ICC yakiri kupokea rasmi malalamiko kutoka Tanzania juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi uliopita

Uchaguzi umekwisha!
Tunawashukuru kwa kushiriki
Tukutane tena uchaguzi ujao panapo majaliwa
Mkuu mama D kwa hili nilijua utakimbia,ni juzi nilikua na rafiki kada mzuri wa ccm katika story tukagusia hili ,da rafiki akaniambia mkuu ukigusa hili japo Lina tija katika kuleta mshikamano wa wawatanzania lakini unafanya moyo wangu kwenda Kasi Sana ,nilicheka, Sasa leo pia yanatokea kwa MAMA D, kukimbia na mpila kwenye kwapa katikati ya mjadala
 
Political persecution itawapoteza MaCCM ...haina tofauti na Apertheid
Nani amekuwa Persecuted Budha, amekaa Belgium almost 3 yrs. Amerudi Hakuna aliyemgusa, amepewa haki yake ya msingi ya msingi ya kuchagguliwa.

Amezunguka Nchi Nzima na kutoa vitisho na mda huo wote alikuwa akilindwa na vyombo vya ulinzi vya Nchi hii, amenadi sera na na kwenye moja ya mahojiano alikiri na kuwaeifia Polisi, baaada kupiga kura akatoa neno. Sasa baaada ya kipigo ndiyo hiyo Persecution, hawajamsumbua wakati anazunguka na kutoa shombo, waje wamtishie baaada ya kumpa kipigo Cha Mbwa Koko.
Hivi huyo boya wa hapo Arusha angeshinda ubunge angekimbia.
Yaani ashindwe yeye, halafu atishiwe yeye, teh teh teh teh!
 

Hicho chama mbadala kinaoperate vipi kwenye mazingira haya? Au umejitia upofu?
 
Watu wanaangalia ushahidi uliowasilishwa mezani unaowatia hatiani, hii hoja yako ya "kidunia" ni ya hovyo kabisa.
Mkuu nmekushauri toka jana kwamba wekeza nguvu zako kupigania tume huru achana na hizi ngonjera
 

DC anavamia kwa Mbowe usiku wa manane kabeba bunduki wakati sio askari...kazi mnayo mmejaa kwenye mtego wa mabeberu safari hii..Marehemu Ruge alisema muogope Mungu na technology
 
Kule mwanzo ulianza vzr ila hapa mwisho naona umeingia woga
 
Uchaguzi wa kenya na machafuko yale ya wazi wazi akina Ruto na Kenyata kesi ikaota mbawa, ifikie mda viongozi wa chama wawe responsible na mambo wanayo yafanya, kiufupi upinzani bara ulijifia 2015
Hivi mnatumiaga vigezo gani kusema upinzani umekufa..!!...mnaongea huo ujinga kwenye chaguzi mnatumia bunduki kubaki madarakani
 
hiyo Mahakama iandae wakalimani wa kutosha, JPM na genge lake hawajui kizungu
 
Hii ni habari mbaya kwa CHADEMA...wait and see ushahidi utakaotolewa dhidi ya CHADEMA na ACT-Wazalendo
 
Tunakwenda mbele mkuu haturudi nyuma. Kwenye maendeleo yetu muda ndio kila kitu

Jipangeni Uchaguzi ujao
 
Vitendo vilivyotokea havina uzito wa kuingiliwa na mahakama za kimataifa - ni migogoro midogo iwezayo kumalizwa na mahakama za ndani ya nchi

Mara ya mwisho nimefuatilia zaidi ya watu kumi ilisemekana waliuwawa, na wengine walijeruhiwa wewe unaita hiyo ni kidogo ? hiyo Mahakama haipo kushughulikia makosa makubwa hata hivo bali makosa yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu, uhalifu wa kivita nk ila ukiwa na pesa huko haufungwi Jean Pierre bemba mtoto wa Jeannot bemba wa Congo hakufungwa licha ya kupelekwa huko alikaa kama miaka 6 alitembeza pesa akaachiwa
 
Hii ni habari mbaya kwa chadema...wait and see ushahidi utakaotolewa dhidi ya chadema na Act-wazalendo
Nimekuelewa sana mkuu

Na nimeelewa kwanini tunataka maridhiano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…