilinipigisha magoti kwa lazima chini nilivyotaka kunyanyuka moja ya visu vyake viwili ambavyo huwa haviachi sehemu yoyote anayo kuwepo kimoja kilizama kwenye bega langu kingine tumboni, yule ni kiumbe katili sana huwa kila nikikumbuka natamani kulia kila siku nilipigwa ngumi kali ya uso wakati naona kizungu zungu “aaaaaaaaaaaaaaaaah”, Timotheo Jordan alipiga kelele za uchungu humo ndani akiwa anatoa machozi akionekana wazi alifanyiwa kitu kibaya sana mpaka Jamal akabaki anamshangaa

“Baba shida nini?” Swali la Jamal lilimfanya mzee huyu atulie kidogo akiwa ameshikilia sehemu ya moyo wake.

“Ni siku ambayo siwezi kuisahau kwenye yaisha yangu, ni siku iliyo nifanya nikakosa kuwa na familia, ni siku ambayo haikunifanya nikawa na uhakika wa kusimama mbele ya wanawake nikajisifia urijali wangu, wanadamu ni wabaya sana yule mtu alizikata sehemu zangu za siri. Nililia sana ile siku, sehemu za siri kwa mwanaume ni zaidi ya utajiri wowote ule unao ujua wewe hapa duniani, hakuna mwanaume aliyekikosa hicho kiungo akasimama kwa ujasiri na kujisifia mbele za watu kwa sababu anaweza kuishia kwenye michezo mibaya sana, sikuamini nikiwa kwenye kilio kikali niliona amezishika sehemu zangu hizo za siri akazitupa mbali na hapo sikuweza kuelewa kilicho endelea tena” stori ya mzee huyu akiwa anatoa machozi ilimsisimua sana Jamal alikuwa amefumba macho kwa hisia mpaka nayeye chozi lilimtoka, alimfikiria mwanaume huyo amewezaje kuishi akiwa kwenye hali hiyo, kwenye hii dunia yenye masimango makubwa sana ukiwa na matatizo kama haya, alimuonea huruma sana huyo mbele yake kwake alikuwa ni kama baba lakini pia kwa nchi alikuwa ni jasusi hatari mno ila hakuna ambaye alikuwa anajua kwamba huyo mtu hana hicho kitu.
.
Hii ndio dunia na hao ndio wanadamu tunao ishi nao.

Binafsi sijui nini kilifuata na kivipi huyu mzee aliweza kupona na kama alipona ni nani alimsaidia?, je kumfuatilia Jonson Malisaba ndo kuliishia pale? Na vipi ilikuaje mpaka yeye ndo akamsaidie mtoto Lenovatus?, Alexander alikuwa chini ya Mr Jonson Malisaba? Kama ni hivyo na tumemuona alikuwa anamlinda mzee huyu kivipi tena yeye ndiye amuue?

Niseme tu sehemu ya 25 natandika daruga tukutane tena wakati ujao.

Tupo sehemu ya 25 tukiwa tumebakisha episodes 75 ili tufike mwisho kabisa ambayo ni episode ya 100, basi leo nakupa episodes 50 Kwa shilingi 2500 tu kama bure na kwa ambaye anahitaji full yote unalipia 4000 tu Kwa leo nakupatia mpaka nukta ya mwisho kabisa episode ya 100.

Namba za malipo ni
0621567672
0745982347

Zote majina ni FEBIANI BABUYA

Usisahau GEREZA LA HAZWA Ipo episode ya 18 mpaka sasa.

Njoo uburudike na kalamu ya Bux the story teller
 
  • Thanks
Reactions: ADK

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

TULIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO........

“Niko wapi hapa” lilikuwa ni swali langu la kwanza tu baada ya kushtuka kutoka kwenye usingizi wa kifo, macho yangu yalikuwa bado yana ukungu kiasi chake kwa mbali nilikuwa namuona mtu mmoja ambaye alikuwa amenipa mgongo, suti kubwa mwilini mwake ndicho nilicho fanikiwa kukiona kwa wakati ule. Mkono wangu mmoja na sehemu ya bega ulikuwa imejaa bandeji kiasi kwamba hata nyama za mkono zilikuwa hazionekani kabisa, sikuwa nakumbuka chochote nilishangaa nikiwa kwenye hiyo hali, macho yangu niliyageuza pembeni ndipo nilipo ziona mashine kubwa zikiwa zinaonyesha mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda kwa utaratibu mzuri kama ilivyokuwa inatakiwa, mikononi kulikuwa na drip mbili ambazo zilinifanya kugundua kwamba nilikuwa mgonjwa na hapo huenda ilikuwa ni hospitalini. Nilitaka kuinuka niliuma meno kwa maumivu makali ya tumbo hiyo sehemu kilikuwa kimezamishwa kisu nadhani bado palihitaji muda wa kutosha ili kuweza kupona na kuwa kwenye hali ya usawa kabisa kama ilivyokuwa mwanzo.

Mguu ulikuwa umepigwa plasta maeneo ya paja ulikuwa hauna nguvu kabisa, nilitulia kidogo ndipo nilipoanza kuvuta kumbu kumbu ya nyuma juu ya matukio yaliyokuwa yamepita ili nielewe kivipi nimeweza kufika ile sehemu nikiwa hata sijitambui kabisa. Nilitoa machozi mengi sana baada ya kukumbuka mpaka muda huo sikuwa na sehemu zangu za siri, nilitamani sana ningeachwa nife pale pale na sio kusaidiwa nikiwa kwenye hali kama hii iliniuma mno, nilikuwa bado hata familia sina kabisa ila ndio hivyo maisha yangu mapema sana yalikuwa yamesha haribika kwa siku moja tu nikiwa kijana mdogo wa miaka ishirini pekee.

“Kwanini umenisaidia kuja kuteseka kwenye huu ulimwengu” mpaka muda huo bado mtu huyo alikuwa amenipa mgongo hivyo sikuweza kujua kabisa kama alikuwa ni nani yupo humo ndani japokuwa nilihisi tu kwamba ni lazima yeye ndiye aliyeweza kunisaidia kwani hakukuwa na mtu mwingine yeyote.

“Hongera sana kwa kuweza kurudi kwenye maisha mengine mr Timotheo Jordan” nilishtuka baada ya kuona mtu huyo alikuwa akinijua kwa usahihi sana, aligeuka kutazama nilipokuwa nilitamani sana ningesimama lakini sikuwa na huo uwezo kabisa, mwanaume huyo ndiye mtu aliyekuwa amesababisha mimi kuwa kwenye hiyo hali Jonson Malisaba ndiye mwanaume aliyekuwa mbele ya macho yangu nilikuwa kwenye ndoto na nilipaswa niamke sasa ndivyo akili yangu ilivyoweza kunidanganya kabisa kwa mara ya kwanza lakini hii haikuwa ndoto kila nilichokuwa nakiona mbele yangu kilikuwa cha kweli kabisa huyo ni mtu ambaye nilihitaji sana kukutana naye tuweze kuongea kwa mapana na marefu leo alikuwa yupo mbele yangu nikiwa kwenye hali ya majuto makubwa sana kwenye maisha yangu.

“Huyu mtu aliye nitendea haya yuko wapi kwa sasa?” niliuliza kwa hasira ni dhahiri nilitamani sana kumuona huyo mwanaume ila hata angekuja kiuhalisia kwa hali niliyokuwa nayo nisingeweza kusimama naye hata kidogo hasira hasara ndicho kilichokuwa kikiniendesha kwa wakati ule.

“Mshukuru sana MUNGU wako umeweza kuamka na kuiona siku nyingine, ni siku saba sasa tangu umelala kwenye hicho kitanda, ukipona utachukua vitambulisho vyako kwenye kabati lililopo pembeni yako hapo na usije ukarudi tena kufanya hicho ulichokuwa unajaribu kukifanya ni hatari sana kwako” alinishangaza maneno yake machache alitaka kuondoka baada ya kumaliza maelezo yake alianza kuondoka mle ndani.

“Ina maana umesha nijua mimi ni nani?”

“Hiyo ndiyo sababu iliyonifanya nikusaidie baada ya kukujua kwamba wewe ni mtu wa serikali”

“Wewe ni nani hasa mpaka uweze kunisaidia mimi mtu wa serikali ambaye ulikuwa na mpango wa kuniua na umenifanyia ukatili mkubwa kama huu kwenye maisha yangu?” aligeuka na kutabasamu baada ya kulisikia swali langu

“Dunia imebadilika sana, wanadamu siku hizi ni wajuaji kupitiliza yaani wanaweza kutengeneza stori kukuhusu wewe na watu wa huko nje wakaamini kwamba ni kweli wewe kweli ndivyo ulivyo, mimi nawewe ni watu sawa ila tumepishana tu namna ya ufanyaji wa kazi ndiyo maana wewe uliamua kuhisi unanijua sana ndiyo sababu ukapata mpaka ujasiri wa kunifuata majira yale ya usiku pale kichwani mwako ukiwa tayari una jibu lako kuhusu mimi kitu ambacho sio cha kweli kabisa” maelezo yake kiukweli yaliniacha njiapanda nilidhani labda ni kwa sababu sikuwa na elimu lakini alikuwa mtu wa kutumia akili kubwa sana kwenye kila neno lake ambalo alikuwa analitoa mdomoni mwake.

“Wewe ni nani hasa mpaka useme mimi nawewe ni watu sawa?” nilikuwa na hamu sana ya kuweza kumjua huyu mtu, alijongea taratibu akatoa kitu mfano wa mashine ndogo sana ambayo ni mojawapo ya mashine ambazo huwa zinatumika kukagulia watu kwenye mageti ya sehemu maalumu hasa Ikulu au sehemu kubwa sana za serikali, kwanza nilishangaa kitu kama hicho kakitoa watu, mle ndani ghafla kiza kilitawala zilibaki tu mashine ambazo ndizo zilikuwa zipo pale kuhakikisha maisha yangu yanasalimika kutoka kwenye kifo.

“Mehesh Prakash ndilo jina langu, sijazaliwa India ila maisha yangu nikiwa mdogo nimelelewa na mhindi mmoja ambaye alikuwa mfanya biashara mkubwa sana hapa nchini na ndiye aliyeweza kunipatia hilo jina, Jonson Malisaba ndilo jina langu la kuzaliwa, kwa sababu yule mhindi alinilea kama mwanae baada ya kunichukua kwenye kituo kimoja cha watoto yatima aliweza kunipenda kama mwanae wa kumzaa hivyo alinipa kila kitu nilicho kihitaji kwake nilikuwa mwanae kabisa hivyo namimi nilimzoea kama baba yangu, nilisoma kwenye shule nzuri sana na kufanikiwa kumaliza masomo yangu, nilikuwa nimekuwa kijana wa kujielewa ndipo yule mzee alipoweza kutoweka duniani, kwa sababu kila kitu alinirithisha mimi utajiri wake wote ulikuwa upo mikononi mwangu. Nilikuwa mtu mwenye pesa nyingi nikiwa bado kijana mdogo tu hivyo kuna mtu mmoja kutoka kwenye idara nyeti ya serikali alinifuata na kuniomba nitumie baadhi ya mali zilizopo kuisaidia serikali, kwa sababu ilikuwa ni nia ya kuisaidia nchi yangu mwenyewe nilikubali kuufuata ushauri wake kwa asilimia zote miamoja.

Ilifika siku akawa amenikalisha chini ndipo aliponipa hadithi kamili ya umoja ambao unaitwa M96 OWNER’Z, aliniomba niingie kwenye huo umoja kama moja ya wawekezaji ili nikajue unahusiana na nini hasa kwa sababu walikuwa wamesha utilia shaka mapema. Lilikuwa suala ambalo halikuhitaji mimi kukurupuka sana kulianza lakini nilitolewa wasi wasi baada ya kuweza kukutanishwa na mheshimiwa raisi ambapo yeye kwa mdomo wake aliniomba nifanye hivyo. sikuzubaa tena nilikubali moja kwa moja ilikuwa ni heshima kubwa sana kuweza kuombwa na mheshimiwa raisi. Huo ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kuingia kwenye huo umoja nikiwa bado kijana, watu wale pesa zangu ziliwashawishi sana kuweza kunikubalia haraka kwa mara ya kwanza nilitamani sana kuweza kujua kilichokuwa kinaendelea kwenye kampuni ile iliyokuwa ikijihusisha na usindikaji wa nyama. Pesa nyingi nilizowekeza pale zilinifanya kuwa na nafasi kubwa, kuna siku nikiwa nipo nyumbani baada ya kutoka kwenye kazi zangu walikuja wanaume kumi na mtu mmoja ambaye mpaka leo sijawahi kufanikiwa kumuona sura yake wala kumjua baada ya yeye kufika tu umeme ulizima kila sehemu kwenye ule mtaa hivyo tuliongelea gizani nadhani huyo ndiye kiongozi mkuu wa huu umoja, ni mtu makini, hatari, analindwa kuliko hata ikulu panavyo lindwa, ana watu makini sana kiasi kwamba hata nzi hawezi kuigusa hata kola ya shati lake.

Jadesh Mikasa ndilo jina ambalo aliweza kunitajia kama ni la kwake japo kwenye kufuatilia kote hatukuwahi kulikuta hilo jina kwenye data zozote zile hapa duniani hivyo nilijua huenda ni mtu ambaye utambulisho wake haujulikani kabisa. Kwa mara ya kwanza alinipa mambo machache sana ambayo yanafanyika mle ndani kwa sababu tayari nilikuwa miongoni mwa wawekezeji wakubwa kwenye ile kampuni, mambo niliyokuwa nasimuliwa yalikuwa yanatisha mno ila nilipewa onyo kali sana licha ya kuificha familia yangu mbali watu wale walikuwa na taarifa zangu zote mpaka familia yangu ilipo, ni watu makini kupita kiasi hawafanyi kosa lolote lile kwenye mambo yao ambayo wanayafanya, sikuwa na namna ilinibidi nikubaliane na matakwa yao na kuwaaminisha hilo walianza kunipa mitihani ambayo kuna muda ilinilazimu kumwaga damu zisizokuwa na hatia yoyote ile, ni kazi ambayo nilikuwa nimekabidhiwa na nchi hivyo ilitakiwa niifanye kwa asilimia miamoja. Imani ndicho kitu pekee ambacho kitafanya wanadamu waweze kukupatia kila kitu kwenye maisha yako kama mtu hawezi kukuamini basi hakuna kitu utaweza kuambulia ndio maana waanadamu tunakumbushwa sana kuwa waaminifu kwenye kila jambo tunalo lifanya hasa pale unapokuwa mbele ya watu wanao kuamini sana. ndicho kitu nilichoweza kukifanya ilinibidi kwanza nifanye waniamini ndio maana nilikuwa tayari kufanya kila kitu ambacho wao walihitaji nikifanye ili waniamini” maelezo yake yalinifanya jasho linitoke sikuwahi kufikiria kama huyo mtu alikuwa ni mtu wa serikali na alikuwa pale kutekeleza majukumu ya kitaifa ila nilitatizwa na kitu kimoja ambacho mpaka muda huo sikukielewa kwa mtu huyo. Nilihema kwa nguvu mpaka hasira zangu zote zilikuwa zimeisha kabisa kwa mwanadamu aliyekuwa yupo mbele yangu kitu alichokuwa anakifanya ndicho ambacho hata mimi nilikuwa nakihangaikia kila siku kwa muda huo na ndicho kilinifanya kuwa kitandani kwa wakati huo.

“Sasa kama wewe ni mtu wa serikali kwanini watu wa usalama wakutafute sana namna hiyo na jina lako kule linaonyesha wazi wewe ndiye mtu unaye tafutwa zaidi?” nadhani swali langu lilikuwa mhimu sana kwa wakati ule hata kama ungekuwa ni wewe lazima ungemuuliza iweje mtu wa serikali atafutwe na serikali? Ilikuwa lazima anipe maelekezo ya kutosha kuhusu hilo.

“Serikalini najulikana kwa watu wachache sana hata mkurugenzi wa usalama wa taifa hanijui na ndiyo sababu unaona watu wa usalama wa taifa wananiandama, hata wewe nimekusaidia baada ya kujua unatoka ndani ya idara ya usalama wa taifa” alinieleza kwa kifupi bila wasi wasi

“Kama haupo chini ya idara ya usalama wa taifa sasa unafanya kazi chini ya nani?” swali langu lilimfanya atabasamu sana

“Inakubidi uwe na mdomo mfupi sana kwa maana ukijaribu kuurefusha unaweza kuwa miongoni mwa vijana watakao ingia kwenye historia mbaya ya kuweza kufa mapema wakiwa bado hawajatimiza kabisa malengo yao” aliweka kituo kidogo baada ya kuona siongei chochote aliendelea tena.

“Nafanya kazi na watu wawili, mkuu wa majeshi pamoja na mheshimiwa raisi” maelezo yake yalinishtua sana watu alio wataja walikuwa watu wakubwa mno hapa nchini, nilijikuta naanza kumuogopa mtu huyo baada ya kugundua inawezekana kuna mambo mengi sana ambayo siyajui bado kuhusu yeye

“Kwenye hiyo kazi wewe unasimama kama nani?” nilimuuliza nikiwa natokwa na jasho pale kitandani

“Mimi ni mtoa taarifa za mhimu zaidi ambazo zitaweza kuisaidia nchi kuhusu huu umoja ambao unaonekana ni hatari sana kwa maisha ya baadae”

“Kama walisha ujua kwanini wasiwakamate tu mambo yote yaishe?” niliuliza swali ambalo mimi mwenyewe baadae nililiona kuwa la kijinga sana kwani kama wangekuwa na huo uwezo wa kuwakamata kirahisi wangekuwa wameshafanya hivyo.

“Kwanini wewe umeshindwa kunikamata?” aliniuliza swali ambalo lilinipa mwanga juu ya uhatari wa hilo kundi kama huyu analindwa hivi huyo kiongozi wao itakuaje.

“Na huyo kiongozi wenu uliye mwita Jadesh alikwambia siri gani alipokuja kwako ambayo umesema ilikufanya mpaka uogope sana?” alibadilisha kidogo sura baada ya kumuuliza hilo swali.

“Ukiwa kama mwanaume jifunze namna ya kukitumia kifua chako kwa usahihi vinginevyo kitakuponza, upana wa kifua chako ndio usalama wa maisha yako ukihisi unayajua sana mambo hautafika hata kesho ukiwa bado unahema, ukitoka hapa nitafute kwa hiyo namba 911, hiyo ni namba ya polisi ukipiga we ongea nao kwa kuzuga zuga mpaka mmalize kuongea usitoke hewani hata ikikatwa baada ya dakika tano simu itaita kupitia namba hiyo hiyo ipokee utaongea namimi, tumia simu ya mezani na hakikisha hakuna anaye lijua hili” baada ya kumaliza maelezo yake kwa usahihi aliiweka kola ya shati yake vizuri iliyokuwa ndani ya suti, kiza kilichokuwa humo ndani kilinifanya nisimuone ila hatua za viatu zilinipa taarifa mwanaume huyo alikuwa anatoka humo ndani, dakika mbili baadae umeme uliwaka kama kawaida mle ndani.

Mimi mwenyewe sielewi elewi kinacho endelea kwenye hii hadithi akili yako ndiyo mafanikio yako ya haraka kuielewa.

Niseme tu 26 sina nyongeza tena nadondosha kalamu chini

Bux the story teller
 
Mkubwa Bux aisee na buku 2 ndugu yako unaweza nisaidia kipande?
 
Judge sio Hakimu mkuu. Judge anahudumu mahakama kuu hadi mahakama ya rufani kwa mfumo wa Tanzania.

Hakimu anahudumu kuanzia ngazi ya Mahakama ya mwanzo, Wilaya na Hakimu mkazi.
 
Naomba nisaidie maana ya HAKIMU kwa kiingereza na JUDGE kwa kiswahili[emoji3578] nitakuwa nimekujibu nadhani
 
Judge sio Hakimu mkuu. Judge anahudumu mahakama kuu hadi mahakama ya rufani kwa mfumo wa Tanzania.

Hakimu anahudumu kuanzia ngazi ya Mahakama ya mwanzo, Wilaya na Hakimu mkazi.
English ni pana sana mkuu huwa inaelezea maneno either kwa DENNOTATIVE their original meaning or CONNOTATIVE-extra or additional meaning .....JUDGE in Swahili kwa kutumia urban dictionary inaielezea kama HAKIMU.....nadhani kuna difference in translation ndo imeingia hapo katikati[emoji3578] asante kwa maoni[emoji122][emoji2768]
 
Back
Top Bottom