Najua unataka wazo la Biashara la kimtandao.
Anza na hizi pengine zipo sijui au hazipo.
Fanya Research yako
1. Luku Token ( ila hii iko chini ya serikali ni ngumu)
Iwe inaingia direct.
2. App ya kuuza vitu ambavyo hautumii tena.
Mtumba, iwe nguo, meza kiti, baiskeli nk
Mtu anaingia anakuwa na akaunt na anauza vitu ambavyo hatumii
3. App ya harusi.
Mtu akiwa na harus yake anajiunga, anaweka details za wahusika na namba zao na app iwe ina waremind wahusika kila due date waliyoahidi michango ikifika. Iwe pia ina mremind bwana bibi harus vitu muhimu vya kufanya as check list.
Iwe na option pia ya kupokea michango ili iwe transparency zaidi.
4. App ya kukodisha nyumba bila madalali.
Madalali wanachosha sana kwa kweli! Dah!
5. App ya wajenzi.
Iwakitanishe mafund ujenzi na wanaotaka kujenga.
Mafund wajisajili na watoe monthly fees
Na waweke kazi zao kwa picha na makadirio openly. Pamoja na bei zao za ufund