Idara ya Uhamiaji sasa kuwa Jeshi kamili na litawajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Idara ya Uhamiaji sasa kuwa Jeshi kamili na litawajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Checks and balances ziko wapi? Mamlaka na vyombo vya dola vyote viko chini ya Amiri Jeshi. Hatari sana.
Nadhani hii ndiyo ipo hivyo pote tu. Amiri jeshi ndiyo mkuu wa majeshi yote yaliyopo na yatakayokuwapo.

Sema kuna namna anaweza kujipunguzia majukumu kwa kuamua kuwa asiwe briefed kwa issue fulani ili mwisho awe na plausible deniability.

Hata hivyo ni mara chache rais kuyakimbia majukumu, mara nyingi huyakumbatia ili azidi kuwa na power maana with great responsibility comes great POWERS
 
Uhamiaji kuanzia enzi za kuanzishwa kwa Taifa hili ni Askari sijajua huo ujeshi mpya ni upya au labda makaratasi na sheria ndo havikusoma hivyo.

Lakini Duniani kote Hawa watu uingia kwenye kundi la maafisa usalama, Hawa ni watu wanaopaswa kuwa na ueledi wakung'amua ujasusi wa kiuchumi,kisiasa na kitamaduni kutoka nje. Bila kuwa na maafisa usalama kwenye chombo Kama hiki nchi itavamiwa kirahisi Sana.

Miaka ya nyuma Hawa watu walikuwa hawafahamiki wengi walikuwa wanaficha utambulisho wao, baadhi wanaofanya kazi mipakani ndo walikuwa wanafahamika......

Nadhani hakuna jipya maana Kama TISS Ni Jeshi kwanini tunatangaza uhamiaji kuwa ni Jeshi leo wakati ni tawi moja?

Nadhani wanatafuta sheria yakuwaingiza mtaani rasmi wakiwa na mitutu Jambo ambalo kwangu sioni Kama Lina tija, wabaki na ukachero Kama zamani waache kuwatisha wageni na ujeshi.....hatuahitaji ujeshi kushughulika na wageni nchini tunahitaji welcome face
Hakikaa t7nahitaji welcome face 😆
 
Hii idara inaitaji maafisa ambao hawana amri za kijeshi. Ni dalili za ushamba na ulimbukeni wa madaraka.
 
Back
Top Bottom