ITR
Dalili za kuanza kuanguka kwa IDF ilianza kuonekana toka Vita Vya Yom Kippur mwaka wa 1973.
Nakuwekea hapo chini sehemu ya mada niliyowasilisha State University of Zanzibar (SUZA) mwaka wa 2017:
''Katika kitabu chake, ‘’The Road to Ramadan,’’ Mohamed Heikal anaeleza barua aliyoandika Hafiz Al Asad kwenda kwa Sadat akimsihi kuendelea na mapambano.
Hii ilikuwa baada ya Misri kusimamisha majeshi yake kusonga mbele baada ya Sadat kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Henry Kissinger.
Barua hii Hafiz Al Asad aliiandika kwa mkono.
Barua hii haikumbadilisha Sadat.
Kwa kitendo hiki cha kuacha mashambulizi dhidi ya Israel, majeshi ya Syria yakalazimika kupigana na Israel bila ya mshirika wake Misri na hii ikatoa ahueni kubwa kwa Wayahudi na matokeo yake ikawa Israel kunusurika.
Inasemekana kwa usaliti huu ndipo vijana wa Ikhwan Egyptian Islamic Jihad ndani ya jeshi la Misri wakampitishia fatwa ya Sadat kuuawa na hakika hilo likafanyika mwaka wa 1981.
Mwaka wa 1991 nikiwa ''transit'' Cairo nikielekea London, nilifika Heliopolis moja ya vitongoji vya mji nikaona kuna mnara kajengewe Sadat kama shujaa wa Vita Vya 1973.
Kitu muhimu kilichojitokeza katika Vita Vya Yom Kippur ilikuwa kule kujitokeza kwa mara ya kwanza udhaifu katika jeshi la Israel kuwa linaweza kushindika.
Baada ya vita hizi mbili (1967 na 1973) Wapalestina walifanya kile kilichokuja kujulikana kama Intifada kati ya mwaka 1987 – 1993 kisha mwaka wa 2000 – 2005.
Intifada ilidhihirisha kwa Wayahudi kuwa mapambano dhidi yao kutoka kwa Wapestina bado yangalipo na hayatakoma.
Vita iliyokuja kumaliza kile kilichokuwa kimeaaminika na dunia kuwa Wayahudi hawawezi kushindwa katika vita, ni vita vya mwaka wa 2006 kati ya Hizbullah na Wayahudi.
Vita vilipoanza fikra za wengi katika nchi za Kiarabu zilirejea katika Vita Vya Siku Sita vya mwaka wa 1967 na wengi waliamini kuwa Hizbullah watamalizwa kwa muda mfupi kwa kusagwasagwa na Israel.
Hili halikutokea.
Vita vilipiganwa kwa siku 34 katika mwezi wa Julai na Agosti hadi pale Umoja wa Mataifa ilipoingia kati na kuweka makubaliano ya kuweka silaha chini na kumaliza vita.
Wayahudi kwa mara ya kwanza katika historia ya mapambano yao na Waarabu walionekana katika stesheni nyingi kubwa za televisheni duniani wakirudi Israel kutoka uwanja wa mapambano wameinamisha chini vichwa vyao.
Israel ilikuwa kwa mara ya kwanza imeonja kipigo katika vita.
Hapakuwa na shamrashamra ziliyozoeleka za ushindi dhidi ya majeshi ya Kiarabu.
Hizbullah ilikuwa imevunja, ‘’myth,’’ ile fikra ya kuwa Wayahudi hawawezekani.
Hassan Nasrallah kiongozi wa Hizbullah alikuwa akiuliza wakati wa vita, ‘’Wako wapi askari wa Kiyahudi mbona hatuwaoni katika uwanja wa vita?
Tunachoshuhudia ni ndege za Kiyahudi wakipiga mabomu nyumba za raia.’’
Baada ya vita, ilipofika wakati wa kubadilishana mateka Wayahudi walipata fadhaa zaidi pale walipokuwa wao wanapokea majeneza ya askari wao waliouliwa vitani Israel ikiwaachia huru askari hai wa Hizbullah.''
Wanafunzi wa SUZA wakifuatilia mhadhara