kajekudya
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 2,466
- 4,916
Yes vizuri kabisa. Juzi kati hapa walitaka ku investigate wanajeshi wa Marekani kuwa walifanya Makosa hayo huko Afghanistan. Marekani imewapiga marufuku kukanyanga Ndani ya Nchi hiyo, though Marekani siyo member wa hiyo Mahakama kwakuwa siyo signatory wa Mkataba unaoinzisha( The Rome Statute for the International Criminal Court).Asante sana kiongozi kwa tafsiri yako. Ngoja tuone na hao prosecutors wa ICC tafsiri yao ikoje...
Labda swali moja la nyongeza mkubwa; assuming Bensouda anasema haya malalamiko waliyoyapokea ICC ina mamlaka kuyasikiliza hivyo wanaanzisha investigation, je, sisi kama nchi tunaweza kupingana na maamuzi yao? Au tunaweza kuchukua hatua gani. Asante sana.
Aliyekuwa Rais wa Sudani Ali Bashir hadi leo hajapelekwa pamoja na kutolewa kwa warrant ya kukamatwa mda mrefu. Moja ya Changamoto ya International Law ni uncertainty kwenye enforcement Mechanism. Hawana Police Wala Gereza
So mtu anaweza kukataa kutii amri and nothing happens zaidi labda ya kelele na vikwazo.
Lakini pia Kama nilivoeleza awali, hii Mahakama watu wameanza kuipuza sana kwa kuwa ni Kama inatumika na baaada ya USA kuwapigia biti ndo kabisa kila mtu anawadharau. Lakini pia ni Kama inatumika.
Mfano, Kule Mymal Kuna Malalamiko ya watu wenye Imani ya Kiislam kufanyiwa Makosa hayo na Kuna watu wamelalamika na kupeleka mashtaka nadhani Gambia. Lakini nothing will be done kwa Sababu ya Mama kiongozi wa Mymal ni pro Western, ndio maana hata huskii kelele Kama mambo ingekuwa if hizo allegations zingekuwa angainst African state.
Juzi kati hapa, walifanya kituko. Wakati Uchaguzi wa Kongo umekaribia walimwachia Jean Pierry Bemba aende agombee Urais baaada ya kumshiklia kwa mda mrefu na alivoenda Mambo yakawa ndivyo sivyo wakamkamata tena.
Unaweza ukaona, kwamba hii Mahakama inavyopoteza heshima yake kwa kasi ya ajabu sana!