IDF Jeshi bora kabisa duniani na MOSSAD idara bora zaidi ya ujasusi duniani!

IDF Jeshi bora kabisa duniani na MOSSAD idara bora zaidi ya ujasusi duniani!

Ni wiki 2 tu zimepita iran wamemuua afisa mwandamizi wa Mossad ndani ya Israel we unasema nini
Jina lake na cheo chake katika mossad na shirika gani la ujasusi katika serikali ya iran limehusika ni vyema ukatujuza kaka
 
T14...
Uliyoandika ndivyo upande mmoja unavyosema.

Ukiangalia upande mwengine ni kinyume na hayo.
Mimi nimekaa na wahusika wa pande zote mbili namaanisha maveteran wa vita hii ya mwaka 1973!!!Mzee said unaongea story sio experience ya vita!!!!Na mada ni ubora wa IDF kwenye uwanja wa mapambano
T14,
Sijakukwepa ukiona kimya jua nimetingwa nami si kijana kama wewe.

Sikawii kusinzia.
Udhaifu wa Israel si katika Yom Kippur bali baada ya pale katika tathmini na walipoingia vitani na Hizboullah IDF haikuwa ile iliyozoeleka.

Israel haikutoka katika uwanja wa vita kama ilivyozoeleka.

Watangazaji wa CNN walikuwa wanasema Wayahudi wamerudi kwao vichwa chini wamejiinamia.

Haya yalikuwa matangazo mubashara.

Sasa hili ni suala la mtazamo wa kila mtu anavyoona.

Lakini nimependa sana hii ya Israel kupigana na Hizboullah kundi la kigaidi.

Iko siku ikipatikana nafasi nitakueleza matatizo makubwa yaliyonifika na serikali ya Marekani kwa kusema maneno kama yako katika mkutano wa kimataifa.

Niliwaita Marekani magaidi.

Pasi yangu ya kusafiria ikaorodheshwa "for Special Treatment," ikawa dunia nzima "Passport Control" na Airport Security hawakai mbali na mimi.

Hii kwa miaka mingi.

Nilipofika New York nikagundua pia hata banks zina taarifa zangu.

Kisa kirefu.

Kuna mtu anaitwa Nelson kanitisha sana hapa kila saa ananiuliza kama nimewahi kujifunza silaha.
Unategemea CNN kujua experience ya uwanja wa vita kwa vikosi vya IDF au Hezbollah!!!!Ebu kua serious kidogo na millitary issues mzee wangu
 
Mzee Said hii mada niliyoleta wewe unaongea story za vitabuni hujawahi kuingia frontline au kushika bunduki na kupambana!!!Mada nazungumzia ubora wa IDF uwanja wa mapambano kulinganisha na majeshi mengine!!!Wewe unaleta siasa na vitabu wakati mada ni ubora wa jeshi kupigana hata katika mazingira magumu na kusurvive!!!2006 vita vya IDF na Hezbollah wewe unaongea story za wapambe wasio na weledi wa kijeshi na hukua frontline kushuhudia mapigano
 
Ahsante,
Naendelea kujadili na wengine kama unavyoona wananiuliza maswali.
Ningependa wenye uzoefu na vita ndio wajadili hili!!!Wewe mzee wangu ni mwanasiasa sio mtaalamu wa medani za vita utatoka nje ya mada!!!!Tunazungumzia ubora wa IDF kupambana na kusalimika hata katika mazingira magumu na tunazungumzia uzoefu wa uwanja wa mapambano!!!!Au mzee ushawahi kua mwanajeshi wa kikundi au jeshi lolote lile utupe uzoefu wako hapa???
 
Proved,
Hili suala la ushindi wa Hizbullah limezungumzwa sana.

Nami nimelieleza kwa kirefu katika mhadhara niliofanya State University of Zanzibar (SUZA) 2017.

Angalia post #189:

''Vita vilipoanza fikra za wengi katika nchi za Kiarabu zilirejea katika Vita Vya Siku Sita vya mwaka wa 1967 na wengi waliamini kuwa Hizbullah watamalizwa kwa muda mfupi kwa kusagwasagwa na Israel.

Hili halikutokea.

Vita vilipiganwa kwa siku 34 katika mwezi wa Julai na Agosti hadi pale Umoja wa Mataifa ilipoingia kati na kuweka makubaliano ya kuweka silaha chini na kumaliza vita.

Wayahudi kwa mara ya kwanza katika historia ya mapambano yao na Waarabu walionekana katika stesheni nyingi kubwa za televisheni duniani wakirudi Israel kutoka uwanja wa mapambano wameinamisha chini vichwa vyao.

Israel ilikuwa kwa mara ya kwanza imeonja kipigo katika vita.
Hapakuwa na shamrashamra ziliyozoeleka za ushindi dhidi ya majeshi ya Kiarabu.

Hizbullah ilikuwa imevunja, ‘’myth,’’ ile fikra ya kuwa Wayahudi hawawezekani.

Hassan Nasrallah kiongozi wa Hizbullah alikuwa akiuliza wakati wa vita, ‘’Wako wapi askari wa Kiyahudi mbona hatuwaoni katika uwanja wa vita?

Tunachoshuhudia ni ndege za Kiyahudi wakipiga mabomu nyumba za raia.’’

Baada ya vita, ilipofika wakati wa kubadilishana mateka Wayahudi walipata fadhaa zaidi pale walipokuwa wao wanapokea majeneza ya askari wao waliouliwa vitani Israel ikiwaachia huru askari hai wa Hizbullah.''
Mzee Said wewe umetoka nje ya mada mfano mdogo ni kua hujui hata pande zote mbili kwenye vita vya 2006 zilipoteza askari kiasi gani na mateka kila upande walikua kiasi gani,aina gani za mbinu walipigana,aina za mabomu yaliyotumiwa,aina za makombora yaliyotumika na nani aliharibu working structure ya kijeshi kwa kiasi kikubwa!!!Huna taarifa ya uhalisia kwenye uwanja wa mapambano unaleta siasa na taarifa za waandishi ambao hata bunduki hawajui kushika na kuingia frontline kushuudia vita na makali yake!!!
 
Proved,
Hili suala la ushindi wa Hizbullah limezungumzwa sana.

Nami nimelieleza kwa kirefu katika mhadhara niliofanya State University of Zanzibar (SUZA) 2017.

Angalia post #189.
Hii ni mada ya kijeshi tunazungumzia uzoefu na ubora wa jeshi husika wewe unaleta siasa na udini!!!Ubora wa IDF na zanzbar wapi na wapi mzee wangu!!!!Ndio maana nikakuuliza ushawahi kua katika uwanja wa mapambano ukikabiliana na mpinzani ana kwa ana????Utazungumziaje mambo ya kijeshi hata bunduki hujui kushika mzee wangu?????Au unadhani vita vinapiganwa mdomoni na kwenye mihadhara????
 
Mzee wangu Mohamed Said napingana na wewe hapa. Unasema Israel ilionyesha udhaifu tangu Yom Kippur mwaka 1973 kwa sababu zipi. Iipigwa surprise invasion na majeshi ya Egypt na Syria, Syria wakachukua Golan heights na Egypt wakachukua Sinai kwenye battle za mwanzo. Israel ikapiga counterattack ikaichukua Golan heights nzima na hata eneo ambalo hawakuwahi kuwa nalo na mpaka leo ni lao. Udhaifu wao uko wapi, kama ni dhaifu si Syria ingeteka Golan heights ikabaki nayo, mpaka leo inadai lile eneo.

Eneo la Sinai ni la Egypt lilikuwa limekaliwa na Israel kimkakati kama ambavyo Golan heights ni ya Syria ingawa imekaliwa na Israel, Sinai ilirudishwa kwa Egypt ili Anwar Saddat aitambue Israel kama nchi halali. Ndio maana Egypt ikaondolewa kwenye Arab League. Win win situation kwa Israel na Egypt. Hata Syria inaweza rudishiwa milima yake inhabitable ikifikia makubaliano na Israel.

Saddat alisimamisha mapigano baada ya jeshi lake kuzingirwa na Israel. Hakulazimishwa kusimamisha mapigano, angeendelea ili jeshi lake lipigwe na mateka wawe wengi. 3rd Army ya Misri ilizingirwa na majeshi ya Israel yakiongozwa na General Adan na 401st Armoured Brigade. Wanajeshi 20,000 wa Misri wamewekwa katikati, Israel iko inafanya advancement kuitafuta Cairo iliyokuwa less than 40 miles. Ulitaka Anwar Saddat afanyeje, ujue Waarabu wanafiki kina Saudi Arabia na wenzake wametuma misaada kidogo wako wanakunywa kahawa uko Egypt na Syria zinateseka zenyewe.

Wakati huo pale Syria kama unavyojua Damascus ni mji uko located eneo baya huwa sipendi vile, Israel ilikuwa imepanga shambulizi na imebakiza 10 miles kuifikia Damascus na Al Assad yuko desperate anaomuomba Saddat apigane mpaka mwisho ili kuipa relief Syria. Ambacho hawa wakurupukaji hawakuzingatia ni kwamba kila mtu anapigana kwa interest zake, Egypt za kwake zikitimizwa Syria shauri yako.

USSR ikatishia kuingia vitani zaidi, kumbuka hapo walishatoa misaada wa kila aina. Marekani na Uingereza zimesaidia Israel na Arab League plus USSR zimesaidia Waarabu. Israel ikaachana na kuiteka Damascus ila ikabaki na Golan heights ili ifanye monitoring.

Hakuna aliyelazimishwa ceasefire. Wangeendelea kupigana waambulie kupoteza maeneo mengine.

Na hapo kwa Hezbollah. Hicho ni chama chenye military wing, wala Hezbollah haijawahi unda serikali ya Lebanon. Iko termed kama kundi la kigaidi na usijifanye hujui tofauti ya kupigana na magaidi na kupigana na nchi. Israel haikupigana na Lebanon mwaka 2006, walipigana na kundi la kigaidi. Ile vita ingekuwa ni dhidi ya Lebanon ingeisha mapema sana. Na hata hivyo Israel haikushindwa, iko palepale ilipokuwa hadi leo. Wewe mwenyewe unajua lengo la Hezbollah ni lipi, limekamilika?
Vita Ya Israel na Hezbollah iliisha kwa Israel kukimbia na kuondoa Naval Blockade Lebanon.

Report ya Israel Jeshi bungeni kwao wanakiri Vita ilikua ni failure why mnapenda kudanganya danganya?

Hio full report ya Jeshi, je Jeshi la Israel halijui ila nyie huku mnafahamu zaidi?

Pia ukiongelea vita ya Yom kipur ongelea na Tarehe, bila kuweka tarehe ni rahisi Sana kulishwa propaganda.

Event zilikuwa hivi
1. Egpty anampiga Israel ghafla na kuvunja defense system yote
2. Israel Hana cha kujibu amepanic anamtishia marekani anapiga Nyuklia
3. Marekani wanaingilia vita a namsaidia Israel na Mazungumzo ya Kusitisha vita yanaanza
4. Sharon anafikiri anaweza kuiteka Cairo ila alibutuliwa vizuri tu ushahidi upo wa kutosha, Jeshi la Israel lilistopishwa Ismailia halikuvuka hapo na wala haijawahi hata kufika km 100 kabla ya Cairo
5. Israel wakakubali kurudisha eneo la Sinai Egpty
6. Propaganda zikaanza

Nina ushahidi wa vita u, magazeti na source za kipindi vita vinatokea na immediate baada ya vita, Kuna vitabu kibao Tena Vimeandikwa na west.
 
Wakati bin Laden alishusha majengo katikati ya marekani
Uwe unakaa kimya kama huna unalolijua. Unataka kuonekana unajua lakini hakuna unachojua wala kuelewa.

Hata serikali ya TANZANIA inajua Bin-Laden hakuhusika na lile tukio...

Uwe unauliza au unatafiti jambo kwa kina kabla hujalizungumza. Humu vinazungumzwa vitu smart na watu smart. Osama hakuhusika, nenda katafute documentaries usome na kusikiliza utajua source ya tukio na achievement zilikuwa ni zipi.
 
Mna stori za kisengerema nyie, ndege ikiwa kwenye runway inajiandaa kuruka unaweza ikimbilia?
Humu hapakufai nenda kwenye mada za watu wenye mawazo rahisi kule na wenye elimu za kusuasua. Elimu za kutetea wenye division zero kufeli kwao na kuwaponda wenye division one kwamba watakuja kuishia kutaabika na kuajiriwa na wenye zero! 😂😂😂

Kwa sababu huna ujualo unahisi vinashindikana. Wale ni makomando sio kama polisi jamii wa Tanzania wanaovizia mkojoe kwenye ukuta wawakamate wakawapandishe vizimbani mahakama ya Ilala
 
Hii ni mada ya kijeshi tunazungumzia uzoefu na ubora wa jeshi husika wewe unaleta siasa na udini!!!Ubora wa IDF na zanzbar wapi na wapi mzee wangu!!!!Ndio maana nikakuuliza ushawahi kua katika uwanja wa mapambano ukikabiliana na mpinzani ana kwa ana????Utazungumziaje mambo ya kijeshi hata bunduki hujui kushika mzee wangu?????Au unadhani vita vinapiganwa mdomoni na kwenye mihadhara????
Nelson....
Mimi naendelea kufanya mjadala na nachangia na wengine hapa JF.

Wewe bakia na uchunguzi kama nina leseni ya silaha mpaka utakapo jiiridhisha.
 
Vita Ya Israel na Hezbollah iliisha kwa Israel kukimbia na kuondoa Naval Blockade Lebanon.

Report ya Israel Jeshi bungeni kwao wanakiri Vita ilikua ni failure why mnapenda kudanganya danganya?

Hio full report ya Jeshi, je Jeshi la Israel halijui ila nyie huku mnafahamu zaidi?

Pia ukiongelea vita ya Yom kipur ongelea na Tarehe, bila kuweka tarehe ni rahisi Sana kulishwa propaganda.

Event zilikuwa hivi
1. Egpty anampiga Israel ghafla na kuvunja defense system yote
2. Israel Hana cha kujibu amepanic anamtishia marekani anapiga Nyuklia
3. Marekani wanaingilia vita a namsaidia Israel na Mazungumzo ya Kusitisha vita yanaanza
4. Sharon anafikiri anaweza kuiteka Cairo ila alibutuliwa vizuri tu ushahidi upo wa kutosha, Jeshi la Israel lilistopishwa Ismailia halikuvuka hapo na wala haijawahi hata kufika km 100 kabla ya Cairo
5. Israel wakakubali kurudisha eneo la Sinai Egpty
6. Propaganda zikaanza

Nina ushahidi wa vita u, magazeti na source za kipindi vita vinatokea na immediate baada ya vita, Kuna vitabu kibao Tena Vimeandikwa na west.
Baba...
Inabidi niseme kitu.

Nimefika Ismailia, Suez na Port Said na nimeona yote yaliyotendeka katika vita ya Wayahudi na Waarabu.

Nimeona ilipokuwa Bar Lev Line.

Nimesafiri Desert Road kutoka Cairo hadi Alexandria na nimerudi Cairo kwa njia ya kawaida kupitia Port Said na Damieta.

Jangwa zima kati ya Cairo na Alexandria ni kambi za jeshi.
Hii Damieta ilikuwa bandari mpya inajengwa jangwani lakini imeanza kazi.

Nimefika kwingi Misri - Tanta, Mehalla El Kubra hadi vijiji vidogo ndani ndani.

Baada ya safari hii nikatembelea Sudan na nikafika Haj Yusuf nikapiga kambi muda mrefu kisha nikaenda Jazeera katikakati ya Sudan.

Hapa ndipo Mahdi alipoongoza vita dhidi ya majeshi ya Gordon Pasha na kuiteka Khartoum miaka ya mwishoni 1800.

Nelson ajifunze kuwa na heshima kama yeye kapita jeshini katika ngazi zenyewe lazima atazijua sehemu hizi nilizotaja Misri na Sudan.

Ajiulize kote huko nani kanifikisha na kwa sababu zipi.

Nimefika pia na Zero Ground (Twin Towers), New York baada ya 9/11.

Nimehudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa Tehran.

Katika moja ya agenda iliyokuwa nzito ilikuwa haki ya Iran kutumia nguvu za nuklia kwa maendeleo.

Bahati mbaya Marekani na marafiki wa Israel hawakuwapo katika mkutano huu.
 
Mimi nimekaa na wahusika wa pande zote mbili namaanisha maveteran wa vita hii ya mwaka 1973!!!Mzee said unaongea story sio experience ya vita!!!!Na mada ni ubora wa IDF kwenye uwanja wa mapambano

Unategemea CNN kujua experience ya uwanja wa vita kwa vikosi vya IDF au Hezbollah!!!!Ebu kua serious kidogo na millitary issues mzee wangu
Nelson...
Mimi siko hapa kuhukumu CNN au chombo chochote kilichokuwa kinarusha taarifa za vita vile vya 2006.

Wala siko hapa kupambana na wewe nikushinde.
Maisha yangu yote mimi ni mtu wa kueleza ninachojua.

Nisome toka toka nilipoanza kuchangia uzi huu.

Nina hakika utanifahamu kama nina elimu ya somo lililoko mezani au sina nijuacho.

Nimekuwekea picha niko State University of Zanzibar, (SUZA) natoa mhadhara kuhusu vita vya Hizbullah na Israel 2017.

Kwa nini nialikwe mimi.
Kwa nini hukualikwa wewe?
 
Nelson...
Mimi siko hapa kuhukumu CNN au chombo chochote kilichokuwa kinarusha taarifa za vita vile vya 2006.

Wala siko hapa kupambana na wewe nikushinde.

Maisha yangu yote mimi ni mtu wa kueleza ninachojua.

Nisome toka toka nilipoanza kuchangia uzi huu.

Nina hakika utanifahamu kama nina elimu ya somo lililoko mezani au sina nijuacho.

Nimekuwekea picha niko State University of Zanzibar, (SUZA) natoa mhadhara kuhusu vita vya Hizboullah na Israel 2017.

Kwa nini nialikwe mimi.
Kwa nini hukualikwa wewe?
Babu

Kwani kutoa mhadhara si kukusanya tu taarifa based on your sources na kuzipackage na kudeliver?

Hizi podiums zisitudanganye sana
 
Humu hapakufai nenda kwenye mada za watu wenye mawazo rahisi kule na wenye elimu za kusuasua. Elimu za kutetea wenye division zero kufeli kwao na kuwaponda wenye division one kwamba watakuja kuishia kutaabika na kuajiriwa na wenye zero! 😂😂😂

Kwa sababu huna ujualo unahisi vinashindikana. Wale ni makomando sio kama polisi jamii wa Tanzania wanaovizia mkojoe kwenye ukuta wawakamate wakawapandishe vizimbani mahakama ya Ilala
Hahahaaa, eti komando, acha story za movie wewe, unajua ili ndege iruke inakuwa kwenye Kasi gani? Hilo tukio nilishaona movie yake miaka ya 90 na majuzi tu nimeona wameliigiza tena kwenye vipindi vya real responders
 
Humu hapakufai nenda kwenye mada za watu wenye mawazo rahisi kule na wenye elimu za kusuasua. Elimu za kutetea wenye division zero kufeli kwao na kuwaponda wenye division one kwamba watakuja kuishia kutaabika na kuajiriwa na wenye zero! 😂😂😂

Kwa sababu huna ujualo unahisi vinashindikana. Wale ni makomando sio kama polisi jamii wa Tanzania wanaovizia mkojoe kwenye ukuta wawakamate wakawapandishe vizimbani mahakama ya Ilala
Kaka wewe endelea tu kuwadanganya wagalatia wenzio, hao Israel vita kibao wamefeli, ndiomaana hata Hitler aliwachinjilia mbali
 
Back
Top Bottom