Ibada ya Wakristo kuabudu Jumapili imeanza Karne ya nne. Ni kwanini Karne 3 za kwanza watu waliabudu Jumamosi?

Utatambua vipi kuwa hii ni siku ya saba?
Ukisoma kwenye biblia kifo cha Yesu katika luka 23 mwishoni na 24 mwanzoni, zimetajwa siku tatu kwa kufuatana.

1. Siku ya maandalio(hii ni ijumaa na biblia ya wakatoliki imeandika kabisa ijumaa) Hii ndio siku aliyokufa Yesu.

2. Siku ya sabato (hii imetajwa baada ya siku ya maandalio maana yake ni siku baada ya ijumaa ambayo ni jumamosi). Hii siku mwili wake ulishinda kaburini.

3. Siku ya kwanza ya juma (hii imetajwa baada ya siku ya sabato kwa maana hiyo ni jumapili) Na asubuhi yake ndio walienda kaburini kwa Yesu.

Kwa maelezo zaidi soma Luka 23:53-56 na Luka 24:1 ni maneno machache sana ila yameeleza sabato ni siku gani?
 
Mie nikifika hapo tu kwenye mambo ya dini vile kila mtu alikaririshwa imani yake ndo sahihi halafu wanachokiamini wengine sio sahihi huwa nachoka!
Kila dhehebu wanaamini ya kwao ndo njia sahihi! Mie naona hata kwenye hizi dini huenda tulipigwa ili angalau dunia iwe rahisi kutawalika ila sasa hawa walioleta dini walikosea wangehakikisha dini inakuwa moja dunia nzima na vizazi vyote wangekaririshwa dini moja tu mpaka hapa ingekuwa poa sana
Ila wakaacha dini mbili ukristo na uislamu halafu imani zao na vitabu vyao vinapishana sana mbaya zaidi dini hizi kwa sasa zimezaa matawi ya madhehebu tofauti ambapo kila mmoja anaamini ya kwake.
Anyway acha nibaki na kile nnachokiamini tu.
Mungu hajakuumba kama mnyama, amekupa utashi na akili, Maana yake kwa akili na utashi wako unao uwezo wa kuutafuta ukweli na ukaujua.

Nakupa challenge, kwa kutumia simu yako ifuatilie historia ya hizi dini ilikoanzia,

Tuuweke uislam pembeni maana umekuja zaidi ya miaka 600 baada ya ukristo.(Mungu asingekuwa na sababu ya kutuletea imani nyingine kama maovu ya watu yameongezeka sababu anazo njia nyingine na alishazitua miaka ya nyuma).

Tena zingatia hili, Biblia imeweka wazi, fuata mafundisho ya Mungu, usifuate mafundisho ya wanadamu, kwa hiyo katika kusoma kwako angalia tu kile Mungu anasema katika biblia na katika historia(maana ni matukio ambayo kweli yametokea).

Chimba hayo niliyokuambia deep down utajua kwanini madhehebu yamekuwa mengi duniani. Na utajua wapi mahali sahihi unapotakiwa kuwa.
 
Tuache hayo majina ya sunday na saturday. . .

Nazungumzia ibada ya siku ya 7 na ibada ya siku ya kwanza
Hivi mkuu masaa, siku, mwezi na mwaka ni nani alianzisha? Na pia hata hiyo sabato una uhakika ni siku ya jumamosi? Na kama ni Ndio Je jumamosi na jumapili zina utofauti gani?
 
Kwanza kabisa naomba msingi wa uzi huu uwe kwenye ukristo, maana tukiongea kwa misingi ya madhehebu yetu hatutafika lengo letu.

Karne ya kwanza ya 1, 2, 3 watu walipumzika na kuabudu siku ya Jumamosi mwanzoni mwa Karne ya nne watu fulani waliamua kubadili siku hii na kuhamia Jumapili. Je tunafuata maagizo ya wanadamu wenzetu au tunafuata Maagizo ya Mungu?

Kila aliyeuona uzi huu ninaamini ana access ya mtandao, unaweza kugoogle ibada ya jumapili imeanzishwa lini na mwanzilishi ni nani.

Tangu kuumbwa kwa dunia Mungu alishaweka wazi kwamba Sabato ni siku takatifu na aliitakasa. Na katika amri zote za Mungu hii ndio amri imeandikwa kwa maelezo marefu.

Pia wakati Musa yupo kule mlimani zile siku 40 Mungu alimgusia pia kuhusu sabato na akamuambia ni agano lake la milele.

Pia hata katika agano jipya bado watu waliendelea kuabudu siku ya sabato kuanzia Yesu mwenyewe mpaka mitume baada ya Yesu.

Mfano Luka 4:16 "Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome"

Luka 4:16 imeweka wazi kwamba ilikuwa ni desturi ya Yesu kuingia katika Sinagogi siku ya ya Sabato.

Mafungu ya sabato ni mengi na siwezi kuyaweka yote hapa, ila nataka kujibu hoja za baadhi ya watu kuhusu ibada ya J2.

1. Ibada ya J2 kama kusheherekea ufufuko wa Kristo.

Hili la kusheherekea ufufuko wa Kristo na kubadili mpaka siku aliyoweka Mungu kama siku ya ibada limeanza lini? Kwenye biblia limeandikwa wapi? Kwanini katika historia watu wameanza kutekeleza hili katika karne ya 4?

2. Yesu ndio Bwana wa Sabato, hivyo tukimfuata Yesu sabato haina haja.

Yeye mwenyewe ambaye alijiita kuwa ni Bwana wa Sabato alizishika Sabato, nimetoa mfano kwenye Luka 4:16. Lakini pia kwenye mathayo 5:18 akasema "Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie." Kwa maana hii sheria ya Mungu haibadiliki.

Na fungu la 5:19 akaonya juu ya wanaozivunja amri hizo "Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni."

3. Siku zote ni za Mungu,

Hakuna mtu aliyekukataza kuabudu siku yoyote, ila sabato ni siku ya kuacha kazi zako zote unazozifanya siku zile 6 za week na kupumzika na kuwa karibu na Mungu wako. Hata sisi wengine tunakuwa na ibada zetu kama kawaida siku zote za week ila sabato ya Bwana lazima tuitunze.

Swali langu kuu bado linabakia pale pale kwa wachangiaji wote.

Je, ni kwanini ibada ya J2 ianze karne ya nne baada ya watu kukaa na kuamua watu wapumzike na kuabudi jumapili? Je tunamfuata Mungu au tunawafuata Binadamu wenzetu kwa sababu tu wameamua mambo ambayo tumeyaona ni mema machoni petu?

Mungu atusaidie sana, Muwe na Sabato Njema.
Wengi wamenaswa na mafundisho ya udongo kuwa ipo siku iliyopangwa kuabudu
Hakuna andiko Hilo siku hiyo inayopigiwa kelele na wapotoshaji ni kukwepa Ibada kujitengea siku maalumu ya kuabudu ni kumkosea heshima muumba
Aya ya 20:8-11 katika kitabu cha kutoka kinazingumzia/kinaweka sheria ya kuto kufanya kazi hakiongelei juu ya kuabudu kitabu kinacho ongelea kuhusu kuabudu na taratibu zake no mambo ya walawi
Kutoka 20:8-11 kinazuia kufanya kazi wewe mwanzo aliye kwenye malango yako hata mifigo wako wote wametajwa ni siku ya kupimzika Tu
Siku ya kuabudu ni kila siku na kila saa hakuna siku wala saa maalumu Kwa ajiri ya Ibada unaujua mwisho wako? hata unacho kifanya ni Ibada kama kinamtukiza MUNGU
Hizo ni siku ziliwekwa maalumu Kwa ajiri ya kukutana Kwa kua wakutanapo waamini MUNGU hufanya maombi
Ikageuzwa kua ni Ibada kumbuka hata mwalimu wetu mkuu kila wakati alijitenga faraghani kuabudu hakusibiri mpaka sabatho ifike
Hebu fikiria watu wanavyo vunja hiyo amli wakihisi wako Sawa niwangapi wanawatumikisha watu na kuwalipa. Ujira wa kazi ya kuwafikisha katika kwenda huko siku ya sabatho wakati imekatazwa hata mtumwa wako asifanyishwe kazi?NK
Huku nyuma watunza sabatho wlitupa jiwe litakapo komea huluhusiwi kulivuka je wangeendaje hekaluni/sinagogi kama unataka tuamini hivyo
 
Wengi wamenaswa na mafundisho ya udongo kuwa ipo siku iliyopangwa kuabudu
Yes ipo siku iliyopangwa kuabudu, Soma Isaya 66:23 inasema "Na itakuwa Mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana"

Hakuna andiko Hilo siku hiyo inayopigiwa kelele na wapotoshaji ni kukwepa Ibada kujitengea siku maalumu ya kuabudu ni kumkosea heshima muumba
Sasa hiyo siku ameitenga yeye mwenyewe Mungu, Je sisi tunamkoseaje Heshima? Kwa sababu hatukujipangia sisi.

Aya ya 20:8-11 katika kitabu cha kutoka kinazingumzia/kinaweka sheria ya kuto kufanya kazi hakiongelei juu ya kuabudu kitabu kinacho ongelea kuhusu kuabudu na taratibu zake no mambo ya walawi
Okay inazungumzia kutokufanya kazi, Je watu hawafanyi kazi hiyo siku ya Sabato kama ilivyoamriwa?
Siku ya kuabudu ni kila siku na kila saa hakuna siku wala saa maalumu Kwa ajiri ya Ibada unaujua mwisho wako? hata unacho kifanya ni Ibada kama kinamtukiza MUNGU
Shida niliyoiona kwako umeshindwa kutofautisha kati ya kuabudu na kumuomba Mungu, Kuabudu ni neno pana sana, kuomba tunaomba kila siku,
Ikageuzwa kua ni Ibada kumbuka hata mwalimu wetu mkuu kila wakati alijitenga faraghani kuabudu hakusibiri mpaka sabatho ifike
Alijitenga kuomba na siyo kuabudu, mbona hili liko wazi?

Huku nyuma watunza sabatho wlitupa jiwe litakapo komea huluhusiwi kulivuka je wangeendaje hekaluni/sinagogi kama unataka tuamini hivyo
Ishike sabato kama alivyoishika Yesu, usiishike kama walivyoishika watu wa kale.
 
Hivi mkuu masaa, siku, mwezi na mwaka ni nani alianzisha? Na pia hata hiyo sabato una uhakika ni siku ya jumamosi? Na kama ni Ndio Je jumamosi na jumapili zina utofauti gani?
Masaa, siku, mwezi na Mwaka alianzisha Mungu mwenyewe,

Yes nina uhakika sabato ni siku ya jumamosi(Soma Luka 23:54-56 na Luka 24:1) Haya mafungu yanaeleza kufa kwa Yesu mpaka ile Jumapili wanaenda kaburini, na hapo katikati imetajwa sabato.

Biblia imewekwa wazi kwamba Mungu aliitakasa na akaibariki siku ya sabato na akatuamuru tustarehe,

Pia Yesu aliabudu siku ya Sabato soma Luka 4:16 "Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome."

Kama Biblia inaniamuru Kupumzika Jumamosi, kwanini nipumzike jumapili ambayo kihistoria imeletwa na wanadamu?
 
Kwanza kabisa naomba msingi wa uzi huu uwe kwenye ukristo, maana tukiongea kwa misingi ya madhehebu yetu hatutafika lengo letu.

Karne ya kwanza ya 1, 2, 3 watu walipumzika na kuabudu siku ya Jumamosi mwanzoni mwa Karne ya nne watu fulani waliamua kubadili siku hii na kuhamia Jumapili. Je tunafuata maagizo ya wanadamu wenzetu au tunafuata Maagizo ya Mungu?

Kila aliyeuona uzi huu ninaamini ana access ya mtandao, unaweza kugoogle ibada ya jumapili imeanzishwa lini na mwanzilishi ni nani.

Tangu kuumbwa kwa dunia Mungu alishaweka wazi kwamba Sabato ni siku takatifu na aliitakasa. Na katika amri zote za Mungu hii ndio amri imeandikwa kwa maelezo marefu.

Pia wakati Musa yupo kule mlimani zile siku 40 Mungu alimgusia pia kuhusu sabato na akamuambia ni agano lake la milele.

Pia hata katika agano jipya bado watu waliendelea kuabudu siku ya sabato kuanzia Yesu mwenyewe mpaka mitume baada ya Yesu.

Mfano Luka 4:16 "Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome"

Luka 4:16 imeweka wazi kwamba ilikuwa ni desturi ya Yesu kuingia katika Sinagogi siku ya ya Sabato.

Mafungu ya sabato ni mengi na siwezi kuyaweka yote hapa, ila nataka kujibu hoja za baadhi ya watu kuhusu ibada ya J2.

1. Ibada ya J2 kama kusheherekea ufufuko wa Kristo.

Hili la kusheherekea ufufuko wa Kristo na kubadili mpaka siku aliyoweka Mungu kama siku ya ibada limeanza lini? Kwenye biblia limeandikwa wapi? Kwanini katika historia watu wameanza kutekeleza hili katika karne ya 4?

2. Yesu ndio Bwana wa Sabato, hivyo tukimfuata Yesu sabato haina haja.

Yeye mwenyewe ambaye alijiita kuwa ni Bwana wa Sabato alizishika Sabato, nimetoa mfano kwenye Luka 4:16. Lakini pia kwenye mathayo 5:18 akasema "Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie." Kwa maana hii sheria ya Mungu haibadiliki.

Na fungu la 5:19 akaonya juu ya wanaozivunja amri hizo "Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni."

3. Siku zote ni za Mungu,

Hakuna mtu aliyekukataza kuabudu siku yoyote, ila sabato ni siku ya kuacha kazi zako zote unazozifanya siku zile 6 za week na kupumzika na kuwa karibu na Mungu wako. Hata sisi wengine tunakuwa na ibada zetu kama kawaida siku zote za week ila sabato ya Bwana lazima tuitunze.

Swali langu kuu bado linabakia pale pale kwa wachangiaji wote.

Je, ni kwanini ibada ya J2 ianze karne ya nne baada ya watu kukaa na kuamua watu wapumzike na kuabudi jumapili? Je tunamfuata Mungu au tunawafuata Binadamu wenzetu kwa sababu tu wameamua mambo ambayo tumeyaona ni mema machoni petu?

Mungu atusaidie sana, Muwe na Sabato Njema.
Ni wapi Mungu aliagiza watu kusali Jumamosi?
 
Wewe mbinguni unataka uwe unafanya nini? Uwe Unakesha unaimba milele na milele bila kupumzika? Si Bora ufe tu.
Huoni Raha kupatiwa mabikra watamu walionawiri kutoka kwa Allah?
Kuhusu wanawake Mimi sijui, Allah ndiye anajua

Deen ya haq Kwa bin Adam ni moja tu, Islam.
Umepitia ulicho kiandika mkuu?
 
Yes ipo siku iliyopangwa kuabudu, Soma Isaya 66:23 inasema "Na itakuwa Mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana"
Kwa hiyo hiyo sheria iliweka katika nyakati za isaya siyo Musa tea
Sasa hiyo siku ameitenga yeye mwenyewe Mungu, Je sisi tunamkoseaje Heshima? Kwa sababu hatukujipangia sisi.
Maana ya siku hiyo ni yakuwatoa Wana wa Israel kasumba za utumwa wasiwafanyishe kazi watu wao na mifugo Yao kama walivyokua wanafanyishwa wao kazi
Wametoka utumwani kwenye mateso wameingi rahani awafanyisshwi kazi tena ndiyo maana ya Raha ya sabatho
Okay inazungumzia kutokufanya kazi, Je watu hawafanyi kazi hiyo siku ya Sabato kama ilivyoamriwa?

Shida niliyoiona kwako umeshindwa kutofautisha kati ya kuabudu na kumuomba Mungu, Kuabudu ni neno pana sana, kuomba tunaomba kila siku,
Rejea mambo ya walawi utaona jinsi makuhani walifika katika hema /hekalu kila siku asubuhi kabla ya jua kuchomoza walienda kuabudu na wayahudi kila siku si chini ya mara tano wanaabudu
Alijitenga kuomba na siyo kuabudu, mbona hili liko wazi?
Kusujudu ni kuomba tuwe wakweli
Hebu no fafanulie nini tofauti ya kuabudu na kuomba
Yesu alisujudi huko ni kuomba
Ishike sabato kama alivyoishika Yesu, usiishike kama walivyoishika watu wa kale.
Sabatho ya sasa tofauti na ya zamani lmekuja sabatho nyingine
Si ajabu kama hiyo unayotaka kusema wayahudi walimshitaki Kwa kuhalifu sabatho Yao
Soma Kwa utulivu wakolosai 2:8-23 utabarikiwa
 
huu mstari huwa ni mwiba mkali sana kwa wasabato, akikutana nao tu lazima augue jipu la usaa na anashindwa kuongea chochote.

Wakolosai 2:16-17​

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
 
Deen ya haq kwa bin Adam ni moja tu, Islam
Islam au unyenyekevu ni matakwa ya MUNGU Kwa Waja wake sio dini
Hicho mnacho taka kua dini ni maamrisho yaliyo tolewa yangu zamami so Mapya kama unavyotaka tuamini soma
Mith29:24
Mika 6:8
Zaburi 34;2
Petro5:5
Hilo sio Jambo/maamrisho/itikadi mpya
Hapo ni lugha Tu labda nimekosea maana ya uislam ni unyenyekevu
Naomba nisahihishwe kama nimekosa maana
 
Hakuna Mungu isipokuwa Allah na Muhamad ni mtume wake.
 
Siyo kweli..

Matendo ya Mitume 20:7
Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.

Kutoka 12:16
Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu.
Hii comment sikuiona 😅😅
 
kiuhalisia, hatumwabudu Mungu jumapili tu au jumamosi tu, tunamwabudu Mungu kila siku maishani mwetu kwasababu tunaabudu rohoni sio mwilini. na hiyo haina siku. ninyi mnaong'ang'ania siku mnapoteza muda sana.

Wakolosai 2:16-17​

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

Warumi 14:5-6​

5 Mtu mmoja anahesabu siku fulani kuwa ni bora kuliko nyin gine na mwingine anaona kuwa siku zote ni sawa. Basi kila mmoja awe na hakika na yale anayoamini. 6 Anayehesabu siku moja kuwa takatifu hufanya hivyo kwa kumheshimu Bwana. Naye anayekula nyama hufanya hivyo kwa kumtukuza Bwana, kwa maana humshukuru Mungu. Hali kadhalika akataaye kula nyama hufanya hivyo kwa kum heshimu Bwana na humshukuru Mungu.
Hii pia nili iover look 😅😅
 
Back
Top Bottom