Hakika kaka....Hivi na sisi haiwezekani akatokea mjeda mmoja akawa Traole wetu kweli??
Au kama inashindikana basi tupate tu hata kama Jerry Rawlings, achukue nchi aseti mifumo na katiba sawa alafu arudishe kwa raia, ili wananchi tuwe na nguvu ya kuchagua viongozi.
Mimi natamani tumpate mtu kama Juan Francisco Velasco yule wa Peru ambaye alimpindua Fernando Belaunde baada ya kumuona anawapa kila kitu waingereza, kwanzia pwani ya bahari mpaka maeneo ya mafuta.. ile ameshika tu nchi akawanyang'anya vyote na kuvurudisha kwa wanainchi chini ya usimamizi wa serikali yake, na kisha akawakimbiza wale vibaraka wote waliokuwa wanamuunga mkono Belaunde.
Nikiangalia Samia anavyoiendesha hii nchi natamani nataman atokee mjeda mmoja mwenye ujasiri afanye kitu kama hicho, ila kwa bahati mbaya sana hili taifa halina mtu wa aina hiyo huko jeshini.