Ibrahim Traore : Umeme bure Maji bure kwa Wazee Burkina Faso Hakuna Kulipa

Hivi na sisi haiwezekani akatokea mjeda mmoja akawa Traole wetu kweli??

Au kama inashindikana basi tupate tu hata kama Jerry Rawlings, achukue nchi aseti mifumo na katiba sawa alafu arudishe kwa raia, ili wananchi tuwe na nguvu ya kuchagua viongozi.
Hakika kaka....

Mimi natamani tumpate mtu kama Juan Francisco Velasco yule wa Peru ambaye alimpindua Fernando Belaunde baada ya kumuona anawapa kila kitu waingereza, kwanzia pwani ya bahari mpaka maeneo ya mafuta.. ile ameshika tu nchi akawanyang'anya vyote na kuvurudisha kwa wanainchi chini ya usimamizi wa serikali yake, na kisha akawakimbiza wale vibaraka wote waliokuwa wanamuunga mkono Belaunde.

Nikiangalia Samia anavyoiendesha hii nchi natamani nataman atokee mjeda mmoja mwenye ujasiri afanye kitu kama hicho, ila kwa bahati mbaya sana hili taifa halina mtu wa aina hiyo huko jeshini.
 
Demokrasia kitu cha mwisho kabisa ambacho afrika inakihitaji hili kupata maendeleo...
 
Wakati Mwalimu Nyerere anatangaza Azimio la Arusha, Mzee Mtei na Balozi Christopher Kassanga Tumbo walimwambia Tanzania haiwezi kuwa ya Kijamaa kwasababu uchumi wake bado! Nikuulize swali, tulifanikiwa?
Narudia tena, Burkina Faso HAINA uwezo wa kutoa huduma bure!
 
Anaamini kwamba Umeme na Maji ni huduma za Msingi ambazo binadamu anahitaji kuzipata

Tunayakujifunza kwa Watawala na Wapiga kura huku Kusini mwa Jangwa la Sahara

Mungu ambariki huyu KIJANA !!!

Earthmover Kasumbalesa
Kwenye matumizi ya maji na umeme, unamtofautishaje kijana na mzee!? Au mita zitafungwa CCTV!?
 
Hapa mkuu umenifanya kuridhika na hil swali. Umejibu sawiaa sina swali la ziada
Ahsante sana
 
100%
 
Mimi najiulizaga huyu dogo captain aliwezaje kupindua nchi wakati ma general wapo na usalama wa taifa wapo? Yan atoke yeye rank ya chini akakalie kiti ambacho mkuu wa majeshi naamin si kama hakua anakitamani!!.
Mapinduzi ya kijeshi yakipangwa na Kanali Damiba na yatatokea mwaka 2022 jambo lilopelekea kuondolewa raisi Roch Marc Kabore.

Baada ya Mapinduzi Damiba akampeleka Traore (ambae alipanda cheo kuwa Kapteni mwaka 2020) kule kaskazini mwa Burkina Faso kuongoza kikosi cha mizinga.

Lakini Damiba umaarufu wake ukawa wapotea kiasi cha kutishia Mapinduzi mengine ambayo yangehusisha maofisa wa kijeshi ambao hawakuwa kwenye mpango wa 2022.

Kuona hivyo Kapteni Traore akaunda kikosi kamili kikiwa na maofisa wa vyeo vya chini na wakafanya Mapinduzi makubwa yaloua wanajeshi 11 na namba kubwa ya raia. Hivyo utawala wa kijunta wa Traore wakusanyisha wanajeshi ambao hawajahusika na Mapinduzi na hata hawajafahamu namna ya kuyapanga hivyo kufanya Traore aendelee na kazi yake licha ya kuwepo majaribio kadhaa ya Mapinduzi mengine kutoka vikozi vingine.

Hivyo hapo ni kwamba Mapinduzi yalikuwa ni viongozi waandamizi wa kijeshi wakawa wameondolewa na maofisa wa kijeshi wa ngazi za chini ambao waliongozwa na Traore. (weye fikiria Damiba kampandisha cheo Traore na Traore kaja kumpindua Damiba).

Yasemwa kuwa kiasi kikubwa cha wanajeshi waandamizi walokuwa na Traore au Damiba wengi wamekimbia nchi au wapo kifungoni na damiba yuko nchi Jirani ya Togo.

Kuhusu muundo wa utawala wa kijeshi ni kwamba kapteni Traore ni Kamanda mkuu au commander in chief, akifuatiwa na Waziri wa ulinzi na kisha mnadhimu mkuu wa majeshi au Chief of general staff.

Source: Wikipedia, Centre for African strategic studies.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…