IDF Jeshi bora kabisa duniani na MOSSAD idara bora zaidi ya ujasusi duniani!

IDF Jeshi bora kabisa duniani na MOSSAD idara bora zaidi ya ujasusi duniani!

Nelson...
Ningekuwa mwanasiasa ningefahamika hivyo kote kwa sifa hiyo.

Mimi sijapata kuwa mwanasiasa.
Sio fani mbaya wala uhaini kua mwanasiasa!!!!Ni jambo jema na ni karama pia sababu sio wote wana kipawa cha kua wanasiasa mzee wangu
 
Nelson...
Unaonekana kichekesho.
Humvutii msomaji kukusoma.
Upo sahii mzee wangu kabisa kwa maoni yako ila nilileta mada kuhusu ubora wa IDF kwenye uwanja wa mapambano!!!Ukijadili ubora wa IDF kama raia au mwanasiasa huwezi kunielewa!!!!!
 
Vita Ya Israel na Hezbollah iliisha kwa Israel kukimbia na kuondoa Naval Blockade Lebanon.

Report ya Israel Jeshi bungeni kwao wanakiri Vita ilikua ni failure why mnapenda kudanganya danganya?


Hio full report ya Jeshi, je Jeshi la Israel halijui ila nyie huku mnafahamu zaidi?

Pia ukiongelea vita ya Yom kipur ongelea na Tarehe, bila kuweka tarehe ni rahisi Sana kulishwa propaganda.

Event zilikuwa hivi
1. Egpty anampiga Israel ghafla na kuvunja defense system yote
2. Israel Hana cha kujibu amepanic anamtishia marekani anapiga Nyuklia
3. Marekani wanaingilia vita a namsaidia Israel na Mazungumzo ya Kusitisha vita yanaanza
4. Sharon anafikiri anaweza kuiteka Cairo ila alibutuliwa vizuri tu ushahidi upo wa kutosha, Jeshi la Israel lilistopishwa Ismailia halikuvuka hapo na wala haijawahi hata kufika km 100 kabla ya Cairo
5. Israel wakakubali kurudisha eneo la Sinai Egpty
6. Propaganda zikaanza

Nina ushahidi wa vita u, magazeti na source za kipindi vita vinatokea na immediate baada ya vita, Kuna vitabu kibao Tena Vimeandikwa na west.
Israel alishindwa vita akabaki na Golan heights. Yaani how comes Tanzania ilishindwa vita na Iddi Amin ila ikabaki na Kagera salient?

Sinai ilirudishwa kwa Egypt, aliyekwambia Israel ilikuwa inalitaka jangwa lenye mchanga na mazalia ya magaidi nani? Sinai ni eneo la Egypt lilichukuliwa na Israel kwa muda kama adhabu ya Egypt kuwavamia mwaka 1967 kwenye Six Days war. Israel haikuiendeleza Sinai, haikuijenga wala haikuweka makazi ya raia. Eneo liliendelea kuwa na Egypt inhabitants mpaka 1982 Israel ilipowarudishia kwa kuitambua kama taifa huru, maana yake kukataa matakwa ya Palestina.
Hiyo ni ushindi wa kidiplomasia kwa Israel, Egypt ndio nchi ya kwanza ya Kiarabu kuitambua Israel (kuikana Palestina) na kufanya nayo amani. Ndio maana ikafukuzwa Arab League ambako ilikuwa kinara na Saddat akaja kuuliwa. Unajifanya hujui?

Marekani wakati anaingilia vita nchi zaidi ya kumi si zilikuwa zinasaidia Egypt na Syria? Na hayo makubaliano kuna aliyelazimishwa, si wangeendelea kupigwa kama wangetaka. Mbona Waarabu waliweka hadi mgomo wa kuiuzia mafuta Marekani.
 
Upo sahii mzee wangu kabisa kwa maoni yako ila nilileta mada kuhusu ubora wa IDF kwenye uwanja wa mapambano!!!Ukijadili ubora wa IDF kama raia au mwanasiasa huwezi kunielewa!!!!!
Nelson...
Uraia una uhusiano gani na uwezo
wa akili?

Mimi si mwanasiasa nimekueleza mara nyingi umeshindwa kuelewa lau wewe si raia.
 
Sio kweli, mbona wakati wa WW 2 walikua na jeshi kabisa kule Poland la wayahudi ila walichakazwa na Hitler kama Wana uwezo wa intelijensia au ni geniuses kwanini hawakuzuia mauaji Yale?

Hata hapo palestina hakuna maajabu zaidi ya kupewa matrillion Kila mwaka obviously hiyo pesa hata angepewa Jordan au Lebanon wangekuwa hatari sana. So labda useme pesa za mmarekani ndio za muhimu ila sio Mossad.

Kuwa na pesa haimaanishi kuwa na jeshi bora.
La si hivyo falme za kiarabu zingingekuwa na best armies ever.

Umetoa mfano wa WWII, to be honestly they we outnumbered, lack experience and training, haalf upigane na german forces by then wenye experience, numbers na technology uwanjani. Technicaly wangeshindwa tu

But wakajifunza from their mistakes, wakajifunza na ku adopt. Na ile hali ya kuishi kwenye constant threats imewafanya wawe alert muda wote, kimsingi hawakujisahau is why wako hapa walipo leo
 
Smart...
Sijui umetumia vigezo vipi kusema Marekani ikiingia vitani ni Iran itashinda vita.
Marekani walishindwa vita na Vietnam 1975.

Kipi kitakachowafanya washinde vita na Iran?

Kuhusu vita vya Israel na Iran Mungu apishie mbali madhara yake yatakuwa makubwa sana.

Israel haiwezi kuhimili vita vya muda mrefu hata kama itasaidiwa na Marekani.
[emoji706][emoji706]
 
Mleta mada una hoja nzuri zenye mantiki lakini jaribu kuepuka kuwekeza nguvu kubwa kwenye kupinga hoja kinzani.
Hoja inapingwa kwa hoja na sio kutengeneza mazingira ya kila hoja yako ikubalike na wote. Hii inatengeneza kuwe na wigo finyu wa mambo mengi kutanabaishwa bayana kwa wasomaji wenzangu.

Wengine tuko hapa kujifunza hivyo wekeni chakula cha ubongo mezani ili na sisi "Ngumbalo" wa haya mambo tujifunze.

Binafsi sina cha kuchangia ktk mada hii maana sina ABC's zozote juu ya intelijensia wala mambo yanayofanyika uwanja wa vita.


Cc: Mohamed Said, Nelson Jacob lushasi, Detective J, ,HIMARS
 
Back
Top Bottom