Mzee said unatoka nje ya mada sisi tunazungumzia uzoefu wa vitani afu wewe unaleta siasa za vitabuni!!!!Ndio maana nikakuuliza ushawahi hata kushika bunduki au kusikia mlio wa guruneti au risasi?????
Nelson...
Sijatoka nje ya mada.
Unataka nikufahamishe kama najua kutumia silaha au kama nimepata mafunzo ya jeshi.
Unatafuta nini wewe?
Umeandika kuwa mimi nilihusika na Mwembechai na kuvunjwa mabucha na mambo mengi yasiyo na maana.
Tena umeandika haya baada ya kukueleza kazi ninazofanya vyuo nilivyoalikwa hapa nyumbani, Afrika, Ulaya na Marekani na paper na vitabu nilivyoandika.
Nimekueleza haya nikiamini utakuwa na akili ya kunitambua.
Leo unataka kujua kama nina ujuzi wa matumizi ya silaha.
Kipi unachokitafuta kwangu?
Bahati mbaya umetokea kunichukia kwa kuwa huniwezi.
Huyu ndiye Allah anatoa bila kuhesabu.
Mimi nimemwagiwa haya unayoona naandika hapa.
Wenzako wanafaidi.
Wanasoma wanaelimika.
Naandika mambo ya historia yalipotendeka nina akili zangu na huko yalikotendeka nimefika.
Tulia soma historia ya Wayahudi baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia.
Ndani ya historia hii utasoma vita vyao vyote na Waarabu.
Nakuwekea hapo chini nikiwa Giza, Cairo kwenye Pyramids, 1988.