Nelson kaja kiushabiki akakutana na mhenga Mohamed Said dakika mbili nyingi kapigwa za uso
Trainee,
Uzee dawa.
Huyu kijana hatafanikiwa kitu.
Elimu ukiitaka sharti upinde mgongo ukunje goti kwa walimu usome.
Ukielelezwa jambo usilojua ndiyo ushajua hulirudii katika makosa kamwe.
Angalia nimemuelekeza mara ngapi kuhusu kuweka!!!???kwenye "text."
Prof. Shivji na jopo lake walipokuja nyumbani kwangu nilikataa kukaa juu ya kiti nilikaa miguuni kwao.
Wakaniuliza kwa nini.
Nikawaambia nyie mmenipokea Chuo Kikuu mkanisomesha na leo mie nimekuwa mtu kutokana na niyinyi laiti mngeniambia mnataka kunihoji kuhusu Mwalimu Nyerere mimi ningekufateni.
Leo wamekuja walimu wangu nyumbani kwangu mimi kuwaonyesha adabu siwezi kuning'iniza miguu yangu mbele yao.
Hii ndiyo adabu ya elimu.
Huyu Nelson nimetoka na yeye mbali katika uzi mwingine kuhusu historia ya Zanzibar.
Kanijua kuwa mimi si makamo yake mimi ni mzee, nimekaa darasani vyema, nimeandika vitabu na papers nyingi, nimesafiri dunia hii nimekuta na watu wengi muhimu katika historia ya Tanganyika.
Haya yalitosha kwake kunifahamu vyema kabisa na kama yeye yko hapa JF kupata na kutoa elimu tungekuwa tumeshikana na akaonyesha hesgima hata kama hatukubaliani fikra.
Badala yake anaandika anawaambia wasomaji kuwa mimi nahusilka na vurugu za Mwembechai na uvunjaji wa mabucha ya nguruwe na kuwa nataka Tanzania iwe nchi ya Kiislam.
Anajaribu kunivunjia heshima yangu.
Abubakar Sadik alipotawafu Mtume SAW alipopanda kwenye member ya Mtume SAW alikataa kukikalia kiti cha Mtume SAW alikaa pale Mtume SAW alipokuwa anakanyaga.
Siku niliposomeshwa mlango huu na mwalimu wangu nililia.
Hii ndiyo adabu ya elimu wengi hapa hawakujaaliwa kuipata na ndiyo sababu ya haya tunayoshuhudia hapa jamvini.
Kejeli, uongo, kibri na matusi.
Kulia Prof. Issa Shivji, Prof. Said Yahya Othman na Dr. Ng'wanza Kamata
kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam